Matokeo chanyA+ online




Saturday, May 29, 2021

RC SENDIGA AMEIGAIZA TRA IRINGA KUWASILISHA MAJINA YA WAFANYABISHARA WALIOSHINDWA KULIPA MADENI


Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiongea na baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Iringa katika ukumbi wa chuo cha Afya kwa lengo la kujitambulisha na kusikiliza changamoto
Mkuu wa mkoa wa Iringa mh. Queen Sendiga akiwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiingia ukumbinu kuongea na baadhi ya viongozi wa wafanyabiashara wa mkoa wa Iringa
Mfanyabiashara Dickson Lulandala akichangia maoni yake kwenye kikao cha pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga alipokuwatana nao kwa mara ya kwanza.
Baadhi ya viongozi wa wafanyabiashara na machinga mkoa wa Iringa waki msikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

Mkuu wa mkoa wa Iringa mh. Queen Sendiga ameigaiza Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa kuwasilisha ofisini kwake majina ya wafanyabishara walioshindwa kulipa madeni yao baada ya makubaliano ya kisheria baina ya wafanyabiashara na mamlaka hiyo.

akizungumza kwenye kikao na wawakilisha wafanyabiashara na machinga wa mkoa wa Iringa alisema kuwa hata wafumbia macho wafanyabishara wote ambao tayari wamepewa maagizo ya kisheria kulipa madeni hayo lakini bado wamekuwa wanakaidi agizo hilo kutoka kwa mamlaka husika.

Akiwa katika kikao hicho mkuu wa mkoa wa Iringa alimuagiza meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa kuhakikisha anapeleka majina  na kukutana na wafanyabiashara hao wanaokimbia kulipa madeni yao licha ya serikali kuagiza kulipa madeni hayo.

 Mh: Sendiga alisema kuwa wadaiwa hao wakilipa kodi inachangia katika kuboresha sekta mbalimbali kama miundombinu, Afya, elimu, utalii, Ardhi, na kilimo katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya nchi.

Alisema kuwa akaunti za wafanyabisha wakubwa ambao wanaodaiwa madeni makubwa zilikuwa zimefungwa hapo awali na kufunguliwa kwa mjibu wa sheria na makubaliano na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa kulipa madeni hayo ili waendelee na biashara kama iliyokuwa awali.

Mh:Sendiga alisema kuwa jukumu la kulipa kodi ni kwa kila mwananchi anaishi nchini kwa lengo la kuchangia juhudi ya serikali kukuza uchumi wa wananchi na kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla hivyo wananchi wa mkoa wa Iringa wanatakiwa kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka kuwa na madeni makubwa hapo baadae.

“Ngoja niwaambie kuwa bila kulipa kodi nchi haiwezi kukuza uchimi wake wala haitaweza kuleta maendeleo kwa wananchi kwa wakati kwa kuwa itakuwa inakosa fedha za kuanzisha miradi mikubwa ambayo inafaida kwa serikali” alisema Mh: Sendiga

Mh: Sendiga alimalizia kwa kuitaka Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa kuhakikisha inatoa elimu ya mlipa kodi mara kwa mara ili kuepusha wafanyabiasha kufunga biashara zao au kushindwa kulipa madeni ya kodi wanayokuwa wanadaiwa.

Akipokea maagizo hayo meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa Lamson Tulyanje alisema kuwa wameyapokea maagizo hayo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Iringa na watayafanyia kazi ili kuwawezesha wafanyabishara hao kufanya biashara kwa uhuru na kukuza mitaji yao.

Tulyanje aliongeza kuwa watahakikisha wanaendelea kutoa elimu ya mlipa kodi mara kwa mara ili kuwakumbusha wafanyabishara kulipa kodi kuwa ni wajibu wao wa msingi kwa maendeleo ya nchini yao.

Tulyanje alisisitiza kuwa wananchi kudai risiti pale wanaponunua bidhaa yoyote kwa wafanyabishara hivyo hivyo kwa wafanyabiashara nao wanatakiwa kutoa risiti kwa wateja wao wanaonunua bidhaa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo mkoa wa Iringa Edmund Mkwawa aliwamuomba mkuu wa mkoa wa Iringa kuhakikisha anatatua changamoto za wafanyabiashara ili kukuza mitaji yao.

Alisema kuwa Iringa kunafursa nyingi za kibiashara ambazo zinaweza kukuza uchumi wa mkoa kwa haraka endapo changamoto walizozitoa zitafanyiwa kazi kwa kiwango kinachostahili.

Nao baadhi ya wawakilishi wa wafanyabiashara mkoa wa Iringa wamtaka mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga kuacha kusikiliza majungu ya baadhi ya wafanyabisha bali anatakiwa kujikita kutatua changamoto walizomueleza kwa lengo la kukuza uchumi wa mkoa huo.

 

Sunday, May 23, 2021

WIZARA YA AFYA YAANZA UTEKELEZAJI WA MABORESHO HUDUMA ZA MATIBABU KWA WAZEE


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeanza kufanya ufuatiliaji  wa maelekezo yake  katika kuboresha huduma za matibabu kwa wazee kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma na kujionea jinsi walivyoweza kutekeleza maagizo ya utoaji wa huduma za afya kwa wazee wanaofika kupata matibabu hospitalini hapo.

Dkt. Gwajima amesema mahitaji ya maboresho ni mengi  hivyo wizara yake imeona ianze na vitu  vile vya msingi  ambavyo wazee wamekuwa wakiyalalamikia   kila siku wanapofika kwenye vituo vya kutoalea huduma za afya.

Ametaja malalamiko yanayokuwa yakilalamikiwa na wazee  wanapofika kwenye vituo vya afya ni pamoja na mapokezi yasiyoeleweka na kutokupata huduma iliyokusudiwa na kuongeza kuwa   wazee nguvu zimekwisha hivyo wanahitaji kuongozwa kwahiyo wizara yake wamefanya maboresho kwa kuwa na watu maalumu wa kuwapokea wazee hao pale wanapoifika hadi kuondoka na kuwatambulisha kwa kuvaa sare maalumu.

“Kila kituo lazima kiwe na nesi mmoja, afisa ustawi wa jamii pamoja na daktari aliyepangwa zamu na lazima wavae sare ambayo itamtambulisha na imeandikwa ‘Mzee ni Tunu, Tunakupenda, Tunakuheshimu’  pamoja na kuweka mabango yanayomuelekeza au kumuongoza mzee wapi atapata huduma anazozihitaji na ambayo yameandikwa "Mpishe Mzee apate huduma kwanza".

Dkt. Gwajima amesema maelekezo hayo wameyatoa katika hospitali na vituo vya afya vyote na kwa hatua hiyo sasa wizara inaenda kutengeneza muongozo ambao utakua wa uwiano kwa hospitali zote.  Hata hivyo ameipongeza hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma kwa kuanza utekelezaji huo na kuwa itakuwa ya mfano wengine kujifunza utaratibu unaotumika na kuboresha kulingana na mazingira yao.

Aidha, Dkt. Gwajima amewataka hospitali zingine kutokusubiri miongozo katika kutekeleza  maelekezo yanayolewa na kusiwe na visingizio vingi kwamba haiwezekani kwani maagizo yanayotolewa yanawezekana na utekelezaji wake ni wa mara moja hususan katika hospitali za kuanzia halmashauri hadi ngazi ya Taifa.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Vivian Wonanji  amesema idara yake imeandaa mkakati wa huduma wa wazee wa  miaka kumi na ifikapo mwezi Juni mwaka huu wataanza kuandaa mpango wa utekelezaji wake.

Dkt. Wonanji amesema mpango mkakati huo utakuwa na mambo makuu yakiwemo kuzalisha wataalam wa kutoa huduma za wazee,"kama tunavyofahamu wazee wanahitaji mambo mengi ikiwemo masuala ya lishe na utengamao hivyo mkakati huo utakua na maono muhimu ambayo yatasaidia kuboresha huduma za wazee nchini”.

