Matokeo chanyA+ online




Thursday, February 11, 2021

NAIBU WAZIRI KATAMBI AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI WCF


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Patrobas Katambi amezindua Baraza la Wafanyakazi Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na kutoa wito kwa wafanyakazi kuchapa kazi kwa bidii kwani ndio nguzo kuu katika mafanikio ya Mfuko.

Mhe. Katambi ameyasema hayo mjini Morogoro  Februari 10, 2021 wakati akizindua baraza la Wafanyakazi WCF kwenye ukumbi wa Magadu.

“Lazima tujue uwajibikaji ni nguzo kuu ya mafanikio katika sehemu yoyote ya kazi, hivyo wajumbe mnaowawakilisha wafanyakazi wa Mfuko mnapaswa kuwahimiza wenzenu kuhusu  swala hilo.” Alifafanua  Mhe. Katambi.

Alisema Serikali inatambua mchango wa wafanyakazi wote nchini lakini vile vile inatambua sana  na kuheshimu mchango wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi katika kukuza uchumi wa nchi yetu kwa kuhakikisha kuwa nguvu kazi ya wafanyakazi wanaougua au kuumia kutokana na kazi haipotei kwa wakati wote kupitia huduma ya matibabu inayotolewa kwa waathirika.

“Napenda niwahakikishie kuwa Serikali ya awamu ya tano inaendelea kushirikiana na Mfuko katika kuhakikisha unanufaisha watu walio wengi na kufanikisha malengo ya kuanzishwa kwake.”

Naibu Waziri Katambi pia aliupongeza Mfuko huo kwakuwa na wafanyakazi wachache lakini waliouwezesha Mfuko kupiga hatua kubwa katika utekelzaji wa majukumu yake.

“Mnatupa heshima kubwa sana Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri mama Jenista Mhagama, tangu mmeanza kutekeleza majukumu haya mmeanzia ziro baada ya mwaka mmoja mkalipa shilingi bilioni 1.5 na bado mnaendelea kufanya vizuri kwakweli habari hizi zilifurahisha na hata kamati ya bunge ilishukuru na kuwapongeza hongereni sana sana.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Katambi.

Alisema hata baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge wametoa ushuhuda jinsi Mfuko huo umekuwa ukihudumia vema katika suala la fidia na HUDUMA za utengamao (rehabilitation aervices).

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba alisema katika kipindi cha miaka sita ya uhai wa Mfuko kumekuwepo na mafanikio kadhaa chini ya nguvu kazi ya wafanyakazi 129 ambao wameweza kutekelza vema majukumu yao

“Sambamba na hilo tumekuwa tukiwapatia mafunzo ya mara kwa mara ili kuongeza weledi katika utendaji wa kazi.” Alifafanua Bw. Mshomba.

Bw. Mashomba pia alisema miongoni mwa maeneo ambayo Mfuko umeboresha sana HUDUMA zake  ni kuweka mfumo wa utoaji taarifa kwa njia ya mtandao.

“Huduma zetu hivi sasa zinatolewa kwa kiasi kikubwa sana kwa njia ya mtandao karibu asilimia 85 ya shughuli zetu, kujisajili, kuwasilisha michango, uchatakati wa malipo lakini pia muhimu zaidi ni kutoa taarifa pale mfanyakazi anapougua au kupata ajali ya kikazi na hata inapotokea bahati mbaya akafariki kutokana na kazi tumeweka mfumo mzuri unaowezesha taarifa hizo kutufikia kwa haraka kupitia mtandao.” Alifafanua Bw. Mshomba.

Alisema Mfuko unatambua kuwa nchi ni kubwa na sio sehemu zote mtandao unapatikana kwa urahisi hivyo Mfuko umefungua ofisi za kikanda, kuna ofisi Makao makuu ya Serikali Dodoma, Mbeya, Arusha, Morogoro, Mtwara na mwisho wa mwaka huu wa fedha Mfuko utafungua ofisi kwenye mikoa ya Tabora, Geita na Shinyanga hususan maeneo ya migodi kama Kahama.

“Ukiacha hayo Mfuko wetu kifedha tumejenga uwezo wa kutosha kwa mujibu wa hesabu zilizokaguliwa na CAG tarehe 30/06/2020 tulikuwa na ukubwa wa thamani (Assets) wa Bilioni 333, lakini pia hesabu ambazo hazijakaguliwa na CAG hadi Desemba 2020 tumefikia bilioni 389.” Alifafanua Mkurugenzi Mkuu Mshomba.

Lakini pia Mfuko umeboresha sana huduma za tathmini kwa kutoa mafunzo kwa madaktari wapatao 1,085 ambao ndio wanaofanya kazi ya kutathmini pale mfanyakazi anapougua au kuumia kutokana na kazi.

Naye Katibu Mkuu wa  chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Heri Mkunda alisema Mafanikio yaliyopatikana WCF ni kutokana na wafanyakazi kufanya kazi kwa kujituma kushauri vizuri uongozi na kushirikishwa katika masuala mbalimbali yanayohusu taaisi.

“Niipongeze Menejimenti na kuwaomba waajiri wengine kujifunza kutoka WCF, hawa wafanyakazi ndio walio jikoni wanaweza kushauri vizuri kuhusu masuala mbalimbali inayohusu taasisi ili kufikia malengo.”

