Matokeo chanyA+ online




Monday, October 7, 2019

SIMBACHAWENE AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA, UK AID KUJADILI MRADI WA KUKABILI ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI

Waziri wa Nchi Ofisi Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao na ujumbe kutoka Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) kujadili kuhusu Mradi wa Tanzania Urban Resilience Programme (TURP) unaotekelezwa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ambao umelenga kuzisaidia Halmashauri na Serikali Kuu katika kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.

Waziri wa Nchi Ofisi Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo wakati wa kikao na ujumbe kutoka Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) pamoja na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kilichofanyika jijini Dodoma.

Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Maendeleo Mijini na Usimamizi wa Majanga Kanda ya Afrika kutoka Benki ya Dunia Eric Dickson akitoa maelezo kuhusu Mradi wa kuzisaidia Halmashauri na Serikali Kuu katika kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi

Watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa na Naibu Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine (kulia) wakiwa katika kikao na Benki ya Dunia (WB) pamoja na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) katika kikao kuhusu mradi wa TURP ambao ukitekelezwa utaleta manufaa makubwa katika Jiji la Dar es Salaam na utaokoa maeneo yaliyo hatari kwa mafuriko na kuyafanya salama kwa maendeleo ya Jiji, utapendezesha kwa kuweka maeneo mazuri ya maegesho ya magari  maeneo kwa ajili ya shughuli za umma kama mikutano na matamasha na kubadilisha eneo la Mto Msimbazi linalokumbwa na mafuriko kuwa eneo linalofaa kwa ajili ya michezo na lenye manufaa ya kiikolojia kwa jiji la Dar es Salaam. 

Waziri wa Nchi Ofisi Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akisikiliza maelezo ya mradi kutoka ujumbe wa Benki ya Dunia na Shirika la Mendeleo la Uingereza. kikao kilicofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Raos jijini Dodoma.  


Watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa na Naibu Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine (kulia) wakiwa katika kikao na Benki ya Dunia (WB) pamoja na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) katika kikao kuhusu mradi wa TURP ambao ukitekelezwa utaleta manufaa makubwa katika Jiji la Dar es Salaam na utaokoa maeneo yaliyo hatari kwa mafuriko na kuyafanya salama kwa maendeleo ya Jiji, utapendezesha kwa kuweka maeneo mazuri ya maegesho ya magari  maeneo kwa ajili ya shughuli za umma kama mikutano na matamasha na kubadilisha eneo la Mto Msimbazi linalokumbwa na mafuriko kuwa eneo linalofaa kwa ajili ya michezo na lenye manufaa ya kiikolojia kwa jiji la Dar es Salaam. 

LIVE: RAIS DKT.JOHN MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI KATIKA UWANJA WA NELSON MANDELA MKOANI RUKWA


LIVE: ZIARA YA RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI MKOANI RUKWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli anafanya ziara ya siku tatu Mkoani Rukwa ambapo anafungua na kukagua miradi ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi wa Maeneo mbalimbali ya Rukwa na Wilaya zake

MAKAMISHNA WANNE WA JESHI LA POLISI WAKIONGONZWA NA MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI WATEMBELEA MRADI MKUBWA WA KUZALISHA UMEME MTO RUFIJI

Mhandisi Manda akitoa maelekezo juu ya Ujenzi mradi wa
uzalishaji Umeme katika Mto Rufiji kulia kwake ni Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Intelijensia ya Jinai CP Charles Mkumbo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz wa kwanza kutoka kulia ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas (PICHA NA JESHI LA POLISI)
Makamishna wa Polisi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz, katikati na kulia kwake ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas, Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Maabara na Uchunguzi wa Kisayansi CP Shaban hiki na kushoto kwa CP Boaz ni Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Intelijensia ya Jinai CP Charles Mkumbo wakiwa katika picha ya pamoja na Wahandisi wa Ujenzi wa mradi wa Umeme Rufiji baada ya kufanya ziara ya siku moja katika mradi huo.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz, akiongoza kikao cha Maafisa na Wahandisi wa Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa kuzalisha Umeme katika Mto Rufiji mkoani Pwani baada ya kufanya ziara ya siku moja katika mradi huo.

