Matokeo chanyA+ online




Monday, January 13, 2020

WANANCHI WA NYANDA ZA JUU KUSINI CHANGAMKIENI FURSA ZA UTALII

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Rebeka Msambusi  akiongea na waandishi wa habari wa mikoa ya Mbeya na Iringa juu ya fursa za kiutalii zinavyokuza uchumi wa mwananchi moja moja na jamii kwa ujumla.
Paulina Boma mfanyabiashara wa Mugumu Serengeti akizungumza waandishi wa habari mikoa ya Mbeya na Iringa juu ya fursa za kiutalii zinavyokuza uchumi wa mwananchi moja moja na jamii kwa ujumla.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Rebeka Msambusi  akiongea na waandishi wa habari wa mikoa ya Mbeya na Iringa juu ya fursa za kiutalii zinavyokuza uchumi wa mwananchi moja moja na jamii kwa ujumla.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wananchi wanaozungukwa na hifadhi za taifa wametakiwa kutumia fursa za kiuchumi ambazo zinapatikana katika hifadhi hizo ili kuleta maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.

Akizungumza waandishi wa habari mikoa ya Mbeya na Iringa Paulina Boma mfanyabiashara wa Mugumu Serengeti alisema kuwa amefanikiwa kupata mafanikio mengi kutokana na biashara ya bidhaa za kitalii katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.

“Nimefanikiwa kupitia uuzaji wa bidhaa za kitalii kwa kuwasomesha watoto wangu wane kwa ngazi ya chuo kikuu na wengine wanaendelea kusoma ngazi za chini za elimu ya sekondari,lakini pia nimewasidia vijana wengine kuwaongezea elimu kwenye vyuo mbalimbali kulingana na vipaji vyao” alisema Boma

Boma aliongeza kwa kusema kuwa kupitia biashara ya kuuza bidhaa za kitamaduni kwa watalii wanatembelea hifadhi hiyo amefanikiwa kujenga nyumba nne na amenunua gari kwa ajili ya shuguli zake binafsi na ndoto zake ni kuhakikisha anakuwa na kampuni ya utalii ambayo itamuongezea kipato na kuleta maendeleo kwa taifa kwa ujumla.

Aidha Boma aliwataka wananchi wa mikoa ambayo inazungukwa na hifadhi za taifa kuchangamkia fursa zilizoko kwenye hifadhi hizo ili kuleta maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.

“Kwenye hifadhi hizi kuna kila aina ya fursa za kibiashara ambazo zipo wazi kwa kila mtanzania anaweza kuzitumia hivyo watanzania wanatakiwa kuwa wabunifu tu,labda ukiangalia bidhaa nazoziuza hapa nazinunua katika mikoa ya nyanda za juu kusini,Iringa,Mbeya,Njombe na songwe na nakuja kuziuza huku hivyo hata wao wanaweza kuziuza kwa watalii wanaotembelea vivutio vya mikoa yao” alisema Boma

Lakini Boma aliwataka wanaume kuwaruhusu wanawake kufanya shughuli za kiamendeleo kwa kuwa wanauwezo wa kufanya kazi na kuongeza kipato kwenye familia hivyo ukimpa fursa mwanamke basi umeikomboa jamii kwa ujumla.

“Niwaombe wananchi wa nyanda za juu kusini waje huku kaskazini wajifunze shughuli hizi za kitamaduni ambazo tumekuwa tukiwauzia watalii mbalimbali na kupata faida ambayo imekuwa inaendesha maisha yangu vizuri na kuchangia maendeleo ya taifa” alisema Boma

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Rebeka msambusi alisema kuwa utalii umesaidia kukuza uchumi kwa wananchi wa wilaya hiyo kutokana na kuuza bidhaa mbalimbali kwa watalii.

“Saizi wanauza vyakula mbalimbali kwenye hotel na kambi za kitalii ambazo zipo hifadhi ya taifa ya Serengeti na usafiri pia umechangia kukuza uchumi wa wananchi” alisema Msambusi

Msambusi aliwataka wananchi wa nyanda za juu kusini kuchangamkia fursa zilizopo katika hifadhi ya taifa ya Ruaha ili kukuza uchumi kama ilivyo katika mikoa ya kaskazini ambao wamekuwa wakitumia vizuri fursa ya utalii kwa kujipatia maendeleo.

Ikumbukwe kuwa  Hifadhi ya Ruaha ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania ambapo ina ukubwa wa kilomita za mraba 20,226 na ni ya pili kwa ukubwa katika Bara la Afrika baada ya hifadhi ya Kafue iliyopo nchini Zambia.