Awali kabla ya uzinduzi wa baraza hilo, wajumbe walifanya uchaguzi wa kuchagua Katibu wa Baraza na Katibu Msaidizi, ambapo Bw.Mbarikiwa Masinga alichaguliwa kuwa Katibu wa Baraza na Bi.Irine Mngure alichaguliwa kama Katibu Msaidizi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Patrobas Katambi (kulia) akipeana mikono na MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa WAFANYAKAZI (WCF) Bw. Masha Mshomba Mara baada ya kuzindua Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko huo mjini Morogoro Februari 10, 2021. Anayeshuhudia ni Karibu Mkuu wa TUGHE Bw. Heri Mkunda
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Patrobas Katambi, akitoa hotuba ya uzinduzi. Kulia ni MKURUGENZI Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Patrobas Katambi, akitoa hotuba ya uzinduzi.

Baadhi ya wajumbe wa baraza la Wafanyakazi WCF wakishangilia kwa kupiga makofi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba (wapili kulia) akimkabidhi Katibu wa Baraza Hilo Bw.Mbarikiwa Masinga Mkataba Kati ya Baraza na Menejimenti huku Katibu Msaidizi Bi. Irine Mngure akishuhudia.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Patrobas Katambi, (katikati) na Karibu wa Baraza la Wafanyakazi WCF, Bw. Mbarikiwa Masinga wakimsikiliza MKURUGENZI Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba wakati akitoa hotuba take.
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Baadhi ya wajumbe wa baraza Hilo wakifuatilia kikao
Bw. Julius Lwenje akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mhe. Katambi (kulia) na Bw. Mshomba wakiimba wimba was solidarity forever
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya WCF.

Picha ya pamoja ya wajumbe na mgeni rasmi

Wednesday, February 10, 2021

CHIKOTA ASHAURI MAMBO MATATU KATIKA KILIMO CHA KOROSHO

Mbunge wa Nanyamba Abdallah Chikota ameishauri serikali kuzingatia mambo matatu katika kuendeleza kilimo cha Korosho ikiwemo kuondoa tozo na kodi zilizopo wakati wa uingizaji wa mashine za kubangua korosho ili mashine nyingi ziweze kuingizwa nchini.

Aidha ameshauri kuwekwa kwa vivutio maalum kwa wawekezaji wapya na kuondolewa kwa kodi na tozo katika vifungashio.

Akichangia mpango wa kitaifa wa maendeleo wa mwaka 2021/2022 na mpango wa tatu wa maendeleo wa miaka mitano 2021/2022 hadi 2025/2026 februari 10 jijini Dodoma,Chikota amesema ushauri huo ukizingatiwa itapunguza gharama na hivyo kupata wawekezaji wengi wan je na ndani.

“Suala la ubanguaji ndio njia pekee ya kuhakikisha korosho inapata bei nzuri kwenye soko la dunia na korosho yetu ni mkakati ambao tulianza nao huko nyuma,lengo ni kuweka Oxport levy ili wasafirishe korosho ghafi,”amesema.

Amesema uwezo wa kubangua korosho katika viwanda vyetu ni kama tani 70,000 na sasa hivi wanazalisha kama tani 120,000 na korosho nyingi inauzwa ikiwa ghafi.

“Mheshimiwa Mwenyekiti mimi nashauri tukose fedha kidogo leo ili tupate fedha nyingi baadae hii itawezekana kama tutaondoa tozo na kodi zilizopo wakati wa uingizaji wa mashine za kubangua korosho ili mashine nyingi ziweze kuingizwa,”aliongeza.

Amesema kiwanda kidogo cha ubanguaji mtaji wake ni kama milioni 60 na kwa sababu Korosho inalimwa katika mikoa zaidi ya 12 hivyo badala ya kutoa zile fedha za mfuko wa vijana kwa kijana mmoja mmoja wanaweza kuanzisha viwanda vidogo vya kubangua korosho na vikaongeza ajira pia kwa wanawake na thamani ya fedha itaonekana.

Ameongeza kuwa “Wenzetu  wa Vietnam na India wanatumia sana Korosho zetu  kuongeza ajira kwao na mipango hii wakiisikia watakuwa na hofu na korosho ghafi haitaenda kwao,sasa tuwekeze katika ubanguaji ili tuongoze ajira,

Akizungumzia kuhusu mradi wa Mchuchuma na Liganga amesema wakati umefika wa kuweka fedha za kutosha sambamba na ujenzi wa reli kutoka Mtwara Mbababay ili kuweza kupata fedha za kutosha kuwekeza kwenye reli ya kusini na hivyo kuwezesha bandari ya Mtwara kutumika ipasavyo kusafirisha tumbaku na kuwezesha nchi nyingine ya Malawi Zambia na DRC Congo kutumia reli hiyo.

WANUFAIKA 50 WA MKURABITA WAKABIDHIWA HATIMILIKI WELEZO ZANZIBAR, WAPIGWA MSASA



Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Utendaji ya Mkurabita, Immaculata Senje (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanufaika wa Mkurabita waliokabidhiwa Hatimiliki za kumiliki ardhi Shehia ya Welezo, Wilaya ya Magharibi A, Unguja Zanzibar Februari 9,2021. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Utendaji ya Mkurabita, Immaculata Senje  (kushoto), akimkabidhi hatimiliki Said Mbarouk Rajab.
Senje akimkabidhi hatimiliki Ghashima  Juma Salum
Senje akimkabidhi hatimiliki Sheha wa Shehia ya Welezo, Mohamed Amour Khamis 
Moja ya mfano wa hatimiliki walizokabidhiwa wakaazi wa Shehia ya Welezo.

Wakaazi wa Shehia ya Welezo wakikabidhiwa hatimiliki za kumiliki Ardhi


Afisa Sheria  Benki ya Watu Zanzibar (PBZ),  Ali Alhaj Masoud akihamasisha wanufaika wa Mkurabita waliokabidhiwa hatimiliki za ardhi katika Shehia ya Welezo kuzitumia hati hizo kwenye benki hiyo kuomba mikopo .
 Afisa Mahusiano wa  Amana Bank Tawi la Zanzibar,  Anuar  Rashid Said akitoa mafunzo jinsi ya kuzitumia  hati hizo kukopa benki kwa masharti nafuu.
 Msimamizi wa Mikopo wa Amana Bank Zanzibar, Abdalah Mtunguja akitoa ufafanuzi wa masharti ya benki baada ya mmoja wa wakaazi wa Welezo aliyekabidhiwa hatimiliki.
Sehemu ya wakaazi wa Shehia ya Welezo wakiwa katika mkutano huo.
 Afisa Ushirika wa Wilaya ya Magharibi A, Hassan Ali Mbarouk akielezea jinsi ofisi yake inavyosaidia wakaazi kusajiri ardhi na mali zao zingine kupata hatimiliki. 
Mrajis wa Ardhi Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Abdul Nasser Hikimany akielezea umuhimu na faida za hatimiliki walizokabidhiwa.
Afisa Mrasimishaji  (Mtambuzi)  wa Ardhi Unguja, Shawana  Said Khamis akielezea utaratibu wa kupata haimiliki hizo.
Mratibu wa Mkurabita,  Dkt. Serphia Mgembe akitoa neno la utangulizi wakati wa shughuli ya kukabidhi hatimiliki.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Utendaji ya Mkurabita, Immaculata Senje akizungumza wakati wa kukabidhi hatimiliki ambapo aliwaasa kuzitumia kukopa fedha benki badala ya kuzifungia kabatini.


Wanufaika wakiwa na furaha baada ya kukabidhiwa hatimliki hizo.

Na Richard Mwaikenda, Zanzibar

Wanufaika 50 wa Mpango wa Kurasimisha Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), wamekabidhiwa Hati za Hakimiliki  katika Shehia ya Welezo, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.

Hati hizo zinazoandaliwa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar, zimekabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Utendaji ya Mkurabita, Immaculata Senje katika hafla iliyofanyika leo Februari 9,2021 shehia ya Welezo, wilaya ya Magharibi A.

Kabla ya kukabidhiwa  hati hizo, wanufaika walipata mafunzo ya jinsi ya kuzitumia hati hizo  kama dhamana kukopa fedha Benki na taasisi zingine za fedha kwa ajili ya kuinua biashara zao hivyo kunufaika kimaisha.

Wananchi hao walipigwa  msasa na maofisa wa  baadhi ya benki na maafisa wa serikali kwa kuwaeleza kuwa hati hizo zina thamani kubwa  hivyo wazitunze vizuri na kuzitumia kukopa kwenye benki zao badala ya kuzifungia  kabatini.

Maofisa waliotoa mafunzo ni Afisa Sheria  Benki ya Watu Zanzibar (PBZ),  Ali Alhaj Masoud, Afisa Mahusiano wa  Amana Bank Tawi la Zanzibar,  Anuar  Rashid Said,  Msimamizi wa Mikopo wa Amana Bank Zanzibar, Abdalah Mtunguja na Afisa Ushirika wa Wilaya ya Magharibi A, Hassan Ali Mbarouk.

Awali kabla ya kukabidhi vyeti, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita, Immaculata Senje amesema kuwa katika moja ya hotuba za Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi alitaja moja ya vipaumbele vyake katika uongozi wake kuwa ni  urasimishaji wa ardhi itakayopelekea kupunguza migogoro ya ardhi, hivyo wananchi wanatakiwa kumsaidia Rais kwa kujitokeza kwa wingi kurasimisha ardhi zao.

Amesema ardhi inayorasimishwa inatoka kwenye mtaji mfu kuwa mtaji hai, hivyo  hati walizokabidhiwa wazitumie kukopea fedha benki zitakazowasaidia , kujikwamua kimaisha.

"Jambo tulilozindua leo si jambo dogo ni jambo kubwa na tungetamani lienee katika kila eneo, na utaratibu  huu tuliofanya leo wa kutoa elimu ya utoaji hati tutaendelea nao,kila  mahali tutakapozitoa mara tutaendelea kuwapa faida ya hati hizo. ili ifikie lengo la mkurabita la wananchi kujikwamua kiuchumi, kuondokana na hali ya umasikini kuingia kwenye uchumi mzuri," amesema Senje.

Ametoa wito kwa wananchi wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono Rais  kumalizana na migogoro ya ardhi,kupandisha thamani ya ardhi, inakuwa tofauti na ilivyokuwa awali kabla ya kupimwa na kuwataka waliopata hati wawe walimu kwa wengine.

Mratibu wa Mkurabita, Dkt. Seraphia Mgembe aliwapongeza maafisa wa benki waliotoa mafunzo lakini vilevile aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika hafla hiyo.

"Kila mmoja ajipange vizuri apange kuwa atafanya jambo lake la kufanya kwa kutumia hati hizo kukopea fedha benki na kwamba fursa waliyoipata waitumie kwa ukamilifu," amesema Dkt Mgembe.

Aliziomba benki zitakazofaidika kwa wanufaika wa Mkurabita waliopata hatimiliki kukopa kwao zisaidie kutoa msaada wa kifedha wa kukamilisha mchakato wa kuwapatia hati wananchi katika maeneo ambayo hawajapata bado.

Tuesday, February 9, 2021

KATIBU MKUU KADIO AFUNGUA KIKAO CHA KUPITIA, KUJADILI NA KUPITISHA KATIBA YA MFUKO WA FARAJA WATUMISHI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI (FUNGU 51)

 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (Aliyesimama) akifungua Kikao cha kupitia, kujadili na kupitisha Katiba ya Mfuko wa Faraja wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Fungu 51). Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mkutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Emmanuel Kayuni (Wakwanza kulia) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (Katikati) pamoja na Watumishi wa
Wizara hiyo (Hawapo pichani) katika Kikao cha kupitia, kujadili na kupitisha Katiba ya Mfuko wa Faraja wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Fungu
51). Wakwanza kushoto ni Mjumbe wa TUGHE Tawi la Wizara hiyo, Bi. Sabina Ntonda, ambaye amewakilisha Uongozi wa chama hicho. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jijini Dodoma leo.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (Wakwanza aliyevaa miwani) akiwasili katika Ukumbi wa Mkutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambapo alifungua Kikao cha kupitia, kujadili na kupitisha Katiba ya Mfuko wa Faraja wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Fungu 51). Kikao hicho kimefanyika Jijini Dodoma leo Februari 08, 2021.

Mkaguzi wa Zimamoto, Rehema Menda (Aliyesimama) akifafanua jambo kuhusiana na Mfuko wa Faraja wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (Hayupo pichani), baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo na Watumishi waliohudhuria Kikao cha kupitia, kujadili na kupitisha Katiba ya Mfuko wa Faraja wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Fungu 51).

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Christopher kadio (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na Watumishi hao katika Kikao cha kupitia, kujadili na kupitisha Katiba ya Mfuko wa Faraja wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Fungu 51). Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dodoma Februari 08, 2021.

Monday, February 8, 2021

SERIKALI KUTUMIA ZAIDI YA SH. MILIONI 100 KUIMARISHA KITUO CHA KUTOTOLESHA VIFARANGA VYA SAMAKI CHA RUHILA


Afisa Mfawidhi, Kituo cha kutotolesha Vifaranga vya Samaki cha Ruhila, Emmanuel Maneno (wa kwanza kushoto) akimueleza jambo Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati) alipotembelea Kituo hicho kilichopo Mkoani Ruvuma jana.  Wa kwanza Kulia ni Mkurugenzi, Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji WMUV), Dkt. Nazael Madalla.
  1. Mkurugenzi, Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji (WMUV), Dkt. Nazael Madalla (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa tatu kutoka kushoto) alipotembelea Kituo cha kutotolesha Vifaranga vya Samaki cha Ruhila kilichopo Mkoani Ruvuma jana.
  1. Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akinawa maji ya Ziwa Nyasa alipotembelea Kituo cha Udhibiti wa Rasilimali za Uvuvi Ziwa Nyasa kilichopo Mbamba Bay, Wilayani Nyasa, Mkoani Ruvuma jana. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi, Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji (WMUV), Dkt. Nazael Madalla.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa tatu kutoka kulia - aliyevaa koti) akieleza jambo wakati akiangalia moja ya Mabwawa ya kufugia Samaki alipotembelea Kituo cha Kutotolesha Vifanga vya Samaki cha Ruhila kilichopo Mkoani Ruvuma jana. Wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi, Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji (WMUV), Dkt. Nazae.

Na Mbaraka Kambona, Ruvuma

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah amesema kuwa Serikali imepanga kutumia Shilingi Milioni 110 kwa ajili ya kuimarisha miundo mbinu ya Kituo cha Kutotolesha Vifaranga vya Samaki cha Ruhila ili kiweze kuzalisha vifaranga vitakavyokidhi mahitaji yaliyopo sasa. 

Dkt. Tamatamah aliyasema hayo alipotembelea kukagua shughuli zinazofanywa na kituo hicho kilichopo Mkoani Ruvuma jana. 

Alisema kuwa kwa mwaka huu wa fedha 2020/2021 Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepanga kuzalisha vifaranga Milioni 22, na kati ya hivyo, vifaranga Milioni 16 vitazalishwa na vituo vya kutotolesha vya watu binafsi na vifaranga Milioni 6 vitazalishwa na vituo vya Serikali. 

Dkt. Tamatamah aliongeza kuwa hivi karibuni Wizara itatangaza zabuni kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha kituo hicho ili kiweze kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuzalisha vifaranga utakaowezesha kukidhi mahitaji yaliyopo sasa. 

“Baada ya kukiimarisha kituo hiki mwaka huu, mwaka ujao wa fedha tutafanya ukarabati mkubwa na ukarabati huo ukikamilika tunatarajia uwezo wa uzalishaji wa kituo hiki kuongezeka mara tatu zaidi ya sasa na hivyo kutaongeza uhakika wa upatikanaji wa vifaranga vya samaki,’’alisema Dkt. Tamatamah. 

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Nazael Madalla alitoa rai kwa Watanzania hasa wale wanaoishi mbali na vyanzo vikubwa vya maji kama maziwa kujihusisha na shughuli za ufugaji wa samaki kwani kwa kufanya hivyo kutawasaidia kupata kipato na lishe bora. 

“Naomba Watanzania watembelee kituo hiki ili waweze kujifunza kwa vitendo namna ya kuchimba mabwawa makubwa na kufugaji samaki ili kujiongezea kipato na lishe bora kwa ajili yao na Watoto wao,” alisema Dkt. Madalla. 

Kaimu Katibu Tawala anayeshughulikia Uchumi na Uzalishaji, Mkoani Ruvuma Deogratius Sibula alisema kuwa Ruhila kimekuwa kituo muhimu sana kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa sababu wafugaji wengi wanategemea kituo hicho kupata vifaranga vya samaki kwa ajili ya kufuga. 

“Katika Mkoa wa Ruvuma kuna Wafugaji wa Samaki takriban Elfu nne (4000) na kuna mabwawa ya Samaki zaidi ya Elfu Sita (6000) na wote wamekuwa wakitegemea kituo hiki kwa ajili ya kupata mbegu na kupata elimu ya ugani, hivyo ni kituo muhimu sana katika kuchagiza ongezeko la ufugaji wa samaki na upatikanaji wa lishe bora kwa Wananchi,” alisema Sibula. 

Naye, Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Ruhila, Emmanuel Maneno alisema kuwa baadhi ya Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inakabiliwa na Utapiamlo hivyo fursa ya uhakika ya kuondokana na tatizo hilo ni kufuga samaki ambao watawahakikishia kupata lishe bora na kipato cha kujikimu kimaisha. 

Maneno aliongeza kuwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ina mazingira mazuri ya kufuga samaki kwa sababu hali ya hewa ni nzuri, maji yapo ya kutosha lakini pia malighafi kwa ajili ya kutengenezea chakula cha samaki inapatikana kwa urahisi na hivyo kufanya gaharama za ufugaji wa samaki kuwa chini.

UWANGUTA KUFIKISHA KILIO KWA WAZIRI WA NISHATI KWA KUTOLIPWA FEDHA ZA NGUZO KWA WAKATI


Mwenyekiti wa UWANGUTA Negro Sanga akiongea kwenye kikao cha kujadili safari ya kwenda kumuona waziri wa nishati kuelezea changamoto ya malipo kutoka katika kapuni ambazo hununua nguzo ambazo hazijawekwa dawa.
Baadhi ya wafabishara wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa wakiwa kwenye kikao cha kujadili safari ya kwenda kumuona waziri wa nishati kuelezea changamoto ya malipo kutoka katika kapuni ambazo hununua nguzo ambazo hazijawekwa dawa.
Baadhi ya wafabishara wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa wakiwa kwenye kikao cha kujadili safari ya kwenda kumuona waziri wa nishati kuelezea changamoto ya malipo kutoka katika kapuni ambazo hununua nguzo ambazo hazijawekwa dawa.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Chama cha wafanyabiashara wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa (UWANGUTA) wamepanga kupeleka kilio kwa waziri wa nishati kwa kutolipwa kwa wakati kutoka kwenye viwanda na makapuni ambayo yamekuwa yakinunua nguzo hizo kutoka kwa wafanyabiasha hao.

Akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabishara hao,mwenyekiti wa UWANGUTA Negro Sanga alisema kuwa makampuni ambayo yamekuwa yakinunua nguzo hizo yamekuwa yakiwacheleweshea malipo wafanyabisha hao na kuwa pelekea kupata hasara mara kwa mara.

 

Alisema wafanyabishara hao wanakutana na changamoto ya mitaji kutokana na kutegemea kukopa kwenye benki mbalimbali ili kuendesha biashara ya nguzo hivyo kucheleshwa kwa malipo kutoka kwenye kampuni hizo kunawasababishia kulimbikiza au kukua kwa riba katika benki ambazo wanakuwa wamekopa fedha hizo.

Sanga aliongeza kwa kusema kuwa lengo la kwenda kumuona waziri wa nishati Dr Medard Matogolo Kalemani ni kufikisha kilio cha kutolipwa kwa wakati kutoka kwenye kampuni ambazo wamekuwa wakiziuzia nguzo hizo tofauti na alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli alipokuwa kwenye ziara mkoani Iringa.

“Mheshimiwa Rais alitoa wiki mbili kuhakikisha kuwa sisi wafanyabisha wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa tuliambiwa tulipwe baada ya wiki mbilia ila hadi sasa bvaadhi yetu wamelipwa na wengine hadi hizi sasa tunavyoongea Zaidi ya wafabiashara mia moja (100) hawajalipwa fedha zao” alisema Sanga

Sanga alimalizia kwa kusema kuwa wameamua kwenda kwa waziri baada ya kufanya kila jitihada kushindikana kutatua changamoto hiyo ya kulipwa kwa wakati kama iliyokuwa miaka ya nyuma hivyo kwa pamoja wameamua kufunga safari kwa kwenda kutoa malalamiko kwa waziri wa nishati.

Nao baadhi ya wafanyabisha wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa waliomba serikali kuzitambua kampuni zote na viwanda ambavyo vinanua nguzo hizo kutoka kwa wafanyabisha hao ili kuondoa ubabaishaji kutoka kwenye kampuni hizo.

Walisema kuwa kampuni nyingi mara kwa mara husema kuwa hawajalipwa kutoka katika shirika la umeme Tanzania (TANESCO) hivyo kunasababisha kuwacheleweshea malipo hayo kwa wafanyabishara wa nguzo ambazo hazina dawa.

Waliongeza kuwa kuna baadhi ya wafanyabishara hao wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa hawajalipwa toka mwaka jana 2020 mwezi wa tisa kutoa kwenye kampuni ya New forest iliyopo mkoani Iringa.

Sunday, February 7, 2021

WADAU WA MISITU WAIPONGEZA TFS KUPITIA SAO HILL KWA KUGAWA MICHE YA MITI MILIONI MOJA KILA MWAKA


 Katibu wa umoja wa wavunaji miti mkoa wa Iringa (UWASA)Dr Bazir  Tweve akipokea miche ya miti kwa niaba ya wananchi wengine mbele ya Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti la Sao hill Juma Mwita 

Na Fredy Mgunda,Iringa. 

Wadau wa misitu mkoani Iringa wameipongeza wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi kwa kugawa miti milioni moja kila mwaka kwa wananchi na taasisi mbalimbali zinazolizunguka shamba hilo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa miche ya miti ,katibu wa umoja wa wavunaji miti mkoa wa Iringa (UWASA)Dr Bazir  Tweve alisema kuwa uongozi wa shamba la Sao Hill umekuwa ukitoa miti na elimu ya utunzaji wa miti kwa wananchi wanalizunguka shamba hilo.

Alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu ya uhifadhi misitu kwa wananchi na wadau mbalimbali wanajihusisha nawasiojihusisha na zao la miti kwa kuendelea kutunza na kulinda mazingira yasihalibike kwa njia mbalimbali kama vile kuchoma moto au kukata miti hovyo.

Dr Tweve aliongeza kuwa kitendo cha TFS Mufindi kutoa miche milioni moja kunasaidia kuwakumbusha wananchi kupanda miti na kuitunza vizuri hadi pale itakapofika muda wa kuvunwa kutoakana na aina ya mitia ambayo wameipanda.

Alisema kuwa uchumi wa wilaya ya Mufindi na Mkoa wa Iringa kwa ujumla unategemea misiti hivyo zao la miti linachangia kukuza uchumi wa wananchi mmoja mmoja na kueleta maendeleo kwa ujumla kwa wananchi wa mkoa wa iringa nan je ya Iringa.

Dr tweve aliwaomba uongozi wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindikutoa elimu ya uvunaji wa miti ili kuepukana na wananchi kuvuna miti ikiwa bado haijakomaa kuvunwa na kupeleka bidhaa ambayo haihitajiki sokoni.

“Sasa hizi imezuka tabia ya wananchi wanaomiliki mashamba binafsi kuvuna miti ambayo haijakomaa kuvunwa kutoka na hali ya uchumi hivyo niwaombe mfike kwa wananchi na kutoa elimu hiyo kipindi mnatoa miche na baada ya miche hiyo kupandwa” alisema Dr tweve

Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi,Peter Tweve aliwashukuru wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi kwa kazi kubwa wanayifanya ya kutunza maziringa na kutoa elimu ya mazingira kwa wananchi wanaolizunguka shamba hilo.

Alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Mufindi kwa kiasi kikubwa uchumi wake unategemea Misiti hiyo kitendo cha Sao Hill kutoa miche kwa wananchi kunahamasisha wananchi kuendelea kupanda miti na kutunza mazingara.

Naye Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti la Sao hill Juma Mwita alisema kuwa wameyapokea mawazo ya wadau na kuahidi kuyafanyia kazi ikiwapo swala la kutoa elimu kwa wananchi wanaovuna miti mapema kabla ya muda wake.

Alisema kuwa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi wamekuwa wakitoa elimu hiyo na wataendelea kutoa elimu mara kwa mara lengo la wananchi wawe na uelewa wa utunzaji wa mazingira. 

Thursday, February 4, 2021

The world largest mounted skeleton of dinosaur discovered in Tendaguru, ...

RIDHIWANI AMPA HEKO AWESO, AMUOMBA KUMALIZA TATIZO LA MAJI CHALINZE


Na Andrew Chale, Dodoma

Mbunge Jimbo la Chalinze,  Ridhiwani Kikwete amempongeza Waziri wa Maji, Juma Awesu kwa kuitendea haki Wizara hiyo ambapo pia amemuomba kuongeza kasi katika kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji kwa kukamilisha miundombinu ya miradi ya maji inayojengwa katika Jimbo hilo la Chalinze.

Ridhiwani Kikwete amebainisha Bungeni wakati wa kujadili hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Ufunguzi Rasmi wa Bunge la Kumi na Mbili.

"Nitumie nafasi hii kumpongeza sana ndugu yangu Bwana Awesu Waziri wa maji kwa kazi nzuri sana anayoifanya. Wana Chalinze wanakushukuru na wanaendelea kushukuru kwa kiasi kikubwa unayoendelea kuyafanya.

Wito wao mmoja tu, ni kwamba zile pampu zinazojengwa pale Msoga na pale  Chamakweza wanaomba ziharakishwe  kuona zinakamilika mapema ili lile tatizo la maji linalowakabiri wananchi wale liweze kuisha na liwe hadithi ambayo imepita." Alisema Ridhiwani Kikwete wakati wa kuunga mkono hoja pamoja na kuunga mkono Hotuba ya Rais.

Serikali kupitia Wizara yake hiyo ya Maji na Mamlaka ya Maji DAWASA,  tayari wapo katika ujenzi wa vituo vya kusukuma maji (buster stations)  na pamu kwenye maeneo ya Chamakweza na Msoga ambapo mradi huo utakapokamilika utamliza tatizo la maji Jimbo la Chalinze pamoja na maeneo ya jirani ikiwemo Morogoro Vijijini.

WANAMUZIKI ZAIDI YA 500 KUHUDHURIA KONGAMANO LA FURSA JIJINI ARUSHA


Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la fursa la wanamuziki litakalofanyika Februari 20 jijini Arusha.

Mwanamuziki mkongwe hapa nchini, Kida Waziri atakabidhiwa kadi ya matibabu ya NHIF kwenye kongamano hilo.
Wanamuziki Madamu Flora (kulia) na Stellah Joel watakuwepo kwenye kongamano hilo.

Mwanamuziki Emmanuel Mbasha atakuwepo kwenye kongamano hilo.


Mwanamuziki Goodluck Gozibeth atakuwepo kwenye kongamano hilo.
Mwanamuziki Mabisa atakuwepo kwenye kongamano hilo.
 


Na Dotto Mwaibale.

Wanamuziki zaidi ya 500 kutoka kada mbalimbali nchini wanatarajia kuhudhuria kongamano la fursa litakalofanyika Februari 20 jijini Arusha.

Katika kongamano hilo baadhi ya wanamuziki hao watakabidhiwa kadi za bima ya afya ya Taifa (NHIF) na Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

  "Wanamuziki watakao pata kadi hizo ni wale ambao wametimiza vigezo kama walivyoeleza Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Eric Kisanga na Katibu Mkuu wa umoja huo, Stella Joel ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo.

Baadhi ya wanamuziki watakao kabidhiwa kadi hizo wametajwa kuwa ni mwanamuziki mkongwe hapa nchini, Kida Waziri,  Emmanuel Mbasha, Madamu Flora, Goodluck Gozibeth, Stara Thomas, Hafsa Kazinja Renatha Sedekia na Rehema Tajiri.

Akiwazungumzia Wanamuziki hao Katibu Mkuu wa TAMiUFO Stella Joel alisema wanaishukuru Serikali kwa kuwakumbuka kuwapatia kadi hizo ambazo zitawasaidia kupata vipimo na matibabu katika hospitali za Serikali na binafsi.

Joel alisema kabla ya hapo wanamuziki wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa kushindwa kumudu gharama za vipimo na matibabu.

" Kwa hatua hii iliyochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano hakika wanamuziki wote tunakila sababu ya kuipongeza  kwa kutekeleza ahadi yake kwa vitendo ya kutusaidia wasanii" alisema Joel.

Rais wa TAMUFO,  Eric Kisanga alisema kongamano hilo ni la kipekee kwani litawahusisha wanamuziki wa kada zote  na kuwa maandalizi yote yamekwisha kamilika.

" Maandalizi yote ya kongamano letu ili la fursa kwa wanamuziki yamekwisha kamilika kwa asilimia kubwa na sasa tupo kumalizia mambo madogo yaliyosalia" alisema Kisanga.

Kisanga alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi na wadau wengine kwenye kongamano hilo.

DKT. NDUGULILE AFUNGUA MAFUNZO YA UONGOZI KUWANOA MENEJIMENTI NA WATUMISHI WA WIZARA YAKE

 

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (kushoto) akizungumza katika mafunzo ya uongozi kwa menejiment ya Wizara hiyo, yanayotolewa na Chuo cha utumishi wa Umma Tanzania, jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wake Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndenjembi.
 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile ameiagiza Menejimenti  na watendaji wa Wizara hiyo kuhakikisha wanafanya maamuzi na kutoa ushauri wenye tija  kulingana na nafasi zao ili kufikia malengo ya Wizara hiyo na kuharakisha michakato ya Serikali.

