Matokeo chanyA+ online




Wednesday, October 28, 2020

MAJALIWA APIGA KURA KIJIJINI KWAKE NANDAGALA WILAYANI RUANGWA

 


 




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Mkewe Mary Majaliwa wamepiga kura katika kituo cha kupigia kura kilichopo shule ya msingi Nandagala wilayani Ruangwa mkoani Lindi leo Oktoba 28, 2020








RAIS DK.JOHN MAGUFULI APIGA KURA, ATOA UJUMBE WA AMANI KWA WATANZANIA

 

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Chamwino

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli ametimiza wajibu wake wa kikatiba wa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo Oktoba 28 mwaka huu huku akitumia nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa kutunza amanĂ­ kabla na baada ya uchaguzi.


Dk.Magufuli amepiga kura katika kituo cha kupiga kura Idara ya Maji Chamwino-Ikulu ambapo alifika kituoni hapo saa tatu asubuhi akiwa ameongozana na mkewe mama Janeth Magufuli.

Baada ya kufika katika hicho Dk.Magufuli na Mama Janeth walipanga foleni kama ambavyo wamepanga wapiga kura wengine na alifuata mstari hadi jina lake lilipfika, hivyo akaingia ndani kupiga kura yake.Jina la Mama Janeth Magufuli lilikuwa la kwanza kuitwa na kuingia kupiga kura.

Alipomaliza kupiga kura,Dk.Magufuli ametumia nafasi hiyo kueleza amefurahishwa na utaratibu mzima wa upigaji kura kituoni hapo huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha amani kabla na baada ya uchaguzi mkuu.

“Nimeshapiga kura yangu na kidole change hiki hapa(akaoesha) , napongeza utaratib mzuri uliopo hapa kituoni, wananchi wengi wamejitokeza kupiga kura na niendelee kuwasisisitiza wale ambao bado hawajapiga waende wakatimize wajibu wao kikatiba,”amesema Dk.Magufuli.

Amewasisitiza wananchi wote nchini kuhakikisha wanendelea kuwa watulivu na kuendelea kulinda na kuitunza amani yetu kala na baada ya uchaguzi mkuu kwani kuna maisha baada ya uchaguzi.”


Kwa upande wake ,Msimamizi wa uchaguzi katika kituo hicho Othman Masasi amesema wananchi wengi wamejitokeza kupiga kura huku akitumia nafasi hiyo pia kuelezea kwamba Dk.Magufuli na mkewe Mama Janeth wamepiga kura katika kituo hicho.

“Uchaguzi unaendelea vizuri, watu wengi wamejitokeza na wanafuata utaratibu ambao umewekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), changamoto sio nyingi sana kwani inaonesha wananchi wengi wamekuwa na uelewa kuhusu kupiga kura,”amesema Masasi.


    

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakipiga kura ya Urais na Mbunge katika Kituo cha Kupigia Kura cha Idara ya Maji kilichopo katika Kijiji cha Chamwino Ikulu mkoani Dodoma leo tarehe 28 Oktoba 2020.

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwasili katika Kituo cha Kupigia Kura cha Idara ya Maji Chamwino Ikulu kwa ajili ya kupiga Kura leo tarehe 28 Oktoba 2020.

  

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa wamepanga mstari pamoja na Wapiga kura wengine katika Kituo cha Kupigia Kura cha Idara ya Maji kilichopo katika Kijiji cha Chamwino Ikulu mkoani Dodoma leo tarehe 28 Oktoba 2020.

 

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakifanya uhakiki kabla ya kupiga Kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Idara ya Maji Chamwino kwa ajili ya kupiga Kura leo tarehe 28 Oktoba 2020.

 

 

MAKAMU WA RAIS APIGA KURA SOS ZANZIBAR


 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipiga kura kwa ajili ya kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani katika kituo cha SOS Mombasa Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu unaofanyika leo Octoba 28,2020 (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika foleni ya kupiga kura kwa ajili ya kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani katika kituo cha SOS Mombasa Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu unaofanyika leo Octoba 28,2020.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea karatasi za kupiga kura kutoka kwa Muwandishi Yussuf Haji  katika kituo cha SOS Mombasa Zanzibar  kwa ajili ya kupiga kura kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani kwenye Uchaguzi Mkuu unaofanyika leo Octoba 28,2020.

