Matokeo chanyA+ online




Tuesday, April 30, 2019

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TEMEKE LAZINDUA KAMPENI YA NINACHO, NAJUA KUKITUMIA

Kamanda wa Viwanja vya Ndege wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini (ACF) Maria Kulaya, akisalimiana na Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Bi. Bupe Mwakibete (kulia), alipowasili katika viwanja vya Mwembe Yanga, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia, iliyofanyika katika viwanja hivyo Temeke Dar es salaam mapema leo asubuhi tarehe 30/04/2019
Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Bi. Bupe Mwakibete akitoa hotuba kwa wananchi na wakazi wa Wilaya ya Temeke, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es salaam, mapema leo asubuhi.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kizimamoto Temeke (ASF) Puyo Nzalayaimisi, akihutubia wananchi na wakazi wa Wilaya ya Temeke, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es salaam mapema leo asubuhi.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya akitoa salamu kwa niamba ya Makamanda wa Mikoa na Kumkaribisha Mgenia Rasmi Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es salaam mapema leo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke Bi. Bupe Mwakibete (kulia) akimsikiliza Sajini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Lugendo Rashidi (kushoto), alipotembelea Banda la kutolea elimu, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es salaam, mapema leo. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji Makao Makuu)

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MEI MOSI YAPAMBA MOTO SOKOINE MBEYA

Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu  Jenista Mhagama amekagua maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi na kusema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa.

Ametoa kauli hiyo Aprili 29, 2019 baada ya kupokea taarifa ya mbalimbali za Kamati ya Maandalizi walipokutana kujadili na kupanga mipango katika kuelekea kilele cha sherehe hizo zinazotarajiwa kuadhimishwa katika Viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya.

Waziri amesema Kamati ya Mkoa kwa kushirikiana na Ofizi yake imeendelea na maandalizi hayo na kuendelea kutoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kufika kwa wingi katika viwanja hivyo siku ya tarehe 1 Mei, 2019.

“Hadi sasa maandalzi yamefikia hatua nzuri na watu wanafanya kazi kwa umoja ili kuhakikisha shughuli hii inafana, wito wangu wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kuunga mkono wafanyakazi wa Tanzania katika siku yao hii muhimu.”Alisema waziri Mhagama.

Waziri aliwataka wanakamati hao wahakikishe wanasimamia vizuri wageni, pamoja na shughuli zote zitakazofanyika uwanjani hapo ili kuhakikisha wanaifikia siku hiyo kwa ushindi mkubwa.

Aidha Waziri aliongezea kuwa, uwepo wa maadhimisho hayo Jijini Mbeya wanachi wayatumie kama fursa ya kimaendeleo kwa kuwa mkoa utapokea wageni wengi hivyo waendelee kuwahudumia vyema.

Aidha kwa Upande wake rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya aliendelea kuhamasisha wananchi hususan wafanyakazi wote kujitokeza kwa wingi kuja kuiadhimisha siku hiyo.

 “Ni wakati sahihi kwa wafanyakazi wote nchini kuitumia siku hii maalum katika kuiadhimisha na kuienzi ikiwa ni sherehe ya upekee sana hivyo mjitokeze kwa wingi pamoja na wananchi wote kwa ujumla.”Alisisitiza Nyamhokya.

Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi yatahadhimishwa Kitaifa katika Mkoa wa Mbeya ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, aidha maonesho hayo yatapambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo; Maandamano ya wafanyakazi na magari, Kwaya maalum, Nyimbo maalum kutoka kwa Vyama vya Wafanyakazi, wimbo maalum kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya, vikundi vya ngoma kutoka mikoa mbalimbali, Nyimbo maalum kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Kauli mbiu ya maonesha ya mwaka huu inasema; “Tanzania ya Uchumi wa Kati Inawezekana, Wakati wa Mishahara na Masilahi Bora kwa Wafanyakazi ni SASA”
2
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akizungumza jambo kwa kamati ya maaandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya Wafanyakazi za Mei Mosi walipokutana nao kukagua maandalizi hayo katika Viwanja vya  Sokoine Jijini Mbeya Aprili 29, 2019.
3
 Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akichangiua jambo wakati wa kikao hicho.
4
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
5
 Mjumbe Kamati ya Utendaji CWT Mwalimu Joyce Julius akichangia jambo katika kikao cha maandalizi ya sherehe za Mei Mosi kilichofanyika katika Viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya aprili 29, 2019.
6
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akiangalia mazingira ya uwanja wa Sokoine utakaotumika kwa ajili ya Maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi kitaifa Jijini Mbeya alipokutana na kamati ya maandalizi ya sherehe hizo.
7
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama pamoja na wajumbe wa kamati wakiwa katika ukaguzi wa maadalizi ya sherehe za Mei Mosi katika viwanja vya Sokoine Mkoani Mbeya.
8
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na kamati hiyo wakiangalia mtaro unaopitisha maji katika viwanja vya Sokoine ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kufikia Kilele cha Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) Jijini Mbeya.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