Wakati huo huo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma Dkt. Ernest Ibenzi amesema hospitali yake imejipanga kuwahudumia wazee wa rika tofauti wakiwemo wenye uoni hafifu na hivyo waratibu wa wazee huwafuata wazee mara wafikapo hospitalini  hivyo wanashukuru mapokeo ya wazee pamoja na wagonjwa wanaofika kupata huduma. 

Mnamo tarehe 7 Mei, mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiongea na wazee wa Mkoa wa Dar es salaam aliahidi kuboresha tiba kwa wazee  kwani tiba ni haki yao ya msingi  katika daraja lolote lile watakalokua wanaugua kuanzia vituo vya afya, zahanati hata hospitali za Taifa.
Waziri Dkt.Gwajima akiangalia mfumo wa kuwahudumia wagonjwa uliopo Kwenye hospitali hiyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akipima afya Kwenye jengo wa wagonjwa wa nje kwa kutumia  'patient monitor' ambayo unapima Presha,mapigo ya Moyo na wingi wa hewa ya Oksjeni.
Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima akiangalia Bango linaloelezea huduma za wazee wakati wa ziara ya kuona utekelezaji wa maboresho ya Huduma ya Wazee Kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma.
Mmoja wa mzee aliyefika kupata matibabu kweenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma
Waziri wa Afya Dkt.Gwajima akiwa Kwenye chumba Cha kuwahudumia Wazee kilichopo Kwenye jengo la wagonjwa wa nje,mbele yake ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma Dkt.Ernest Ibenzi
Waziri Dkt.Gwajima akiwa amevalia vazi maalumu la kumtambulisha mtoa huduma ambaye anawahudumia Wazee kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma.Mkakati huo itatekelezwa nchi nzima Kwenye vituo vya kutolea huduma.

HAFLA YA MAKABIDHIANO YA MAGARI YA MRADI WA REGROW JIJINI DODOMA.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akikata utepe katika hafla ya makabidhiano ya magari ya mradi wa REGROW huku akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa na mwakilishi wa Tawiri, Dkt. Wilfred Mareale. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akimkabidhi funguo za gari mwakilishi wa TAWIRI, Dkt. Wilfred Mareale kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya mradi wa REGROW jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa Taasisi baada ya kukabidhiwa funguo za magari kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya mradi wa REGROW jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akizungumza katika halfa ya kukabidhi magari 9 kwa taasisi za TAWIRI, Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Bodi ya Utalii (TTB) ,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) ,Bonde la Mto Rufiji (RBWB) ,na Timu ya Uratibu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi wa taasisi hizo katika shughuli za mradi wa REGROW. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dodoma.

Mratibu wa Mradi , Aenea Saanya akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya Mradi wa Regrow iliyofanyika jijini Dodoma.

(Picha zote na Gladys Lukindo- Afisa Habari, Wizara ya Maliasili na Utalii)

WIZARA ZATEKELEZA MAELEKEZO YA WAZIRI MKUU

  



Na Shamimu Nyaki, Dar es Salaam 

 

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetekeleza maelekezo yote aliyoyatoa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa jana Mei 21,2021 wakati akizindua Kongamano la kuenzi mchango wa Tanzania kwenye ukombozi wa Afrika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam ya kuitaka Wizara ikae na Wizara ya Utumishi na TAMISEMI kutatua changamoto za kimuundo kwenye Sekta za Utamaduni na Michezo.

 

Katibu Mkuu wa Habari Dkt. Hassan Abbasi ameongoza kikao hicho kilichoshirikisha Makatibu Wakuu wa Wizara za TAMISEMI na Utumishi, kwenye kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo nchi nzima ambapo amesema maelekezo yote yamefanyiwa kazi na kukamilika kilichobaki  ni kuandaa nyaraka ili fanikisha  utekelezaji wa maelekezo hayo. 

 

"Kikao hiki kimejadili na kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa aliyotoa Mei 21,2021 wakati akifungua Kongamano la Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ikiwemo kufanya marekebisho ya Muundo wa kada za Maafisa Utamaduni na Michezo, na tayari kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora tumeyafanyia kazi" amesema Dkt.Abbasi.

 

 Amesema Muundo kama huo unatengenezwa kwenye Sekta ya Sanaa ili taaluma za Sekta hizo zitumike kwa ufanisi.

Aidha Dkt. Abbasi amesema kuwa Sera ya Michezo haina changamoto yoyote na inaendelea kutekelezwa kwa namna inavyoelekeza ikiwemo kuwa na miundombinu ya michezo, kutambua michezo kama taaluma, kuwa na vituo vya kukuza vipaji na mambo mengine yaliyoanishwa katika Sera hiyo.

 

Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Dkt. Francis Michael amefafanua kuwa muundo wa sasa umeboreshwa ambapo mtaalam mwenye fani nyingine ambazo siyo za michezo lakini ana uzoefu kwenye michezo na amepata mafunzo ya michezo anakuwa na nafasi ya kuwa kwenye kada Afisa Michezo.

 

Dkt.Michael amesema muundo wa awali ulikuwa unashindwa kuitambua kada ya maafisa michezo hivyo kuwafanya wataalam  kushindwa kufanya majukumu yao kwa ufanisi.

 

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anaeshughulikia Elimu Gerald Mweli amesema kuwa Kitengo cha Utamaduni, Sanaa na Michezo kitatengewa bajeti kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya sekta hizo ambapo amesisitiza maafisa hao kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha ili waweze kupimwa utendaji wao kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma

Naye, Afisa Utamaduni wa Tabora Tito Lulandala kwa niaba ya maafisa Utamaduni na Michezo ameishukuru Serikali kwa namna ilivyotatua changamoto za Maafisa hao hatua ambayo itaboresha utendaji kazi wao.

NAIBU WAZIRI DKT.MOLLEL AIPONGEZA BOHARI YA DAWA (MSD)


Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Brig. Jen. Dkt. Gabriel Sauli Mhidize, akimtambulisha kwa Wafanyakazi wa MSD, Naibu Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin  Mollel, (wa pili kulia) alipokitembea jana  kiwanda cha kuzalisha dawa, kinachosimamiwa na Bohari ya dawa (MSD) Keko Pharmaceuticals.
Utambulisho ukiendelea.
Utambulisho ukiendelea.

 Naibu Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin  Molle, akizungumza na Wafanyakazi wa MSD. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Brig. Jen. Dkt. Gabriel Sauli Mhidize.
Mkutano na Waziri ukiendelea.
 

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin  Mollel amewapongeza MSD kwa kufufua uzalishaji wa dawa katika kiwanda cha kuzalisha dawa, kinachosimamiwa na Bohari ya dawa (MSD) Keko Pharmaceuticals.

Dkt. Mollel ametoa pongezi hizo alipotembelea kiwanda hicho,katika ziara yake aliyoifanya jana Bohari ya Dawa (MSD) kujionea uzalishaji wa dawa na barakoa unaofanywa na MSD.

Kiwanda cha Keko Pharmaceuticals kinazalisha aina 10 za dawa zikiwemo za maumivu aina mbili na nyingine 8 zikiwa ni dawa za kuua vimelea vya magonjwa ya kuambukiza (antibacteria/antibiotics)

Mwishoni mwa wiki Naibu Waziri huyo atatembelea mradi wa kiwanda kingine cha MSD cha kutengeneza mipira ya mikono, kilichopo Idofi,Makambako mkoani Njombe.

WAISLAMU SINGIGA WAOMBWA KUINUSURU NYUMBA YAO YA BAKWATA ISIPIGWE MNADA


Nyumba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida iliyopo karibu na Msikiti wa Kati, Block H  No 13  ambayo ipo mbioni kupigwa mnada.
Mapokezi ya Kaimu Sheikh Nassoro baada ya kuwasili Shelui jana katika ziara yake ya kikazi ya siku moja. 

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro (wa tano katikati) akiongoza kuomba dua mbele ya kaburi la Sheikh Yusuf Iddi Katalama ambaye alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa dini ya Kiislamu Bonde la Iramba wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja Shelui mkoani hapa jana. Wengine ni viongozi wa dini ya kiislamu wilayani Iramba.

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro, akiongoza dua katika arobaini ya Marehemu Maalim Selemani Kingu.

Swala ikiendelea .

Sheikh wa Wilaya  ya Iramba,  Hussein Mgmbaika, akizungumza katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Wilaya  ya Iramba, Ali Katembo, akizungumza katika mkutano huo.

Mwanafunzi, Ali Mohamed akisoma Qulaan katika mkutano huo.

Dufu likipigwa  katika mkutano huo.

Mzee Juma Kengele, akizungumza katika mkutano huo.

Mzee Abdallah Katembo, akizungumza katika mkutano huo.
Mzee Ismail Mang'oma, akizungumza katika mkutano huo.

Mjumbe wa Kamati ya Msikiti wa Kata ya Shelui, Ibrahim Kingu, akizungumza katika mkutano huo

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro, akiingia Msikiti wa Kata ya Shelui kuzungumza na Waislamu.


Mkutano ukiendelea.

Dua katika arobaini ya Marehemu Maalim Selemani Kingu, ikiendelea. Kutoka kushoto ni Sheikh wa Msikiti wa Kata ya Shelui, Iddi Yusuf, Mjumbe wa Kamati ya Msikiti wa Kata ya Shelui, Ibrahim Kingu na Sheikh wa Msikiti wa Al-Jabir, Abdruazizi Ngololo ' Maarufu Sheikh Nyambo'


 Wakina Mama wakiwa katika Arobaini ya Marehemu Maalim Selemani Kingu.



Na Dotto Mwaibale, Singida 


Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro amewaomba Waislamu mkoani hapa kuinusuru nyumba yao iliyopo mjini hapa isipigwe mnada.

Sheikh Nassoro alitoa ombi hilo  juzi wakati akizungumza na Waislamu wa Shelui katika ziara yake ya kikazi ya siku moja.

"Waislamu wenzangu nina ujumbe muhimu kwenu ambao nitawaachia Sheikh na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wilaya  ambao watausambaza hadi kwenye kata nao si mwingine tuna nyumba ya Bakwata ipo pale mjini karibu na Msikiti wa Kati ni Block H  No 13 inapigwa mnada.Kabla sijawa Kaimu Sheikh wa mkoa nilimfuata Mufti Sheikh Abubakar Zubery kumuomba kumuambia kwanini nyumba hiyo hiuzwe hivyo nilimuomba anipe jukumu la kusimamia suala hilo kwa maana ya kuepuka isipigwe mnada ndio maana nimekuja kwenu ili tuinusuru kwani zinahitajika Sh.Milioni 70 ambazo si pesa nyingi kwa watu wengi kwani tukifanya kila mmoja atoa Sh.10,000 kwa wilaya zote saba za Singida tutapata Sh.Milioni 47 na hizo zitakazo salia tutatafuta njia nyingine ya kuzipata ili tuigomboe nyumba hiyo tukijipanga  vizuri naamini hatutakosa fedha hizo" alisema Nassoro.

Katika hatua nyingine Sheikh Nassoro aliwataka Waislamu wa Mkoa wa Singida kuacha kugombana na kueleza kuwa kata, wilaya, mkoa na Taifa lenye magomvi haliwezi kupata maendeleo na ili maendeleo yapatikane kuanzia ngazi ya familia, jamii hadi katika nyumba za ibada nikuacha magomvi.

Aidha Sheikh Nassoro akizungumza na Waislamu hao alisema mbele yao wana majukumu mengi  makubwa na moja ya jukumu alilonalo ni kuboresha taaluma ya dini hasa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari.

Alisema licha ya Serikali kuweka vipindi vya dini katika shule hizo kwa ajili ya kuwaelimisha vijana wa kiislamu kumekuwepo kusuasua na kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Bakwata wenye jukumu la kusimamia vipindi hivyo ni baraza la masheikh wa kata waliopo kwenye maeneo zilipo shule hizo.

" Jambo ninalolisisitiza ni masheikh wa kata wajitahidi kutoa walimu katika kata zao ili vijana wa kiislamu waweze kupata taaluma za dini." alisema Nassoro.

Akizungumza katika mkutano huo Mzee Ismail Mang'oma alisema kazi kubwa ya kwanza ambayo Sheikh Nassoro anatakiwa kuifanya ni kuwaunganisha Waislamu wa Mkoa wa Singida na kuwa wamoja baada ya kupalaganyika kwa kila mtu kuwa kivyake.

Alitaja kazi ya pili ambayo anatakiwa kuifanya ni kuwainua waislamu kiuchumi.

Katika ziara hiyo Sheikh Nassoro alipata fursa ya kuzuru kaburi la Sheikh Yusuf Iddi Katalama ambaye alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa dini ya Kiislamu Bonde la Iramba pamoja na kuongoza dua katika arobaini ya Marehemu Maalim Selemani Kingu.

WAZIRI NDUMBARO - TEMBO ZAIDI YA 200 WAPO NJE YA HIFADHI YA MWL.NYERERE

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kitanda kilichopo katika wilaya ya Namtumbo ambapo amewataka Wananchi kuacha kulima katika maeneo ya Kingo (Bufferzone) katika Hifadhi ya Taifa ya Mwl. Nyerere ili kuepukana na athari zitokanazo na wanyamapori wakali na waharibifu katika ziara ya kikazi anayoifanya mkoani Ruvuma ya kutoa elimu kwa Wananchi.



Baadhi ya Watumishi wa Jeshi la Uhifadhi wa Misitu na Wanyamapori wakiwa wamesimama mbele ili wananchi wa Kijiji cha Kitanda kilichopo katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma waweze kuwafahamu ili pindi matatizo ya Wanyamapori wakali na Waharibifu wanapotokea waweze kupigiwa simu wafike kwa ajili ya kutoa msaada


Mbunge wa Namtumbo Mhe.Vita Kawawa akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kitanda ambapo amemueleza Mhe.Waziri Ndumbaro kuwa jumla ya Wananchi 36 pamoja na mashamba 63 ya mazao yameathiriwa na Wanyamapori wakali na waharibifu hivyo ameomba mchakato wa vifuta jasho na vifuta machozi ufanyike haraka ili Wananchi wake waweze kulipwa. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Namtumbo, Mhe.Sophia Mfaume Kizigo.


Baadhi ya Maaskari Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu wakiwa wamesimama mbele ya Wananchi ili waweze kuwafahamu ili pale tembo wanapotokea waweze kupoigiwa ili waweze kufika kwa ajili ya kutoa msaada wa kuweza kuwaondoa tembo hao kabla hawajaleta madhara kwa wananchi

(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Damas Ndumbaro ametoa tahadhari kwa Wakazi wa Ruvuma kuwa tembo zaidi ya 200 wapo nje ya Hifadhi Taifa ya Mwl.Nyerere kutokana na Wafugaji kuingiza makundi ya ng’ombe ndani ya Hifadhi hiyo.

Dkt. Ndumbaro ametoa tahadhali hiyo hususania kwa wakazi wa wilaya Tunduru na Namtumbo wakati alipotembelea vijiji sita vilivyoathiriwa zaidi na tembo ili kukutana na wananchi na kujibu kero mbalimbali zinazotokana na uvamizi wa tembo katika maeneo yao wakitokea Hifadhi ya Taifa ya Mwl.Nyerere.

Amesema Wenyeviti wa Vijiji wamekuwa wakiwakaribisha Wafugaji kutoka katika mikoa mbalimbali kuhamia katika maeneo ya vijiji hivyo na makundi makubwa ya ng’ombe na kisha kuingiza mifugo hayo ndani ya Hifadhi kwa ajili ya kupata malisho.Amesema kwa mujibu wa utafiti wa Satelite uliofanyika hivi karibuni umeonesha tembo zaidi 200 wapo nje ya Hifadhi, Hivyo amewatahadharisha wananchi kutoa taarifa haraka pindi wanapoona makundi ya tembo yakiwa karibu kwenye makazi yao.

Amesema kufuatia ng’ombe hao kuingia ndani ya Hifadhi wamekuwa wakilazimika kutoka nje ya maeneo yao kwa sababu tembo hawapendi kuchangamana na ng’ombe kutokana na harufu ya madawa wanayotumia kuoshewa wakiwa katika majosho.Kutokana na hali hiyo, Waziri Dkt.Ndumbaro ameagiza ng’ombe walioingizwa ndani ya Hifadhi hiyo wafugaji walipe faini na ng’ombe hao wataifishwe na wasipouzika wapewe magereza kwa ajili ya chakula cha Wafungwa.

Aidha, Waziri Ndumbaro ametaja sababu nyingine iliyochangia Tembo kutoka nje ya Hifadhi kuwa ni tabia ya baadhi ya Wananchi kulima kwenye kingo za Hifadhi hali inayowavutia tembo kutoka nje kwa ajili ya kula mazao hayo.Amesema idadi ya mashamba pamoja na wananchi kujeruhiwa inazidi kuongezeka siku hadi siku si kwa sababu idadi ya tembo imeongezeka bali ni kutokana na idadi ya watu kuongezeka na kulazimika kufanya shughuli ndani ya Hifadhi.

Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro amewaonya Wananchi kuacha kulima katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wananchi kuwa hali hiyo imechangia tembo kutoka nje ya Hifadhi kula mazao

Awali akieleza kuhusu kero za wananchi wa jimbo lake la Namtumbo Mhe. Vita Kawawa, amesema kuwa wananchi wa Jimbo lake la Namtumbo kwa muda mrefu sasa wamekuaa wakiathiriwa na tembo wanaovamia makazi na mashamba yao na kumuomba Waziri wa Maliasili na Utalii kuharakisha kulipa vifuta jasho na vifuta machozi kwa Wananchi waliopata adha zitokanazo na adha ya tembo.

Kwa upande wa Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Hassan Kungu amemuomba Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Ndumbaro kuongeza fedha za vifuta jasho na vifuta machozi kwa sababu fedha wanayolipwa wananchi wake hailingani na thaman ya mashamba waliyoharibiwa na tembo

RAIS DK.MWINYI AKABIDHIWA RIPOTI YA CAG ZANZIBAR


 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiangalia Vitabu vya Ripoti ya Uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu Zanzibar,baada ya kukabidhiwa na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Zanzibar Dkt.Othman Abbas Ali.(hayupo pichani) hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar 23-5-2021.




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mawaziri na Viongozi wa Serikali (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa taarifa ya ripoti ya hesabu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Zanzibar,hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kulia) ni Vitabu vya Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu.



Baadhi ya Mawaziri wa SMZ, wakifuatilia mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza baada ya kukabidhiwa Ripoti ya Hesabu na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.




Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumushi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar.Mhe. Haroun Ali Suleiman, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza baada ya kukabidhiwa Ripoti ya Hesabu na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Ripoti ya Hesabu za Serikali na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Zanzibar.Dkt.Othman Abbas Ali, hafla hiyo ya kukabidhi imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Zanzibar, wakati ikiwasilishwa na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Zanzibar Dkt.Othman Abbas Ali.(hayupo pichani) wakati akisomwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.




Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Zanzibar Dkt.Othman Abbas Ali akisoma Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kabla ya kumkabidhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar




Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Zanzibar Dkt.Othman Abbas Ali akisisitiza jabo wakati akiwasilisha Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)