SERIKALI YAMAMISHA MNARA WA MAWASILIANO KUMALIZA MGOGORO

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akiielekeza kampuni ya Vodacom kuhamisha mnara na ujengwe eneo la shule ili kuepusha mgogoro na mmiliki wa eneo ulipojengwa mnara huo wakati wa ziara yake kwenye mnara huo, kijiji cha Bukuku, kata ya Rufita wilayani Nyang’hwale, Geita


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ameielekeza kampuni ya simu ya Vodacom kuhamisha mnara wake uliopo kijijii cha Bukuku, Kata ya Kafita wilayani Nyang’hwale mkoani Geita ili kumaliza mgororo uliopo baina ya Serikali na mwananhi anayemiliki eneo ulipojengwa mnara huo na kuujenga kwenye eneo la shule ya Msingi kulumbai iliyopo karibu na mnara huo ili wananchi wa kata hiyo waendelee kupata za mawasiliano
Nditiye amtoa maelekezo hayo alipofika kwenye eneo la kijiji cha Bukuku ulipojengwa mnara huo wakati wa ziara yake wilayani Nyang’hwale ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwa wananchi na kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo,  Hamim Guyama kuwa mmiliki wa eneo hilo Bi. Rukia Kashokelo na mme wake Clement Fungameza amekataa kusaini mkataba wa Vodacom na ameridhia mnara huo ung’olewe
“Mnara huu kwa huyu mama uhame tu kwa kuwa upo kwenye jiwe na anataka alipwe shilingi mioni kumi kwa mwaka na anakosesha mawasiliano, amegoma kupokea shilingi milioni mbili na laki nne kwa mwaka na eneo hili kuna migodi mitatu na mapato ya takribani bilioni 20 kwa mwaka na ni eneo linalohitaji mawasiliano kwa uchumi na ulinzi na usalama wa kata ya Kafita,” amesema Guyama

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akipata maelezo ya mgogoro wa mnara kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji cha Bukuku kilichopo kata ya Kafita, Nyang’hwale mkoani Geita, Eunice Gombanila wakati wa ziara yake kwenye eneo ulipojengwa mnara huo
Guyama amefafanua kuwa mmiliki wa eneo amefanya jitihada za kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ili kuhakikisha kuwa wanapata malipo hayo kwa kukodisha eneo lao ulipojengwa mnara na kukataa kusaini mkataba na Vodacom wa malipo ya awali waliyokubaliana
Nditiye ameipata kampuni ya simu ya Vodacom kuhakikisha kuwa inahamisha mnara huo ndani ya mwezi mmoja na amepiga marufuku kwa kampuni za simu zinazojenga minara kwa kutumia ruzuku ya Serikali wanayopewa kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kujenga mnara kwenye eneo la mtu binafsi ili kuepusha migogoro kwa kuwa Serikali haiko tayari kuingia migogoro na wananhi wake bali minara ijenge kwenye maeneo yanayomilikiwa na Serikali ya kijiji, shule au maeneo ya kanisa au misikiti ili wananchi wanufaike na fedha zinazolipwa na kampuni za simu


Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Hamimu Guyama akitoa taarifa ya mgogoro wa mnara wa Kata ya Kafita kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) wakati wa ziara yake wilayani humo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano. Wa kwanza kushoto ni mbunge wa jimbo hilo, Houssein Amir
Naye Mtendaji wa Kijiji cha Bukuku kilichopo kata ya Rufita wilayani Nyag’hwale mkoani Geita, Eunice Gombanila ulipojengwa mnara huo amemweleza Nditiye kuwa mama huyo amekataa kupokea na kusaini mkataba baina yake na Vodacom ambapo alilazimika kukaa na mkataba huo ofisini kwake kwa muda wa wiki nne bila ya mafanikio na alipomfuata mmmiliki wa eneo hilo alikataa kusaini mkataba huo na maeridhia ung’olewe
Mkuu wa Uedeshaji wa UCSAF, Mhandisi Albert Richard amesema kuwa ujenzi wa mnara huo umegharimu dola za marekani 180,000 ambazo ni zaidi ya shiingi milioni 200 za kitanzania na kuongeza kuwa mnara huo umehujumiwa kwa kung’olewa paneli tatu za sola ambazo zinazalisha umeme wa jua kwa ajili ya kuwasha mnara huo ili uweze kuwaka na kusambaza mawasiliano kwa wananchi

