Matokeo chanyA+ online




Tuesday, March 5, 2019

SERIKALI YAJIPANGA KUZIWEKEA TAASISI ZAKE MIKATABA


Serikali kupitia wizara ya maji imejipanga kuleta utaratibu wa kuziwekea mikataba ya utendaji kazi taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo ili kuimarisha usimamizi wa sekta ya maji katika ngazi mbalimbali nchini.

Hayo yamezungumzwa  Jijini Dodoma na Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa wakati alipokuwa akifungua mkutano uliowahusisha  Makatibu Tawala wa Mikoa nchini kwa ajili ya kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu uendeshaji mpya wa sekta ya maji kufuatia kupitishwa kwa sheria mpya ya Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Sheria Namba 5 ya mwaka 2019.

Prof. Mbarawa amesema kuwa wizara imeamua kuja na mikataba hiyo itakayokuwa na malengo maalum ya kuzipima taasisi kwa kila mwaka mmoja ambapo nia ya serikali sio kumkomoa mtendaji bali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyokusudiwa.

“Mamlaka hizi zikisimamiwa kwa malengo zitafanya kazi vizuri zaidi na zitakuwa na uwezo mkubwa wa kujiendesha pia kupimana utendaji kazi ni jambo zuri kwa sababu tukifanya kazi kimazoea mamlaka na taasisi zetu hazitoweza kufanya kazi vizuri wala kuimarisha utoaji wa huduma za maji safi na salama kwa wananchi wetu,” amesema  Prof. Mbarawa.

Ameendelea kusema kuwa, mkutano huo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Magufuli alilolitoa mwezi Mei, 2018 kuhusu mfumo wa uendeshaji wa sekta ya maji ambapo aliagiza sekta ya maji isimamiwe na wizara moja ili kurahisisha usimamizi na uwajibikaji wa watendaji.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Kitila Mkumbo amefafanua kuwa Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Namba 12 ya mwaka 2009 imepitiwa na kutungwa upya na kwa sasa inajulikana kama Sheria ya Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019 ambapo kikubwa katika sheria hiyo ni kuanzishwa kwa Wakala wa Maji Vijijini.

“Haitawezekana kukamilisha mipango ya sekta ya maji bila ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa hivyo kupitia mkutano huu Makatibu Tawala watapata nafasi ya kupitia na kuielewa sheria mpya kwa kina na kubaini nafasi zao katika usimamizi na uendeshaji wa sekta ya maji kwenye sheria hii," amesema Prof. Mkumbo.

Kuanza kutumika kwa sheria hiyo mpya kutaimarisha mfumo wa utoaji huduma za maji na usafi wa mazingira nchini, kutaongeza ufanisi na uwajibikaji katika kutoa huduma za maji, kutaimarisha ujenzi na usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji, kutachochea utendaji katika sekta  nyingine na kuongeza mchango wa sekta ya maji katika uchumi wa nchi.
IMG_09974
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa nchini (hawapo pichani) walioshiriki katika mkutano wa kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu uendeshaji upya wa sekta ya maji kufuatia kupitishwa kwa sheria mpya ya Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Sheria Namba 5 ya mwaka 2019. Ufunguzi huo umefanyika leo Jijini Dodoma.
IMG_9977
 Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akizungumza wakati akifungua mkutano uliowahusisha Makatibu Tawala wa Mikoa nchini kwa ajili ya kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu uendeshaji upya wa sekta ya maji kufuatia kupitishwa kwa sheria mpya ya Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Sheria Namba 5 ya mwaka 2019. Ufunguzi huo umefanyika leo Jijini Dodoma.
IMG_09992
Mwenyekiti wa Makatibu Tawala wa Mikoa nchini, Mama Rehema Madenge akitoa neno la shukrani baada ya Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa kufungua mkutano huo.
IMG_9961
 Baadhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa nchini na wafanyakazi wa Wizara ya Maji waliohudhuria katika mkutano huo.Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

SERIKALI YAPATIWA MKOPO WA SH. BILIONI 589.26 KUTOKA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) KWA AJILI YA UJENZI WA BARABARA YA KABINGO (KAKONKO) –KASULU-MANYOVU KM 260 KWA KIWANGO CHA LAMI