Monday, October 26, 2020

BARABARA YA KILWA-NANGURUKURU-LIWALE KUJENGWA KWA LAMI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema sh. bilioni 1.3 zimetolewa ili kuanza kazi ya upembuzi yakinifu wa barabara ya Kilwa-Nangurukuru-Liwale.

Ametoa kauli hiyo  (Jumapili, Oktoba 25, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata za Likongowele, wilayani Liwale, mkoani Lindi kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Ujenzi wilayani humo. Pia alizungumza na wakazi wa kata za Kibutuka, Ngunichile, Lionja, Ruponda na Chiola kwa nyakati tofauti alipokuwa akirejea Ruangwa kutoka Liwale kupitia Nachingwea.

Alisema barabara ya Kilwa-Nangurukuru-Liwale yenye urefu wa km. 258 upembuzi wake unatarajiwa kuanza wakati barabara ya Liwale - Nachingwea - Ruangwa yenye urefu wa km.185 usanifu wake wa kina unaendelea na ukikamilika zitatafutwe fedha za kuzijenga kiwango cha lami. “Barabara hizi zinapatikana uk. 75 wa Ilani ya CCM ya 2020-2025.”

Akifafanua zaidi kuhusu barabara za mji wa Liwale, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. bilioni 1.7 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Liwale huku sh. milioni 891 zikitolewa kwa ajili ya matengenezo ya muda maalum na kwa kiwango cha lami kwa barabara za Sanabu – Mangota - Mponda, Mchanda - Ngosha Bucha, Wamao- Soko la Zain na Reiner Club- Nyanga.

Akielezea maboresho yaliyofanyika kwenye sekta ya afya, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. milioni 500 zimetolewa kwa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Liwale ambapo ujenzi wa jengo la OPD lipo hatua ya linta na ujenzi wa jengo la maabara lipo hatua ya kuezeka.

Alisema kwa mwaka 2020/2021 Halmashauri imepangiwa sh. bilioni moja kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo. Kwa upande wa vituo vya afya, alisema sh. bilioni moja zimetolewa kwa ajili ya ujenzi Kituo cha Afya cha Mpengere ambacho kimekamilika na huduma zinatolewa kwa wananchi. “Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kibutuka nao umekamilika na wananchi wanahudumiwa,” alisema.

Alisema sh. milioni 69.4 zimetumika kwa ukamilishaji wa zahanati za Mkundi, Chigugu na Barikiwa pamoja na kuchangia ujenzi wa jengo la mama na mtoto. “Pia shilingi bilioni 1.43 zilitolewa kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi. Fedha za ununuzi wa dawa ni wastani wa shilingi milioni 22.6 kwa mwezi,” alisema.

Mheshimiwa Majaliwa alikuwa wilayani Liwale ambako alienda kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Liwale, Bw. Zuberi Kuchauka na mgombea ubunge wa jimbo la Nachingwea, Dkt. Amandus Chinguile na madiwani wa kata alizopitia.

Akiwafafanulia mambo yaliyofanywa na Serikali ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya miaka mitano wilayani humo, Mheshimiwa Majaliwa alisema kwenye sekta ya maji, sh. bilioni 2.9 zimetolewa kwa ajili ya miradi mikubwa ya maji ikiwemo mradi wa Kipule – sh. milioni 559.2, ambao alisema umekamilika na unatoa huduma maeneo ya Kipule na Mkonganaje.

Aliitaja miradi mingine kuwa ni mradi wa maji Likombola ambao umegharimu sh. milioni 355.1 na kwa sasa umekamilika na unatoa huduma maeneo ya Likombola na Kitamamuhi. Mwingine ni mradi wa Maji Mangirikiti uliotumia sh. milioni 135.5 na sasa umekamilika na unatoa huduma vijiji vya Mangirikiti na Kimbamba.

Aliitaja miradi mingine ambayo bado inaendelea kujengwa na fedha zake kwenye mabano kuwa ni mradi wa maji Kibutuka (sh. milioni 213.1) ambao unakamilishwa kwa ajili ya Kijiji cha Kibutuka na mradi wa maji Kitogoro (sh. milioni 214) ambao unakamilishwa kwa ajili ya kijiji cha Kitogoro.