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Hamimu Guyama kitabu cha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote chenye orodha ya minara iliyojengwa na Serikali wilayani humo wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano.
Mhandisi wa Vodacom, Benedict Mara ameishukuru Serikali kwa kutoa maelekezo ya kuhamisha mnara huo na watatekeleza maelekezo hayo ili waweze kuendelea kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi na wakazi wa kata ya Kafita
Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kulumbai iliyopo Kata ya Kafita wilayani Nyang’hwale, James Jacob amefurahia uamuzi wa Serikali wa kujenga mnara huo kwenye eneo la shule baada ya mmiliki wa eneo ulipojengwa mnara huo hapo awali kuridhia ung’olewe kwa kutaa malipo ya Vodacom na amesema kuwa malipo hayo yataiwezesha shule kujiendesha
Mbunge wa Nyang’hwale, Houssein Nassoro Amir amemweleza Nditiye kuwa anaiomba Serikali kuboresha mawasiliano ya kata ya Nyamtukuza, Nundu, Nyijundu, Kafita, Kaboha na Shabaka kwa kuwa kuna shida ya mawasiliano na ukitaka kupata taarifa saa tano asubuhi unapata saa kumi jioni hivyo inaleta changamoto ya ulinzi na usalama
“Serikali inatumia mtandao kukusanya mapato yake ila mtu analazimika kukaa na fedha kwa muda mrefu kwa sababu usikivu wa mawasiliano sio mzuri hivyo tunashindwa kukusanya mapato ya Serikali kwa wakati,” amesisitiza Amir

Mhandisi wa Kampuni ya Vodacom, Benedict Marwa, akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) kwa niaba ya Serikali kwa kuielekeza kuhamisha mnara wa kata ya Kafita ili kuepusha mgogoro na mmiliki wa eneo wakati wa ziaa yake wilayani Nyang’hwale, Geita.
Katika hatua nyingine, Nditiye amemwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba na Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta kufika wilayani Nyang’hwale ndani ya mwezi huu wa Oktoba, 2019 na kufungua ofisi zao ili kuweza kuwahudumia wananchi na kusogeza karibu huduma zao. Na Prisca Ulomi, Nyang’hwale, Geita

NAIBU WAZIRI NDITIYE AKAGUA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa Vodacom, Benedict Mara (wa kwanza kulia) kuhakikisha mawasiliano yanapatikana muda wote Kata ya Ilolangulu wakati wa zaiara yake ya kukagua upatikanaji wa hudumaza mawasiliano wilayani Mbogwe, Geita

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye yuko ziarani mkoani Geita kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano, kuhamasisha wananchi kusajili laini za simu kwa njia ya alama ya vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA na kufuatilia utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi mkoani humo
Wakati akiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Mbogwe, Nditiye amesema kuwa malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanawasiliana, huduma za mawasiliano zinakuwa zenye ubora unaotakiwa, za uhakika na kunakuwa na usikivu mzuri wa mawasiliano kwa kuwa Serikali inataka wananchi wawasiliane
“Serikali tunataka wananchi wawasiliane kwa kuwa wakiwasiliana tunapata mapato ambayo yanaendesha shughuli mbali mbali za kuhudumia wananchi,” amesema Nditiye
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi amemweleza Nditiye kuwa wanashida ya mawasiliano kwenye wilaya yao na mara nyingine wanakwama kukusanya mapato ya Serikali hivyo inawapa changamoto katika kuwatumikia wananchi na utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Serikali



Mkuu wa uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) kuhusu mnara wa Ilolangulu wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano Mbogwe mkoani Geita 

Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Agostino Masele akimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye vijiji ambavyo havina mawasiliano ya uhakika wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano wilayani Mbogwe mkoani Geita

Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi akitoa taarifa ya hali ya mawasiliano kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake wilayani humo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano
“tunashida ya mawasiliano kwenye wilaya yetu na mara nyingine tunakwama hata kukusanya mapato na kupeana taarifa za ulinzi na usalama hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi,” amefafanua Mkupasi
Nditiye amemweleza kuwa amekagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano wilayani humo na amegundua kuwa Wilaya ya Mbogwe inapata mawasiliano kwa kiwango cha asilimia 90 na ina mitandao mingine ya mawasiliano ila wananchi wanaonekana wanapenda mtandao wa Vodacom
Naye Mbunge wa Mbogwe, Agostino Maselle amekiri kuwa wanapata huduma za mawasiliano za mitandao mingine ya TTCL, tigo, halotel, airtel na yote iko vizuri ila mtandao wa Vodacom unasumbua na huduma za m-pesa kwenye kata ya Ilolangulu, Itobe na Isesya
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kata ya Ilolangulu, mkazi wa kata hiyo Daniel Mishigitu amemweleza Nditiye kuwa wanapata kero ya mawasiliano ya Vodacom na wakitumiwa hela inakaa muda mrefu kwenye mtandao. Naye Vedastus Rwechungura amemshukuru Nditiye kwa kufika na kusikiliza shida ya mtandao huo na mzunguko wanaoupata wakitaka kutoa pesa ambapo mara nyingine wanalazimika kusafiri kwenda Ushirombo
Akijibu malalamiko ya wananchi, Nditiye amewaeleza kuwa amegundua kuwa kuna mzunguko wa hela kwenye kata hiyo na uchumi wa wananchi uko vizuri, hivyo ameielekeza kampuni ya Vodacom kuwa ndani ya muda wa miezi sita mnara uwepo ili wananchi waweze kuwasiliana, kutuma na kupokea pesa kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanawasiliana na wakiwasiliana inapata mapato
Nditiye amefanunua kuwa sehemu inapokuwa na mawasiliano ya kampuni moja inatosha na sio lazima kuwa na mitandao yote ila kwa kuzingatia kuwa wananchi wamehitaji mtandao huo hivyo UCSAF kwa kushirikiana na Vodacom ihakikishe kuwa mnara huo unajengwa na TCRA wafuatilie na kusimamia jambo hilo
Katika ziara hiyo, Nditiye ameambatana na wataalam kutoka wizarani kwake Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na watoa huduma wa kampuni ya VodacomPrisca Ulomi, Geita

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA VIJANA WA KWAYA YA RIGHT ANGELS MORAVIAN CHURCH IKULU NDOGO YA TUNDUMA

Wana Kwaya ya Vijana wa Right Angels Moravian Church ya Tunduma wakipata chaikatika Ikulu ndogo ya Tunduma walipokaribishwa kuonana na Rais Dkt. John. Pombe Magufuliambaye aliwaita na kuonana nao baada ya kufurahishwa na wimbo waomzuri wa kulaani rushwa waliomwimbia wakati wa zira yake mkoani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduma Mhe. Juma Irando akiwa na Katibu Tawala wa  Mkoa wa Songwe Mhe. David Kafulila wakiwa wameongozana nawanaKwaya ya Vijana wa Right Angels Moravian Church ya Tunduma
wakiwasili Ikulu ndogo ya Tunduma kuonana na Rais Dkt  John. Pombe Magufuliambaye alikaribisha na kuonana nao baada ya kufurahishwa na wimbo waomzuri wa
kulaani rushwa waliomwimbia wakati wa zira yeke mkoani humo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pompe Magufuli na mkewe Mama Janeth Mafuguli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela, Mkuu wa Wilaya ya
Tunduma Mhe. Juma Irando akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Mhe. David Kafulila na wanaKwaya ya Vijana wa Right Angels Moravian Church ya Tunduma walipokuwa Ikulu ndogo ya Tunduma kuonana na Rais Dkt John. Pombe Magufuli ambaye alikaribisha na kuonana nao baada ya kufurahishwa na wimbo wao mzuri wa kulaani rushwa waliomwimbia wakati wa zira yeke mkoani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pompe Magufuli na mkewe Mama Janeth Mafuguli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela, Mkuu wa Wilaya ya
Tunduma Mhe. Juma Irando akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Mhe. David Kafulila na wanaKwaya ya Vijana wa Right Angels Moravian Church ya Tunduma walipokuwa Ikulu ndogo ya Tunduma kuonana na Rais Dkt John. Pombe Magufuli ambaye alikaribisha na kuonana nao baada ya kufurahishwa na wimbo wao mzuri wa kulaani rushwa waliomwimbia wakati wa zira yeke mkoani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pompe Magufuli na mkewe Mama Janeth Mafuguli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela, Mkuu wa Wilaya ya
Tunduma Mhe. Juma Irando akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Mhe. David Kafulila na wanaKwaya ya Vijana wa Right Angels Moravian Church ya Tunduma walipokuwa Ikulu ndogo ya Tunduma kuonana na Rais Dkt John. Pombe Magufuli ambaye alikaribisha na kuonana nao baada ya kufurahishwa na wimbo wao mzuri wa kulaani rushwa waliomwimbia wakati wa zira yeke mkoani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pompe Magufuli na mkewe Mama Janeth Mafuguli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela, Mkuu wa Wilaya ya
Tunduma Mhe. Juma Irando akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Mhe. David Kafulila na wanaKwaya ya Vijana wa Right Angels Moravian Church ya Tunduma walipokuwa Ikulu ndogo ya Tunduma kuonana na Rais Dkt John. Pombe Magufuli ambaye alikaribisha na kuonana nao baada ya kufurahishwa na wimbo wao mzuri wa kulaani rushwa waliomwimbia wakati wa zira yeke mkoani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pompe Magufuli na mkewe Mama Janeth Mafuguli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela, Mkuu wa Wilaya ya
Tunduma Mhe. Juma Irando akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Mhe. David Kafulila na wanaKwaya ya Vijana wa Right Angels Moravian Church ya Tunduma walipokuwa Ikulu ndogo ya Tunduma kuonana na Rais Dkt John. Pombe Magufuli ambaye alikaribisha na kuonana nao baada ya kufurahishwa na wimbo wao mzuri wa kulaani rushwa waliomwimbia wakati wa zira yeke mkoani humo.