1
4
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James kulia akisaini mkataba wa Mkopo wa Masharti nafuu wenye thamani ya Shilingi bilioni 589.26 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB iliyowakilishwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo hapa nchini Dkt. Alex Mubiru (kushoto akisaini) katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. Fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 mkoani Kigoma.
5
6
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akibadilishana mkataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) hapa nchini Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kutiliana saini mikataba miwili ya  mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Shilingi bilioni 589.26 itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 mkoani Kigoma.
7
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akionesha mkataba wa mkopo wa masharti nafuu pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kusaini katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.
8
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo kuhusiana na ramani ya ujenzi wa barabara ya kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 zitakazojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Kigoma.
11
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo na wanahabari kuhusiana na mkopo huo wa masharti nafuu ambao utatumika katika ujenzi wa barabara mkoani Kigoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya (Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga.
9
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya (Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga
10
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kusaini mikataba hiyo ya mkopo wenye masharti nafuu katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.

Monday, March 4, 2019

MATUKIO KATIKA PICHA KAMATI YA BAJETI YAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

ARUSHA 1-min
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti ofisini kwake wakati Kamati hiyo ilipomtembelea kabla ya kuanza ziara yake katika Mkoa huo.
ARUSHA 2-min
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo wakati Kamati hiyo ilipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza ziara yake katika Mkoa huo.
ARUSHA 4-min
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. George Simbachawene wakiangalia mitambo iliyotumika kutengeneza matairi katika kiwanda cha General Tyre kilichoko Arusha, mwenye suti nyeusi ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo (NDC), Profesa Damian Gabagambi. Wajumbe hao wapo katika ziara ya siku saba Mkoani Arusha
ARUSHA 6-min
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti , Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo na uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha  (AIA) wakati Kamati hiyo ilipotembelea chuo hicho.kushoto kwake ni Naibu Mkuu wa Baraza la Chuo hicho,  Ndugu Juma Kaniki na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo.
ARUSHA 7-min
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. George Simbachawene wakiwa katika kikao cha pamoja na uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA) wakati Kamati hiyo ilipotembelea chuo hicho.
PICHA NA OFISI YA BUNGE

RC WANGABO AAGIZA USHIRIKIANO KWA MA-DC KATIKA KUTEKELEZA MIRADI YA SERIKALI

IMG_7395
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda (aliyeshika tofali) akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo wakati wa ziara fupi ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya hiyo ulioanza mapema mwaka huu na kutakiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka 2019.
IMG_6844
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (rainboot za kijani) akiangalia uimara wa matofali yaliyojengewa msingi katika moja ya majengo saba ya hospitali ya wilauya ya Sumbawanga inayojengwa katika bonde la ziwa Rukwa, kata ya Mtowisa. (mwenye shati ya kitenge) Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wakuu wa Wilaya za Mkoani Rukwa kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa pamoja katika kutembeleana na kuelezana changamoto na mafanikio katika maeneo ya mradi wa ujenzi wa hospitali za wilaya ili kujenga hospitali hizo katika hadhi sawa na hatimae kupeana ujuzi wa utekelezaji wa mradi huo.
Amepongeza ushirikiano unaoonyeshwa na uongozi wa wilaya ya Nkasi unaoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo mh. Said Mtanda pamoja na wabunge, madiwani na mkurugenzi na kusifu mafunzo waliyoyapata na kuyarekebisha wakati wa utekelezaji wa ujenzi wa vituo vitatu vya afya katika wilaya hiyo na kuonyesha dalili za kutojirudia kwa makosa waliyoyafanya wakati wakitekeleza ujenzi wa vituo hivyo.
“Wakuu wa Wilaya waweke program ya kutembeleana kwa pamoja ili kujifunza, wanakuja kwa mfano (wilaya ya) Nkasi, wanakwenda wilaya ya Sumbawanga, Wanakwenda wilaya ya Kalambo halafu watakaa chini wafanye tafakari ili waone ni namna gani wanweza wakasimamia vizuri hizo hospitali zetu za wilaya kwasababu tunapaswa tuwe na kitu bora, hospitali zote tatu ziwe bora ndani ya mkoa wetu,” Alisisitiza.
Alisema kuwa halitakuwa jambo jema kwa wilaya moja kuwa na ufanisi sana ilihali wilaya nyingine inakuwa na changamoto na hivyo vyema wakaungana kama timu na kutembelea miradi hiyo ya ujenzi wa hospitali za wilaya ili kila mmoja aweze kujifunza kutoka kwa mwenzie.
Ameyasema hayo baada ya ziara yake ya kutembelea ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi pamoja na ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga ili kujionea changamoto mbalimbali zinazoukabili mradi huo ambao unatakiwa kuisha mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu.

SERIKALI KUENDELEA KUDHIBITI MATUMIZI YA KEMIKALI NCHINI

Mgeni Rasmi na Mwenyekiti wa Mkutano, Mhe. Ummy Mwalimu (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Bodi Tendaji ya Mamlaka wakiwa pamoja na baadhi ya wadau walioshiriki Mkutano (picha ya juu). 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema Serikali itaendelea kusimamia na kudhibiti matumizi ya kemikali ili kuhakikisha hazileti madhara kwa afya za wananchi na Mazingira.
Waziri Ummy ameyazungumza hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano na wadau wanaojishughulisha na shughuli za kemikali ulioandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa lengo la kujadili namna ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara ya kemikali nchini.
“Kemikali zisipodhibitiwa vizuri zinaweza kuleta madhara katika afya, mazingira pamoja na kuhatarisha usalama wa nchi, ipo haja ya kuweka mazingira mazuri ya kusimamia na kudhibiti uingizaji na matumizi ya kemikali nchini ili zisilete madhara,” alisema Ummy.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akifafanua jambo kwa Mheshimiwa Ummy Mwalimu, wakati wa Mkutano na Wadau leo.

Alifafanua kuwa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za mwaka 2014 zinaonyesha vifo milioni 12.6 vilitokana na mazingira duni ya kuishi, mojawapo ya kichocheo ni athari za kemikali ambazo zimekuwa zikisababisha magonjwa na vifo.”
Waziri Ummy aliongeza kuwa kemikali zimekuwa na athari kubwa kwa binadamu kwa kusababisha magonjwa zaidi ya mia moja yakiwemo magonjwa ya moyo, saratani, ngozi, athari katika mifumo ya fahamu, upumaji pamoja na chakula kuathiri zaidi wananchi wengi.
“Tukubali kuwa kemikali zina madhara kwa wananchi lakini sasa tuwe na mazingira mazuri ya kuzidhibiti, Serikali itaendelea kuboresha mazingira mazuri kwa wafanya biashara ya kemikali nchini,” Ummy aliongeza.
Aidha, Waziri Ummy amezitaka Taasisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) kuangalia upya tozo zinazotozwa kwa wafanyabiashara wa kemikali nchini pamoja na kupunguza changamoto zisizo za lazima ili kuwawekea mazingira rafiki wafanya biashara za kemikali.
Amezitaka Taasisi hizo kutokuwa na vikwazo kwa uwekezaji na biashara, kikwazo cha kushamiri na kukua kwa uwekezaji nchini na badala yake wawe mawakala wa kukuza biashara na uchumi nchini ili kuvutia wawekezaji kwa kuweka mazingira rafiki kwa biashara.
Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (katikati), akiongoza Mkutano na Wadau wa Kemikali uliokuwa na lengo la kujadili namna bora ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara ya kemikali nchini. kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Mamlaka, Profesa Esther Hellen Jason na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto).

Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Mhandisi Anthony Swai akichangia mada
Mfanyabiashara Bw. Azim Dewji akichangia mada wakati wa Mkutano.

ZOEZI LA UTOAJI ELIMU UNAENDELEA KWA WASAFIRISHAJI MKOANI MBEYA

1
 Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Julius Chambo, akitoa elimu kwa madereva wa malori kuhusu utekelezaji wa Sheria mpya ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, mjini Tunduma, mkoani Mbeya. Sheria hiyo imeshaanza kutumika.
2
 Dereva wa malori ya mizigo Bw. Juma Nachikolo, akiuliza swali kwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Julius Chambo (hayupo pichani), mara baada ya kupewa elimu ya Sheria mpya ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoanza kutumika tarehe 1 Machi, 2019, mjini Tunduma, mkoani Mbeya.
3
Baadhi ya madereva wa malori wakisikiliza elimu inayotolewa juu ya utumikaji wa  Sheria mpya ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoanza kutumika tarehe.

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAFUNGUA VITUO VYA KUBADILISHIA FEDHA ZA KIGENI

Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Meneja Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo na kushoto ni Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Mwanaisha Ali Said.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akizungumza wakati akimkaribisha Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Hassan Mwang'ombe (kulia), kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea mkakati wa shirika katika kuimarisha maduka yake ya kubadilishia fedha za kigeni nchini. Katikati ni Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Mwanaisha Said. 
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakimsikiliza Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, wakati akizungumza na waandishi leo jijini.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakijadiliana jambo wakati wa mkutano huo.  
Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (katikati), akuzungumza na waandishi wa habari kuelezea mkakati huo wa shirika.
Baadhi ya wateja wakipata huduma kwenye maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ya Shirika la Posta leo, Ofisi ya Posta Kuu jijini Dar es Salaam. 
Wateja wakiwa katika Kituo cha huduma mbalimbali za shirika wakisubiri kupatiwa huduma, Ofisi ya Posta Kuu jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ya Shirika la Posta, jijini Dar es Salaam. 

CHINI ni Taarifa iliyotolewa na Postamasta Mkuu kwa waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGULIWA KWA MADUKA NA VITUO VYA KUBADILISHIA FEDHA ZA KIGENI VYA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Tarehe 28 february 2019 Benki kuu ya Tanzania ilitangaza kwamba maduka ya kubadilishia fedha yatabaki kwenye mabenki, taasisi za kifedha pamoja na maduka ya fedha za kigeni za Shirika la Posta Tanzania tu.

Tunapenda kuutarifu umma wa watanzania kuwa Shirika la Posta limejizatiti katika kutoa huduma hiyo kwa umma wa watanzania na tunapenda kuwajulisha kuwa mpaka sasa tunavyo vituo kumi (10) vinavyotoa huduma ya kubadilisha fedha ambapo ni Kariakoo, Posta Mpya, Kijitonyama, Oysterbay, City drive (Sokoine ) , Libya Posta, Uwanja wa ndege, vituo hivi vyote vipo jijni Dar es Salaam na mpaka ifikapo tarehe 15 Marchi 2019 tutakuwa na vituo ishirini(20) vya kubadilishia fedha za kigeni.

Pia tuna mikoa miwili ambayo tayari huduma hii imeanza nayo ni ofisi kuu ya Posta Zanzibar na Arusha, Pia tunatarajia mwishoni mwa mwezi Marchi mikoa 17 yenye ofisi za posta zitaanza kutoa huduma hiyo. Tungependa kuutaarifu Umma ,watembelee katika vituo vyetu vya posta kupata huduma hii ya ubadilishaji fedha za kigeni.

Shirika la Posta Tanzania linapenda kuujulisha Umma kupokea taarifa hii muhimu kwao na kwa maendelea ya Taifa.

 imetolewa na ;
POSTAMASTA MKUU NA MTENDAJI MKUU
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI WAWILI, BALOZI MMOJA PAMOJA NA KUSHUHUDIA UAPISHWAJI WA MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI


3
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Dkt. Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Ikulu jijini Dar es Salaam.
4.
5
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es Salaam.
6
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Yahya Simba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia Ikulu jijini Dar es Salaam.
7
8
9
10
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwaapisha Mawaziri wawili, Balozi mmoja na kushuhudia uapishwaji wa Maofisa watano wa Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
11
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna Benedict Michael Wakulyamba mara baada ya hafla ya uapisho kukamilika Ikulu jijini Dar es Salaam.
12
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na Makamishna watano kutoka jeshi la Polisi, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi, pamoja na Balozi Yahya Simba mara baada ya hafla ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
14
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Dini mara baada ya hafla ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
15
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na Maofisa Mbalimbali wa Jeshi kutoka Jeshi la Polisi mara baada ya hafla ya Uapisho wa viongozi mbalimbali  Ikulu jijini Dar es Salaam.
17
 Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustine Mahiga akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma   na  Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na Makamishna watano kutoka Jeshi la Polisi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
18
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akimvalisha cheo kipya cha Kamishna Liberatus Sabas ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
19.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akimuapisha Kamishna Liberatus Sabas ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
20
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akimvalisha cheo kipya cha Kamishna Leonard Paul Lwabuzala ambaye ameteuliwa kuwa kamishna wa kamisheni ya polisi Fedha na Lojistiki, Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU