Matokeo chanyA+ online




Saturday, November 30, 2019

WAZIRI MKUU AFUNGUA MSIKITI WA HAQ KIONGA MAGOMENI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, wakati aliwasili kwenye Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, ambao ameufungua rasmi, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, wakati aliwasili kwenye Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, ambao ameufungua rasmi, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwakilishi wa Mufti wa Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa na Sheikh Hamid Jongo, kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, kabla ya kuufungua rasmi, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Waumini wa Kiislamu, kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waumini wa Kiislamu, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati  akiwahutubia kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waumini wa Kiislamu, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati  akiwahutubia kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kufungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wakati akifungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wakati akifungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisikiliza mawaidha kwenye swala ya Ijumaa, baada ya kufungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS MAGUFULI ATOA POLE KWA FAMILIA YA MZEE SUGWA ALIYEFIWA NA MKEWE BI. SABINA NDEGE KILANDA NA MWANAE SHIJA SUGWA , CHATO MKOANI GEITA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za mwisho katika kaburi la Bi. Sabina Ndege Kilanda Mke wa Mzee Sugwa aliyefariki duni Septemba 15, 2019 katika kijiji cha Katende Wilayani Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli ametoa pole
kwa Mzee Sugwa kufuatia kifo cha Mkewe pamoja na Mwanae Shija Sugwa.
PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kaburi la Bi. Sabina Ndege Kilanda Mke wa Mzee Sugwa aliyefariki duni Septemba 15, 2019 katika kijiji cha Katende Wilayani Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli ametoa pole kwa Mzee
Sugwa kufuatia kifo cha Mkewe pamoja na Mwanae Shija Sugwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea Makaburini kwaajii ya kutoa heshima zake mwisho kwenye kaburi la Bi. Sabina Ndege Kilanda Mke wa Mzee Sugwa aliyefariki duni Septemba 15, 2019 katika kijiji cha Katende Wilayani Chato mkoani
Geita. Rais Dkt. Magufuli ametoa pole kwa Mzee Sugwa kufuatia kifo cha Mkewe pamoja na Mwanae Shija Sugwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama Makaburi ya Familia ya Mzee Sugwa mara baada kutoa heshima za mwisho kwenye kaburi la Bi. Sabina Ndege Kilanda Mke wa Mzee Sugwa aliyefariki duni Septemba 15, 2019 katika kijiji cha Katende
Wilayani Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli ametoa pole kwa Mzee Sugwa kufuatia kifo cha Mkewe pamoja na Mwanae Shija Sugwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waombolezaji nyumbani kwa Mzee Sugwa kijiji cha Katende Wilayani Chato mkoani Geita aliyefiwa na Mwanae Shija Sugwa,pia alimtembelea na kutoa pole kwa kufiwa na Mkewe Marehemu Bi. Sabina Ndege Kilanda aliyefariki dunia Septemba 15, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bi. Beatrice Masanilo aliyefiwa na mumewe walipokutana nyumbani kwa Mzee Sugwa kijiji cha Katende Wilayani Chato mkoani Geita, alipomtembelea na kutoa pole kwa kufiwa na Mkewe Marehemu Bi. Sabina Ndege Kilanda aliyefariki dunia Septemba 15, 2019 na mwanae Shija Sugwa.
 