Ni maarufu kwa kuwa na wanyama aina ya Kudu wakubwa na wadogo ambao hupatikana kwa wingi ambapo hustawi wa hifadhi hii unategemea mto ruaha ambao aina mbalimbali za Samaki, Mamba na viboko hupatikana katika mto huu.

Wanyama kama Pofu na swala hunywa maji katika mto huo wa Ruaha ambao ni mawindo makubwa ya wanyama wakali wakiwemo Simba, Chui, Mbweha, Fisi na Mbwa mwitu. Pia eneo hili Tembo hukusanyika kwa wingi kuliko eneo lolote la hifadhi zilizopo katika nchi za Afrika Mashariki.

Katika hifadhi hii utajionea Magofu yanayosadikiwa kuwa yalikuwa makazi ya watu wa kale katika Kijiji cha Isimila kiasi cha Kilomita 120 kutoka Iringa. Magofu haya ni miongoni mwa historia ya kale barani Afrika.

Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii ili kuangaliwa wanyama wakubwa ni wakati wa kiangazi kuanzia Mei hadi Desemba, lakini kuangalia ndege na maua wakati wa masika ni Januari –April .


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, AZINDUA JENGO LA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA (TAKUKURU) WILAYANI RUANGWA.)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jenerali John Mbungo, wakati alipozindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wakati alipozindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jenerali John Mbungo, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikata utepe, wakati alipozindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jenerali John Mbungo, wakati alipozindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jenerali John Mbungo, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya ruangwa, wakati wa uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), lililopo katika Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwa Naibu Waziri Ofisi Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa, katika uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Naibu Waziri Ofisi Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa, akizungumza, katika uzindua wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza, mara baada ya kuzindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza, mara baada ya kuzindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipanda mti, baada ya kuzindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipanda mti, baada ya kuzindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WASANII WANAJUKUMU KUBWA LA KUELIMISHA JAMII - BALOZI SEIF ALI IDDI

Balozi Seif Ali Iddi wan ne kutoka Kulia akiwa katika Picha ya pamoja na Timu ya Msanii wa Kizazi Kipya Tanzania King Ali Kiba pamoja na wenyeji wake wa Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Wasanii Nchini lazima wakumbuke kwamba wanabeba jukumu kubwa ndani ya Jamii katika sanaa yao wanayopaswa zaidi kuifanya katika misingi ya Kuelimisha.
Alisema sanaa licha ya kuchukuwa nafasi kubwa katika njia ya kutoa burudani lakini pia ina nafasi pana zaidi iwapo itatumiwa katika kutoa Taaluma ambayo hufika kwa haraka kwa Wananchi waliowengi.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akizungumza na Msanii Maarufu Tanzania King Ali Kiba aliyepo Zanzibar kusaidia Jamii akiwa katika Kampeni yake Maalum aliyoianzisha iitwayo Ali Kiba un forgettable.
 
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akizungumza na Msanii Maarufu wa Kizazi Kipya Tanzania King Ali Kiba wa kwanza Kushoto aliyepo Zanzibar na Kampeni yake ya Un Forgettable. Aliye katiu kati ni Mkurugenzi Mkuu wa Zanzibar Cable Television {ZCTV} Mohammed Abdullah Al – Jabir.
 
“ Itapendeza zaidi kama Jamii itaendelea kushuhudia Sanaa inatumiwa vyema katika kuelimisha Jamii kwa vile ni moja ya sehemu inayoweza kufundisha kwa urahisi”. Alisisitiza Balozi Seif.
Alisema Wasanii wengi wa Kikazi Kipya hivi sasa wamekuwa wakilenga zaidi kujishughulisha na nyimbo zinazokiuka maadili hasa eneo la mavazi jambo ambalo ni hatari kuigwa mara moja na Watoto Wadogo wanaotegemewa kuwa Taifa la hapo baadae.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimpongeza na kumshukuru Msanii huyo wa Muziki wa Kizazi Kipya King Kiba kwa ubunifu wake wa kuisaidia Jamii na kuamua kutenga sehemu ya Kipato chake kutokana na Sanaa anayoiendeleza.
 
 Msanii Maarufu wa Kizazi Kipya Tanzania King Ali Kiba akielezea azma ya Kampeni hiyo katika lengo la kuendelea kusaidia Jamii katika Huduma muhimu za Afya.
 
