Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu akiangalia namna watoa huduma wanavyopokea simu kutoka kwa
wananchi kwa ajili ya kupata elimu kuhusu ugonjwa wa Corona
WAMJW- Dar es Salaam
“Hapa nimeelezwa
kwamba kituo hiki kitahudumia kwa saa 24 kwa mwaka na kina uwezo wa kuhudumia
watu 300,000 kwa siku,” amesema Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, amependekeza kituo hicho kipatiwe jina la
‘Afya Call Centre’ badala ya kituo cha huduma za simu ambacho kitakuwa
kikishughulikia magonjwa yote.
“Kituo hiki kitakuwa kikizungumzia chanjo kwa watoto wenye
umri chini ya mwaka mmoja, tutazungumzia masuala ya liche kwa kina mama wenye
umri wa kuzaa, lishe kwa watoto wenye
umri chini ya miaka mitano, masuala ya huduma ya uzazi ya mama na mtoto,
tutanzungumzia mapambano ya ugonjwa wa kifua kikuu na masuala ya tiba,”
amesema.
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe amesema
kituo hicho kitatumika kutoa taarifa sahihi kwa jamii na kwa wakati.
Awali, Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Elimu ya Afya kwa
Umma, Dkt. Ama Kasangala alimweleza Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwamba kazi
kubwa ya kituo hicho ni kupokea maswali, maoni na ushauri kutoka kwa wananchi
na kufanyiwa kazi na wataalamu wa afya.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani Tanzania (WHO),
Dkt. Tigest Ketsela amepongeza kuanzishwa kwa kituo hicho kwa kuwa kitatumika
kujibu maswali ya wananchi kuhusu magonjwa mbalimbali.
Dkt. Ketsela taarifa zitakazotolewa katika kituo hicho zitatumika kuandaa jumbe
za kuielimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya afya.
Wadau wengine walioshiriki katika ujenzi wa kituo hicho
wameipongeza Serikali na Wizara ya Afya kwa kizindua kituo hicho kwani
kitasaidia kujenga imani kubwa kwa wananchi katika masuala yanayohusu afya.
|
No comments:
Post a Comment