“Mradi wa Maji Mikunya uliogharimu sh. milioni 359 unakamilishwa kwa ajili ya vijiji vya Mikunya na Legezamwendo wakati mradi wa maji Mpigamiti uliojengwa kwa sh. milioni 11 unakamilishwa kwa ajili ya vijiji vya Mpigamiti, Namakororo na Mitawa.

Akielezea mpango wa elimu bila ada, Mheshimiwa Majaliwa alisema kwa shule za msingi  55 zilipatiwa sh. bilioni 1.5 kwa ajili ya ukarabati, utawala, michezo, mitihani na posho kwa maofisa elimu kata na walimu wakuu.

“Kwa shule za sekondari, shule 16 zilipatiwa kiasi cha shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya fidia ya ada, chakula kwa shule za bweni na posho ya madaraka kwa wakuu wa shule.

HATUA ZA KUCHUKUA KWA KAMATI ZA USIMAMIZI WA MAAFA NA SEKTA MBALIMBALI KUTOKANA NA UTABIRI WA MVUA ZA MSIMU

Ofisi ya Waziri Mkuu ina jukumu la kuratibu shughuli za maafa kwa kuhakikisha Wizara, Idara, Taasisi, Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na asasi zote zisizo za kiserikali zinashiriki kikamilifu katika kuzuia, kupunguza madhara na kujiandaa kukabiliana na kurejesha hali kwa mujibu wa Sheria ya Menejimenti ya Maafa namba 7 ya mwaka 2015. 


Hivyo, kufuatia utabiri wa mwelekeo wa mvua za Msimu katika kipindi cha miezi ya Novemba, 2020 hadi Aprili, 2021 uliotolewa leo na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imeonekana kuna haja ya Serikali na wadau wengine kuchukua hatua kama ilivyoelezwa taarifa ya utabiri huu ni kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua. 

 

Imeelezwa kwamba mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi.Hali inaweza kusababisha madhara mbalimbali kama uharibifu wa miundombinu, mazao na mifugo kusombwa na maji na milipuko ya magonjwa katika maeneo husika. Taasisi zote na wananchi wanaelekezwa kuchukua hatua kuzuia madhara ya maafa. Kabla mvua kubwa kuanza kunyesha kwa kipindi kilichoelezwa cha miezi ya Januari na Aprili 2021. 

Mikoa husika ni Dodoma, Singida, Mbeya, Songwe, Ruvuma, Njombe, Iringa, Lindi, Mtwara, kusini mwa mkoa wa Morogoro na mashariki mwa mikoa ya Tabora na Katavi. 

Vilevile, mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatabiriwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kanda ya Magharibi. Wadau wote na wananchi wanaelekezwa kuchukua hatua za kuzuia madhara yanayoweza kusababishwa na mvua kuwa ndogo ikiwemo kupanda mazao yanayokomaa mapema, kuvuna maji na kutunza malisho ya mifugo. Maeneo yanayo husika ni Mikoa ya Kigoma, Rukwa pamoja na magharibi mwa mikoa ya Tabora na Katavi. 


Kufuatia utabiri huo Ofisi ya Waziri Mkuu inatoa maelekezo kwa Kamati za Usimamizi wa Maafa za Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji katika mikoa husika nchini, ambazo ndizo zenye jukumu kubwa la kusimamia menejimenti ya maafa, kuchukua hatua mara moja za Kuzuia au Kupunguza, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali endapo maafa yatatokea. 

