Monalisa Yvonne Cherrie akisoma Sehemu ya Hotuba ya wasanii kwa Mhe. Rais Magufuli katika Tamasha la #MwalimuNyerereArtsFestival
Friday, November 15, 2019
Hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Kasssim Majaliwa ktk Kongamano la Sanaa Mwali...
Hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Kasssim Majaliwa katika Kongamano la Sanaa #MwalimuNyerereArtsFestival #MatokeochanyA+
Thursday, November 14, 2019
SERIKALI YABORESHA UTOAJI HUDUMA ZA VIVUKO NCHINI
| Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wakala huo kwa kipindi cha miaka minne toka Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani leo tarehe 14/11/2019 jijini Dodoma. Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano maalum ya Watendaji Wakuu wa Taasisi,Wakala na Idara za Serikali inayoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO kuzungumzia mafanikio ya taasisi zao |
Na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma
Serikali imepiga hatua katika utoaji huduma za vivuko kwa asilimia 131 huku huduma za karakana zikizidi kuimarika nchini tangu Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) uanzishwe mwaka 2005.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma.
“Wakala umeendelea kuboresha na kusimamia uendeshaji wa vivuko vya Serikali nchini kwa kuongeza idadi ya vivuko kutoka 13 wakati Wakala unaanzisha mwaka 2005 hadi kufikia 30 katika vituo 19 Tanzania Bara,” alisema Mhandisi Maselle.
Akizungumzia mafanikio iliyopata ndani ya kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mhandisi Maselle amesema kuwa Wakala umefanikiwa kununua vivuko vipya vitatu ambavyo ni MV KAZI kinachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni mkoani Dar es Salaam,kilichogharimu sh bilioni 7.3, MV MWANZA kinachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza kilichogharimu shilingi bilioni 8.9 na MV TANGA kinachotoa huduma kati ya Pangani na Bweni mkoani Tanga ambacho kimegharimu shilingi bilioni 4.02.
Ujenzi wa Vivuko vyote umegharimu jumla ya shilingi bilioni 20.22 ambazo ni fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Ameongeza kuwa pamoja na utoaji wa huduma za vivuko Serikali imenunua boti ndogo tano ambazo ni MV TANGAZO inayotoa huduma ya dharura kati ya Kilambo na Namoto mkoani Mtwara, MV KUCHELE kinachotoa huduma ya dharua kati ya Msangamkuu na Msemo mkoani Mtwara, MV MKONGO kinachotoa huduma kati ya Utete na Mkongo mkoani Pwani, MV BWENI inayotoa huduma dharura kati ya Pangani na Bweni mkoani Tanga pamoja na MV SAR III ambapo ujenzi wa boti zote umegharimu shilingi milioni 415.
Aidha amesema kuwa pamoja na uwepo wa vivuko hivyo TEMESA inaendelea na ujenzi wa vivuko vipya kwa ajili ya maeneo ya Mafia – Nyamisati uaogharimu shilingi bilioni 5.3, Bugorola – Ukara ambao unagharimu kiasi cha shilingi bilioni4.2, Chato – Nkome shilingi bilioni 3.1 na Kayenze – Bezi shilingi bilioni 2.7
Akizungumzia huduma za karakana, Mhandisi Maselle amesema kuwa hadi sasa TEMESA ina karakana 26 katika mikoa yote ya Tanzania Bara na moja iliyopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ambayo imejengwa mahususi kusogeza huduma kwa wateja wa Wilaya za Mlimba, Malinyi na Ifakara ambazo ziko mbali na karakana ya mkoa wa Morogoro.
Amesema kuwa katika kuboresha huduma za karakana Wakala umeanzisha karakana inayotembea ambayo imegharimu shilingi milioni 95 na ambayo itakuwa ikitoa huduma katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Karakakana hii inayotembea pia itahudimia kwa makundi magari ya Bohari ya Dawa (MSD) yapatayo 100, pia itatoa huduma mkoani Pwani katia wilaya za Bagamoyo, Utete, Mkuranga, Kisarawe pamoja na kutoa huduma ya dharura kwa magari ya umma maeneo ya barabara ya Morogoro.
Wakala umefanikiwa kununua vitendea kazi vya karakana vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni 260 ambavyo tayari vimeanza kusambazwa katika karakana 12 zilizopo Katavi, Geita, Songwe, Pwani, Dodoma, Shinyanga, Mwanza, Rukwa, Morogoro, Kahama, Ifakara, Singida na Lindi.
Katika hatua nyingine Mhandisi Maselle amemshukuru Rais Dkt. Jon Pombe Magufuli kwa kutoa fedha zote bilioni 15 zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa vivuko na kusema kuwa hiyo ndiyo dhamira halisi ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Wednesday, November 13, 2019
MATUKIO YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA BUNGENI
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Arusha, Joyce Mukya, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na Mbunge wa Ndada, Sesil Mwambe (chini kushoto) na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Edalardus Kilangi, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni,
kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Novemba 13, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
|
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiakisalimiana na Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Novemba 13, 2019. Katikati ni Mbunge wa Viti Maalum, Hamida Abdallah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
| Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama(chini kushoto) akijadili jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki (juu kushoto) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa(kulia),Bungeni jijini Dodoma, Novemba 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Tuesday, November 12, 2019
WADAU WALIOMBA BUNGE KURIDHIA ITIFAKI YA MITANDAO YA TEHAMA
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amewasilisha Itifaki ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mitandao ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (EAC
Protocol on ICT Networks) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ili
waweze kuipitia na kuridhia kabla ya kuiwasilisha kwenye Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
Baada ya Kamwelwe
kuwasilisha Itifaki hiyo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu
chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Selemani Kakoso, Kamati ilipokea Itifaki
hiyo na kualika wadau wa Sekta ya Mawasiliano ili waweze kufika mbele ya Kamati
hiyo na kutoa maoni yao
Kamwelwe
aliwaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa madhumuni ya Itifaki hiyo ni kuendeleza
uunganishaji wa miundombinu ya TEHAMA mipakani; kuwezesha matumizi ya pamoja ya
miundombinu ya TEHAMA, ikiwa pamoja na masafa na namba; kuwezesha matumizi ya
huduma za mitandao ya TEHAMA bila upendeleo; kuendeleza matumizi ya huduma za
mitandao ya TEHAMA Serikalini na kwenye sekta binafsi ikijumuisha Serikali
Mtandao, Biashara Mtandao, mfumo wa “Geospatial Information System (GIS)” na
utangazaji; kuwianisha sera, sheria na programu za TEHAMA zitakazowezesha
kufikiwa kwa malengo ya itifaki; kutoa elimu bora na mafunzo yanayohitajika kwa
ajili ya uongozi wa kimkakati, usimamizi, utafiti na ujuzi katika eneo la
mitandao ya TEHAMA ndani ya Jumuiya; kuendeleza mashirikiano baina ya sekta ya
umma na binafsi; kuwezesha upatikanaji wa mawasiliano kwa wote hususan
kuunganisha visiwa na nchi zisizopakana na bahari; na kuhakikisha usalama na
ubora wa huduma za mawasiliano na kuwezesha matumizi salama ya mtandao.
Aliongeza
kuwa kwa upande wa Tanzania, nchi yetu imejiimarisha kwa kuweka miundombinu
muhimu ya TEHAMA ambayo ni pamoja na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambao
umejengwa na kufika katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara pamoja na Zanzibar na kufikisha
kwenye maeneo tisa ya mipaka na nchi jirani ikiwemo Kenya, Rwanda, Burundi na
Uganda ambapo kuna watoa huduma za mawasiliano wa nchi hizo wanaotumia Mkongo
wa Taifa. Pia, nchi za Rwanda, Uganda, Zambia na Malawi zinategemea uwepo wa
miundombinu ya TEHAMA ya Tanzania kuwasiliana kimataifa. Vilevile, watoa huduma
wa nchini Kenya wanatumia Mkongo wa Taifa wa Tanzania kupitisha mawasiliano
yake kwenda nchi nyingine. Miundombinu mingine iliyopo ni Kituo cha Taifa cha
Kuhifadhi Data, Vituo sita vya maunganisho ya watoa huduma za intaneti
(Internet Exchange Point – IXPs), miundombinu ya utangazaji pamoja na Mfumo wa
Kuratibu na Kusimamia Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring
System-TTMS).