Wednesday, November 27, 2019

MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI ATOA POLE KWA FAMILIA YA BORAFIA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema vyombo vya Dola kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zilizopo wakati wote hubeba dhima ya kufanya uchunguzi dhidi ya hujuma zinazoibuka na hatimae kuleta hatari ya uvunjifu wa Amani ndani ya Jamii.
Alisema uchunguzi wa hujuma zozote zile pale unapokamilika na kupatikana ushahidi kamili vyombo hivyo havitasita  kuchukuwa hatua za kisheria katika kutoa haki kwa muhusika.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi atoa pole kwa Familia ya Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Mzee Borafia Silima Juma kufuatia Nyumba yake kuwaka moto na kuteketeza vitu vyote vilivyomo ndani hapo Mtaa wa Muembe Rikunda nyuma ya Jumba Nambari Mbili Michenzani.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara fupi ya kuipa pole Familia ya Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Mzee Borafia Silima Juma kufuatia Nyumba yake kuwaka moto na kuteketeza vitu vyote vilivyomo ndani hapo Mtaa wa Muembe Rikunda nyuma ya Jumba Nambari Mbili Michenzani.
Balozi Seif alisema Wananchi wanapaswa kuendelea kufuata Sheria na taratibu zilizopo Nchini kwa kuviamini vyombo vya Dola  vilivyopewa jukumu kubwa na Serikali la kulinda Mali na Maisha yao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliitaka Familia ya Mzee Borafya kuwa na subra katika kipindi hichi cha mpito kufuatia mtihani uliowapata na kuithibitishia kwamba Serikali itaangalia utaratibu wa kuihami Familia hiyo kutokana na mazingira halisi ya Nyumba hiyo ilivyo hivi sasa.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed alisema utafiti wa awali uliofanywa na Wataalamu wa Kamisheni ya kukabiliana na Maafa Zanzibar muda mfupi baada ya tukio hilo umebaini kwamba huo ulikuwa ni moto wa kutiwa kwa makusudi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi atoa pole kwa Familia ya Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Mzee Borafia Silima Juma kufuatia Nyumba yake kuwaka moto na kuteketeza vitu vyote vilivyomo ndani hapo Mtaa wa Muembe Rikunda nyuma ya Jumba Nambari Mbili Michenzani.
Waziri Aboud alisema Wataalamu hao hivi sasa wanaendelea na uchambuzi wa kina wa utafiti wa tukio hilo na baadae kuona jinsi gani Kamisheni hiyo inaweza kuisaidia Familia hiyo kwa njia za Kitaalamu.
Mapema Mmoja wa Wanafamilia wa Nyumba hiyo Bwana Salum Borafia Silima alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Wanafamilia hao wanaamini kwamba tukio hilo ni hujuma ya makusudi kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha saa Ishirini na Nne.
Bwana Salum alisema hujuma ya kwanza ilitokea Jumamosi majira ya saa moja ya Usiku  pale Mmoja miongoni mwa Wanafamilia hao ambae ni mgonjwa alipobaini harufu ya moshi dirishani na kupiga kelele zilizosaidia kubaini moto huo ambao uliunguza waya na pazia la Dirisha hilo.
Alisema tukio hilo likatokea tena Siku ya Pili ya Jumapili muda unaolingana ambalo ni kubwa zaidi lililopelekea moto mkubwa kuripuka na kusababisha kuunguza kila kilichomo ndani ya Nyumba hiyo ambapo baadae akalazimika kutoa Ripoti kituo cha Polisi kwa hatua zinazofaa.