Kamati zote za usimamizi wa maafa katika ngazi zote, zieleze mipango na hatua za kuchukua kwa taasisi na wananchi juu ya menejimenti ya maafa ya mvua za msimu katika ngazi husika.
Ili kutekeleza agizo hili kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa namba 7 ya Mwaka 2015, ninaziagiza Kamati za Usimamizi wa maafa ziwajibike kutekeleza mambo yafuatayo katika sekta za kilimo, maji, afya, mifugo, miundombinu na nishati; 

1.    Wananchi washauriwe kutumia mvua hizi katika shughuli za maendeleo ikiwemo; kilimo, kuandaa mabwawa na malambo kwa ajili ya kuvuna maji, kupanda mazao yanayo hitaji maji mengi kama vile mpunga, uzalishaji wa samaki, kuandaa malisho na nyasi za akiba za mifugo katika mikoa inayotarajiwa kupata mvua nyingi.
2.    Kamati zote za Usimamizi wa maafa katika ngazi zote, ziweke mipango ya kuzuia milipuko ya magonjwa kama homa ya matumbo na kipindupindu na magonjwa ya milipiko ya mifugo.
3.    Kamati hizo zishirikiane na idara na taasisi zinazohusika na mazingira na miundombinu, ili kuhakikisha barabara zinapitika wakati wa msimu huo na mitaro, makalvati yanasafishwa kwa ajili ya kuruhusu maji kutiririka.
4.    Kamati zishirikiane na sekta za maji na umeme kuweka mipango yao na tahadhari kuhakikisha kuwa usumbufu unaotokana na ukosefu wa maji na umeme unapewa ufumbuzi mapema.
5.    Ili kukabili maafa na kurejesha hali kwa wakati endapo maafa yatatokea kamati katika ngazi zote ziainishe na kuandaa rasilimali za usimamizi wa maafa kwa kila sekta kushiriki kikamilifu katika eneo lake.
6.    Kamati zishirikishe wadau wa maafa (Wananchi, Taasisi na Sekta binafsi) katika mipango yao yote ya menejimenti ya maafa hayo.
7.    Kamati zishirikishe wadau wa maafa kuhakikisha upatikanaji wa mbegu zinazokomaa kwa muda mfupi pamoja na utunzaji wa chakula cha binadamu na mifugo katika maeneo ya mikoa inayotabiriwa kuwa na mvua chini ya wastani.

Ofisi ya Waziri Mkuu inatoa wito kwa kila mwananchi, kaya, kijiji, ngazi ya wilaya na mkoa kuhakikisha kuwa tunatimiza wajibu wetu katika suala zima la kushughulikia maafa kwa mujibu wa sheria ili mvua hizi ziwe na manufaa kwa taifa.  
Aidha, Serikali itaendelea kuutaarifu umma hatua za kuchukua kupitia taasisi husika
na vyombo vya habari kwa kadri Mamlaka ya Hali ya Hewa itakavyokuwa ikitoa utabiri wake. Hivyo basi, wananchi wote mnaombwa kufuatilia kwa makini tahadhari na kutumia taarifa hizo za wataalam kutoka sekta mbalimbali kwa usahihi na kuchukua hatua stahiki kwa ustawi wa uchumi wa nchi yetu. 

UCHAGUZI UMEKARIBIA, MJIHADHARI NA WANAOHUBIRI UDINI - KASSIM MAJALIWA

 

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema uchaguzi mkuu umekaribia sana na amewaonya wana-Lindi na Watanzania wote wajihadhari na viongozi wanaohubiri udini.

 

Ametoa onyo hilo jana (Jumapili, Oktoba 25, 2020) wakati akizungumza kwa nayakati tofauti na wakazi wa kata tano za Kibutuka, Ngunichile, Lionja, Ruponda na Chiola alipokuwa njiani akirejea Ruangwa kutoka Liwale kupitia Nachingwea.

 

Alikuwa wilayani Liwale ambako alienda kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Liwale, Bw. Zuberi Kuchauka na mgombea ubunge wa jimbo la Nachingwea, Dkt. Amandus Chinguile na madiwani wa kata alizopitia.

 

“Uchaguzi mkuu umekaribia, tuwe makini na wanaohubiri udini. Kiongozi anayehubiri udini huyo hafai kuwa kiongozi wa Watanzania. Wako wengine wanaoanza kuigawa nchi kwa ukanda, ukianza kuigawa nchi kwa ukabila, unaua misingi ya Taifa hili.”

 

“Leo tuko wamoja kwa sababu ya amani iliyodumishwa na waasisi wa Taifa hili. Leo makabila tofauti wanaishi pamoja bila kubaguana. Ndiyo umekuwa utamaduni wetu. Hata hapa kuna Wamasai, Wangindo, Wachaga na kadhalika. Tunahitaji tumchague kiongozi atakayetunza amani ya nchi yetu,” alisisitiza.

