Wednesday, July 31, 2019
Tuesday, July 30, 2019
WAZIRI WA NISHATI AAGIZA MKANDARASI KUTOA AJIRA 50 KWA VIJANA WA KARATU
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
Waziri
wa Nishati Dk.Medard Kalemani amemwagiza Mkandarasi wa Kampuni ya
Nipo Group Mhandisi Shija Magese kuhakikisha anatoa ajira kwa vijana 50
wa Kijiji cha khusumay Wilayani Karatu, ili wasaidie kazi za uwekaji
umeme kwenye Vijiji 39 vya wilaya hiyo.
Alitoa
agizo hilo jana alipotembelea Wilaya hiyo na kuzindua Rea awamu ya
tatu, iliyofanyika kiwilaya katika Shule ya Sekondari ya Baray Khusumay
na kuhudhuriwa na wananchi wa Wialaya hiyo.
Alisema
ameagiza utoaji wa ajira hiyo kwa sababu mkandarasi huyo amepewa
kumaliza kazi ya uwekeaji miundombinu ya umeme na kuwaunganishia
wananchi nishati hiyo kwa muada wa miezi 24, lakini mpaka sasa bado nusu
ya kazi hajamaliza.
“Sasa
naagiza ajiri vijana 50 wa eneo hili ili muda wako tuliowekeana mkataba
umalize ni Juni mwaka 2020, lakini nataka umalize kazi hii Desemba 30
mwaka huu, sasa hawa vijana watakusaidia na wakati huo watanufaika na
ajira na Meneja wa Wilaya simamia hawa,”alisema
Dk.Kalemani
aliahidi kurudi kijijini hapo kufuatilia kama kazi hiyo imeisha kwa
wakati muafaka ili wananchi wapate umeme na kuzalisha viwanda
vidogovidogo.
Aidha
aliagiza Meneja wa Wilaya hiyo Tanesco, Edward Mwakapuja kufungua vituo
kwenye vijiji husika ili wananchi wapate unafuu wa kuwafikia na kulipa
Sh.27,000 ili waunganishiwe umeme huo wa Rea.
Pia
aliwataka Wafanyakazi wa Tanesco kuhakikisha wanafanya kazi za kuhudumia
wananchi na kuepuka kuvaa suti kama wanakwenda Kanisani.
“Nimepiga
marufuku wafanyakazi Tanesco kuvaa suti labda kama mnaenda kanisani
Jumapili, sababu hapa kazi tu, suti na kazi wapi na wapi acheni kabisa
pigeni kazi,”alisema Aliwasisihi pia wanachi hao kutunza miundombinu ya umeme wakiwekewa ili waendelee kunufaika nao na kupata maendeleo.
Dk.Kalemani
aliwaagiza wanafunzi wa Shule yya Sekondari ya Baray Khusumay
kuhakikisha wanafanya vizuri masomo yao na kufaulu vizuri kwa sababu
umeme wameshapata.“Someni
usiku na msachan lakini pia umeme huu utawamulika msifanye maovu maana
shule hii ya wavulana na wasichana mkisimama kwa yale mambo yenu umeme
huu utawamulika, someni mfaulu na shule hii mpya,”alisema
Kuhusu
suala la kukatika kwa umeme aliagiza Tanesco kuhakikisha wanamaliza
tatizo hilo harka, sababu umeme upo wa kutosha hadi ziada.
Mkuu
wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo alishukuru serikali kwa
kuwafikishia umeme kijiji hicho ambacho tangu Uhuru hakijawahi pata
umeme, lakini aliomba Waziri kufuatilia changamoto ya kukatika kwa umeme
mara kwa mara wilayani humo.
“Tunaamini
tatizo hili litaisha baada ya uzinduzi wa Rea awamu ya tatu kufanyika,
sababu kukiwa na umeme tunaamini usalama utakuwa juu na hata ufaulu
kwenye shule utaongezeka,”aisema
Akijibu
suala la kukatika kwa umeme, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Mhandisi
Herin Mhina alisema sababu ya kukatika kwa umeme huo kulitokana na
utengenezaji wa nguzo zaidi ya 600 ambazo zimewekwa mpya.
Kwa
upande wake Mkandarasi wa kampuni ya Nipo Group Shija Magese, aliahidi
kumaliza kazi hiyo Desemba mwaka huu na mpaka sasa kati ya Vijiji 39
anavyotakiwa kuweka umeme wa Rea, vijiji 23 ameshajenga miundombinu ya
kuweka umeme na kati ya hivyo nane ameshawasha umeme.