Tuesday, November 26, 2019

WAZIRI JENISTA MHAGAMA ATANGAZA PUNGUZO LA BEI UNUNUZI WA NYUMBA ZA PSSSF ZA BUYUNI-CHANIKA JIJINI DAR ES SALAAM



Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb), (wapili kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe (wakwanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba walipotembelea mradi wa nyumba za bei nafuu za PSSSF huko Buyuni-Chanika jijini Dar es Salaam
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
Waziri  wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb), ametangaza punguzo la bei kwa karibu asilimia  50 kwa atakayehitaji kununua nyumba  zilizo katika mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazomilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) huko Buyuni-Chanika jijini Dar es Salaam.
Mheshmiwa Waziri ametangaza uamuzi huo wa Serikali wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili kutembelea vitegauchumi vinavyomilikiwa na Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Novemba 26, 2019 katika eneo la Mradi ambapo nyumba zilizoingia kwenye punguzo hilo ziko 480.
Akitoa mchanganua wa bei mpya Mhe. Waziri alisema, nyumba yenye vyumba viwili vya kawaida awali iliuzwa kwa shilingi milioni 66.80, sasa itauzwa kwa shilingi Milioni 36.58, nyumba ya vyumba vitatu vya kawaida awali iliuzwa kwa shilingi Milioni 67.260 na sasa itauzwa kwa shilingi Milioni 41.30.
Nyumba yanye vyumba viwili vya kawaida na Master Bedroom ilikuwa inauzwa shilingi Milioni 74.340 na sasa itauzwa Shilingi Milioni 46.20, aidha nyumba yenye vyumba vitatu na Master Bedroom iliyokuwa ikiuzwa shilingi Milioni 83.780 na sasa itauzwa kwa shilinhgi Milioni 61.360.
“Naielekeza Bodi na Menejimenti kuanzia leo (jana Novemba 26, 2019) ninapotoa tamko hili, nyumba hizo zote 204 ambazo hazijapata wanunuzi kabisa na zile 276 ambazo malipo yake yalikuwa bado hayajakamilika ambazo wafanyakazi walikuwa hawawezi kulipa hizo bei za mwanzo, nyumba hizo zote ziingie katika bei niliyotamka leo kwa niaba ya Serikali.” Alisisitiza na kuongeza……
“Baada ya kuona ununuzi wa nyumba hizo si wa kuridhisha, Menejimenti ya Mfuko imenifahamisha juu ya juhudi mbalimbali zilizofanywa kwa maelekezo ya Bodi ya Wadhamini wa Mfuko, na hatua hizi zililenga kupata njia bora ya kuuza nyumba hizi, kwani lengo kuu lilikuwa ni kujenga na kuuza nyumba kwa watumishi na watanzania kwa ujumla na sio kukaa nazo kama sehemu ya uwekezaji wa Mfuko.” Alifafanua Mhe. Waziri Jenista Mhagama.
Mheshimiwa Waziri   alisema uamuzi huo wa serikali unatokana na ripoti ya Mthamini Mkuu wa Serikali baada ya kukamilisha tathmini na thamani halisi ya nyumba hizo kwa sasa.
"Nilipata taarifa kuwa katika mradi huu walikuwepo madalali kuanzia sasa hakuna haja ya kuwa na madalali kwani Mlango uko wazi kwa watu binafsi watakaohitaji kununua nyumba hizi kwani na wao ni watanzania wenzetu, 
Waziri  wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) (katikati) akitangaza punguzo hilo la bei Novemba 26, 2019., Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe na kulia na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF, Bw. Aggrey Mlimuka.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe, (aliyesimama), akizungumza kabla ya Mheshimiwa Waziri kutoa tamko hilo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF, Bw. Aggrey Mlimuka akitoa maelezo ya awali kabla Mhe. Waziri kutangaza punguzo hilo la bei.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kw aWatumishi wa Umma, (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba akitoa maelezo kuhusu mradi huo.
 Rais wa Shirimkisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw., Tumaini Nyamhokya akizungumza.
Wakazi kwenye nyumba hizo wakimsikiliza Mhe. Waziri
Moja ya nyumba zilizofanbyiwa punguzo kubwa la bei

 Waziri Mhagama na Katibu Mkuu, Bw. Massawe, wakitembelea moja ya nyumba hizo Novemba 25, 2019.
 Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akisalimiana na mmoja wa wakazi kwenye nyumba hizo za mradi wakati alipofanya ziara ya kutembelea mradi huo Novemba 25, 2019.
 Moja ya nyumba zilizofanbyiwa punguzo kubwa la bei
 Maofisa wa PSSSF wakipitia taarifa mbalimbali kuhusiana na mradi huo.

SERIKALI HAINA MZAHA UMEME UTAFIKA KOTE - WAZIRI DKT. KALEMANI

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akizungumza na wananchi wa kijiji cha Musasa, kilichopo wilayani Chato, alipofika kuwasha rasmi umeme, Novemba 23, 2019.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli haina mzaha katika kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi na kwamba itafikisha umeme katika vijiji vyote nchini ifikapo mwisho wa Desemba mwaka huu kama ilivyoahidi.

Aliyasema hayo kwa nyakati tofauti, Novemba 23, 2019 wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Musasa na Mutundu, vilivyopo wilayani Chato, Mkoa wa Geita.
“Nafahamu kiu ya umeme mliyonayo wananchi. Tafadhali muiamini Serikali yenu. Umeme utawafikieni nyote kama tulivyoahidi.”
Diwani wa Kata ya Butengolumasa, wilayani Chato, Jeremia Mswanzali, akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (Meza-Kuu, kulia), kwa kuwasha rasmi umeme katika kijiji cha Mutundu, Novemba 23, 2019.

Akitoa mfano kuthibitisha namna serikali inavyochapa kazi ili kutimiza ahadi zake, hususan katika kuwapelekea umeme wananchi; Waziri Kalemani alisema kwa Wilaya ya Chato yenye jumla ya vijiji 115, tayari vijiji 101 vimeunganishwa kutoka vijiji 9 tu vilivyokuwa na nishati hiyo mwaka 2015.

