Matokeo chanyA+ online




Wednesday, November 6, 2019

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania,  Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike  alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma kwa mazungumzo maalum.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiagana na Kamishna Jenerali wa  Magereza nchini, Phaustine Kasike  mara baada ya mazungumzo alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike  akisaini kitabu cha Wageni alipomtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania,  Mhe. Job Ndugai(hayupo pichani), leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma.
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Job Ndugai (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike (katikati) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Tuesday, November 5, 2019

MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA MWANASIASA MKONGWE WILAYANI RUANGWA MZEE MMUYA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitupa udongo kwenye kaburi la mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa zamanı wa CCM wa wilaya ya Ruangwa, Kaspar Selemani Mmuya katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Nangumbu kwenye kitongoji cha Mtakuja  wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa zamanı wa CCM wa wilaya ya Ruangwa, Kaspar Selemani Mmuya katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Nangumbu kwenye kitongoji cha Mtakuja wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 


MATUKIO YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA BUNGENI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Salma Kikwete, Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa Tablets na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai wakati la ugawaji wa tablets kwa Wabunge wote, katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Wabunge, wakati akiingia Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, AFUNGUA MAONESHO YA WIKI YA ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI 2019

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Balozi wa Canada nchini Tanzania Bi.Pamela O’Donnell, wakati akiwasili katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, kufungua Maonesho ya Wiki ya Asasi Zisizo za Kiserikali 2019, Novemba 4.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe, wakati akifungua Maonesho ya Wiki ya Asasi Zisizo za Kiserikali 2019, katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, Novemba 4.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia kitabu, wakati akitembelea mabanda, kabla ya kufungua Maonesho ya Wiki ya Asasi Zisizo za Kiserikali 2019, yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, Novemba 4.2019. Kutoka kushoto ni Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Vickness Mayao, Mkurugenzi Mtendaji wa Wajibu Ludovick Utouh, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa, iliyotengenezwa na Mjasiriamali ambaye ni mlemavu wa macho, Angela Sebastian, wakati akitembelea mabanda, kabla ya kufungua Maonesho ya Wiki ya Asasi Zisizo za Kiserikali 2019, yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, Novemba 4.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mjasiriamali ambaye ni mlemavu wa macho, Angela Sebastian, wakati akitembelea mabanda, kabla ya kufungua Maonesho ya Wiki ya Asasi Zisizo za Kiserikali 2019, yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, Novemba 4.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkurugenzi wa Policy Forum, Semkae Kilonzo, kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Asasi Zisizo za Kiserikali 2019, yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, Novemba 4.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Rais wa Foundation for Civil Society, Stigmata Tenga, kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Asasi Zisizo za Kiserikali 2019, yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, Novemba 4.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Asasi Zisizo za Kiserikali 2019, yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, Novemba 4.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi, kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Asasi Zisizo za Kiserikali 2019, yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, Novemba 4.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi, kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Asasi Zisizo za Kiserikali 2019, yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, Novemba 4.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi, kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Asasi Zisizo za Kiserikali 2019, yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, Novemba 4.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


WAZIRI WA MAMBO YA NJE PROF. KABUDI AKUTANA NA MABALOZI WA NCHI ZA AFRIKA NA NORDIC WALIOPO NCHINI



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza alipokutana na waandishi wa habari kuwaelezea Maandalizi ya mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic unaotarajiwa kufanyika tarehe 7 – 8 Novemba 2019 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Mwinyi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika kikao cha pamoja na mabalozi kutoka nchi za Afrika na Nordic wakizungumzia maandalizi ya mkutano wa 18 wa mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic utakaofanyika tarehe 7 – 8 Novemba 2019 jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwaelezea waandishi wa habari maandalizi ya mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic unaotarajiwa kufanyika tarehe 7 – 8 Novemba 2019 jijini Dar es Salaam
Baadhi ya mabalozi kutoka nchi za Afrika na Nordic wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Hayupo pichani) wakati alipokutana nao kuzungumzia maandalizi ya mkutano wa 18 wa mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic utakaofanyika jijini Dar es Salaam.

Monday, November 4, 2019

Sisi Tunaweza Tuliposema kwamba Tutazilinda Rasilimali zetu walisema tun...

Sisi Tunaweza Tuliposema kwamba Tutazilinda Rasilimali zetu walisema tun...

Sisi Tunaweza Tuliposema kwamba Tutazilinda Rasilimali zetu walisema tun...

RAIS DKT. MAGUFULI AWA APISHA CAG, MAJAJI 12 WA MAHAKAMA KUU, MAKAMISHNA WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU PAMOJA NA BALOZI MMOJA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Charles Edward Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG). Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Bw. Charles Edward Kichere mara baada ya kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG). Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Joachim Chrles Tiganga kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Deo John Nangela kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Angela Anthony Bahati kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Angaza Elias Mwaipopo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kanali Francis Ronald Mbindi kuwa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu Kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam. Novemba 4, 2019. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Amina Talib Ali Kuwa Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, Novemba 4, 2019. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Aisha Amour kuwa balozi wa Tanzania Nchni Kuwait. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, Novemba 4, 2019. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Katarina Tengia Revocati kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, Novemba 4, 2019.

   Viongozi walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakila kiapo cha Maadili kwa viongozi wa umma Ikulu jijini Dar es salaam,  Novemba 4, 2019. 
 Viongozi walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiweka sahihi kwenye hati ya kiapo cha Maadili kwa viongozi wa umma Ikulu jijini Dar es salaam,  Novemba 4, 2019. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada kuwaapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG), Majaji 12 wa Mahakama kuu, Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Balozi wa Tanzania Nchni Kuwait pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam novemba 4, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada kuwaapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG), Majaji 12 wa Mahakama kuu, Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Balozi wa Tanzania Nchni Kuwait pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam novemba 4, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada kuwaapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG), Majaji 12 wa Mahakama kuu, Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Balozi wa Tanzania Nchni Kuwait pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam novemba 4, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada kuwaapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG), Majaji 12 wa Mahakama kuu, Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Balozi wa Tanzania Nchni Kuwait pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam novemba 4, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge  Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Fedha Dkt. Isidori Mpango  pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG), Majaji 12 wa Mahakama kuu, Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Balozi wa Tanzania Nchni Kuwait pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam novemba 4, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG) mpya Bw. Charles Kichere, Watendaji wa Ofisi ya CAG pamoja na Makamu mwenyeki wa Kamati ya Bunge ya PAC Aesh Hilaly  Ikulu jijini Dar es salaam novemba 4, 2019.

PICHA NA IKULU

Sunday, November 3, 2019

WAZIRI KIGWANGALLA KUOGOZA KAMPENI YA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla akipanda mlima Kilimanjaro akiwa ameambatana na kunndi la wasanii na wadau mbalimbbali kwa lengo la kuutangaza mlima Kilimanjaro  hivi karibuni.

Waziri wa Malisili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema  ataongoza kampeni ya kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika ukanda wa kusini na ukanda wa Kaskazini magharibi kwenye hifadhi mpya za Taifa zilizotangazwa hivi karibuni.
Amesema kampeni hiyo itawahusisha wasanii na watu maarufu wenye ushawishi katika jamii na inalenga kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza vivutio vya utalii vilivyo katika hifadhi za Taifa za Ruaha,Mikumi, Nyerere na Burigi – Chato.
Dkt.Kigwangalla ameyasema hayo alipokuwa akizugumza na Menejimenti ya Shirika la hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) na wakuu wa Kanda wa shirika hilo jijini Arusha.
Amesema hatua hiyo ya kuwatumia wasanii na watu maarufu wenye ushawishi katika jamii inalenga kuogeza hamasa kwa watanzania wavijue na kuvitembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika hifadhi hizo hivyo kuogeza idadi ya watalii wa ndani.
Dkt.Kigwangalla amesema wasanii hao na watu maarufu wana wafuasi wengi wanaofuatilia kazi zao na matukio wanayofanya katika jamii kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii hivyo ni vyema wakatumika kutangaza utalii katika maeneo hayo.
Amesema hatua kazi hii ya kuhamasisha utalii wa ndani ni vyema wadau na watumishi walio kweye sekta husika wakawa wa kwanza kuvijua vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo mbalimbali ili iwe rahisi kuvielezea na kuvitagaza.
“Tukitaka kutagaza soko la utalii wa ndani lazima sisi wenyewe tuanze kwanza kuyajua maeneo ya vivutio tuliyonayo ili iwe rahisi kuwafikia watu wengine, tuna marafiki zetu ndani na nje ya Tanzania inakua rahisi kwetu kuwaalika na kuwakaribisha kwenye vivutio hivyo kwa kuwa sisi wenyewe tunavijua” Amesisitiza Dkt.Kigwangalla.
Amesema mkakati wa sasa ni wa kusambaza uelewa kuhusu vivutio vilivyopo ndani ya nchi ili kuwahamasisha watanzania wengi zaidi kutembelea vivutio hivyo akibainisha kwamba mkakati huo utakuwa na matokeo ya haraka na gharama nafuu ya kuhamasisha utalii wa ndani katika maeneo mengine ya nchi tofauti na ilivyo sasa ambapo watu wengi wanayafahamu maeneo machache na hasa yaliyo mikoa ya Kaskazini.
“Nilipoamua kuutangaza mlima Kilimanjaro na mimi mwenyewe kushiriki kupanda mlima kila mtu alishuhudia nini kilichotokea, kila mtu alikua akiuzungumzia mlima na hii inaongeza umaarufu wa mlima ndani ya nchi huu ni mkakati tunaotakiwa kuutumia katika maeneo mengine” Amesema.
Dkt. Kigwangalla ameiagiza TANAPA iendelee kukusanya takwimu za makundi mbalimbali ya watalii wa ndani wanafanya utalii katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo watazania wanaoshiriki mbio za marathon.
Katika hatua nyingine Waziri wa Maliasili na Utalii ameiagiza TANAPA kuifanyia kazi na kuikamilisha miradi ya ujenzi wa magati na ununuzi wa vivuko na Boti zitakazokuwa zikitumika kusafirisha watalii katika ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi kwenye eneo la Hifadhi ya Taifa ya Saadani.
Amesema gati hizo zitajengwa Dar es salaam, Saadani, Pangani, Pangani na Tanga ili kuwezesha boti hizo kusimama katika maeneo hayo yenye vivutio vya utalii na kushusha watalii wanaotaka kutembelea maeneo hayo.
“Hili ni eneo muhimu sana kwetu na rahisi kuuza huduma zetu za utalii wa ndani ya maji kutokana na uwepo wa visiwa na idadi ya watu wanaokwenda kuvitembelea, Ni lazima tujipange kuzitumia fursa hizi kwa kuwa na boti nzuri zitakazowawezesha watu kufanya utalii, mikutano, harusi na sherehe mbalimbali ndai ya maji na hii itakua ni Biashara kubwa kwetu na njia moja nzuri ya kulitumia vizuri eneo la bahari tulilo nalo” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.
Amesema ili kuitangaza hifadhi ya Taifa ya Saadani ni lazima kuiunganisha na utalii wa fukwe ili kuwavutia watalii wengi zaidi na kuongeza kuwa hifadhi hiyo kutokana na maeneo mazuri yaliyopo,sehemu za kulala na ukaribu wake na Bagamoyo na Dar es salaam.
Dkt. Kigwangalla amefafanua kuwa uanzishaji safari za boti za siku kutokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo na kurudi Dar es salaam utawawezesha watalii kwenda kati katika maeneo hayo kwa haraka na ni rahisi kuuza huduma hiyo kwa wageni watakaokuwa wanakwenda kufanya utalii mwisho wa wiki na kuiwezesha Serikali kupata faida ya kiuchumi kutokana na uwepo wa huduma hizo.
Na.Aron Msigwa – WMU

 

RAIS MAGUFULI AAGIZA KUFANYIKA MABADILIKO HALMASHAURI YA MJI IFAKARA NA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOMBERO



Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amemuelekeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo kufanya mabadiliko kwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara na Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, zilizopo katika Mkoa wa Morogoro kama ifuatavyo;
1.    Halmashauri ya Mji wa Ifakara iongezwe idadi ya Kata, kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

Makao Makuu yawe Ifakara Mjini.

2.     Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero ibadilishwe jina, na iitwe Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba.

Makao Makuu yawe Mgeta kama ilivyoamuliwa na Baraza la Madiwani.
Mhe. Rais Magufuli amewasisitiza viongozi wa halmashauri kutowayumbisha wananchi na watumishi kuhusu utekelezaji wa maelekezo hayo.
Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mhe. Waziri Jafo kusimamia utekelezaji wa maelekezo hayo kwa mujibu wa sheria


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Novemba, 2019

Friday, November 1, 2019

WAZIRI KIGWANGALLA AAIGIZA MABORESHO YA HUDUMA MLIMA KILIMANJARO

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) lifanye maboresho ya miundombinu ya huduma za dharula na uokoaji ndani ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro ili kuogeza usalama wa watalii wanaokweda 2kupanda mlima huo.
Pia, amelitaka shirika hilo liedelee kuboresha miudombinu ya malazi katika hifadhi hiyo ili iweze kuendana na mahitaji ya sasa ya wapanda mlima na kuangalia uwezekano wa kutafuta wawekezaji watakaojenga hoteli za kisasa kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla akizungumza  na Menejimenti ya TANAPA na Wakuu wa Kanda wa Shirika hilo jijiini Arusha.
Dkt.Kigwangalla ametoa maagizo hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya TANAPA na Wakuu wa Kanda wa Shirika hilo jijiini Arusha.
Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia changamoto mbalimbali alizokutana nazo wakati akipada mlima Kilimanjaro Septemba, 28 mwaka huu, akiwa ameambatana na kundi la Wasanii na wadau mbalimbali kutoka taasisi za umma na binafsi.
Dkt. Kigwangalla ameieleza Menejimenti hiyo kuwa katika zoezi lake la kupanda mlima Kilimanjaro kuna changamoto alizibaini zikiwemo za kukosekana kwa miudombinu ya kutosha ya huduma za uokoaji na malazi ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka ili kuongeza ufanisi na idadi ya watalii wanaopanda mlima huo.
Kufuatia hali hiyo ameiagiza TANAPA ianze kuboresha huduma za dharula na uokoaji pia ijenge vituo vya kutolea tiba na huduma ya kwanza mlimani vitakavyokuwa na wataalam wa kuhudumia watalii wanaopata matatizo wakiwa mlimani pia kuboresha huduma za malazi katika baadhi njia za mlima huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla akizungumza  na Menejimenti ya TANAPA na Wakuu wa Kanda wa Shirika hilo jijiini Arusha
Dkt.Kigwangalla amesema changamoto hizo zikitatuliwa kwa haraka zitauwezesha mlima huo kupata idadi kubwa ya watalii kuliko ilivyo sasa na kuiogezea serikali mapato.
Kuhusu uboreshaji wa huduma za uokoaji (Rescue services) kwa watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro ameiagiza TANAPA ifanye utaratibu wa kuazisha huduma ya viberege maalum (Zip line) vitakavyokua vinatumika kushusha wapada mlima watakaokua wakipata matatizo ya kiafya kwa haraka hata wakati wa hali mbaya ya hewa.
“Suala la matumizi ya “Zip line” mliongezee nguvu ya kulitekeleza, hii itakua njia rahisi ya uokoaji na itawajengea ujasiri wapada mlima waelewe kwamba hata kama watapata shida yoyote ya kiafya wakati wa kupanda mlima wanajua wana uhakika wa usalama wa maisha yao hata pale ambapo hali ya hewa ni mbaya na helikopta haiwezi kutua mlimani” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.
Amesema uwepo wa huduma hiyo ya kisasa ya kushusha watalii wanaopata chagamoto za kiafya itawezesha watalii kupata huduma mlimani kupitia vituo vya kutolea huduma ya kwanza vitakavyojegwa mlimani ambavyo vitakua na wataalam wenye mafumzo watakaokuwa na jukumu la kutoa huduma muda wote.
Kuhusu uboreshaji wa huduma ya malazi mlimani Dkt. Kigwangalla ameonesha kuridhishwa na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na TANAPA kuboresha miundombinu ya malazi mlimani na kuitaka iangalie uwezekano wa  kuhamasisha wawekezaji wakubwa kwenye ujenzi wa hoteli za kisasa.  
Amesema uwepo wa hoteli hizo pamoja na mambo mengine utaongeza siku za watalii kukaa mlimani akitoa mfano wa hoteli nzuri na za kisasa zilizojengwa katika milima ya Alaps ambazo zinatembelewa na watu maarufu kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Kufuatia maagizo hayo, Kamishna wa uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dkt. Allan Kijazi amesema kuwa TANAPA inaendelea kufanya maboresho kwenye maeneo ya kulala wageni ili yaweze kwenda na wakati pia yawe na uwezo wa kupokea wageni wengi pia kuishirikisha sekta binafsi katika utoaji wa huduma mlimani.
Amesema kazi ya kuainisha maeneo kwa ajili ya ujenzi wa hoteli za kisasa inaendelea na kwa kuanzia maeneo manne yamekwishaainishwa kwa ajili ya uwekezaji na kuongeza kuwa baadhi ya wawekezaji wamekwishajitokeza na kuonesha nia ya kujenga hoteli za kisasa katika mlima huo.
Kuhusu uboreshaji wa huduma za ukoaji mlimani amesema kwa sasa kuna maeneo yana miundombinu ya barabara zinazowezwsha magari ya kubebea wagonjwa kufika katika baadhi ya maeneo na kutoa huduma ya uokoaji.
 Pia amesema wamekua wakitumia helikopta kutoa huduma za uokoaji licha ya huduma hiyo kushindwa kufanyika kazi wakati wa hali mbaya ya hewa na hivyo kulazimika kutumia machela za matairi zinazoendeshwa na watu kuhudumia watalii wanaopata matatizo ya kiafya.
Aidha, Dkt. Kijazi amesema TANAPA inaendelea kufanya maboresho ya huduma za dharula na uokoaji na itawasilisha kwake taarifa ya utekelezaji itakayoainisha mpango wa ujenzi wa njia za kisasa zitakazotumia viberenge maalum vya uokoaji vitakavyokua vikipita kwenye waya (Zip line) ili kazi ya ujenzi wa njia hizo ianze mara moja.