Matokeo chanyA+ online




Tuesday, June 4, 2019

SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KUMBUSHENI VIONGOZI, WATUMISHI KUTIMIZA WAJIBU WAO - RC MTAKA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema ni vema Sekreatarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma iendelee kuwakumbusha viongozi na watumishi wa umma nchini kutimiza wajibu wao ili kuweza kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali.

Mtaka ameyasema hayo Juni 03, 2019 Mjini Bariadi, wakati akifungua mafunzo kwa Viongozi wa Umma mkoani Simiyu, ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora.

Amesema ikiwa kila mmoja katika Utumishi wa Umma atatimiza wajibu wake jamii na nchi kwa ujumla wake itaweza kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali katika nyanja mbalimbali kwa wakati.

“Ni vizuri Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiendelea kuwakumbusha watu wote wanaofanya kazi zinazoihusu jamii kutimiza wajibu wao, kila mmoja akitimiza wajibu wake yapo mambo mengi sana sisi kama jamii, nchi, mkoa na kwa namna ambavyo uongozi na mgawanyiko wa .nchi yetu ulivyo tutafikia malengo yetu kwa wakati” alisema Mtaka.

Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa Umma ambao ni watoa maamuzi katika maeneo yao ya kazi kuwa makini katika kutoa maamuzi na wahakikishe wanafanya maamuzi kwa wakati.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele amesema viongozi wa Umma wanapaswa kutoa maamuzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa ili kutoiletea hasara Serikali.

Ameongeza kuwa Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma itaendelea kutoa elimu kwa viongozi wa umma juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi ya uadilifu katika uongozi na endapo ikitokea kiongozi yeyote atakengengeuka na kutofuata maadili sheria itachukua mkondo wake.

Kwa upande wake Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio ameshukuru Sekretarieti ya Maadili kwa kutoa mafunzo ya maadili kwa viongozi wa Umma na akatoa wito kwa viongozi hao kuwa waadilifu, kutekeleza majukumu yao na kutojilimbikizia mali kinyume na taratibu na maadili ya viongozi wa Umma.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa ametoa wito kwa Sekretarieti ya Maadili kwa viongozi wa Umma kutoa elimu ya maadili kila viongozi wapya wanapoteuliwa au kuchaguliwa, hususani madiwani wanapochaguliwa na kuunda Mabaraza mapya ya madiwani ili wajue misingiya uadilifu inayopaswa kuwaongoza katika kazi zao
PICHA%2BA
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Umma mkoani humo, wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
PICHA%2BB
 Baadhi ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
PICHA%2BC
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani humo, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
PICHA%2BD
 Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele, akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
PICHA%2BE
 Afisa Maadili kutoka Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Onesmo Msalangi akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
PICHA%2BF
 Baadhi ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
PICHA%2BG
 Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
PICHA%2BH
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.

SPIKA JOB NDUGAI AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI TAASISI YA KINGDOM LEADERSHIP NETWORK TANZANIA JIJINI DODOMA


 Spika wa Bunge, Job Ndugai (Kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi kutoka Taasisi ya Kidini ya Kingdom leadership Network Tanzania (KLNT), Mhe. Ibrahim Kaduma alipomtembelea nyumbani kwake Kisasa Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (Kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi kutoka Taasisi ya Kidini ya Kingdom leadership Network Tanzania (KLNT), Mhe. Ibrahim Kaduma alipomtembelea leo nyumbani kwake Kisasa Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (Kushoto) akimsikiliza na Mwenyekiti wa Bodi kutoka Taasisi ya Kidini ya Kingdom leadership Network Tanzania (KLNT), Mhe. Ibrahim Kaduma alipomtembelea leo nyumbani kwake Kisasa Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na viongozi wakuu kutoka Taasisi ya Kidini ya Kingdom leadership Network Tanzania (KLNT), walioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo Mhe. Ibrahim Kaduma, walipomtembelea leo nyumbani kwake Kisasa Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa tatu kulia) akiwa katika sala ya pamoja na viongozi wakuu kutoka Taasisi ya Kidini ya Kingdom leadership Network Tanzania (KLNT), walipomtembelea leo nyumbani kwake Kisasa Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Job Ndugai (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu kutoka Taasisi ya Kidini ya Kingdom leadership Network Tanzania (KLNT), walioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo Mhe. Ibrahim Kaduma (wa tatu kulia), walipomtembelea leo nyumbani kwake Kisasa Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WAZIRI BITEKO AKUTANA NA KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA NGWENA


Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Mwekezaji wa Kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena” na kufanya nao mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali, kubwa likiwa ni kutoa Ufafanuzi kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Madini inavyotoa fursa na mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya madini hapa nchini.
 Hatua hiyo inafuatia ombi la kampuni hiyo kuomba kukutana na waziri Biteko ili kupata ufafanuzi wa moja kwa moja kutoka kwake kuhusu mabadiliko hayo ya sheria.

Ombi la kutaka kuonana na waziri ni kutokana na kampuni ya Ngwena kupata taarifa za upotoshaji na zisizo sahihi kuhusu mabadiliko ya sheria ya madini yaliyofanywa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu taratibu mbalimbali za uwekezaji na shuguli nyingine zinazo husu sekta ya madini.

Upotoshaji unaofanywa kwa maksudi na baadhi ya watu ndani nan je ya nchi kwa lengo la kutaka kuifanya Tanzania kama sio mahali sahihi pa kuwekeza. 
Biteko ameuambia ujumbe wa kampuni ya Ngwena kuwa, mabadiliko ya sheria yamefanyika kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili mwekezaji na taifa kwa upande mwingine. 

Amefafanua kuwa, tangu mabadiliko hayo yapitishwe hakuna malalamiko ya kupingwa kwa marekebisho hayo kwakuwa yalizingatia maslahi mapana ya kila upande na kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanakuwa rafiki na ndio sababu mpaka sasa tangu marekebisho hayo yafanyike hakuna kampuni au muwekezaji alie acha wala kuonyesha nia ya kufunga shuguli zake kwa sababu ya marekebisho ya sheria.

Ameongeza kuwa, Tanzania inawahitaji sana wawekezaji na mara zote kila panapokuwa na jambo haliendi sawa mara moja hukaa na kujadili na mwekezaji na kutatua changamoto.
 Ameitaka kampuni ya Ngwena kwenda kuwa mabalozi ili kuwaeleza  wengine kuhusu ukweli ulivyo kuhusu marekebisho ya sheria yaliyofanywa na kuachana na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu ambao hawana dhamana ya kuyazungumzia masuala hayo. 

Amewakaribisha watu na wawekezaji wote wanaotaka kupata ufafanuzi wa jambo lolote kutembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
Aidha, kwa upande wa kampuni ya  Ngwena ukiongozwa na Meneja Mkuu H.E Kavishe amemshukuru Waziri kwa ufafanuzi mzuri alioutoa na kwamba walichokuwa wanakisikia na alichokisema waziri ni vitu tofauti na kuongeza kuwa, kuonana kwao kumewafungua masikio na kupata ukweli kutoka kwenye mtu sahihi na mwenye dhamana ya sekta ya madini.

Ameongeza kuwa, ni kweli upotoshaji waliokuwa wanaupata ungeweza hata kuwarudisha nyuma, hivyo watakwenda kufikisha ujumbe kwa wenzao.
Kikao hicho pia, kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Edwin Igenge, na Mkurugenzi wa Sera na Mipango  Wizara ya Madini, Augustine Ollal, Kamishna masaidizi anaeshuugulikia Migodi na Biashara Ali Ali na  Kamishna masaidizi anaeshugulikia Lesseni Maduh.
 Waziri wa Madini Doto Biteko wa Kulia katikati akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na ujumbe wa Kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena” waliomtembelea waziri kupata ufafanuzi kuhusu marekebisho ya sheria ya madini. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila.

 Waziri wa Madini Doto Biteko wa Kulia na Katibu Mkuu wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila kushoto  katikati wakiwasikiliza wageni wao wakati wa kikao cha pamoja na ujumbe wa Kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena” waliomtembelea waziri ofisini kwake kupata ufafanuzi kuhusu marekebisho ya sheria ya madini. 
Waziri wa Madini Doto Biteko hayupo pichani akimsikiliza kwa makini mmoja wa wajumbe wa Kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena” waliomtembelea ofisini kwake kuja kupata ufafanuzi kuhusu marekebisho ya sheria ya madini. 
Na Issa Mtuwa – Dodoma

Monday, June 3, 2019

RAIS DKT. MAGUFULI ATINGA SOKO LA SAMAKI FERRY AKIWA KATIKA MATEMBEZI YA JIONI


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara wa Samaki katika Soko la Samaki la Ferry jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kutumia mifuko mbadala na kuachana na kutumia mifuko ya plastiki wakati alipopita katika matembezi ya jioni.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipatana bei ya Samaki aina ya Lobster na mmoja wa wachuuzi katika Soko la Ferry mara baada ya kufika eneo hilo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipatana bei ya Samaki na wachuuzi katika Soko la Ferry mara baada ya kufika eneo hilo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka baada ya kununua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Samaki kabla ya kumnunua kutoka kwa mfanyabiashara wa Samaki Abraham Kaberege wakati alipkuwa katika matembezi ya jioni katika maeneo ya Soko hilo la Ferry jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wauza kahawa katika eneo la Soko la Ferry ambapo aliagiza kuboreshwa kwa sehemu ya biashara hiyo kuanzia siku ya kesho. PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA ASKOFU DKT. JOSEPHAT GWAJIMA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

1..
1
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
2...
2..
2
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima Ikulu jijini Dar es Salaam. 
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Naibu Waziri Ofisi wa Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira Anthony Mavunde wakwanza kutoka kushoto. PICHA NA IKULU

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA BARAZA LA TAIFA LA USHAURI KWA WATU WENYE ULEMAVU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wajumbe wa Baraza jipya la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa baraza hilo kushirikiana na Serikali wakati akizindua Baraza hilo katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF, Jijini Dodoma.

Na; Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amezindua rasmi Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu huku akilitaka baraza hilo kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano ili kuleta tija na mafanikio makubwa kwa Watu wenye Ulemavu nchini.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo alisema kuwa baraza linajukumu kubwa katika kuhakikisha usimamizi wa sekta ya watu wenye ulemavu pamoja na kuishauri Serikali juu ya masuala mbalimbali ya kundi hilo maalumu.
“Mtambue nafasi mliyopewa ni dhamana kubwa katika kuwahudumia watu wenye ulemavu ambao ni takribani asilimia 5 ya watanzania, hivyo ni vyema mkashirikiana na Serikali kubuni mikakati itakayosaidia kutatua changamoto zinazowakabili wenye ulemavu”, alisema Mhagama
Alifafanua kuwa Baraza hilo limeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya Mwaka 2010 na Sheria hiyo imeeleza majukumu ya Baraza ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri.
“Ni matumaini yangu mtakuwa washauri wazuri wa masuala ya watu wenye ulemavu kwa kuzingatia usawa kwa wote na si maslahi binafsi,” alisisitiza Mhagama.

Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akielezea jambo kwa wajumbe wa Baraza wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo uliofanyika tarehe 2 Juni, 2019 Jijini Dodoma.
Sambamba na hilo alimpongeza Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Dkt. Lukas Kija kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Wajumbe wengine kutokana na uaminifu na uwezo walionao katika kusimamia masuala ya Watu wenye Ulemavu.

Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha Watu wenye Ulemavu wanapata haki zao za msingi na kwa ajili ya ustawi wao katika Nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, afya, uchumi, kuwa na miundombinu rafiki pamoja na nyenzo za kujimudu.
Aidha Waziri Mhagama alitoa rai kwa watendaji wa Baraza hilo kuwa na miongozo yote inayohusu masuala ya Watu wenye Ulemavu itakayo wawezesha kufanikisha utendaji wao wa kazi.
Kwa Upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amesema kuwa Serikali katika mwaka 2019/2020 itaanza mapitio ya Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 ili kuwawezesha watu wenye ulemavu kwenda sambamba na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza jipya la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu mara baada ya kuzindua Baraza hilo Jijini Dodoma. Wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti mpya wa Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija, wa pili kutoka kushoto ni Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe na kulia ni Katibu Taifa wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bw. Jonas Lubayo.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija alieleza kuwa wapo tayari kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayosimamia haki na ustawi wa Watu wenye Ulemavu.
Aliongeza kuwa Baraza hilo lipo tayari kutoa ushauri na hoja zenye tija kwa Serikali juu ya masuala mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu.
Pia, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe alieleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa Baraza hilo na kufanya kazi pamoja katika kutatua changamoto zinazowakabili Watu wenye Ulemavu nchini ikiwemo migogoro na migongano kwa wadau.
Uzinduzi wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu umefanyika Juni 2, 2019 jijini Dodoma ambapo Baraza hilo litaongoza kwa kipindi cha miaka mitatu (2019 hadi 2021) likiongozwa na Mwenyekiti Dkt. Lukas Kija. Awali Baraza hilo lilikuwa likiongozwa na Dkt. Edward Bagandanshwa ambalo limemaliza muda wake mwaka 2017.

Sunday, June 2, 2019

MKEMIA MKUU WA SERIKALI AWASITIZA WAKAGUZI KUZINGATIA UELEDI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewasisitiza wakaguzi wa kemikali na maabara za kemia kuzingatia ueledi, uadilifu na uaminifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Mkemia Mkuu wa Serikali amezungumza hayo leo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia kutoka Mamalaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali unaofanyika Baraza la Maaskofu, Kurasini, Dar es Salaam. 
“Serikali imetupa majukumu ya kusimamia Sheria ya Mamlaka ya Maaabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani na Sheria ya Vinasaba vya Binadamu, hivyo tunapaswa kuzingatia ueledi, uadilifu, uaminfu na upendo ili kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa ufanisi.

Tutambue Serikali yetu imejielekeza katika kujenga uchumi wa viwanda na inajitahidi kuwekeza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara ikiwemo wanaojihusisha na kemikali, hivyo  tunapotekeleza majukumu yetu tunapaswa kuelewa uelekeo huo wa Serikali na kufanya maamuzi kwa wakati na haraka ili kutokwamisha wadau wetu huku  tukizingatia Sheria.”

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali alisema Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti inawapongeza wakaguzi hao kutokana na kazi kubwa wanayofanya na inawahamasisha kuboresha zaidi huduma kwa wadau kwa kufuata Sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza kama watumishi wa umma.

“Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti inatambua mchango mkubwa wa wakaguzi katika kusimamia Sheria na kuingiza maduhuli ambayo taasisi inatumia katika kuboresha huduma na kujiendesha. Tunatambua changamoto zipo na tunaendelea kuzifanyia kazi kama kuongeza watumishi na vitendea kazi. Tuna maeneo ya msingi ya kuyawekea kipaumbele hasa kwenye uwekezaji wa mitambo ya kisasa ya maabara na teknolojia ili kuwawezesha wakaguzi kutoa huduma bora na za haraka kwa wadau. Tufanye kazi kama familia ili kuweza kutekeleza majukumu yetu kwa mafanikio.” Alimaliza.

Akitoa neno la shukrani, Mkaguzi wa Kemikali, Bw. Jovitus Mukela, alimshukuru Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko kwa nasaha nzuri za ufunguzi wa Mkutano huo.

Kwa niaba ya wakaguzi wenzangu tunakushukuru sana kwa nasaha na maneno mazuri uliyotuambia maana pia yanatukumbusha majukumu yetu na napenda kuwaomba wakaguzi wenzangu kuzingatia yale yote yaliyozungumzwa na kushirikiana kutoa huduma nzuri, kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeitendea haki Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, sisi wenyewe na nchi kwa ujumla.” alimaliza 
1
 Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akiongea na Wakaguzi wa kemikali (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia ulioandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kufanyika leo katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Kurasini, Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara za Huduma za Ubora wa Bidhaa, Sabanitho Mtega, Maendeleo ya Biashara, George Kasinga, Usimamizi wa Kemikali, Daniel Ndiyo na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Elias Mulima.
2
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Kemikali, Daniel Ndiyo (aliyesimama), akizungumza na Wakaguzi wa Kemikali (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa tatu kulia) kufungua Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali leo.
03
 Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia wakimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo.
4
 Mkaguzi wa kemikali na Maabara za Kemia kutoka Maabara ya Kanda ya Kaskazini, Jovitus Mukela (aliyesimama), akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakaguzi mara baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufungua Mkutano huo.
6

7
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyekaa katikati), akiwa pamoja na Wakurugenzi na Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali mara baada ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi hao uliofanyika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Kurasini, Dar es Salaam.

WAZIR BITEKO ASHUHUDIA MAKABIDHIANO YA DHAHABU ILIYOKAMATWA MWANZA

Na GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameshuhudia makabidhiano ya mali ikiwemo dhahabu iliyokamatwa katika Wilaya Sengerema mkoani Mwanza, ikisafirishwa kinyume na sheria baada ya kutaifishwa na mahakama kuwa mali ya Serikali.

Makabidhiano hayo yamefanyika Mei 31, 2019 jijini Mwanza baina ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango aliyewakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Khatibu Kazungu.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Biteko amewasihi wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuachana na utoroshaji wa madini kwani biashara hiyo kwa sasa ni zilipendwa hivyo wafanye shughuli zao kwa kuzingatia sheria.

Naye DPP Biswalo Mganga amesema mali zilizotaifishwa ni dhahamu kilo 319 yenye thamani ya shilingi bilioni 27.018, fedha taslimu shilingi 305, mzani wa kupimia ubora wa madini, mizani ya kupimia madini pamoja na magari mawili ambapo vyote kwa pamoja vilikamatwa mwezi januari mwaka huu wilayani Sengerema. Aidha ameongeza kwamba dhahabu kilo tano iliyokamatwa mkoani Geita nayo imekabidhiwa serikalini baada ya kutaifishwa pia.

Baada ya kupokea mali hizo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Khatibu Kazungu ametoa shukrani kwa mamlaka zote zilizofanikisha kukamatwa, kutoa ushahidi na kutaifishwa na kwamba zitatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Madini, Khatibu Kazungu (wa kwanza kulia) wakishuhudia vipimo vya madini yaliyokamatwa wilayani Sengerema kabla ya kufanya makabidhiano.
Makabidhiano ya mali hizo yamefanyika leo jijini Mwanza na kushuhudiwa pia na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Madini yaliyokamatwa yakipimwa kabla ya makabidhiano kufanyika, hatua hii inajiri maada ya mahakama kutaifisha madini hayo.
Watuhumiwa 12 wakiwemo wenye mali wanne na askari polisi wanane walikamatwa wakihusishwa kuhusika na utoroshaji wa madini hayo wilayani Sengerema ambapo wenye mali walipatikana na hatia na kuhukumiwa huku askari polisi wakikana mashtaka dhidi yao ambapo bado kesi yao inaendelea mahakamani.
Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Madini, Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella wakishuhudiano vipimo vya madini hayo kabla ya kufanyika makabidhiano.
Viongozi mbalimbali wakishuhudia makabidhiano ya madini hayo.
Tazama BMG Online TV hapa chini