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA VITUO VYA KUPOZA UMEME KWA MIKOA MINNE


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) wakipongezana mara baada ya Waziri Mkuu, kuweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme kilichopo Misuna, wilayani Singida, Mkoa wa Singida. Kituo hicho kinaongezewa nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameweka Jiwe la Msingi katika  mradi wa upanuzi wa vituo vinne vya kupoza umeme vinavyoongezewa nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400 katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga.
Hafla hiyo ilifanyika tarehe 5 Oktoba, 2019 mkoani Singida na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Sima, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula.
 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifunua kitambaa kuashiria uwekaji jiwe la msingi katika mradi upanuzi wa kituo cha kupoza umeme kilichopo Misuna, wilayani Singida, Mkoa wa Singida. Kituo hicho kinaongezewa nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400 
Viongozi wengine waliohudhuria ni Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt Tito Mwinuka, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA), Mhandisi Amos Maganga na watendaji kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA).
Waziri Mkuu, alisema kuwa, tukio hilo linaashiria pia uzinduzi wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme mkubwa wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Singida, Manyara, Arusha, Namanga hadi Isinya nchini Kenya (KTPIP) ambao tayari upo kwenye hatua za ujenzi.
Aliongeza kuwa, kukamilika kwa miradi hiyo kutawezesha gridi ya Taifa kuwa na uwezo mkubwa wa usafirishaji umeme na kuwezesha nchi kuwa na umeme wa uhakika, unaotosha mahitaji  na unaotabirika.
 

Baadhi ya wafanyakazi katika mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme kilichopo Misuna, wilayani Singida, Mkoa wa Singida wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye kituo  hicho kinachoongezewa nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto) akisalimiana Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua mara baada ya kuwasili katika eneo la Misuna wilayani Singida ili kuweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme. Kituo hicho kinaongezewa nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400.

Baadhi ya viongozi, wataalam kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakandarasi pamoja na wananchi  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye kituo cha kupoza umeme kilichopo Misuna, wilayani Singida, Mkoa wa Singida. Kituo hicho kinaongezewa nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia, mbele) na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto, mbele) na viongozi mbalimbali wakipiga makofi mara baada ya Waziri Mkuu kuweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme kilichopo Misuna, wilayani Singida, Mkoa wa Singida. Kituo hicho kinaongezewa nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400.

Alisema, Serikali inaendelea na jitihada za utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme ukiwemo mradi wa umeme wa Julius Nyerere (MW 2115) kwani lengo ni kuwa na megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025 na kusambaza umeme kwenye maeneo yote nchini.
Waziri Mkuu, vilevile aliipongeza Wizara ya Nishati, TANESCO na REA kwa usimamizi thabiti wa miradi mbalimbali ya nishati ikiwemo ya usambazaji umeme vijijini ambapo ameeleza kuwa hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu jumla ya Vijiji 8,102 vimesambaziwa umeme kati ya vijiji 12,268.
Awali, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani alieleza kuwa mradi wa upanuzi wa vituo hivyo vya kupoza umeme ni wa Awamu ya Pili kwani Awamu ya kwanza ilijumuisha ujenzi wa njia kuu ya kV 400 kutoka Iringa hadi Shinyaga, pamoja na upanuzi wa vituo vya kupoza umeme kwa msongo wa Kv 220 kwenye miji ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga na ulikamilika Disemba 2016.
Aliongeza kuwa mradi huo wa awamu ya kwanza ulisambaza umeme kwenye vijiji 121 vilivyopitiwa na miundombinu ya umeme na kwa mradi huu wa Awamu ya Pili, jumla ya vijiji 19 vitakavyopitiwa na miundombinu ya umeme kutoka Singida, Manyara hadi Arusha vitasambaziwa umeme.
Alisema kuwa gharama zitakazotumika kwenye ujenzi wa vituo hivyo vinne vya kupoza umeme ni Dola za Marekani milioni 120  na Kituo cha Singida kinatarajiwa kukamilika mwezi Februari mwaka 2020. Na Teresia Mhagama, WN