Dkt. Ndugulile amezungumza hayo akifungua mafunzo ya uongozi kwa wajumbe wa Menejimenti na watumishi wa Wizara hiyo, yanayotolewa na Chuo cha Utumishi wa umma Tanzania kwa muda wa wiki mbili.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndenjembi akizungumza katika mafunzo ya uongozi kwa Menejimenti na watendaji wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari yanayofanyika jijini Dodoma, wa pili kulia ni Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile na Kushoto ni Naibu wake Mhandisi Kundo Mathew na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Zainab Chaula.

Amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwa sababu Wizara hiyo ni mpya, yenye muundo mpya, majukumu mapya inataka kwenda na viwango vipya kwa kufanya kazi zenye ubora.

Ameongeza kuwa kuna baadhi ya watumishi wanajisahau kuwa wanawatumikia wananchi wa Tanzania na kudhani dhamana walizopewa ni kwa manufaa yao binafsi, na kusisitiza watendaji wa Wizara hiyo wafanye kazi kwa kufuata miiko na maadili ya watumishi wa umma.

“Ninatarajia kuona mabadiliko na maboresho katika utendaji kazi na utoaji wa  huduma zetu kwa wananchi.”  Amesema.Dkt. Ndugulile

Sehemu ya Menejimenti na Watendaji wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akifungua mafunzo ya uongozi yanayotolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, jijini Dodoma

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo,  Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa mafunzo hayo yanatoa mwanga wa kwenda kutekeleza vema ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuikumbusha Menejimenti ya Wizara hiyo kurudi katika misingi ya utumishi wa umma.

“Tukumbuke kwamba tumeaminiwa katika dhamana tulizopewa, tufanye kazi kulingana na matakwa ya nafasi zetu, kwa kila mtu kutimiza wajibu na kutambua mipaka yake kama sehemu ya maadili katika utumishi wa umma”, Mhandisi Kundo Mathew.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Kushoto) akizungumza na Menejimenti na watendaji wa Wizara hiyo (hawapo pichani) katika mafunzo ya uongozi yanayotolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma, jijini Dodoma, anayefuata ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na kulia ni Naibu wake Dkt. Jim Yonazi.

Na Faraja Mpina - WMTH

Kwa upande wa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndembeji aliyehudhuria ufunguzi wa mafunzo hayo amesema  kuwa Chuo cha Utumishi wa umma ni wakala wa Serikali katika kunoa, kuandaa, kushauri na kuboresha utendaji kazi katika utumishi wa umma.

Ndembeji ameupongeza uongozi wa Wizara kwa kukitumia Chuo hicho kupiga msasa watendaji wa Wizara hiyo, ikiwa ni mfano wa kuigwa na taasisi nyingine za Serikali.

Monday, February 1, 2021

WATUMISHI HESLB WAPATIWA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru amesema taasisi hiyo itaendelea kuzingatia miongozo, sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma katika utoaji huduma wa zake kwa wateja.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watumishi wa HESLB jana (Jumapili Januari, 31 2021), Badru alisema HESLB ni miongoni mwa taasisi za umma zinazogusa maslahi ya makundi mbalimbali ya kijamii, hivyo inawajibika kuweka mikakati madhubuti ya kuhudumia wateja.


Badru alisema kwa kutambua umuhimu huo, Ofisi yake imeandaa miongozo mbalimbali kwa watumishi wake ili kuwajengea uwezo wa namna bora ya kuwahudumia wateja na kushughulikia malalamiko yanayojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

“Mafunzo haya ni sehemu muhimu ya kutukumbusha wajibu wetu katika kuhuhudumia wateja, tukiwa kama taasisi ya serikali tumeendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja kwa kuzingatia miongozo ya utumishi wa umma ikiwemo kuandaa mkataba wa huduma kwa wateja na mwongozo wa kushughulikia malalamiko kwa wateja,” alisema Badru.

Aidha Badru alisema kupitia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo, ni wakati muafaka kwa kila mtumishi wa HESLB kutafakari nafasi na wajibu alionao katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa miongozo ikiwemo umuhimu wa kuzingatia uadilifu sehemu za kazi.

“Tunamaliza mwezi Januari tukiwa katika mafunzo haya muhimu yanayotukumbusha utekelezaji wa majukumu yetu, tunapaswa kutimiza wajibu wetu kwa kuzingatia wajibu wa msingi wa kila mtumishi wa umma na kubwa zaidi ni uadilifu katika maeneo yetu ya kazi”, alisema Badru.

Awali, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa HESLB, Neema Kuwite alisema kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo, Ofisi yake inaandaa mpango wa mafunzo kwa watumishi kuhusu utekelezaji wa miongozo ya kuhudumia wateja mahali pa kazi kwa kupitia nyaraka mbalimbali ikiwemo mkataba wa huduma kwa mteja ulioanza kutekelezwa na HESLB.

“Kupitia mafunzo haya tumepokea ushauri, maoni na mapendekezo kutoka kwa watumishi kuhusu namna ya kuhudumia wateja wetu, tunaandaa mpango wa mafunzo kwa watumishi ili kuweza kuwajengea uwezo wa pamoja katika kuhudumia wateja wetu”, alisema Kuwite.

Mafunzo hayo ya siku mbili yalishirikikisha jumla ya watumishi 140 kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya HESLB, Ofisi za Kanda ya Dodoma, Zanzibar, Mwanza, Mtwara, Arusha na Mbeya.