MAKATIBU WAKUU TANZANIA NA UGANDA WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO

Katibu Tawala Mkoa wa kagera Profesa Faustin Kamuzora akizungumza wakati wa mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera, wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe, kushoto ni Balozi Paul Mkumbya kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda na kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Paul Makelele.
Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika (kulia) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Tanzania wanaoshiriki mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazoikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo Elisante Ole Gabriel na anayemfuatia ni Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe.
Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima (Kushoto) akimsikiliza Mpima Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Julius Msofe (wa pili kulia) wakati wa mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoa wa Kagera. Kulia ni Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha.
Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima (wa tatu Kulia) akizungumza wakati wa kujadiliana na ujumbe wa Uganda katika mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera. Kulia ni Mthamni Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).

Na Munir Shemweta, WANMM BUKOBA

Makatibu Wakuu wa Tanzania na Uganda wanakutana mjini Bukoba mkoani Kagera katika mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi hizo ikiwemo Uimarishaji Mpaka wa Kimataifa pamoja na Matumizi endelevu ya rasilimali za Bonde la mto Kagera..

Mkutano huo wa siku mbili umeanza tarehe 29 April 2019 mjini Bukoba na kuwakutanisha Makatibu Wakuu wa nchi hizo mbili kutoka Wizara za Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mifugo, Wizara ya Maji pamoja na Wizara ya Nishati.

Kabla ya mkutano huo, Wataalamu wa sekta shiriki kutoka Tanzania na Uganda walikutana na kujadiliana kuhusiana na changamoto zinazozikabili nchi hizo mbili kwa nia ya kuwasilisha mapendekezo yaliyofikiwa kwa Makatibu Wakuu wa nchi hizo.

Baadhi ya Changamoto zinazojadiliwa  kwenye mkutano huo, ni pamoja na Uimarishaji na Uthamini wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Uganda, Mpango kabambe wa utunzaji mto Kagera na Matumizi endelevu ya rasilimali kati ya Tanzania na Uganda katika Bonde la Mto Kagera.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe alisema mkutano huo ni mfululizo wa mikutano kati ya nchi hizo mbili wenye lengo la kutatua changamoto zinazozikabili nchi hizo kwa nia ya kuleta maendeleo.

Alisema, pamoja na kuwepo changamoto kadhaa lakini Tanzania na Uganda zinaendelea kufurahia mahusiano mazuri yaliyopo kwa kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali yenye lengo la kuleta manufaa kwa nchi na watu wake.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora aliuzungumzia mkutano huo kama njia ya kuzifanya nchi husika kufanya kazi pamoja na kuzidisha ushirikiano wenye nia ya kuleta maendeleo na kusisitiza kuwa, utekelezaji wa makubaliano yatakayofikiwa unapaswa kufanywa kwa wakati.

WAZIRI MKUU AZINDUA MAABARA YA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA

PMO_9195
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza, katika mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka taasisi zinazofanya uhakiki na upimaji bidhaa nchini zijirekebishe na ziongeze kasi ya utoaji matokeo kwa wateja.
“Kumekuwa na malalamiko kutoka mipakani juu ya bidhaa zinazochukuliwa ili zikapimwe kwamba zinachukua muda mrefu. Punguzeni urasmi huo ili kufanya sekta ya biashara iweze kwenda kwa haraka zaidi. Tume yako (TAEC), TBS na TFDA ni miongoni mwa taasisi zinazolalamikiwa na wawekezaji na wafanyabiashara. Tumieni fursa hii kujirekebisha na kuharakisha utoaji wa matokeo,” amesema.

PMO_9201
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Meneja Muandamizi wa Kituo cha Kimataifa cha Sayansi na Teknolojia na Mshauri wa Masuala ya Kidiplomasia (ISTC), Dkt. Kamen Velichkov, baada ya kufungua mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Aprili 29, 2019) wakati akizindua maabara ya Maabara ya kisasa ya Teknolojia ya Nyuklia ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (Tanzania Atomic Energy Commission -TAEC) iliyopo Njiro, jijini Arusha.
“Nafahamu kuwa hii Tume inafanya kazi kwa karibu na bandari vituo vya mipakani ili kudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini. Naamini kuanzia sasa mtaharakisha upimaji wa bidhaa na vifaa na kutoa majibu ya vipimo haraka,” amesema.