 

Alisema: “Natambua, wananchi wenzangu mmekuwa na muda wa miezi karibu miwili wa kufanya tathmini na tafakari ya kina ili nani awe kiongozi wa nchi hii, nani awe mwakilishi wa jimbo hili na nani awe mwakilishi wa kata hii kwa maana ya diwani. Nataka niwahakikishieni kwamba kiongozi anayefaa anatoka Chama cha Mapinduzi,” alisema.

 

“Nimeangalia katika wote wanaotaka kupewa Urais, hakuna kiongozi mwenye hizo sifa zaidi ya Dkt. John Pombe Magufuli. Tulimpa miaka mitano ya kuongoza nchi, amefanya mambo makubwa na nyote mmeona ama kusikia yaliyofanyika kupitia vyombo vya habari.”

 

Akifafanua sifa za kiongozi anayetakiwa, Mheshimiwa Majaliwa alisema: “Tunataka tupate kiongozi mahiri, mzalendo, mwadilifu na mwaminifu ambaye ni lazima tujiridhishe kuwa ataweza kuongoza nchi hii yenye watu zaidi ya milioni 60 na makabila tofauti.”

 

“Hatuhitaji kumchagua Rais ambaye sasa hivi anasema akiwa madarakani ataweka rehani madini yetu ili aweze kupata fedha za kuwawezesha wananchi. Sasa hivi nchi inapata mgao wa madini wa sh. bilioni 500 na ndiyo maana tunajenga hospitali, shule na barabara. Zamani tulikuwa tunapata shilingi bilioni 50 tu.”

 

Aliwataka wakazi hao wamchague Dkt. Magufuli ili apambane na wala rushwa na akawaonya wasimchague kiongozi ambaye amezungukwa na mafisadi au wala rushwa. Aliwataka wakazi hao wamchague Dkt. Magufuli kwa kura nyingi za ndiyo ili aweze kuleta maendeleo na kukamilisha yale mazuri aliyoyaanzisha.

 

“Tunataka kiongozi atakayelinda rasilmali za Taifa hili. Na huyo si mwingine bali ni Dkt. Magufuli. Ndugu zangu wa CHADEMA naomba kura zenu, wana ACT naomba kura zenu, CUF naomba kura zenu, na CHAUMA naomba kura zenu. Mchagueni Dkt. Magufuli awe Rais kwa sababu maendeleo hayana chama,” alisema.

 

Akielezea ni kwa nini anawaomba kura wananchi wa vyama vyote bila kujali itikadi zao za kisiasa, Mheshimiwa Majaliwa alisema: “Ni kwa sababu tunatafuta kiongozi wa nchi. Uongozi wa nchi unataka mtu mchapakazi na mwenye nia ya kuleta maendeleo kwa Watanzania, na huyu si mwingine bali ni Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.”

HATUENDI KWENYE UCHAGUZI KWA JAZBA - KASSIM MAJALIWA

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wasichague kiongozi kwa sababu ya jazba au hasira.

 

Ametoa wito huo (Jumatatu, Oktoba 26, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Nalasi, wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Katani. Mheshimiwa Majaliwa leo amezuru wilaya ya Tunduru akimuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli.


“Hatuendi kwenye chama kwa jazba wala kwa hasira. Hatari ya kipindi hiki unaweza kujikuta unaenda kwenye chama ambacho hakina sera wala hakieleweki. Chama makini kinapaswa kuwa na viongozi wanaoeleweka,” amesema.

 

Akitoa mfano, Mheshimiwa Majaliwa alisema leo hii kuna chama viongozi wake wamegombana na wala hakina mgombea urais. “Je ukikichagua chama hiki na ukawa na changamoto inakukabili, utaipeleka wapi? Au utampelekea nani? Na ukimchagua diwani au mbunge wa chama hicho, hayo masuala yako atayawakilisha kwa nani?”

 

“Ninawasihi, unapochagua viongozi, usichague chama kwa sababu maendeleo hayana chama. Chagueni chama ambacho kina mwelekeo na kinajali kutatua shida za watu. Ukienda kupiga kura, chagua diwani, mbunge na Rais anayetoka Chama cha Mapinduzi. Keshokutwa, tumchague Dkt. Magufuli kwa kura nyingi za ndiyo,” amesisitiza.

 

Mheshimiwa Majaliwa yuko wilayani Tunduru ambako alienda kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Tunduru Kusini, Bw. Adimu Mpakate na wagombea udiwani wa kata nne za jimbo hilo.

 

Akiwa njiani kuelekea Tunduru, Mheshimiwa Majaliwa alifanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya stendi ya mabasi ya Mangaka, wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara.

 

Akizungumza na wakazi wa Mangaka kwenye mkutano huo, aliwasihi Watanzania wasikubali kuandamana kwa kisingizio cha kutokubali matokeo ya uchaguzi kwa sababu huko ni kuvunja sheria.

 

“Ninawasihi vijana mjihadhari, msikubali kuandamana kwani mtakuwa mnavunja sheria na mtajikuta mnajiingiza matatizoni. Kuna mtu anakuja hapa na anatulazimisha kuandamana, huyo hafai kuwa Rais wa nchi.”

 

Mheshimiwa Majaliwa alitumia fursa hiyo kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Nanyumbu, Bw. Yahya Muhata na wagombea udiwani wa kata zote za jimbo hilo.

SINGIDA YATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI BIASHARA USAFIRISHAJI BINADAMU


Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Seperatus Fella, akiweka mkakati wa namna bora ya kukabiliana na biashara hiyo, alipokutana na wadau mbalimbali kwenye mafunzo maalumu mkoani Singida juzi.

Afisa wa Sekretarieti hiyo, Ahmad Said Mwen-dadi, akitoa mada kwenye mafunzo hayo.

wa Sekretarieti hiyo, Alex Lupilya akitoa mada kwenye mafunzo hayo.

Picha ya Pamoja ya baadhi ya wadau walioshiriki mafunzo hayo.

Na Godwin Myovela, Singida

Wakazi mkoani hapa wametakiwa kuwa makini kabla ya kuwaruhusu mabinti kuchukuliwa na kupelekwa maeneo mbalimbali nchini kwa kigezo cha kutafutiwa au kufanya kazi za ndani, badala yake wahakikishe kwanza wanahusisha uongozi wa Serikali ya Mtaa husika ili mchakato huo ufanyike kihalali.

Pia ‘dalali’ au mtu yeyote anayetaka kumchukua binti yako hakikisha anakuwa na mdhamini wa kuwezesha kurahisisha  mawasiliano ya mara kwa mara, lengo hasa ni kuwa na uhakika wa mazingira ya usalama wa mwanao huko aendako.

Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Seperatus Fella aliyasema hayo jana mkoani hapa, wakati akitoa mafunzo kwa wadau mbalimbali ya namna ya kupambana na biashara ya usafirishaji binadamu.

“Singida ikitanguliwa na Wilaya ya Kondoa Dodoma ni miongoni mwa mikoa ambayo wasichana wanachukuliwa na kwenda kutumikishwa kwa kufanyishwa biashara za ngono kwenye majiji kama Dar es Salaam na kwingineko,” alisema Fella.

Aliongeza kwamba tangu kuanza kwa mafunzo hayo kwa kushirikiana na mashirika ya kitaifa na kimataifa mwaka 2017, mkoa wa Singida ulikuwa bado haujafikiwa, na kinachofanyika kupitia mafunzo hayo ni kuwaelekeza wadau mbinu bora za kuzuia na kukabiliana kisheria na biashara hiyo haramu.

 Fella pamoja na mambo mengine, alisema kwa muktadha wa kitaifa hali siyo ya kuridhisha sana kutokana na mabinti wengi kuendelea kusafirishwa nje ya nchi kwa siri, kwa ahadi za kutafutiwa ajira zenye mshahara mnono jambo ambalo sio kweli, na kinyume chake hugeuzwa watumwa kwa kufanyishwa biashara za ngono na madawa ya kulevya kwa maslahi ya waliowasafirisha.

“Tunaendelea na juhudi za kuwaokoa, na hivi karibuni tumewaokoa mabinti wa kitanzania waliokuwa wakitumikishwa kama watumwa kutoka Iraq, Malaysia na India…na wametueleza kuwa bado wamewaacha wenzao wengi wakiendelea kuteseka,” alisema Fella.

Kwa upande wake Afisa wa Sekretarieti hiyo, Ahmad Mwen-Dadi, alisema biashara hiyo ni ya tatu kwa kuingiza fedha nyingi ikitanguliwa na ile ya Madawa ya Kulevya na Uuzaji wa Silaha Haramu, hivyo ni jukumu la kila raia wa Taifa la Tanzania kuchukua tahadhari kwa ulinzi madhubuti wa watoto na mabinti kuanzia kwenye ngazi ya familia.

Alisema madalali wa biashara hiyo wanapokutana na mabinti wamekuwa wakiwahadaa kwenda kufanya kazi kwenye mahoteli makubwa, maduka makubwa (supermarkets), Saluni na kazi nyinginezo zenye maslahi makubwa, jambo ambalo hatimaye huwashawishi mabinti walio wengi kutoroka bila kuaga wazazi.

“Wengi wanasafirishwa kupelekwa nchi za Thailand, China, Malaysia, Bangladesh na hata Iraq na wakifika huko wanajikuta kazi walizohaidiwa sio wanazifanya. Wengi tuliowaokoa wanasema wenzao wapo katika hali mbaya ya kutumikishwa kikatili mpaka pale watakapomaliza kulipa deni la gharama za kuwasafirisha hadi kufika kwenye hizo nchi,” alisema Mwen-Dadi.

Aidha, alitoa tahadhari kwa wana-singida na taifa kwa ujumla kuwa makini kutokana na ukweli kwamba kwa sasa usafirishaji wa ndani kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine hadi Zanzibar umeuzidi ule usafirishaji wa watoto na mabinti wa kitanzania kupelekwa nje.

“Naomba sana tuwe makini, bado hatujafikia umasikini wa kuacha watoto na mabinti zetu kwenda kudhalilishwa na kufanyiwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu. Mapambano dhidi ya biashara hii haramu ni jukumu letu sote kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa,” alisema.

Wadau waliopata fursa ya kushiriki mafunzo hayo ni Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kutoka Singida, Mashirika yasiyo ya kiserikali, kikiwemo Kituo cha Faraja na Jeshi la Wokovu, Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Maafisa Serikali za Mitaa.

Mafunzo hayo pamoja na mambo mengine yanalenga kuelimisha na kutoa taswira ya namna bora ya kukabiliana kisheria na biashara haramu ya usafirishaji binadamu, kuendesha kesi, kupepeleza na kutoa misaada ya utambuzi na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

Saturday, October 24, 2020

KASSIM MAJALIWA: LETENI MTU ANAYETOKA CHAMA MAKINI


Mjumbe wa Kamati Kuu ya halmashauri Kuu ya taifa ya CCM, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipomuombea kura mgombea Urais wa CCM, Rais DKt. John Pombe Magufuli, Mgombea Ubunge wa CCM wa Jimbo la Mchinga, Mama Salma Kikwete, na mgombea Udiwani wa CCM katika Kata ya Milola katika Jimbo la Mchinga, Magreth Namahonji katika mkutano wa Kampeni aliohutubia kwenye Kata ya Milola, mkoani Lindi, Oktoba24, 2020

Wananchi wa Jimbo la Mchinga wakishangilia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa kampeni kwenye Kata ya MIlola kumuombea kura mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mchinga kwa tiketi ya CCM, Mama Salma Kikwete kwenye Kata ya Milola mkoani Lindi, Oktoba 24, 2020.

Mke wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mama Mary Majaliwa akimuombea kura mgombea Urais wa CCM, Rais Dkt. John Pombe Magufuli,  mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo la Mchinga Mama Salma Kikwete (katikati) pamoja na Madiwani wa CCM katika mkutano wa kampeni  uliohutubiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa kwenye Kata ya Milola katika Jimbo hilo, Oktoba 24, 2020.

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa  akizungumza na mgombea Ubunge wa Jimbo la Mchinga kwa tiketi ya CCM, Mama Salma Kikwete katika mkutano wa kampeni aliouhutubia kwenye Kata ya Milola katika Jimbo hilo mkoani Lindi, Oktoba 24, 2020.

