Matokeo chanyA+ online




Wednesday, September 4, 2019

Watanzania 703 wamejisajili kushiriki Kongomano la Biashara Tanzania na Uganda. (UGTZBusinessForum)


Watanzania 703 Kutoka mikoa 22 Tanzania tayari wamejisajili kushiriki kongomano la Biashara Tanzania na Uganda la tarehe 6 - 7 Septemba 2019 katika ukumbi wa kimatafa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam.
 
Takwimu za Washiriki  kutoka katika mtandao wa Kujisajili wa www.businessforum.biz ,  Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa kuwa na washiriki 588, ukifuatiwa na Mkoa wa Pwani washiriki 19, Mwanza washiriki 11, Songwe na Tanga washiriki 8 kila Mkoa Ikifuatiwa na Mkoa wa Arusha na Kagera wenye washiriki 7 kila mkoa. Mkoa mingine wameomba washiriki chini ya saba.
 
Kutoka Zanzibar washiriki kutoka mikoa miwili wameomba kushiriki Kongamano hilo, Mkoa hiyo ni Mjini Magharibi na Unguja Kaskazini.
 
Vile vile washiriki 17 kutoka Tanzania wameomba kutoka  bila kutaja mikoa wanayotoka. Hivyo kufanya jumla wa Watanzani 703 kuwa wamejisajili Kushiriki Kongamano hilo.
 
Malengo ya waandaaji wa kongamano hilo ilikuwa ni kuwa na Washiriki 1000, Hivyo lengo limefikia kwa kusajili washiriki 703 kutoka Tanzania huku Uganda Ikisajili Washiki 300, Hivyo tukio la usajili limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 100.
 
Katika kongamano hili kunatarajiwa kutakuwa na Nchi mbili, Wakuu wa Nchi (marais) wawili, Mawaziri 30, Vikao vya jumla vinne, Paneli 16, Biashara 250, wataofanya maonyesho 25 na washiriki 1000. 
 
 Mkutano wa Biashara  wa Tanzania na Uganda unawaweka pamoja wafanyabiashara kutoka Uganda na Tanzania, wachambuzi wa mambo, wachumi, wataalamu wa sheria, mashirika ya kimataifa, mashirika ya kitaifa, washirika wa maendeleo na taasisi za habari.
 
#UGTZBusinessForum2019 #UGTZBusinessForum #TZUGBusinessForum #TZUGBusinessForum2019
x

Tuesday, September 3, 2019

Afisa Mtendaji Kata ndiye Muwakilishi wa rais ngazi ya Kata



Mhe. Rais Magufuli amewataka Watendaji wa Kata kutowanyanyasa wananchi hasa wanyonge, kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na taratibu na kuhakikisha wanawatembelea wananchi ili kusikiliza na kutatua kero zao badala ya wananchi hao kusubiri mpaka watembelewe na viongozi wa Kitaifa. #AfisaMtendajiKata2019

Mratibu wa Kongamano la Biashara Tanzania Uganda #TZUGBusinessForum


Kongamano la Biashara Tanzania Uganda #TZUGBusinessForumKutokana na umuhimu wa kongamano hilo la kibiashara, (Tarehe 6 n 7 Septemba 2019 JNICC) Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imejipanga vyema kuhakikisha kongamano hilo linakuwa na tija na ushiriki wa Watanzania unakuwa mkubwa zaidi
Naomba nitoe rai kwa wafanyabishara na wawekezaji na wote wanaojihusisha na sekta ya :-
Biashara 
Wachambuzi wa mambo,
Wachumi,
Wataalamu wa sheria,
Mashirika ya kimataifa,
Mashirika ya kitaifa,
Washirika wa maendeleo na Taasisi za habari waliopo nchini Tanzania kuhakikisha wanashiriki kikamilifu na kwa vitendo katika kongamano la #UGTZBusinessForum

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI LEO


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Agustine Ndugai akitoa taarifa ya kuanza kutumia mfumo wa Tehama badala ya badala ya mfumo wa makaratasi katika kuwasilisha orodha ya shughuli za bunge wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.
Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Agustine Ndugai wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kula kiapo wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Kutoka kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adeladus Kilangi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako(kushoto) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (katikati) wakifurahia jambo wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akijibu swali wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa akifafanua jambo walipokuwa akijibu swali katika Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ulinzi, Mhe. Mussa Hassan Zungu akiwasilisha Azimio la Bunge la kupmpongeza Mhe. Rasi Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na kuendesha vyema Mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo wakati wa Mkutano wa 16, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Boniphace Simbachawene (aliyesimama) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga ambaye pia ni Waziri wa Zamani wa Ofisi hiyo, Mhe. Januari Makamba (wapili kushoto) walipokutana katika Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Kulia ni Mbunge wa Kibaha, Mhe. Sylivester Koka. Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akiuliza swali la nyongeza wakatiwa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo tarehe 3 Septemba 2019 jijini Dodoma. Mbunge huyo ameapishwa leo baada ya kupita bila kupingwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika kutokana na nafasi kuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kukosa sifa ya kuendelea na Ubunge. Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki waliomsindikiza Mbunge wao Mhe. Miraji Mtaturu kushuhudia hafla ya kuapishwa kwake wakipunga mikono baada ya kutambulishwa Bungeni katika Mkutano wa 16 wa Bunge kikao cha kwanza leo tarehe 3 Septemba 2019 jijini Dodoma. Mhe. Mtaturu amesindikizwa na zaidi ya wananchi 200 kutoka jimboni kwake. (Picha na Idara ya Habari – MAELEZO)

DK.SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA UJENZI,MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji katika mkutano wa utekelezaji wa  mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,Picha na Ikulu. 03/09/2019.
 Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Sira Ubwa Mamboya (katikati) alipokuwa akisoma muhtasari  wa utekelezaji wa  mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 wa Wizara hiyo katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,(kushoto) Naibu Waziri wa Wizara hiyo  Mohamed Ahmed Salum  na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Kaimu Katibu Kiongozi Salum Maulid Salum (kulia)
 Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji wakiwa katika mkutano wa utekelezaji wa  mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) Picha na Ikulu. 03/09/2019.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji katika mkutano wa utekelezaji wa  mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar, Picha na Ikulu. 03/09/2019.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Kaimu Katibu Kiongozi Salum Maulid Salum (kulia) alipokuwa akichangia katika mkutano wa  utekelezaji  wa  mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,(katikati) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Sira Ubwa Mamboya na Naibu wake Mohamed Ahmed Salum  .Picha na Ikulu. 03/09/2019.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KUAGA MWILI WA KADUMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Sept 03,2019 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu Ibrahim kaduma. 
 
Katika salam zake za pole kwa Wanafamilia, wafiwa na Watanzania wote kwa Ujumla, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaomba kuwa na Subira na Uvumilivu katika kipindi hiki cha Maombolezo na kumuomba Mwenyezi Mungu kuwapa nguvu na Moyo wa Subira.

Wakati wa Uhai wake Marehemu Ibrahim Kaduma aliwahi kuwa Mwanasiasa pamoja na kupitia ngazi mbali mbali za Uongozi hapa nchini.
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu Ibrahim Kaduma katika Kanisa la KKKT Makongo Juu leo Sept 03,2019 ambapo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Msiba huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisani kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Mwanasiasa Mkongwe nchini Marehemu Ibrahim Kaduma alipowasili katika Kanisa la KKKT Makongo Juu kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa huyo leo Sept 03,2019. Kushoto ni Dkt. Alex Malasusa Askofu wa KKKT Dayosis ya Mashariki na Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji, Mjane wa Marehemu Marehemu IBrahim Kaduma katika Kanisa la KKKT Makongo Juu, jijini Dar es salaam leo Sept 03,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Dkt. Alex Malasusa Askofu wa KKKT Dayosis ya Mashariki na Pwani alipowasili katika Kanisa la KKKT Makongo Juu kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu IBrahim Kaduma leo Sept 03,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuwapa pole Baadhi ya Wajukuu na Vitukuu vya Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu IBrahim Kaduma wakati wa shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa huyo leo Sept 03,2019 katika kanisa la KKKT Makongo Juu, Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Msiba huo.

SPIKA NDUGAI AMUAPISHA RASMI MTATURU KUWA MBUNGE SINGINDA MASHARIKI

Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai, leo Jumanne September 3, 2019 amemuapisha Ndugu Miraji Mtaturu kuwa Mbunge wa Singida Mashariki.

Mtaturu amechukua nafasi iliyoachwa na Tundu Lissu kupitia chama cha CHADEMA aliyevuliwa Ubunge  mnamo Juni 28 mwaka huu kwa kupoteza sifa za kuwa mbunge wa Jimbo.

Wakati  shughuli za kumuapisa Mh.Mtaturu, Wabunge wa CHADEMA wamesusia tukio hilo kwa kugoma kuingia ukumbini .

Wakati Mtaturu akichukua nafasi yake, Ndugai amesema jimbo hilo sasa limepata mwakilishi halali

Monday, September 2, 2019

KONGAMANO LA KIBIASHARA KUFANYIKA JIJINI DAR

 Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kongamano la biashara baina ya Tanzania na Uganda.
Mratibu wa Kongamano la biashara baina ya Tanzania na Uganda Ali Gugu akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema Jijini Dar es salaam

Na Mwandishiwetu             
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza Kwa wingi kushiriki katika kongamano la biashara la Tanzania na Uganda linalotaraji kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema leo Jijini hapa Bashungwa amesema kongamano hilo ambalo litafunguliwa na kuhudhuliwa na wakuu
 wa nchi zote Mbili Tanzania na Uganda.

"Rais Magufuli amemualika Rais Museveni  wa Uganda katika ufunguzi wa mkutano hii ambao utawashirikisha wafanyabiashara zaidi ya 1000 ambao  watapata nafasi ya kujadili namna ya kuongeza  biashara mpya baina ya nchi hizi Mbili" amesema Waziri Bashungwa.

Aidha Waziri Bashungwa ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya ziwa ambao wengi wao ndio wamekuwa wakifanya biashara Moja kwa Moja na nchi za jirani hili waweze kupata mtandao mpya wa kibiashara.

Ametaja muungano wa kimtandao baina ya Tanzania na Uganda utafungua njia mpya ya Biashara hadi Sudan ya kusini ambao wamekuwa wakifanya biashara na Uganda kila uchwao.

Ametaja muungano wa kibiashara baina ya nchi hizi Mbili utaongeza mabilioni kwa nchi yetu ya Tanzania kwani mpaka Sasa sisi ndio tumekuwa tukiuza zaidi kwao kuliko wao kuuza kwetu.

Amesema kuwa Uganda imekuwa ikitegemea mazao ya chakula kutoka hivyo wauzaji wa nafaka na Wasindikaji wa vyakula wanatakiwa kutumia fursa hii vizuri kwa kutanua masoko yao.

Amemaliza kwa kutoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza Kwa wingi katika kongamano hili.

JISAJILI KUSHIRIKI MKUTANO WA KIBIASHA NA MAONESHO KATI YA TANZANIA NA UGANDA SEPT 6-7, 2019 JIJINI DAR ES SALAAM

• Sisi ni Zaidi ya Ujirani
• Sisi ni ndugu wa Damu
Tanzania na Uganda katika meza moja ili kukuza na kujenga Uchumi imara na madhubuti!
#TZUGBusinessForum19
#SisiNiTanzaniaMpyA+ ya Wazalendo, Waadilifu, Waaminifu, Wachapa Kazi!

RAIS MSTAAFU WA AFRIKA KUSINI THAMBO MBEKI AKUTANA NA VIONGOZI WAANDAMIZI WASTAAFU WA TANZANIA JIJINI DAR

Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (wa pili kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri Mstaafu, Prof. Mark Mwandosya, Balozi Mstaafu Juma Mwapachu (kulia) pamoja na Balozi Mstaafu Ami Mpungwe walipokutana jijini Dar es salaam hivi karibuni. wa pili kushoto ni Max Boqwana, Afisa Mtendaji Mkuu wa Thabo Mbeki Foundation.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WATENDAJI KATA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Watendaji wa Kata zote za mikoa ya Tanzania Bara Ikulu jijini Dar es Salaam.
Watendaji wa Kata zote za mikoa ya Tanzania Bara wakiimba Wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa Mkutano wao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Watendaji wa Kata zote za mikoa ya Tanzania Bara wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Watendaji Kata wakiwa katika mkutano wao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza Watendaji wa Kata katika Mkutano na Watendaji hao wa Kata zote za Mikoa ya Tanzania Bara Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka 
 
 
 

 
 
Baadhi ya Watendaji Kata kutoka mikoa mbalimbali wakizungumza katika mkutano wao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.