Balozi Seif alimuhakikishia Msanii huyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa vile inafahamu mchango mkubwa unaotolewa na Wasanii wa fani mbali mbali Nchini kwa Jamii itaendelea kushirikiana nae katika kuona Kampeni yake inafanikiwa na kufikia Malengo yake.
Balozi Seif ambae pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar alitoa pongezi Maalum kwa Msanii huyo kwa uamuzi wake wa kushiriki kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 kutimia Miaka 56.
Mapema Msanii huyo wa Muziki wa Kizazi Kipya Nchini King Ali Kiba alisema uamuzi wa kuunda Kampeni hiyo umelenga kuondoa dhana iliyojengeka kwa baadhi ya Watu kufikiria kwamba Muziki ni sehemu ya uhuni.
King Kiba alisema Muziki hutoa ajira nyingi kwa kundi kubwa la Vijana walioamua kuendesha maisha yao kupitia Sanaa zilizomo ndani ya sekta ya ujasiri Amali.
Alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Kampeni yao kwa jamii iliyolenga zaidi kutoa huduma za Afya katika upimaji bure pia huwatembelea Wanafunzi wa Vyuo Vikuu katika dhana nzima ya kuwajengea uwezo zaidi wa kukabiliana na Mafunzo yao.
Naye Meneja wa Kampeni hiyo Anti Esi Mgimba alisema watafuaria kuona wanaendelea kushikwa mkono katika Kampeni hiyo inayowagusa moja kwa Moja Wananchi wa Maisha ya kawaida.
Esi alisema King Ali Kiba amepewa Ubalozi wa Utalii Zanzibar kazi aliyoikubali na kuiridhia kutokana na mapenzi yake makuwa kwa Wananchi wa Zanzibar lakini bado amekuwa na ushirikiano mdogo kwa baadhi ya wadau katika kufanikisha jukumu hilo kubwa la Taifa.
King Ali Kiba yupo Zanzibar na Kampeni yake ya Ali Kiba Un forgettable chini ya uenyeji wa Mkurugenzi Mkuu wa Zanzibar Cable Television {ZCTV} Mohammed Abdullah Al - Jabir.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
13/01/2020.

MARUFUKU TAASISI ZA UMMA KUJENGA MIFUMO YA FEDHA BILA RIDHAA YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO NA eGA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipasngo, Bw. Doto James (wa pili kulia), akizundua Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma

Selikali imezipiga marufuku taasisi zote za Umma nchini kujenga mifumo ya fedha ya kieletroniki bila ridhaa ya   Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).

Agizo hilo limetolewa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, wakati akizundua Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), hafla iliyowakutanisha Wizara ya Fedha na Mipango na Idara, Wakala, Taasisi, Bodi, Mashirika ya Umma yaliyo katika Kanda ya Kati.
Mwakilishi wa Benki nchini Bi. Domina Tarimo, ), akieleza faida ya Mfumo wa GePG katika kuongeza ufanisi na uwazi katika shughuli za kibenki, wakati wa uzinduzi wa toleo la simu za mkononi (GePG App), Jijini Dodoma.
Bw. James alisema kuwa Taasisi zote za Umma nchini zinatakiwa kutekeleza matakwa ya Waraka namba tano (5) wa Hazina unaozitaka taasisi zote kuhakikisha zinapata ridhaa ya Wizara ya Fedha na Mipango na Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) kabla ya kufanya ununuzi, uandaaji, usimikaji na utumiaji wa Mfumo wowote wa kielektroniki wa usimamizi wa Fedha za Umma.

“Imebainika kuwa kuna baadhi ya taasisi za umma ambazo zinakiuka maelekezo hayo ya Serikali kwa sababu wanazozijua wao, nitumie fursa hii kutoa onyo kwa taasisi hizo kutoendelea na vitendo hivyo kwa sababu ni ukiukwaji wa maelekezo”, alisema Bw. James.

Akizungumzia kuhusu GePG App, Bw. James alisema kuwa, uboreshaji wa Mifumo ya Kielektroniki inayoandaa Ankara itawezesha kukusanya fedha kwa wakati na kutoa huduma bora kwa Umma.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James Selikali akiziagiza taasisi zote za Umma nchini kutojenga mifumo ya fedha ya kieletroniki bila ridhaa ya   Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), wakati wa hafla ya  uzinduzi wa Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.

“Baadhi ya faida za Matumizi ya Mfumo huo ni kuongezeka kwa uwazi na udhibiti katika ukusanyaji wa fedha za umma, kupata taarifa sahihi na kwa wakati zinazohusu makusanyo na kuwa na viwango na utaratibu unaofanana katika ukusanyaji wa fedha za umma kwa taasisi zote za umma”, alisema Bw. James.

Alisema faida nyingine ni pamoja na kuchochea ubunifu katika ukusanyaji wa pesa za Serikali na sekta ya fedha kwa ujumla kwa kuweka mazingira rafiki na ya usawa kwa wakusanyaji, kutoa huduma bora na rahisi ya malipo ya fedha za umma hivyo kuchochea ongezeko la makusanyo na kufika haraka katika akaunti kuu za makusanyo za taasisi.

“Kwa kutofanya usuluhishi wa miamala kwa wakati kunaweza kusababisha upotevu wa fedha nyingi za Umma na pia kuwa na taarifa za fedha zisizo sahihi, hivyo nawaagiza nyote kuhakikisha mnafanya usuluhishi wa miamala inayopitia Mfumo wa GePG kwa usahihi na kwa wakati, na kufanyia kazi kwa wakati changamoto mbalimbali zitokanazo na matokeo ya usuluhishi wa Miamala husika”, alisisitiza Bw. James.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, akielezea mafanikio ya Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) ambapo awali miamala 10 ilikua ikifanyika kwa siku na sasa miamala milioni moja inafanyika baada ya matumizi ya mfumo huo.
Aidha alimpongeza Mkurugenzi wa Mifumo ya Usimamizi wa Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi pamoja na timu yake ya wataalam wabobezi kwa kutengeneza Mfumo wa Kieletroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali (GePG) sambamba na toleo la simu za mkononi (GePG App) ambao umerahisisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali pamoja na kuwawezesha wadau kupata huduma kwa wakati.

Aliahidi kuwa Wizara yake itaendelea kuiwezesha Idara hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kubuni mifumo kama hiyo kwa faida ya Serikali na wananchi kwa ujumla.

Aidha, Bw. James ambaye pia ndiye Mlipaji Mkuu wa Serikali, alisema kuwa Wizara kupitia Idara ya Mifumo ya Usimamizi wa Fedha inaandaa mfumo mwingine utakaotumika kwa ajili ya matumizi ya Serikali ujulikanao kwa kifupi kama MUCE.

“Mfumo huu umeshaanza kufanyiwa majaribio kwenye taasisi chache za umma na baadae utasambazwa kwenye taasisi zote na kwamba Mfumo huu utakuwa mwarobaini wa matumizi yasiyo sahihi ya fedha za Umma”, aliongeza Bw. James.

Baadhi ya wajumbe wa Benki nchini, wafuatilia kwa makini maagizo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipasngo, Bw. Doto James (hayupo pichani), wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Alisema Mfumo huo utakuwa suluhisho la matumizi yasiyofaa ya umma na kuongeza kuwa watendaji wengi Serikalini hawataufurahia mfumo huo lakini hilo haliihusu Serikali. Watajua wenyewe! Alisema huku washiriki wakiangua kicheko ukumbini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha, wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, alisema kuwa kabla ya kuwa na Mfumo wa Malipo kwa njia ya Kielektroniki (GePG) ilikua inafanyika miamala 10 kwa siku na baada ya mfumo huo inafanyika miamala milioni moja kwa siku.

Alisema kuwa miongoni mwa mafanikio ni kuongezeka kwa Taasisi zinazotumia Mfumo wa GePG,  kutoka taasisi 300  muda mfupi uliopita hadi kufikia taasisi 620 hivi sasa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na wataalamu wa mifumo ya fedha na wengine, baada ya uzinduzi wa Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.

Bw. Sausi alisema kuwa Mfumo wa GePG kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi uliozinduliwa utasaidia watumiaji kupata huduma mbalimbali kama vile kununua umeme, kulipia Ankara mbalimbali zikiwemo za makosa ya usalama barabarani, maji na nyingine nyingi ndani ya sekunde 30.

Ametoa wito kwa wananchi wanaotumia simu janja (android au IPA App) kupakua application hiyo kupitia play store au App Store na kutafuta neno GePG Tanzania tayari kwa matumizi yao ambayo amesema wananchi watafurahia huduma hiyo.

Naye Mwakilishi wa Benki katika Mkutano huo, Bi Domina Tarimo na Mwakilishi wa kampuni za Simu, Bw. Alafat Ibrahim, walisema kuwa Mfumo wa GePG umezisaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha kazi zao, na kuboresha huduma kwa wateja wao na wameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango na Serikali kwa ujumla kwa jitihada zake za kuhakikisha kuna mifumo imara ya fedha inayoongeza uwazi na uwajibikaji.

MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

Msajili wa Vyama vya Siasa.Mhe. Jaji Mstaafu Francis Mtungi akichangia hoja wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Msaji wa Vyama vya Siasa (ORPP) kilichofanyika katika ukumbi wa Veta jijini Dodoma  tarehe 10/01/2020. Kulia ni Maafisa Utumishi wa ORPP, Bibi Eneja Mwakanyamale na Happiness Muyombo.

FLAVIANA MATATA AONGOZA WANAMITINDO WENZAKE KUTEMBELEA HIFADHI YA SERENGETI




Mwanamitindo maarufu Duniani Mtanzania anayefanya shughuli zake nchini Marekani,Flaviana Matata ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii akiwa ameambatana na Wanamitindo wenzake kutoka Marekani.

Flaviana Matata  ameongozana na wanamitindo hao akiwemo: Shelby Colemans, Daniella Evans na Awa Florence Mafany ambao kila mmoja anafanya shughuli za mitindo huku wakiwa na wafuasi wengi kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Flaviana Matata akiwa na rafiki zake hao, wameweza kushuhudia vivutio vya utalii ndani ya Serengeti ikiwemo wanyama mbalimbali sambamba na uzuri wa Hifadhi hiyo ambayo ni kubwa hapa Nchini.

Ziara hiyo ya kuambatana na Wanamitindo hao ni kwa lengo la kuona vivutio vya utalii vilivyoko katika hifadhi na kuvitangaza.

SERIKALI YAONYA WANANCHI WANAOJENGA MIJINI BILA KUFUATA UTARATIBU

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi aonya wananchi wanaojenga mijini bila kufuata utaratibu. 



Lukuvi ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Ndachi Kata ya Mnadani jijini Dodoma wakati akikagua nyumba ambazo zimejengwa bila kufata utaratibu na kukosa vibali vya ujenzi.

 
Waziri wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Willam Lukuvi

Waziri Lukuvi alifikia hatua ya kusimamisha ujenzi kwa kuziwekea alama nyumba ambazo ujenzi wake umekiukwa na kuwaamuru wamiliki kusitisha shughuri zote hadi wafuate utaratibu.



Hata hivyo Mhe. Lukuvi amesema Serikali haina mpango wa kubomoa nyumba za wananchi isipokuwa wananchi wanatakiwa kujenga kwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kupata kibali cha ujenzi.

Sunday, January 12, 2020

WAZIRI DKT. KALEMANI AKAGUA TENA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA MAJI WA JULIUS NYERERE MW 2115, AAGIZA WAKANDARASI KUHAKIKISHA WAFANYAKAZI WAO WOTE WANAHAMIA ENEO LA MRADI



NA MWANDISHI WETU, RUFIJI

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, amefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere Mw 2115 (JNHPP) uliotimiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa utekelezaji wake. Dkt. Kalemani ameridhishwa na hatua mbalimbali ambazo mradi huo unaotekelezwa kwenye mto Rufiji kwenye mpaka wa mikoa ya Pwani na Morogoro umefikia tangu kuanza kwa ujenzi wa mradi. 

Aidha, alitoa maagizo kwa Wakandarasi kuhakikisha Wafanyakazi wao wote wanahamia eneo la mradi, huku akitoa mwezi mmoja kwa wafanyakazi wengine wa mradi wawe wamehamia. "Wafanyakazi wote wakae eneo la mradi, hii itaharakisha mradi kukamilika mapema na haraka", alisema Dkt. Kalemani. 

Pia, alisisitiza kazi zote zinazohusu utoaji huduma zifanywe na Makampuni ya kitanzania ikiwemo Wakandarasi wasaidizi. Mkataba wa ujenzi mradi wa Julius Nyerere ulisainiwa Desemba 12, 2018 Ikulu Jijini Dar ea Salaam ambapo Mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi Februari 14, 2019 na kuanza kazi za maandalizi ya ujenzi kwa kipindi cha miezi sita, ambapo mwezi Juni 2019 alianza rasmi kazi za ujenzi. Mradi wa Julius Nyerere unatarajiwa kukamilika 14 Juni 2022
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, (kushoto), akimsikiliza Mratibu wa ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius NyerereMw 2115 (JNHPP) wa mto Rufiji mkoani Pwani, Mhandisi Steven Manda wakati alipofanya ziara ya kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi  huo.
 Dkt. Kalemani (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kushoto kwa waziri), wakati wa ziara hiyo  Januari 12, 2019.





Tuesday, January 7, 2020

MFUMO WA MALIPO KWA MATOKEO KUIMARISHA MIOUNDIMBINU YA MAJI VIJIJINI

Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa


Serikali  katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 imepanga kutumia Tsh. Bilioni 301 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maji vijijini inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo fedha za ndani ni Tsh. Bilioni 224.03 na fedha za nje ni Tsh. Bilioni 77.22.

Pamoja na juhudi hizo za Serikali sekta ya maji imekuwa inakabiliwa na changamoto ya upotevu wa maji kutokana na uchakavu wa miundombinu iliyojengwa miaka mingi iliyopita.

Katika kukabiliana na changamoto hizo, Serikali imeendelea na jitihada za uwekezaji katika ukarabati wa miundombinu chakavu maeneo mbalimbali ya mijini ikiwemo Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mwanza, Morogoro, Singida pamoja na ukarabati wa miradi ya kitaifa ya Makonde, Wanging’ombe, Maswa, Mugango Kiabakari na Chalinze.

Tanzania kupitia miradi ya maji vijijini imejenga zaidi ya vituo 80,000 vya maji ambavyo vimeunganishwa na mfumo wa maji ya bomba, ambapo baadhi ya vituo vimechakaa na kuhitaji matengenezo lakini ukosefu wa takwimu sahihi juu ya vituo hivyo kunaikwamisha Serikali kupanga bajeti ya kuwapatia wananchi wa vijijini huduma bora ya maji.

Takwimu zilizopo katika Ripoti ya Maendeleo ya Sekta ya Maji ya mwaka 2016, zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2010/11 na mwaka 2015/16, Serikali ilipanga kujenga jumla ya vituo vya maji 99,515 lakini ilishia kujenga vituo 42,718 pekee.

Ripoti hiyo iliyotolewa Oktoba mwaka 2016 inaeleza kuwa theluthi moja ya miradi hiyo ya maji haikutekelezwa ndani ya awamu ya kwanza ya Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDPI) jambo lililofanya baadhi ya vituo vya maji vichelewe kujengwa.

Ili kuboresha upatikanaji wa maji maeneo ya vijijini, Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo imeendelea kuimarisha Programu ya Uendelevu wa Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini kwa kutumia Mfumo wa Malipo kwa Matokeo (Payment by Results – PbR) unaolenga kuongeza kasi ya uendeshaji, matengenezo na ukarabati wa miundombinu ya miradi ya maji vijijini.

Kupitia Programu hiyo, Serikali imeanza kuziwezesha Halmashauri za Miji nchini kuviendeleza vituo vya maji vilivyopo na kutumia takwimu kujenga vingine vipya katika maeneo yenye uhitaji mkubwa wa maji.

Ili kufikia malengo ya Programu hiyo, mwaka 2017 wataalamu hao walitembelea vituo 9,0000 katika Halmashauri 56 nchini vijiji ili kujionea hali halisi ya utendaji wa vituo vya maji, ambapo ilibainika kutofautiana kwa taarifa za baadhi ya vituo zilizopo Wizara ya Maji na Umwagiliaji na eneo kilipo ikizingatiwa kuwa maeneo mengi ya vijijini hayana anuani na mitaa yenye mpangilio mzuri.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020, Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa anasema katika jitihada za kuhakikisha miradi ya maji vijijini inakuwa endelevu, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) inatekeleza Mpango wa Mfumo wa Malipo kwa Matokeo (Payment by Results – PbR) ambao una lengo la kuimarisha uendelevu wa miradi ya maji vijijini.

Anasema kuwa hadi April 2019, awamu ya pili ya programu hiyo imekamilika ambapo Halmashauri 95 zilifuzu na kupewa Shilingi bilioni 8.55 kati ya Shilingi bilioni 53.6 zilizotengwa katika mwaka 2017/2018, ambapo awamu ya tatu inaendelea na inahusisha Halmashauri 181 ambazo zitapewa fedha kwa vigezo vya idadi ya vituo vilivyojengwa na kutoa maji.

‘Kupitia PbR, Paundi 300 hutolewa kwa kila kituo kilichohakikiwa na kinachofanya kazi na Paundi 1,500 hutolewa kwa kituo kipya kitakachojengwa, Katika mwaka 2018/2019, jumla ya Paundi milioni 10 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza programu hiyo kwenye Halmashauri zote nchini’’ alisema Waziri Mbarawa.

Aliongeza kuwa Hadi mwezi Aprili 2019, fedha zilizolipwa katika awamu ya tatu ni Paundi milioni 8.7 sawa na Shilingi bilioni 25.43. Katika mwaka 2019/2020, Shilingi bilioni 46.47 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa programu hiyo.

Maji ni rasilimali muhimu kwa maisha ya binadamu na maendeleo ya jamii na sekta mbalimbali za kiuchumi zikiwemo viwanda, kilimo, uvuvi na utalii, ili kufikia azma ya Serikali ya kuwapatia wananchi majisafi na salama pamoja na kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kufikia mwaka 2025, Wizara inatekeleza mipango mbalimbali.

Ni wajibu wa wananchi na wadau wote kuhakikisha kunakuwepo na upatikanaji wa takwimu na taarifa za mwenendo wa rasilimali za maji ili kuimarisha usanifu wa miundombinu ya kusambaza maji nchini. 
Na Ismail Ngayonga,MAELEZO

DAR ES SALAAM

WAZIRI JAFO ATAKA WANAFUNZI KUTOZUIWA KUANDIKISHWA SABABU YA KUKOSA VYETI VYA KUZALIWA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI  Selemani Jafo akikagua miundombinu katika shule ya sekondari Bahi wakati wa ziara yake kuangalia mapokezi ya kidato cha kwanza na uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la darasa la kwanza mapema  Mkoani Dodoma
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Selemani Jafo  amesema ni marufuku mwanafunzi kuzuiliwa kuandikishwa darasa la kwanza kwa sababu ya kukosa cheti cha kuzaliwa.

Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara yake Wilayani Bahi kukagua uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa shule za msingi pamoja na mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule za sekondari.

Amesema amepokea malalamiko kutoka baadhi ya maeneo kuwa wanafunzi wa darasa la kwanza hawaandikishi kama hawana vyeti vya kuzaliwa.

“Nimeona nitoe ufafanuzi kuhusu suala hili kuwa cheti cha kuzaliwa ni haki  ya kila mtoto lakini isimzuie mtoto huyo kuanza shule eti kwa sababu tu hajapata cheti hicho; Watoto wote wapokelewa, waandikishwe na waanze masomo huku wazazi wao wakiendelea na mchakato wa kuwatafutia vyeti hivyo.
 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI,  Selemani Jafo akizungumza na viongozi na watumishi wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma alipofika kukagua miundombinu ya Shule ya Sekondari Bahi.
 
Sitaki kusikia eneo lolote mtoto ameachwa kupokelewa na kuanza shule kwa sababu ya kukosa cheti cha kuzaliwa, mzazi ahakikishe ndani ya miezi minne amepata cheti hicho lakini mtoto huyo aanza masomo wakati masuala ya cheti yanaendea kushughulikiwa kwenye mamlaka husika," Amesema Jafo.

Akizungumza wakati akikagua mapokezi ya kidato cha kwanza amesema wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika muda uliopangwa na wapokelewe bila masharti ya kuleta unga, mahindi au maharage.

Pia Waziri Jafo amepongeza uongozi wa Wilaya ya Bahi kwa umakini waliouonyesha katika zoezi zima za uandikishaji wa darasa la kwanza linaloendelea na maandalizi mazuri katika mapokezi ya kidato cha kwanza, halkadhalika katika usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Munkunda amesema katika Halmashauri ya Bahi walishafanya kampeni ya upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano hivyo watoto wengi wanaonza shule hivi sasa wanavyo vyeti hivyo na endapo mtoto yeyote atakua hajapa basi ataandikishwa shule ndipo mchakato kwa cheti utafuata.
 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo (katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Mwanahamisi Munkunda wakati Waziri Jafo alipofika wilayani hapo kukagua miundombinu ya Shule ya Sekondari Bahi.
 
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI


Kwa upande wa mapokezi ya kidato cha kwanza amesema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Wilaya ya Bahi ni 2712 na changamoto iliyopo ni uhaba wa madawati ambayo wameshaanza kuitatua kwa kuchonga madawati yatakayokidhi idadi ya wanafunzi hao.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mkakatika John Laurent Josephat amesema shule yake ina malengo ya kaundikisha wanafunzi 180 na kwa siku ya kwanza tu shule ilivyofunguliwa wameandikisha wanafunzi 134.

“Wanafuzi wote walioletwa shuleni kwetu tumewaandikisha na endapo mtoto hana cheti cha kuzaliwa tulitumia kadi la Kliniki kupata taarifa sahihi za mtoto na hatujarudisha mwanafunzi hata mmoja wote wamewpokelewa na wameanza masomo” Amesema Mwl Josephat.

Ameongeza kuwa uandikishaji huu kwa siku ya kwanza tu ni zaidi ya aslimia 70 hivyo anategemea tutaandikisha zaidi ya malengo waliyojiwekea.

Shule ya msingi Mkakatika ni miongoni mwa shule bora katika Wilaya ya bahi na ndiyo iliyoongoza kwa kuwa shule ya kwanza kiwilaya katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2019.
 

BARABARA YA KOANI -JUMBI ZANZIBAR YAWEKEWA JIWE LA MSINGI



Waziri wa Ardhi Nyumba ,Maji na Nishati Salama Aboud Talib akifungua kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya Kati Unguja .Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Barabara ya kilomita 6.3 ya Koani -Jumbi iliowekwa Jiwe la msingi na  Waziri wa Ardhi Nyumba ,Maji na Nishati Salama Aboud Talib.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi ,Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe akitoa maelezo ya Kitaalamu kuhusu Ujenzo wa Barabara katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya Kati Unguja .Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Naibu Waziri wa Ujenzi ,Mawasiliano na Usafirishaji Mohamed Ahmed Salum akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya Kati Unguja .Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ardhi Nyumba ,Maji na Nishati Salama Aboud Talib akitoa hotuba ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya Kati Unguja .Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.PICHA N A YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
…………………..
Na  Kijakazi Abdalla,Maelezo  .

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kuzijenga barabara kwa kiwango cha lami barabara ambazo hazijajengwa katika Mkoa wa Kusini ili kuhakikisha  wananchi wanaondokana na usumbufu.

Hayo ameyasema Waziri wa Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Salama Aboud Talib mara baada ya kuweka jiwe la msingi Barabara ya Koani Jumbi ikiwa ni shamra shamra za Sherehe za miaka 56 Mapinduzi matukufu ya Januari 12.
Amesema katika kipindi cha miaka 56 ya Mapinduzi Zanzibar mtandao wa barabara za Unguja na Pemba umeimarika hivyo jitihada  zitachukuliwa ili kuhakisha zinakuwa za kiwango kinachohitajika.

Aidha amesema kuimarika kwa miundo mbinu ya barabara ni moja ya jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika awamu ya saba ya uongozi wa Dkt Ali Mohamed Shein.Hata hivyo Waziri Salama aliwataka wakandarasi kuwa makini wanapojaza mikataba ya ujenzi wa barabara ili kuhakikisha ujenzi unamalizika kwa wakati ambao umepangwa.

Vilevile amewataka Madereva wa vyombo vya moto wanaotumia barabara wawe wangalifu na kufuata alama ambazo zilizokwekwa ili kuondoa ajali zisizotarajiwa.Pia amewata wananchi wa Zanzibar kuepuka kujenga katika maeneo ya hifadhi ya barabara ili kuondosha usumbufu na kuepuka kuvunjia pale utanuzi unapohitajika kufanywa.

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Abuod Jumbe amesema jitihda za kuimarisha miundo mbinu ya barabara zinaimarika kwa kuhakisha wananchi wa mjini na vijijini wananapata huduma zenye uhakika.Aidha amesema katika kuhakisha wananchi wanajengewa barabara zenye ubora tayari Wizara imeweza kulipa fidia za vipando kwa wale wote waliongo’lewa.

Nae Mkandarasi  wa Kampuni ya Mecco Nassor Ramadhan Korowa amesema watahakikisha ujenzi wa barabara ya Jumbi Koani unakamilika kwa wakati ili kuhakisha wananchi wanaondokana na usumbufu.Ujenzi wa Barabara wa Jumbi Koani unatarajiwa kuwa na urefu wa kilomita 6.3 na upana wa mita 7 utagharimu Bilioni 5 na unatarajiwa kumaliza mwishoni mwa mwezi wa Febuari mwaka huu.

Friday, January 3, 2020

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, AWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA RUANGWA, MKOANI LINDI

Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, akimjulia hali Mzazi, Zena Issa, wakati altpotembelea Wodi ya Wazazi, katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 2, 2020.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwa na Mkewe Mary, wakimsalimia Mzazi, Zulfa Juma, wakati wakiwajulia hali wagonjwa, katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 2, 2020.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kuwajulia hali wagonjwa, katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 2, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)