 


Amnadi Mama Salma Kikwete, madiwani Margareth na Casmiry

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa jimbo la Mchinga wawachague viongozi wanaotoka chama makini cha CCM.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Oktoba 24, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata za Milola na Rutamba, Manispaa ya Lindi kwenye mkutano uliofanyika Milola kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli.

“Leteni mtu ambaye anatoka kwenye chama makini. Mkipata mtu wa CCM atakuja mwenyewe Bungeni apate kuwasemea masuala yenu. Msimlete mtu wa kusema HAPANA kwa kila jambo. Tunapata nao shida sana,” amesema.

Akiwa Milola, Mheshimiwa Majaliwa aliwanadi mgombea ubunge wa jimbo la Mchinga, Mama Salma Kikwete, mgombea udiwani wa kata ya Milola, Bibi Margareth Namahochi na akiwa njiani kuelekea Lindi mjini, alimnadi mgombea udiwani wa kata ya Rutamba, Bw. Casmiry Mbinga.

Mheshimiwa Majaliwa aliwataka wakazi hao wasichague viongozi kwa presha na ushabiki hata kama ni ndugu zao. “Leo tunahitaji viongozi wenye uwezo wa kwenda kukaa meza moja na wazee, watu wenye umri wa kati na vijana. Kwa hiyo, tarehe 28 Oktoba, ambayo ni Jumatano ijayo ninawasihi mwende mkawachague viongozi wa CCM. Mwende mkampigie kura nyingi Dkt. Magufuli kwa sababu mipango yake imo humu ndani,” alisema huku akionesha Ilani ya CCM ya 2020-2025.

Aliwataka wakazi hao wamchague Dkt. Magufuli na waache michanganyo ya zamani kwani imewanyima maendeleo kwa kipindi kirefu. “Hebu tufanye tuone fursa ambayo Rais ametupa, tuache michanganyo, imetunyima maendeleo kwa muda mrefu.”

Naye Mama Salma Kikwete akiomba kura kwa wakazi hao, alisema hakuna Serikali ambayo imewahi kushindwa kuongoza hivyo akawaomba wampe kura ili aweze kutekeleza vipaumbele tisa ambavyo ameviandaa kwa maendeleo ya jimbo hilo.

“Chagueni viongozi wa CCM ambao tunazungumza lugha moja. Tunataka tushirikiane kuhimiza vipaumbele vya wananchi ambavyo ni afya, elimu, miundombinu, maji, nishati, kilimo, uvuvi, ufugaji na michezo.”

Naye, mbunge mteule wa jimbo la Mtama, Bw. Nape Nnauye alipopewa nafasi kumuombea kura Dkt. Magufuli aliwataka wakazi hao waache ushabiki wa kisiasa na wajifunze kutoka nchi jirani ambayo wananchi wake walipata maafa baada ya uchaguzi na wagombea wakabakia na makundi.

Naye aliyekuwa mbunge wa viti maalum wa CUF kisha akahamia CCM, Bibi Riziki Lulida aliwaonya wakazi hao waache ushabiki wa kisiasa kwa sababu hauna manufaa kwa jimbo la Mchinga na yeye ameyaona madhara ya upande wa pili.

“Mimi ni shuhuda wa mambo ya upande wa pili. Nilirudi CCM kwa mapenzi yangu. Nilikengeuka lakini sasa nimerudi nyumbani. Nataka niwaambie, mkifanya makosa ya ushabiki, mtajutia kupoteza kura zenu.”

“Tarehe 28 ikifika, wanawake wote twende tukampigie kura Mama Salma Kikwete ili idadi ya wanawake iongezeke ndani ya Bunge. Mkimpa kura mgombea mwanaume mtakuwa mmejiabisha ninyi wenyewe.”

Aliwasihi waichague CCM kwa sababu ina sera zinazoeleweka. “Wale wengine wanatuletea sera za ushoga? Chagueni CCM hao wengine wanataka tuangamie sababu dini zote zinakataa ushoga. Tusiwachague hao, la sivyo tutaangamia kwa kuruhusu sodoma na gomora,” alisisitiza.