Pia, Serikali inaendalea kukamilisha Mkakati wa Taifa wa Mtandao
wa Kasi (National Broadband Strategy).
Wakitoa
maoni yao kuhusu Itifaki hiyo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu, wadau mbali mbali wakiwemo Kampuni ya Simu ya Airtel, Shirika la
Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kituo
cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC) wameridhia Itifaki hiyo na kuomba Bunge
kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliridhie na kupitisha Itifaki
hiyo
Meneja
wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Adin Mgendi alisema kuwa, “Itifaki hii
imekuja wakati muafaka, Tanzania imekuwa mdau wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
imejenga miundombinu na kuwezesha nchi za jirani zisizopakana na bahari kupata
mawasiliano. Itifaki hii itatuweka mahali pazuri na tutashirikiana vema, kwa
sasa tunaingia makubaliano baina ya nchi mbili na kupeleka mawasiliano, ila
tukitofautiana hakuna pa kwenda, ila kupitia itifaki hii tutaendelea kufungua
masoko EAC na nchi za SADC ambapo hadi sasa tumeunga Malawi na tunaendelea
Msumbiji,”.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Utekelezaji wa TCRA, Dkt. Phillip Filikunjombe
alisema kuwa Itifaki hii ikipitishwa, nchi wanachama wa EAC tutakuwa na fursa
ya kukaa pamoja na kuja na sheria zinazofanana na zinazoendana na matakwa ya
nchi yetu katika kudhibiti uhalifu mtandaoni
Filikunjombe
alifafanua kuwa Tanzania tumefunga mtambo wa TTMS ambapo Itifaki hii
inazungumzia mifumo ya kudhibiti usalama wa mtandao kwa kuwa Tanzania sio
kisiwa na uhalifu mtandao hauna mipaka, tutahakikisha nchi za wenzetu wanakuwa
na mifumo yenye viwango vinavyohitajika kudhibiti usalama kwa kuwa hawana mfumo
kama TTMS hivyo tutahakikisha nao wanafunga mifumo ya kudhibiti uhalifu wa
mtandao na usalama
Mwakilishi
wa Airtel, Delfina Martin alisema kuwa kampuni yao imeridhia Itifaki hii na
itapunguza gharama za mawasiliano kwa wateja wao wanaowasiliana kutoka nchi
moja kwenda nchi nyingine kwa kuwa hadi sasa Airtel wapo nchi 16 za Afrika na wana makubaliano ya moja
kwa moja ya kutumia miundombinu na huduma za mawasiliano
Baada
ya kupokea maoni ya wadau, Kakoso amesema kuwa Kamati yake imeridhia Itifaki
hiyo na itawasilisha taarifa yake Bungeni na kuunga mkono Serikali kupitia
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ili Itifaki hiyo iweze kuridhiwa kupitishwa
na Bunge
Friday, November 8, 2019
TUENDELEE KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU ULIOPO NCHINI - WAZIRI MKUU MAJALIWA
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza mawaidha, kabla ya Sala ya Ijumaa, kwenye Msikiti wa Nunge, Jijini Dodoma, Novemba 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka
Watanzania waendelee kudumisha amani na utulivu uliopo nchini kwa kuishi kwa
umoja na upendo ili kujiletea maendeleo kuanzia mtu binafsi hadi jamii nzima kwa
ujumla.
Ametoa wito huo leo (Ijumaa, Novemba
08, 2019) wakati akitoa salamu kwa waumini wa dini ya kiislam aliposhiriki sala
ya Ijumaa kwenye msikiti wa Nunge Jijini Dodoma.
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Sala ya Ijumaa, kwenye
Msikiti wa Nunge, Jijini Dodoma, Novemba 8, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
|
“Waislam wenzangu pamoja na jamii
nzima hatuna budi kuendelea kutunza amani iliyopo kwa maombi hasa kuwaombea viongozi
wetu wa kitaifa kuongoza nchi kwa hekima na busara katika kuimarisha umoja na
upendo uliopo nchini.”