Alisema kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha vijiji vyote vya Tanzania Bara vikiwemo vya Chato vinakuwa na umeme ifikapo mwisho wa mwezi Desemba mwaka huu.
Aidha, Waziri Kalemani aliwasha umeme katika Zahanati ya Kijiji cha Mutundu, Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Musasa pamoja na Mradi wa Maji katika eneo hilo huku akisisitiza maelekezo ya serikali kuwa kipaumbele cha umeme vijijini ni kwa Taasisi za Umma ili kuziwezesha kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mutundu wilayani Chato, Loice Katologo (kushoto), akimkabidhi Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, risala iliyoandaliwa na wananchi wa kijiji hicho na kusomwa kwake (Waziri) katika hafla ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji hicho, Novemba 23, 2019.
Aliwataka wananchi kulinda miundombinu ya umeme katika maeneo yao kwani kuihujumu kwa namna yoyote ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa maisha yao.
Vilevile, aliendelea kusisitiza wananchi waliofikiwa na miundombinu ya umeme katika maeneo yao, kulipia gharama za kuunganishiwa nishati hiyo na waachane na kasumba iliyozoeleka na wengi kuwa wanasubiri nguzo kwani hilo siyo jukumu la mwananchi.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akizungumza na wananchi wa kijiji cha Musasa, kilichopo wilayani Chato, alipofika kuwasha rasmi umeme, Novemba 23, 2019.
Kwa upande wao, viongozi wa vijiji husika akiwemo Diwani wa Kata ya Butengolumasa, Jeremia Mswanzali, walitoa pongezi nyingi kwa Rais Magufuli na Waziri Kalemani kwa jitihada wanazofanya kuwapelekea wananchi wanyonge maendeleo hususan umeme vijijini.Veronica Simba - Geita

AGIZO LA RAIS DKT. JOHN MAGUFULI LATEKELEZWA SUMBAWANGA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewapongeza madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa kuweza kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa tarehe 6, Oktoba 2019 alipokuwa katika ziara yake ya siku 3 ambapo aliiagiza halmashauri hiyo kuhamia Laela pamoja na halmashauri nyingine nchini kuhamia katika maeneo yao ya kiutawala. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa pongezi zake kwa Madiwani na Watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga katika baraza la madiwani lililofanyika katika mji wa Laela.
Amesema kuwa ni watumishi 16 tu kati ya watumishi 165 wa makao makuu ya halmashauri wanaotumia mifumo ya watumishi (LAWSON), mfumo wa mapato LGRCIS), Mfumo wa malipo wa EPICOR, TASAF na Kitengo cha Uchaguzi ndio waliobaki mjini wakisubiri miundombinu hiyo kukamilika katika makao mapya ya halmashauri hiyo katika Mamlaka ya mji mdogo wa Laela.
“Nitoe maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kushirikiana na Wadau wengine (Mfano TTCL) ahakikishe anaunganisha Makao Makuu Mapya ya Halmashauri Laela kwenye Mkongo wa Taifa.  Hii itawezesha Mifumo mingine inayotumia Mtandao wa mawasiliano kuweza kufanya kazi kutokea hapa hapa Laela.  Ninamuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha Watumishi ambao bado hawajahamia Laela wawe wamehamia ifikapo tarehe 1 Januari, 2020.” Alisema.
Aidha, ameitaka menejimenti ya halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wadau kufanya tathmini juu ya kuwafikia wananchi waliopo mbali na Laela kama vile kutoka katika vijiji vya mfinga, Mwadui, Kalumbaleza wanaokwenda kupata huduma Laela ambao wanatoka umbali wa zaidi ya kilometa 150.
Ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani la kwanza kufanyika katika makao makuu hayo mapya ya halmashauri hiyo tarehe 21.11.2019, kikao kilichohudhuriwa na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa, madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri.
Awali akitoa taarifa ya maandalizi ya kuhamia katika makao hayo mapya Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule alisema kuwa kitengo cha uchaguzi kimebaki mjini kutokana na kukosekana kwa eneo kubwa la kuhifadhia vifaa vya uchaguzi lakini mara tu uchaguzi utakapopita kitengo hicho kitahamia katika mji wa Laela.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (katikati waliokaa) Katika Picha ya pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga pamoja na viongozi wengine.
“Kwahiyo Wakimaliza uchaguzi wakiandaa ile taarifa tutahakikisha nao wanahamia haa Laela, Watu wa Fedha na watu wa Utumishi wanawasiliana na watu wa TTCL ili mokongo ule wa taifa uweze kupatikana hapa Laela na zile huduma zao ziweze kuhamia hapa Laela, kwa ujumla shughuli zinaenda vizuri na wananchi wanaendelea kuhudumiwa vizuri hapa Laela,” Alisema.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Apolinari Macheta alisema kuwa watumishi wa halmashauri hiyo walikuwa wakishiriki usafi wa Jumamosi ya mwisho wa mwezi katika eneo ambalo halikuwa la kwao na pia walikuwa wakichangia maendeleo katika maeneo ambao sio ya kwao.
“Tulichelewa sana na ni maamuzi ambayo yangefanyika hata huko nyuma tungeweza kuwa parefu zaidi lakini tunakushukuru sana kwa namna mji wetu wa Laela ulivyo hautofautiani na mji wa sumbawanga na hata kama ni changamoto ni za kawaida haziwezi kufanana na za wengine kwakweli tunaonekana tuko mjini.” Alisema.
Wakati akitoa neno la Shukurani mbunge wa jimbo la Kwela Mh. Ignus Malocha alisema kuwa yeye ndio wa kwanza kutangulia kwani ofisi yake ilikuwa ya kwanza kabla ya Mkurugenzi kuhamia katika mji huo baada ya wiki mbili tu tangu Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa agizo hilo, hivyo alimshukuru mkuu wa mkoa kwa kusimamia zoezi hilo la utekelezaji wa agizo la Rais.