PMO_9251
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe wakati alipozindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu ameitaka Bodi na Menejimenti ya Tume, waendelee kubuni na kuibua miradi mingine zaidi ya matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia. “Angalieni uwezekano wa kuanzisha kinu cha utafiti kinachotumia teknolojia ya nyuklia (Research Reactor); mtambo wa kuongeza thamani na ubora wa vitu mbalimbali ikiwemo matunda na mazao mbalimbali (multi-purpose irradiator); na mtambo wa kuzalisha dawa za kuchunguza na kutibu maradhi ya saratani (accelerator).”
 
PMO_9256
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wakati alipozindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.

Amesema kwa kufanya hivyo, maabara hiyo na watumishi wake wataongeza mchango wa teknolojia ya nyuklia kwenye ustawi wa jamii na ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Amesema anatambua kwamba Tume ya Nyuklia Tanzania inakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo uhaba wa wafanyakazi na ufinyu wa bajeti ya ujenzi wa maabara awamu ya pili. “Serikali inazichukua changamoto hizo na itaendelea na juhudi za kuzitafutia ufumbuzi kadiri hali ya kiuchumi itakavyoruhusu,” amesema.

PMO_9289
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa kifaa cha kupimia mionzi na Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi, Dkt Firm Banzi, baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.

Waziri Mkuu ameishukuru Jumuiya ya Ulaya kwa msaada wa vifaa vya maabara hiyo vyenye thamani ya Euro milioni 2.2 (sawa na sh. bilioni 7.5) na kwamba Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano katika sekta mbalimbali.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu ameiagiza Bodi na uongozi wa Tume hiyo wawapandishe vyeo watumishi watatu wa tume hiyo ambao aliwapa vyeti na zawadi ya sh. milioni moja kila mmoja kwa kukataa rushwa na kutokubali vitisho walivyopewa.

PMO_9340
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa kifaa cha kupimia vifaa vya kupimia mionzi na Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi, Dkt Firm Banzi, baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.

“Nimefurahi sana kuona watumishi watatu ambao ni wazalendo na wamekataa kupokea rushwa au kukubali vitisho walivyokuwa wakipewa na kuamua kusimamia misingi ya kazi zao. Hii zawadi mliyowapa haitoshi.”
“Watumishi hawa ni mfano wa kuigwa na wengine. Mwenyekiti wa Bodi waongeze fedha nyingine kila mmoja sh. milioni mbili ili jumla iwe milioni tatu na wapandishwe vyeo huko waliko ili iwe motisha zaidi kwao. Sijui muundo wenu ukoje, lakini nataka nipate taarifa ya utekelezaji wa haya maamuzi kesho kutwa, baada ya Mei mosi,” amesisitiza.

PMO_9357
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akimkabidhi cheti na pesa kwa kutambua uaminifu wao kwa Mtafiti wa Mionzi Daraja la Pili, Machibya Matulanya baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu awape vyeti na zawadi, Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Najat Mohamed aliwataja watumishi hao kuwa ni Machibya Matulanya wa kituo cha Mtwara na mpaka wa Kilambo (Tanzania) na Msumbiji; Patrick Simpokolwe na Geofrey Kalolo wa kituo cha Tunduma (Tanzania) na Zambia.
Machibya Matulanya ambaye cheo chake ni mtafiti wa mionzi daraja la pili (Radiation Health Physics Research Officer II) amekuwa akitegewa mitego ya rushwa na kupokea vitisho kutoka wa wafanyabiashara na watumishi wa Serikali.

PMO_9379 PMO_9388 PMO_9391
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
…………………….
Patrick Simpokolwe ambaye cheo chake ni mkaguzi wa usalama wa mionzi daraja la pili (Radiation Safety Inspector II) na Geofrey Kalolo ambaye ni mtumishi wa kujitolea (volunteer) naye pia anafanya kazi kama mkaguzi wa usalama wa mionzi daraja la pili. Wote kwa pamoja walipokea vitisho walipozuia mzigo kutoka Zambia wenye thamani ya zaidi ya milioni 20 usiingizwe nchini.

Monday, April 29, 2019

WAZIRI WA ELIMU AFANYA UKAGUZI WA HATUA ZA MAANDALIZI YA UWEKAJI JIWE LA MSINGI JENGO LA CHUO KIKUU MZUMBE KAMPASI YA MBEYA

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako leo ametembelea na kukagua hatua za maandalizi ya ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya, ambapo amepongeza Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa hatua za ujenzi ulipofikia.

Akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Pro. Lughano Kusiluka, Prof Ndalichako amemwelekeza Mkandarasi wa Ujenzi kuhakikisha kufikia Juni 2019 ujenzi wa Jengo hilo kuwa umekamilika kama ilivyopangwa.

Kukamilika kwa ujenzi kutawezesha jumla ya wanafunzi 900 kupata vyumba vya madarasa mbali na kumbi za mikutano na ofisi za uendeshaji. Jengo hilo linatarajiwa kuwekwa jiwe la Msingi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Joseph Magufuli Mei 1, 2019.
IMG-20190427-WA0048 
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akiongozwa na Mkandarasi wa mradi akikagua vyuma vya madarasa mara alipowasili kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa tano la Taaluma na Utawala linalotazamiwa kumalizika mwezi Juni,2019. Pamoja naye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka, Naibu Mawakamu Mkuu wa Chuo Utawala na fedha Prof. Ernest Kihanga na wasimamizi wa ujenziIMG-20190427-WA0061Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiweka saini kwenye kitabu cha wageni kwenye eneo la ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya mbeya mara tu baada ya kuwasili. Aliyeshika kitabu ni Injiani Thadeus Koyanga na kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka ( Mwenye Kaunda suti kushoto)IMG-20190427-WA0066 Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (kushoto) akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka ( Mwenye Kaunda suti kushoto) pamoja na Mkandararasi na wajenzi; wakikagua ramani ya jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya.IMG-20190427-WA0044 Profesa Ndalichako (katIkati) akikagua mahali litakapojengwa jiwe la msingi ambalo litawekwa rasmi na Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muuungano wa Tanzania Dr.John Pombe Joseph Magufuli Mei 1, 2019. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka na kulia ni Mkadarasi wa Ujenzi Injinia Thedeus Koyanga (mwenye shati la mikono mirefu) akifuatiwa na Profesa Ernest Kihanga Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.IMG-20190427-WA0067Mhe. Profesa Joyce Ndalichako alikagua muonekano wa nje wa jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya pamoja na kukagua usafi wa mazingira, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi kabla Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli hajafika kuweka jiwe la msingi.

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI AFANYA MABADILIKO YA BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA

KAMISHNA%2BJENERALI%2BWA%2BJESHI%2BLA%2BZIMAMOTO%2BNA%2BUOKOAJI%252C%2BTHOBIAS%2BANDENGENYE
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, (CGF) Thobias Andengenye, amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa hapa nchini.

Makamanda walioguswa na mabadiliko hayo ni Kamishna Msaidizi wa Zimamoto (ACF) Mohamed Kondo, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya.

Kamishna Msaidizi (ACF) Juma Yange, aliyekuwa Kitengo cha Utawala Mkoa wa Kinondoni, anakuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kizimamoto Kinondoni.

Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) John Francis, aliyekuwa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Handeni Mkoani Tanga, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Rukwa.

Vilevile, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma, Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) Athumani Basuka, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Hai – Siha, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Jumbe Juma.

Pia aliyekuwa Kamanda wa Kiwanja cha Ndege Mkoa wa Iringa, Mkaguzi wa Zimamoto (INSP) Hamisi Dawa, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera. 

Mabadiliko haya ni ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea kutoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Makamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mikoa na Wilaya katika suala la Kinga na Tahadhari Dhidi ya majanga.

Imetolewa na;
Joseph Mwasabeja – (INSP)
Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Makao Makuu.

IGP SIRRO AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI IRINGA

1
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kulia)  akizugumza jambo na kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Wilbrod Mutafungwa aliyekutananae mkoani humo wakati akiwa njiani kuelekea mikoa ya Iringa na Njombe kwa ziara ya kikazi.
2
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kushoto) akipokea salamu ya heshima ya kijeshi wakati alipowasili Leo katika mkoa wa Iringa kwa ziara ya kikazi  ya siku moja yenye lengo la kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari pamoja na utendaji wao wa kazi za Polisi. . 
3
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kulia)  akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi (kushoto) wakati alipomtembelea ofisini kwake leo mkoani humo akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari pamoja na utendaji wao wa kazi za Polisi, aliyepo katikati ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire. Picha na Jeshi la Polisi.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIWIRA PAMOJA NA KUFUNGUA KIWANDA CHA MAPARACHICHI KILICHOPO RUNGWE MKOANI MBEYA

1
3
4
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Uyole nje kidogo ya jiji la Mbeya wakati akiwa njiani kuelekea Wilayani Rungwe.
7
 Wananchi wa Kiwira wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo hilo.
5
6
8
9
10
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kiwira Wilayani Rungwe wakati aliposimama kuwasalimia.
12
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Mkoa wa Mbeya, Mawaziri, Wabunge akikata utepe kufungua kiwanda cha Maparachichi cha Rungwe Avocado Campany mkoani Mbeya.
13
 18
19
15
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maparachichi yanayohifadhiwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi katika kiwanda cha Rungwe Avocado Campany mkoani Mbeya. 
17
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mashine maalumu ya kuangalia ubora wa maparachichi katika kiwanda cha Rungwe Avocado Campany mkoani Mbeya.
16
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi pamoja na wananchi katika eneo la kiwanda cha cha Rungwe Avocado Campany mkoani Mbeya. PICHA NA IKULU