Waziri Mkuu alieleza kuwa, ni
muhimu kutambua mchango wa dini katika Taifa kwa kuzingatia kuwa ndicho chombo
chenye nguvu kuleta misingi mema kupitia mawaidha na mafundisho yanatolewa kwa makundi
yote hususan kundi la vijana ambalo linategemewa katika nguvu kazi ya Taifa.
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Alhaji, Ismail Dawood, baada ya Sala ya Ijumaa, kwenye Msikiti wa Nunge, Jijini Dodoma, Novemba 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Aliongezea kuwa, dini zina mchango
mkubwa katika kuimarisha uwepo wa amani ambayo inatoa fursa kwa jamii kushiriki
vema kwenye shughuli za uzalishaji mali za kila siku, hivyo jamii haina budi
kuzingatia yale wanayofundishwa katika dini zao ili kudumisha umoja, mshikamano
na upendo.
“Tuendelee kuungana pamoja bila
kujali tofauti za imani zetu na hii itasaidia kuwa na maendeleo endelevu na
kuendelea kuwaombea viongozi wote nchini wawe na afya njema.”
Aidha pamoja na hayo aliliasa
kundi la vijana ambalo ni nguvu kazi ya Taifa liendelee kutumia nafasi zao
katika kujishughulisha kwa bidii katika kazi za uzalishaji na kuondokana na
makundi yasiyofaa.
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia mkono wananchi, wakati akitoka kwenye Msikiti wa Nunge, Jijini Dodoma, Novemba 8, 2019, baada ya kushiriki sala ya ijumaa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Kwa
upande wake, Mtoa mawaidha katika ibada hiyo Ustadh Omari alimshukuru
Mhe.Waziri Mkuu na akatumia nafasi hiyo kuwakumbusha Watanzania waendelee
kufanya kazi kwa bidii na jitihada ili kuondokana na magenge ya mitaani
yanayoshiriki katika mambo maovu ikiwemo uhalifu unaohatarisha amani na
utulivu.
“Vijana lazima mfanye kazi kwa
bidii na kuendelea kumtumikia Mungu anayewapa uhai bila kusahau ibada na hii
itasaidia kuondokana na makundi ya machokoraa ambao tunaamini wangejifunza
masuala ya elimu ya Mungu ingewasaidia na kuwa na Taifa lenye viongozi wazuri
wa kesho” alisisitiza Ustadhi Salim.
Waziri Mkuu alisema anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume (S.A.W) kwa niaba
ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli zitakazofanyika
Kitaifa Mkoani Mwanza tarehe 09 Novemba, 2019.
Aidha kwa mkoa wa Dodoma
wanatarajia kuadhimisha kwa kuwa na maandamano yatakayoanzia katika viwanja vya
Nyerere Squere hadi msikiti wa Mkuu wa Gadaff.
HUWEZI KUWA HURU KAMA HUWEZI KUJITENGEMEA KIUCHUMI - RAIS MAGUFULI
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. Afrika haitaweza kupiga hatua endapo itaendelea kuwa muuzaji wa bidhaa ghafi na muagizaji wa bidhaa za viwandani. Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joseph Magufuli wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi za Afrika na Nordic unaofanyika jijini Dar es Salaam. |
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
![]() |
| Waziri wa mambo ya nje wa Norway Ine Marie Eriksen Sereide akizungumza katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
Rais
Magufuli amesema kuwa kwa sasa, asilimia 60 ya mauzo ya nje kutoka nchi
za Afrika ni mazao ghafi hivyo ni lazima Waafrika tufike hatua ambapo
tutaweza kusindika na kuongeza thamani ya mazao yetu, ikiwemo mazao ya
kilimo, madini, uvuvi, nk.
“Tunataka tusindike pamba na kutengeneza nguo hapa Afrika; tunataka tuchimbe madini na kuyachenjua hapa hapa Afrika; tunataka tuvue samaki na kuwasindika hapa hapa Afrika. Africa must produce, process, consume and export finished products,” amesema.
“Tunataka tusindike pamba na kutengeneza nguo hapa Afrika; tunataka tuchimbe madini na kuyachenjua hapa hapa Afrika; tunataka tuvue samaki na kuwasindika hapa hapa Afrika. Africa must produce, process, consume and export finished products,” amesema.
![]() |
| Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
![]() |
| Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
![]() |
| Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
![]() |
| Baadhi ya Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
![]() |
| Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa Kwanza kukulia) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba (wa Pili toka kulia) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es Salaam. |
![]() |
| Baadhi ya Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. Ameongeza kuwa Viwanda ni moja ya vipaumbele vyetu vikubwa, na washirika wetu wa maendeleo pamoja na wawekezaji wengine makini watuunge mkono kwenye mwelekeo huo. Amesema hivyo basi, kwa kuwa marafiki zetu wa nchi za Nordic wamepiga hatua kiteknolojia, hususan teknolojia ya viwanda, tushirikiane kujenga viwanda vya kusindika na kuongeza thamani ya mazao yetu kwa manufaa ya pande zetu mbili. Vile vile ameosema ili kuweza ili kuvutia biashara na uwekezaji katika sekta mbalimbali, ni muhimu kwa nchi za Afrika kuweka mazingira muafaka, ikiwemo miundombinu wezeshi pamoja na kuondoa urasimu kwenye sheria na taratibu zetu za biashara na uwekezaji. |
![]() |
| Washiriki katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. Amesema mpaka sasa Tanzania imefanikiwa kupitia na kurekebisha sheria na taratibu mbalimbali za uwekezaji nchini, ikiwa ni pamoja na kutengeneza sheria za kuwalinda wawekezaji. “Tumeanzisha Wizara mahsusi yenye dhamana ya Uwekezaji chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ili ijihusishe moja kwa moja na kurahisisha mazingira na uratibu wa uwekezaji nchini,” amesema. Lakini muhimu zaidi, tunatekeleza Mkakati wa Kurekebisha na Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini, yaani The Blueprint for Regulatory Reforms to Improve Business Environment. Jitihada zingine ni kutenga kanda maalum kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na kanda maalumu za uwekezaji, yaani Export Processing Zones and Special Economic Zones. |
![]() |
| Balozi wa China nchi Wang Ke akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumaro katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
![]() |
| Waziri wa mambo ya nje wa Norway Ine Marie Eriksen Sereide akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. George Simbachawene katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
![]() |
| Washiriki katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. Sambamba na hayo, Tanzania kutambua umuhimu wa miundombinu wezeshi kama kichocheo cha biashara na uwekezaji, hivi sasa, inajenga na kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, ikiwemo barabara, reli, usafiri wa majini na anga. Amesema hivi sasa wanajenga Reli ya Kisasa, yaani Standard Gauge Railway kwenye Ushoroba wa Kati yenye urefu wa kilomita 1,800 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, ambayo baadaye itaunganisha na nchi jirani za Rwanda na Burundi. Ameongeza kuwa ili kuvutia wawekezaji wameza kulifufua Shirika letu la Ndege la ATCL na kuboresha viwanja vyetu vya ndege na kusimika rada za kuongozea ndege. Tunapanua na kuboresha bandari zetu za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga pamoja zilizopo kwenye Maziwa yetu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. |
![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda akisalimiana na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Josephat Gwajima katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
![]() |
| Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kuifungua Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic
unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. Na upanuzi huu umeenda sambamba na ujenzi wa meli na vivuko. Zaidi ya hapo, tutakeleza Mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme wa maji kwenye Bonde la Rufiji utakaozalisha Megawati 2,115, na kuchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa viwandani na kwenye sekta nyingine. Amemalizia kwa kuzikaribisha nchi za Nordic, pamoja na mataifa mengine, yakiwemo ya Afrika, kuja kuwekeza nchini Tanzania ambapo kuna mazingira wezeshi ya uwekezaji ni muafaka na yanatabirika, kutokana na amani na utulivu wa kisiasa, lakini pia mwenendo wa ukuaji wa uchumi ni mzuri ambapo, kwa sasa, ni wastani wa asilimia 7. Zaidi ya hapo, Tanzania ni wanachama wa SADC na EAC, ambazo kwa pamoja zina idadi ya watu wapatao milioni 450. |
Thursday, November 7, 2019
Uchumi wa Bahari ni moja ya Utajiri wa Tanzania ambao haujaguswa
#AfricanNordic2019
الشراكة من أجل التنمية المستدام
Partnering for Sustainable Development.
Partenariat pour une développement durable
English: Welcome to Tanzania
Arabic : "مرحبا بكم في تنزانيا"
French: Soyez les bienvenue à Tanzanie
Wednesday, November 6, 2019
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA KAKA YAKE MZEE BAKARI MAJALIWA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,
Jenerali, Venance Mabeyo (kushoto), Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi, Simon Siro (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa, Diwani Athumani (kulia) baada ya wote kushiriki katika
mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika
katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akishirika katika sala ya kumwombea marehemu kaka
yake, Mzee Bakari Majaliwa iliyofanyika katika kijiji cha Nandagala
wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la kaka yake, Mzee
Bakari Majaliwa katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nandagala
wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika sala ya kumwombea marehemu
kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa iliyofanyika nyumbani kwa marehemu
katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.

Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewashukuru watu wote waliojitokeza katika
mazishi ya kaka yake Mzee Bakari Majaliwa (78), aliyefariki juzi
(Jumatatu, Novemba 04, 2019) nyumbani kwake katika kijiji cha Chimbila
‘B’wilayani Ruangwa, Lindi.
Ametoa
shukrani hizo leo (Jumatano, Novemba 06, 2019) wakati wa ibada ya
mazishi iliyofanyika kijijini Nandagala wilayani Ruangwa na amesema
kwamba hayo ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kila mtu atapita kwenye njia
hiyo.
“Tulikuwa
12 na sasa tumebaki watano, wanaume wawili na wanawake watatu. Msiba
huu kwetu ni mkubwa umepunguza idadi ya watoto wa Mzee Majaliwa lakini
hatuna namna ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu, wajibu wetu ni kuendelea
kumuombea. Nawashukuru wote mlioacha shughuli zenu na kutukimbilia,
familia imethamini sana ujio wenu jambao hili limetokea ghafla.”

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi, Simon Siro katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari
Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa,
Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa, Diwani Athumani katika mazishi ya kaka yake Waziri
Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala
wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,
Jenerali Venance Mabeyo katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee
Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani
Ruangwa, Novemba 6, 2019. Wa pili kulia ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi, Simon Siro.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu pia amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa salamu za pole
alizozitoa. “Jambo hili pia limemgusa Mheshimiwa Rais wetu ambaye
ametutaka tuwe watulivu katika kipindi hiki kigumu na kwamba kila mmoja
kwa dhehebu lake aendelee kumuombea marehemu ili Mwenyezi Mungu amlaze
mahala pema.”

Kwa
upande wake, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Generali, Venance
Mabeyo akitoa salamu za pole kwa niaba ya Maafisa na Askari wa Vyombo
vyote vya Ulinzi na Usalama amesema anajua uzito wa msiba pamoja na
majonzi waliyonayo kwa kuondokewa na mpendwa wao na kwamba wamshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kuwa ndiye anayetoa na anayetwaa. “Hakuna namna ya
kurekebisha maamuzi ya Mwenyezi Mungu, tuendelee kumsindikiza kaka yetu
kwa sala Mwenyezi Mungu ampokee kwa amani.”
Naye,
Mwakilishi wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Othman Kaporo
amesema amewataka wananchi wajiandae na kifo kwa kufanya ibada. “Ni
kawaida kwa binadamu kujisahau lakini Mwenyezi Mungu ametuwekea vitu vya
kutukumbusha juu ya uwepo wake ikiwemo kifo, hivyo tuyatekeleze yale
yalikuwa ya wajibu kuyatekeleza.”
Subscribe to:
Posts (Atom)
