WABUNGE KUTOKA KOREA WATEMBELEA HOSPITALI YA MLOGANZILA

Dkt Magandi katika picha ya pamoja na wabunge walioongozana na mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Bunge la Korea ya Kusini waliokuja kutembelea hospitalini hapa. 
 
Wabunge kutoka Korea wametembelea Mloganzila Wabunge wa Serikali ya Korea ya Kusini wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya afya ya Bunge hilo, leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ili kufahamu huduma zinazotolewa hospitalini hapa.
Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wageni hao, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amewaeleza kuwa hospitali ya Mloganzila ina vifaa tiba vya kisasa na inatoa huduma mbalimbali za afya ambapo kwa siku inahudumia wagonjwa wa nje 400 hadi 450.
 


 Mtaalam wa Maabara katika Hospitali ya Mloganzila, Bw. Mbaruku Kisutu akiwaelezea wageni hao namna wataalam wa maabara wanavyofanya kazi.
 Dkt. Frida Shao kutoka Kitengo cha Magonjwa ya Dharura katika hospitali ya Mloganzila (EMD) akiwaelezea wageni hao kazi zinazofanywa na kitengo hicho.
 
“Hospitali yetu ina vifaa vya kisasa kama vile CT-Scan na MRI pamoja na kutoa huduma kwa wagonjwa ambapo kwa siku tunawahudumia wagonjwa 400 hadi 450,” Amesema Dkt. Magandi.
Aidha Dkt. Magandi amefafanua kuwa lengo la kuanzishwa kwa hospitali kama ya Mloganzila ni ili kupunguza gharama za kupeleka wagonjwa nje ya nchi na badala yake kuimarisha huduma za afya zinazotolewa na wataalam nchini ili kuweza kutibu magonjwa ambayo hapo mwanzo yalihitaji mgonjwa kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
 Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi (kushoto), kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Bunge la Korea ya Kusini, Bw. Kim Se-Youn wakisikiliza utambulisho wa wageni waliofika hospitalini hapa.
 Baadhi ya wabunge waliofika hospitali ya Mloganzila wakisikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa katika kikao hicho.
Mtaalam wa mashine ya CT-Scan, Dkt. Charles Nchimbi akiwaelezea wageni jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Bunge la Korea ya Kusini, Bw. Kim Se-Youn amesema kuwa wamefurahishwa na namna hospitali inavyohakikisha kuwa jamii inayowazunguka inapata huduma bora za afya.
“Tumefurahi sana kuitembelea hospitali hii na tunatumaini kuwa hospitali ya Mloganzila itaendelea kushirikiana na Serikali yetu ya Korea katika kuhakikisha huduma bora za afya zinatolewa kwa watanzania,” Amesema Bw. Kim.

Wageni hao wametembelea kitengo cha magonjwa ya dharura (EMD), radiolojia pamoja na maabara na kujionea namna wataalam wanavyofanya kazi.

Monday, November 25, 2019

SERIKALI YARIDHISHWA NA MAENDELEO MRADI WA MAJI JIJINI ARUSHA UNAOGHARIMU SHILINGI BILIONI 520

Moja ya bomba la Maji likiwa linatoa Maji mengi wakati Wa kusafisha mabomba.
Serikali imesema kuwa imeridhishwa na utekelezaji Wa mradi mkubwa Wa Maji Wa shilingi bilioni 520 unaotekelezwa katika halmashauri ya jiji la Arusha utakao hudumia wananchi .

Akizungumza na Waandishi Wahabari Mara baada ya kukagua miundombinu ya mradi huo ,Mkurugenzi Wa Idara ya usambazaji Wa Maji na Usafi Wa mazingira kutoka Wizara ya Maji ,Nadhifa Kemikimba alisema kuwa amerithishwa na kasi ya ujenzi Wa mradi huo huku akibainisha kuwa nia ya serikali nikuona hadi ifikapo mwaka 2020 upatikanaji Wa huduma za Maji kwa Mjini umefikia asilimia 95% huku vijijini wananchi wanapata Maji kwa asilimia 85%.
 
mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa maelekezo kwa mkandarasi mara baada ya kutembelea moja ya kisima cha maji ya mradi wa shilingi bilioni 520 kilichopo Ngaramtoni ndani ya wilaya ya Arumeru ambapo alimtaka mkandarasi kuhakikisha adi ifikapo November 30 wananchi wawe wameanza kupata maji
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi AUWSA Mhandisi Justine Mwangijomba alisema kuwa mradi huo umefikia hatua ya kusafisha mtandao Wa mabomba yanayopeleka Maji kwenye tanki pamoja na kuweka Maji dawa tayari kabisa kwa ajili ya wananchi kuanza kutumia.

"Kama ulivyoona tumepita katika matanki yetu ya Maji natumeona tanki moja la Lita milioni kumi tumeanza kuweka Maji kwani ujenzi Wa tanki hilo umekamilika hivyo muda sio mrefu wananchi watapata ongezeko la Maji na tutaanza kuwapa wale wenye matatizo ya Maji kama muriet na olasiti" alisema Mwangijomba.
 
Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji AUWSA Mhandisi Justine Mwangijomba akimpa maelekezo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo jinsi maji yanavyoingia katika tanki kubwa la lita milioni 10 ambalo limekamilika na jana november 24 zoezi la usafishaji mabomba kwa ajili ya matumizi ya binadamu ,tanki hilo kubwa lipo mji mdogo wa ngaramtoni ndani ya wilaya ya Arumeru maji haya ni ya mradi wa kiasi cha shilingi bilioni 520 uliotolewa na serikali na yatahidumia jiji zima la Arusha (picha na Woinde Shizza,Arusha).
Mkurugenzi Wa Idara ya usambazaji Wa Maji na Usafi Wa mazingira kutoka Wizara ya Maji ,Nadhifa Kemikimba akiongea na wakandarasi na wafanyakazi Wa AUWSA Mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kutembelea mradi mkubwa Wa shilingi bilioni 520.(picha na Woinde Shizza Arusha) .
 
Akiongelea mradi huo Mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa kuna ujenzi Wa makao makuu ya mamlaka ya Maji safi na Maji taka ambao ulikuwa unasuasua lakini baada ya OFISI yake kwakushirikiana na msimamizi Wa mkandarasi kufatilia kwa makini ujenzi huo umeanza kwenda vizuri

Akibainisha kuwa walipotembelea mradi huo ujenzi ulivyokuwa ukisuasua ulikuwa umefikia asilimia 7.5 lakini baada ya kuusimamia vizuri umeongezeka na kufikia asilimia 10 ambapo alibainisha mbali nakufuatilia mradi huo pia wamempa mkandarasi mashariti ya kufanya Kazi usiku na mchana ,kuwasilisha taarifa za mradi unavyoendelea kila wiki huku akimtaka ajenge kwa kufuata vipimo vinavyotakiwa na katika ubora unaotakiwa 

Kwa upande wake Mkuu Wa wilaya ya Arusha alisema kwamba kumalizika kwa mradi huo kutawasaidia wakazi Wa jiji la Arusha kuondokana na tatizo la Maji .Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha