Matokeo chanyA+ online




Thursday, July 22, 2021

KIVUKO CHA MV. MAFANIKIO KUREJEA MTWARA BAADA YA WIKI TATU

 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akimuonyesha kitu Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Khalid Songoro kulia wakati wakikagua moja ya milango ya kivuko cha MV. MAFANIKIO kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Songoro Marine katika yadi yake iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kivuko hicho kinachotoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kinatarajiwa kurejea Mtwara baada ya wiki tatu kuendelea kutoa huduma. Katikati ni Mkuu wa Kivuko Magogoni Kigamboni Mhandisi Samuel Chibwana

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Khalid Songoro (wa tatu kulia) wakati akikagua maendeleo ya kivuko cha MV. MAFANIKIO ambacho kimeletwa katika yadi ya Songoro Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati. Kivuko hicho kinachotoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kinatarajiwa kurejea Mtwara baada ya wiki tatu kuendelea kutoa huduma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Khalid Songoro (wa pili kulia) na Mkuu wa Kivuko Magogoni Kigamboni Mhandisi Samuel Chibwana kulia wakikagua kivuko cha MV. MAFANIKIO kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Songoro Marine katika yadi yake iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kivuko hicho kinachotoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kinatarajiwa kurejea Mtwara baada ya wiki tatu kuendelea kutoa huduma.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Khalid Songoro akimuonyesha kitu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wakati akikagua kivuko cha MV. MAFANIKIO kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Songoro Marine katika yadi yake iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kivuko hicho kinachotoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kinatarajiwa kurejea Mtwara baada ya wiki tatu kuendelea kutoa huduma. Kulia ni Mkuu wa Kivuko Magogoni Kigamboni Mhandisi Samuel Chibwana

 

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA DAR ES SALAAM)

*****************************

Huduma za Kivuko kwa wakazi wa Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara zinatarajiwa kurejea baaada ya takribani wiki tatu kutoka sasa, hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle leo wakati alipotembelea eneo la Yadi ya Songoro Marine Kigamboni jijini Dar es Salaam kukagua maendeleo ya ukarabati huo unaofanywa na kampuni ya Songoro.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kukagua ukarabati wa kivuko hicho, Mtendaji Mkuu Maselle amesema kivuko hicho kipo mbioni kukamilika kwani Mkandarasi ametakiwa kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda mfupi ili wakazi wanaotegemea kivuko hicho Mkoani Mtwara waweze kurejeshewa huduma zake mapema iwezekanavyo.

‘’Tumekisafirisha kivuko hiki kutoka Mtwara kuja hapa Dar es salaam kwakuwa ni gharama ndogo kukileta hapa kuliko kusafirisha vifaaa vyote vya matengenezo kwenda kufanyia Mtwara ndio maana mkandarasi akaamua kukivuta kivuko hiki kije hapa ili muda wa matengenezo uwe mfupi zaidi’’.

Mhandisi Maselle amesisitiza kuwa utaratibu wa kufanya matengenezo kwa vivuko vya TEMESA ni muhimu sana kwa vyombo vya maji kwakuwa maji ya bahari yana chumvi nyingi na kali hivo kama kivuko kitakuwa hakijafanyiwa ukarabati kwa muda mrefu kitakuwa kinaharibika na kitashindwa kufanya kazi kwani chuma chake kitaliwa na maji ya chumvi na hivyo kushindwa kudumu kwa muda mrefu.

‘’Ni utaratibu wa kawaida kwa TEMESA kila ambapo kivuko kinafikia muda wake wa matengenezo kinga, lazima kitolewe na kupelekwa kufanyiwa ukarabati na matengenezo na hii ni hatua mojawapo ambayo tumefanya na tunaendelea na ukarabati wa vivuko vingine  ambavyo muda wake wa ukarabati umefika’’. Alisema Mhandisi Maselle ambapo amewaomba wakazi wa Mtwara wavumilie wakati kivuko hicho kikiendelea kufanyiwa ukarabati ambapo wakazi hao wamepelekewa boti mbili za MV. TANGAZO na MV. KUCHELE ambazo zinatoa huduma kwa sasa kwa wakazi hao.

 Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Khalid Songoro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya tukio hilo la ukaguzi amesema, ukarabati wa kivuko hicho umefikia asilimia 85% na ameongeza kuwa wanatarajiwa kumaliza ukarabati wake ifikapo Tarehe 15 mwezi Agosti.

‘’Kazi kubwa zote tulizozifanya ziko kwenye hatua ya mwisho ili kuweza kukamilisha ukarabati wa kivuko hicho,’’ amesema Songoro.

Kivuko cha MV. MAFANIKIO kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50 na kinatoa huduma zake kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara mjini.

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA TONY BLAIR WAZIRI MKUU MSTAAFU WA UINGEREZA


 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair wakati Mhe. Blair alipofika  Ikulu Jijini Dar es salaam leo Julai 22,2021. (Picha na Ikulu) 
 
Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair wakati Mhe. Blair , akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipofika  Ikulu Jijini Dar es salaam leo Julai 22,2021. 

(Picha na Ikulu)

Tuesday, July 20, 2021

DAWASA YAPONGEZWA KWA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA ZA MAPATO YAO



Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema mamlaka ya maji  safi na usafi wa mazingira DAWASA imepiga hatua kubwa katika usimamizi wa miradi ya maji nchini ikiwemo matumizi mazuri ya fedha zinazopatikana katika Mamlaka hiyo kwa kuwekeza kiasi cha Shilingi Bilioni 17.8 katika Miradi wa Maji wa Ruvu Juu mpaka Msoga itakayotatua kero ya Maji kwa Wananchi zaidi ya 122,000 wa maeneo hayo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ziara hiyo, Naibu Waziri, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapongeza DAWASA kwa kujituma kutekeleza Miradi hiyo ya kimkakati ili kutatua kero ya Maji katika sehemu mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Pia amepongeza Watumishi, Wasimamizi wa Miradi yote ya DAWASA wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Cyprian Luhemeja katika kufanikisha utekelezaji wa Miradi hiyo takribani 27 sehemu mbalimbali ya Dar es Salaam na Pwani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA, Mhandisi Ramadhani Mketo amesema Mradi wa Maji wa Ruvu Juu hadi Mboga ni Mradi utakaosaidia kuondoa kero ya Maji katika maeneo ya Mlandizi, Chalinze na Mji Mdogo wa Mboga, pia Mradi huu wanalaza mabomba kwa umbali wa Kilometa 59  katika Mitambo ya Ruvu Juu hadi Chalinze, Mji wa Mboga.

Amesema pia mradi huo utatatua kero ya Maji katika Bandari Kavu ya Kwara na kwenye Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR Kwara, amesema Lita 9,300,000 za Maji zitatumika kwa siku baada ya kukamilika Mradi huo.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhwan Kikwete amesema ujio wa Naibu Waziri wa Maji katika Maeneo hayo itasidia katika utekelezaji wa Miradi hiyo ya Maji na kuondoa kero kwa Wananchi wake.
Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mketo akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi kuhusu ulazaji wa Bomba za inchi 10 zinazolazwa kutoka Ruvu Juu mpaka Mboga yenye kilometa 58.9 kwenye Mradi wa Chalinze- Mboga unaotekelezwa na DAWASA. Wa kwanza kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi
Muonekano wa Bomba la inchi 16 linalolazwa kutoka Ruvu Juu mpaka Mboga litakalokuwa na kilometa 58.9 
Kazi ikiendelea
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi kuhusu ulazaji wa Bomba unavyopita kwenye ramani kuanzia Ruvu Juu mpaka Mboga kilichopo Wilaya ya Bagamoyo  wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akikagua mradi wa ulazaji wa mabomba ya inchi 16 katika eneo la Kitongoji cha Mbala kilichopo Kijiji cha Chamakweza wakati wa Ziara yake ya kukagua Miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Kazi ikiendelea 
Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi pamoja na Mbunge wa Chalinze Riziwani Kikwete kuhusu mradi wa kujenga pampu ya kusukuma maji katika Kijiji cha Chamakweza wakati wa Ziara ya naibu Waziri wa maji alipotembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi pamoja na Mbunge wa Chalinze Riziwani Kikwete kuhusu ujenzi wa pampu ya maji ya Msoga wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Maji.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi  akiendelea na Ziara yake ya kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la ujenzi wa pampu ya maji ya Msoga kuhusu kuridhishwa na miradi inayotekelezwa na DAWASA wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka hiyo.
Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mketo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na DAWASA wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna wanavyosimamia miradi hasa ya maji ili kuondoa hadha kwa wakazi wa Chalinze ambao wanachangamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi alipokuwa anatembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.

WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAONESHO YA MADINI SHINYANGA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo.

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, ana tarajiwa kuwa mgeni Rasmi kwenye maonesho ya biashara ya Teknolojia na Madini mkoani Shinyanga.

Maonesho hayo yatafanyika kuanzia Julai 23 mwaka huu hadi Agost Mosi, katika viwanja vya Butulwa, Kata ya Old Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, amebainisha  hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari ,kuwa maonesho hayo ni ya awamu ya pili, ambayo yamelenga kukuza Sekta ya Madini na biashara mkoani humo.

Alisema Mkoa wa Shinyanga una migodi mingi ya madini , hivyo kupitia maonesho hayo, yatatoa fursa kwa wawekezaji kuja kuwekeza mkoani humo, pamoja na kuunganisha mtandao wa wafanyabiashara.

"Maonesho haya ya Biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, yatatusaidia kukuza uchumi wa Mkoa wetu, na  pato la mtu mmoja mmoja, na Taifa kwa ujumla, na tuta yafungua Julai 23, na Mgeni Rasmi atakua Waziri Mkuu Kassim Majaliwa," amesema Dk. Sengati.

"Tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye maonesho haya, kuja kuona madini live, pamoja na wafanya biashara wajumuike ili wapate mtadao na kukuza biashara zao," ameongeza.

Naye Mwenyekiti wa Maonesho hayo Kulwa Meshack, ambaye ni Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA)mkoani Shinyanga, alisema maonesho hayo ni fursa kwa wachimbaji na wafanyabiashara, ambapo watabadilisha uzoefu namna ya kufanya kazi zao.

MAVUNDE AWASHUKURU WANANCHI DODOMA,ASIKILIZA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA WANANCHI NA KUZITAFUTIA UFUMBUZI

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akiwa ameongozana na Kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Dodoma Mjini, jana amefanya mkutano wa kuwashukuru wananchi kwa kuichagua CCM 2020 sambamba na kusikiliza kero,changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Baada ya kusikiliza Changamoto za wananchi wa eneo husika,Mbunge Mavunde alieleza haya yafuatayo;

-Katika kutatua changamoto ya maji mtaa wa Chididimo,tumeshapata fedha za uchimbaji wa kisima kipya cha maji, kazi ambayo itaanza mapema mwezi Agosti.
Kusambaza umeme maeneo yote ya mitaa iliyosalia katika kata ya Zuzu hasa mitaa ya Chididimo na Sokoine.


Kufuatilia malipo ya fidia ya barabara ya mzunguko(Outer Ring Road) kwa wananchi ambao bado hawajahakikiwa na kuingizwa kwenye malipo.


Kufuatilia kwa ukaribu malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha maeneo yao kwa ajili ya uwekezaji,mashamba darasa na hifadhi ya wanyama(Zoo).


Kusimamia uwasilishwaji mapema  wa fedha Tsh 20,000,000 za ujenzi wa miundombinu ya vyoo Shule ya Msingi Chididimo
 

Ujenzi wa Sekondari Mpya kata ya Zuzu kwa nguvu za Mbunge na wananchi kuwapunguzia mwendo watoto wa shule kutembea umbali mrefu.
Kurasimisha vikundi vya wavuvi na kuviwezesha mikopo vikundi vya wakina Mama,Vijana na watu wenye ulemavu.


Kutoa magodoro 30 kwa ajili ya  Hostel ya Wanafunzi wa Sekondari wanaotoka maeneo ya mbali.




 

RAIS SAMIA ATOA MILIONI 100 UJENZI WA PAA SOKO LA MACHINGA COMPLEX.


RC Makalla aelekeza Suma JKT kuanza Ujenzi Mara moja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi Cha Shilingi Milioni 100 kwaajili ya Ujenzi wa Paa la Kisasa la kuzuia Jua na Mvua kwa Wahanga 1,800 wa Soko la Kariakoo waliohamishiwa Machinga Complex ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amethibitisha kupokea fedha hizo.


Akizungumza na Wafanyabiashara hao, RC Makalla amesema baada ya Jana kuwatembelea na kuwasikiliza, Rais Samia aliona changamoto hiyo na alipomuuliza RC Makalla kiasi Cha fedha kinachohitajika alisema ni Milioni 62 za Ujenzi wa Paa la Turubai lakini kwa kutambua umuhimu wa Wafanyabiashara Rais  Samia alitoa Milioni 100 ili lijengwe Paa la Kudumu kwa Bati la Kisasa.


Kutoka na fedha kupatikana, RC Makalla amewaelekeza Suma JKT ambao ndio wajenzi kuanza Ujenzi Mara moja ili Wafanyabiashara hao wafanye biashara bila kero.


Kuhusu suala la Meza, RC Makalla amesema tayari amepatikana Mkandarasi atakaejenga Meza za kisasa za kuhamishika kuendana na hadhi ya Soko.


Aidha RC Makalla ameelekeza Viongozi wa Jiji la Ilala kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya Taka, Mifumo ya Maji, Mifumo ya umeme na wafunge Vizima Moto ili kukabiliana na majanga ya Moto.




Thursday, July 8, 2021

RAIS SAMIA AKISALIMIANA NA WANANCHI WA DUMILA WILAYANI KILOSA NA GAIRO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi  Dumila Wilayani Kilosa alipokuwa njiani akirejea Jijini Dodoma  Julai 08,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Gairo wakati akimalizia ziara yake ya siku mbili mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi pamoja na Wasanii mara baada ya kuhutubia wananchi wa Dumila mkoani Morogoro.
Wasanii mbalimbali kutoka Dar es Salaam wakimpungia mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Dumila mkoani Morogoro
Wananchi wa Dumila wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mara baada ya kusimama katika eneo hilo. PICHA NA IKULU

Wednesday, July 7, 2021

WAZIRI MKENDA ATUA SIMIYU//AZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA KUONGEZA UZALISHAJI NA TIJA KATIKA ZAO LA PAMBA


Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati Akizindua kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tarehe 4 Julai 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akikata utepe kuashiria kuzindua kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tarehe 4 Julai 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati alipotembelea na kukagua shamba darasa la Pamba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tarehe 4 Julai 2021.
Balozi wa Pamba Tanzania Ndg Agrey Mwanri akitoa elimu kwa wakulima wa Pamba kuhusu namna bora ya kulima, kupanda kwa kufuata mistari kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda kuzindua kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tarehe 4 Julai 2021.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Ndg Marco Mtunga akitoa ufafanuzi juu ya dhamira ya Bodi kuhakikisha Tija inaongezeka kwenye zao la Pamba mbele ya mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda kabla ya kuzindua kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tarehe 4 Julai 2021.
Sehem ya wananchi wa Wilaya ya Busega wakifuatilia maelezo ya wataalamu kuhusu namna bora ya kulima zao la Pamba kabla ya rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkend kuzindua kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tarehe 4 Julai 2021.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu

“Tija ya zao la pamba kwa sasa ni kilo 200 hadi 300 kwa ekari. Taarifa nilizonazo, tunaowakulima wanozingatia kanuni 10 za kilimo bora cha pamba na tija yao ni kati ya kilo 1,000 na 1,200 kwa ekari. Tanzania ina fursa kubwa ya kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka wastani wa tani 300,000 hadi tani 1,000,000”      

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo tarehe 5 Julai 2021 wakati Akizindua kampeni ya Kuongeza Tija katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

“Kwa lengo la kufikia lengo la kuzalisha tani 1,000,000 ifikapo mwaka 2025 kama ilivyoainishwa kwenye ilani, leo ni siku muhimu sana. Nimezindua kampeni ya kuongeza tija katika zao la pamba. Wizara iliona ni muhimu kuendesha kampeni kabambe ya kuwahamasisha wakulima wa pamba kuzingatia kanuni 10 za kilimo bora cha pamba” Amekaririwa Waziri Mkenda

Amesema Kwa kuwa pamba inazalishwa katika Mikoa 17 nchini, hivyo Wakuu wa Mikoa na viongozi wote katika ngazi mbalimbali, wanapaswa kuunga mkono juhudi hizo ikiwemo Wabunge kusaidia kuelimisha wananchi katika maeneo yao ili kilimo cha pamba kiwe mkombozi wa maisha wakulima na watanzania kwa ujumla wake.

Waziri Mkenda amesema kuwa kilimo kinakabiliwa na tatizo kubwa la tija kuwa ndogo sana karibu katika kila zao. Hali hiyo inasababisha pato la mkulima kuwa chini.

”Wizara yangu imelitambua tatizo hili la msingi na kwamba tuna jukumu kwanza la kuuelimisha umma na wakulima kwa ujumla juu ya umuhimu wa kuangalia pato la mkulima kama kigezo cha ufanisi katika shughuli zote za kilimo. Pili tuna wajibu wa kuweka mazingira sahihi ili kila mkulima nchini wa zao lolote abadili maisha yake kutokana na shughuli yake. Hivyo, kwa nafasi ya pekee niwapongeze Wadau wa Pamba kuwa wa kwanza kutekeleza maono ya Wizara ya Kilimo katika kuongeza tija” Amesema Waziri Mkenda

Waziri wa Kilimo amesem akuwa Kipato cha mkulima kinategemea kiasi mkulima anachozalisha kwa ekari, ubora wa zao na bei ambayo soko liko tayari kulipa. Mkulima yoyote ana uwezo wa kupata tija kubwa na kuzalisha zao bora. “Muda umefika wa viongozi na wakulima kuelewa kwamba tija ikiwa kubwa kwa bei yoyote itakayokuwepo sokoni, pato litakuwa kubwa” Amesisitiza

Waziri Mkenda amesema kuwa ili kilimo kiweze kutoka kwenye tija ndogo, suala la kuboresha utoaji wa huduma za ugani ni la lazima. Katika mwaka huu wa fedha jumla ya Pikipiki 1,500 zitanunuliwa na kusambazwa katika mikoa mbalimbali baada ya kutosheleza Mikoa ya Dodoma, Singida na Dodoma.

Amesema kuwa kuwa Lengo ni kufanya vizuri katika Mikoa 3 ili mwaka ujao kujipima kiasi cha mafanikio na kuongeza nguvu kuifikia mikoa mingine; ikiwa ni pamoja na Maafisa Ugani kupatiwa mafuta  ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao; na Ili kuimarisha usimamizi vyombo vya usafiri vitafungiwa GPS.

Kwa upande wake Balozi wa Pamba Tanzania Ndg Geofrey Mwanri akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema kuwa ili tija iweze kuongezeka kwenye zao la Pamba ni lazima wakulima Kubadili vipimo vya kupandia kutoka 90x40cm na kuwa 60x30cm ambapo idadi ya mimea kwa ekari itaongezeka kutoka 22,222 hadi 44,400. Mabadiliko yanafanyika baada ya kukamilika kwa utafiti uliofanywa na TARI Ukiriguru na kuonesha ongezeko kubwa la tija kufikia kilo 1,000 kwa ekari.

Mwanri amesema kuwa wakulima wanapaswa Kusomba samadi na kusambazwa mashambani ili kurutubisha udongo ambapo wakulima wa pamba wanapaswa kuondokana na matumizi ya jembe la palizi la kukokotwa na wanyamakazi. Hatua hii itarahisisha palizi kufanyika kwa saa 2 kwa ekari badala ya siku 7 kwa jembe la mkono;

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba  Ndg Marco Mtunga amesema kuwa Bodi ya Pamba imejipanga Kuimarisha huduma za ugani, Kusambaza kamba za kupandia katika wilaya zote ili kuwezesha wakulima wa pamba kuzingatia vipimo vipya vya upandaji; na Pembejeo zote ikiwemo mbegu, viuadudu, vinyunyizi kusambazwa kwa wakati.

Ameongeza kuwa katika maeneo yote ya usukumani na mikoa inayolima Pamba wakulima hawana tatizo la nguvu kinachokosekana ni maarifa machache yanayopatikana kwenye kilimo cha Pamba.

Hata hivyo amewapongeza wakulima wa Pamba kote nchini kwa kuitikia mwito wa serikali wa kuhakikisha uzalishaji unaongezeka katika msimu wa mwaka 2020/2021 hivyo amewaomba wananchi kuitikia tena mwito wa serikali kuhakikisha kuwa uzalishaji na tija unazidi kuongezeka.


Monday, July 5, 2021

WAZIRI PROF MKENDA: USHIRIKA USIINGILIWE KIMAJUKUMU


Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda amewaonya baadhi ya viongozi wenye tabia ya kuingialia Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) huku akiwataka kuacha tabia hiyo mara moja.

Aidha, amesema ushirika sio idara ya serikali hivyo hauwezi kuongozwa kama idara kwakuwa mamlaka yake ina mipaka na hakuna kiongozi anayetakiwa kuingilia matumizi ya fedha wala kuzipangoa matumizi.

Waziri Mkenda ametoa agizo hilo (Jumamosi, Julai 3, 2021) kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya lipuli, Tabora, ambapo alisema kwa kiasi kikubwa serikali imepambana kurejesha mali mbalimbali za ushirika zilizokuwa zimeibiwa kupitia ushirika.

”Tumepambana sana na wabadhilifu kwenye ushirika na kurejesha mali mbalimbali zilizoibiwa kupitia ushirika hivyo kurudisha imani ya wanaushirika, na mali zao haziwezi kufanyiwa ubadhirifu wa aina yoyote.

Tutaendelea kusimamia ushirika kuhakikisha kwamba unaendelezwa kwa weledi, uwajibikaji na uwazi ili watu wengi wakubali kujiunga na ushirika kwa sababu unasaidia sana kunyanyua hali zao za kimaisha kwa kuwa  ni hiari kujiunga hakuna kulazimishwa,”alisema.

Alieleza kuwa ushirika ni hiari na msingi wa kwanza duniani na kwamba ni kweli ushirika sio idara ya serikali hivyo hauwezi kuongozwa kama IDARA YA SERIKALI KWAKUWA mamlaka yake kwenye ushirika yana mipaka yake.

”Na hili ni muhimu kwa sababu kuna mahali ametokea kiongozi mmoja kaingia kwenye AMCOS anatoa amri toa shilingi milioni ishirini na tano hapa peleka kule, hatuna mamlaka hayo, ushirika ni hiyari ya wanaushirika

”Na hapaswi kupelekesha wana ushirika wanapaswa kujisikia kwamba ushirika ni mali yao, wasimame kidete, wasimamie shughuli zao bila kuingiliwa kinyume na taratibu zinazokubalika,”alisema.

Alisisitiza anasema hilo kwa sababu kuanzia Waziri wa kilimo (yeye), Mrajisi wa ushirika, wote lazima wajue mpaka upi wa kwao au si wao

”Mpaka sasa tunakwenda vizuri ukiacha hilo tukio mtu kwenda kutoa amri chukua hela za ushirika kutoka eneo moja kupeleka eneo ambalo ushirika huo hauhusiki nalo kwenda kujenga shule,

”shule ni jambo zuri lakini hakuna mamlaka ya kiongozi yoyote kwenda kuingia kwenye ushirika kuingilia fedha zao kuzipangia matumizi hayo yatafanywa na wanaushirika wenyewe ,”alisema.

Wednesday, June 23, 2021

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MKUTANO WA SADC, MAPUTO NCHINI MSUMBIJI

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Joaquim Chissano uliopo Maputo nchini Msumbiji leo tarehe 23 Juni, 2021.