Matokeo chanyA+ online




Wednesday, February 6, 2019

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI, AZINDUA MAHAKAMA INAYOTEMBEA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuzindua rasmi gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea  akiwa na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Sophia Mjema wakati wa   maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea  baada ya kuizindua rasmi akiwa na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi, Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk, Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird, wakati wa   maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam  Februari 6, 2019. Anayetoa maelekezo ni Mkuu wa Kitengo cha TEHEMA wa Mahakama ya Tanzania Bw. Enock Kalege na Kulia kabisa ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri Mahakama ya Tanzania Mhe. Eva Nkya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitelemka kutoka kwenye gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea baada ya kulizindua rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma wakati alipowasili kuhudhuria  maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza  Mkuu wa Kitengo cha TEHEMA wa Mahakama ya Tanzania Bw. Enock Kalegebaada ya kuzindua rasmi Mfumo wa Kielektroniki wa Kuratibu Mashauri (DSDS ll)  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Majaji Wakuu Wastaafu Mhe. Augustino ramadhani na Mhe. Mohamed Chande Othmana kabla ya kupiga nao picha ya kumbukumbu kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk  baada ya kuhudhuria   kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam

RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA MKUU WA UNHCR . IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Fillipo Grandi aliyeambatana na Watendaji wakuu wa shirika hilo, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Agustino Mahiga . Ikulu Jijini Dar es Salaam. Febuari 6, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamishna Mkuu wa Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Fillipo Grandi aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodrigues (kushoto) mara baada ya kumaliza Mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Kamishna Mkuu wa Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Fillipo Grandi Fillipo Grandi, alipokutana na kuzungumza nae Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kamishna Mkuu wa Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Fillipo Grandi, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Mkuu wa Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Fillipo Grandi aliyesiamama kulia kwa Mhe.Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Agustino Mahiga, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodrigues (wapili kutoka kulia) na watendaji wa UNHCR mara baada ya kumaliza Mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) kushoto kwake ni Kamishna Mkuu wa Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Fillipo Grandi ,mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kamishna Mkuu wa Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Fillipo Grandi, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.

MWENYEKITI WA CCM MHE. RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AMEKAGUA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA CCM SUKITA LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM.

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufguli na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Ujenzi wa ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufguli na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Ujenzi wa ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza Wajasiliamali wadogo Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu pamoja Dunia Seleman Simba Mjasiliamali wa Miwa mara baada ya kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlipa pesa Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu mara baada kununua Madafu yake, alipotembelea ili kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlipa pesa Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu mara baada kununua Madafu yake, alipotembelea ili kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na Katibu Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kunywa Dafu alilonunua kwa mjasiliamali Paschal Sabas mara baada a kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akinywa Dafu alilonunua kwa mjasiliamali Paschal Sabas mara baada a kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.

MISRI YAKUBALIANA NA TANZANIA KUJENGA KIWANDA KIKUBWA CHA NYAMA NA NGOZI

Na. Saja Kigumbe

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema serikali za Tanzania na Misri zimekubaliana kuanzishwa kwa kiwanda kikubwa cha nyama na mazao ya ngozi hapa nchini.

Waziri Mpina amebainisha hayo jana Februari 5,2019 ofisini kwake jijini Dodoma mara baada ya kupata ugeni kutoka nchini Misri ukiongozwa na Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Prof. Ezzaldin Aboussteit.

“Tunaenda kujenga kiwanda kikubwa cha kusindika nyama, cha kusindika ngozi, cha kusindika mazao ya ngozi, kiwanda ambacho hakipo katika nchi hizi zote za Afrika ya Mashariki na Kati.” Alisema Mhe. Mpina

Waziri Mpina amemuhakikishia waziri huyo wa Misri kuwa rasilimali za mifugo na uvuvi zilizopo nchini zipo salama na kwamba wizara imekuwa ikifanya jitahada kuhakikisha samaki hawavuliwi kwa njia haramu na hakuna biashara haramu ili kuhakikisha rasilimali hizo zinanufaisha viwanda vya ndani na wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta hizo.

Aidha Waziri Mpina amemuarifu Waziri wa Kilimo wa Misri Prof. Ezzaldin Aboussteit kuwa hakuna mifugo inayoruhusiwa kuingia nchini kutoka nje ya nchi bila ya kuwa na vibali na kuwa usimamizi wa nchi katika rasilimali za mifugo na uvuvi uko salama.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, makatibu wakuu wa wizara hiyo pamoja na manejimenti ya wizara.
Waziri wa Kilimo wa Misri Prof. Ezzaldin Aboussteit (kulia) akifafanua jambo katika kikao hicho huku akisiskilizwa kwa makini na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallaha Ulega na wajumbe wengine hawapo pichani
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (wa tatu kushoto) akizungumza ofisini kwake baada ya kutembelewa na ujumbe kutoka Misri ukiongozwa na Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Prof. Ezzaldin Aboussteit

Tuesday, February 5, 2019

TUTHAMINI VIPAJI VYA KILA MMOJA WETU











MATUNDA NA VYAKULA VYETU NI URITHI NA UBORA WA AFYA ZETU WATANZANIA







TANESCO,ABB WAENDELEA KUFUNGA TRANSFOMA YA MEGAWATI 240 KITUO KIKUU CHA UBUNGO

Timu ya wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kwa kushirikiana na Mkandarasi ABB wa nchini Switzerland, wameendelea na kazi ya kufunga transfoma yenye uwezo wa Megawati 240 katika Kituo Kikuu cha Kupoza na Kusambaza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya TANESCO iliyoitoa leo imesema transfoma hiyo iliingia hapa nchini Januari 28, 2019 na lengo ni kuendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuleta ufanisi katika usambazaji wa umeme katika jiji la Dar es Salaam na Pwani.

Akielezea uwezo wa Transfoma hiyo, Mkuu wa Kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme Ubungo, Mhandisi Joseph Msumali amesema transfoma hiyo yenye uwezo wa kusukuma takribani Megawati 240 kutoka kwenye msongo wa kilovoti 220 kuelekea Msongo wa kilovoti 132 kwa ajili ya usambazaji na matumizi ya nishati ya umeme katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
 Ufungaji wa Transfoma ukiendelea

SPIKA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAFADHILI WA MRADI WA KULIJENGEA BUNGE UWEZO

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Wafadhili wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wa pili kutoka mwisho upande wa Kulia ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson na wakwanza ni Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson (kulia) akifafanua jambo wakati wa Kikao kati ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai na Wafadhili wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo.
Mtaalam Mwadamizi wa masuala ya Jinsia na Utawala katika Ubalozi Ireland nchini Bi. Aran Corrigan (wakwanza kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao kati ya Spika wa Bunge na Wafadhili wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (watatu kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Wafadhili wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dodoma. Kushoto kwa Spika ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.
PICHA NA BUNGE