Wafanyakazi
kutoka kampuni ya Booygues Energies &services wakiendelea na
Mradi wa ujenzi wa njia za kusafirisha umeme Kenya-Tanzania Power
Interconnection (KTIPIP)ZTK wa laini kubwa ya msongo wa kilovolti 400
inayoanzia Singida unapita Babati nakuja mkoa wa Arusha hadi Namanga
,ujenzi huo unaendelea katika kijiji cha Kisongo jijini Arusha (Picha na
Woinde Shizza, Arusha
WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani akiongea na wananchi .
WAZIRI
wa Nishati Dk.Medard Kalemani alipotembelea Wilaya ya Karatu na
kuzindua Rea awamu ya tatu, iliyofanyika kiwilaya katika Shule ya
Sekondari ya Baray Khusumay
WAZIRI
wa Nishati Dk.Medard Kalemani akiongea na viongozi wa Tanesco pamoja
na mkuu wa wilaya ya karatu wakati alipotembelea kituo cha Tanesco cha
wilaya hiyo .
MAKAMU WA RAIS AZINDUA MRADI WA KUTOKOMEZA UNYANYASAJI DHIDI YA WANAWAKE
Na Charles James, MICHUZI TV
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa kutokomeza vitendo
vya unyanyasaji na udhalilishaji dhidi ya Wanawake na Watoto kwenye
masoko na kushauri elimu iendelee kutolewa kupitia mikutano ndani ya
Mitaa na Kata.
Hayo
ameyasema leo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi huo ambapo amesema katika
kupambana na vitendo hivyo vya kikatili Serikali imeimarisha utendaji
wa madawati 417 ya jinsia na watoto yaliyopo katika vituo vya Polisi
nchini kwa lengo la kuwezesha huduma stahiki kwa watu wanaofanyiwa
ukatili wa kijinsia.
Mama
Samia ameitaka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kushirikiana na Jumuiya ya
Tawala za Mitaa ambao ndio waratibu wa mradi huo katika kuhakikisha afua
zinazotekelezwa kupitia mradi huo zinakua endelevu hata pale
utekelezaji wa mradi unapofikia mwisho.
"
Ndugu zangu kila mmoja wetu ana haki ya kupinga na kutokomeza ukatili wa
kijinsia, hivi vitendo havikubaliki na wala haviruhusiwi kisheria.
Yeyote atakayethubutu kumdhalilisha mwanamke au mtoto tutamchukulia
hatua kali.
" Ni
jambo la aibu kuona tunatumia viungo vya wanawake kama matusi, huyu
mwanamke unayemdhalilisha tukumbuke ni kama mama zetu majumbani mwetu,
hatuwezi kuwa na Taifa lenye amani kama tutaruhusu vitendo hivi,
tuungane katika kupiga vita na kutokomeza ukatili wa kijinsia, " amesema
Mama Samia.
Akizungumzia
ombwe la watoto wadogo kufanya biashara kwenye masoko, Mama Samia
amezitaka kamati za masoko kuhakikisha zinashirikiana na mamlaka husika
katika kuzuia watoto kufanya biashara sokoni na badala yake wawahimize
kwenda shule na kuwaripoti wazazi wanaowatuma watoto wao kufanya
biashara.
"
Serikali yenu ya awamu ya tano iliwaahidi elimu bure kwa shule ya msingi
hadi kidato cha nne. Tunapoona watoto wetu hawaendi shule na wanafanya
biashara sokoni tunakua hatumtendei haki Rais wetu Dk John Magufuli kwa
zawadi ya elimu bure aliyotuletea. Tuwazuie watoto kufanya biashara
sokoni na tushirikiane kuwapeleka shule," amesema Mama Samia.
Aidha
katika kutekeleza mradi huo, Mhe Makamu wa Rais amekabidhi Pikipiki 14
kwa ajili ya wataalam wa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Dodoma kwa Kata
za Halmashauri ya Chamwino na kuielekeza Wizara kuendeleza utaratibu huo
wa kupatia wataalamu hao usafiri ili iwe rahisi kwao kuwafikia wanawake
wengi hususani wa vijijini na kuwaunganisha na fursa za kiuchumi.
Kwa
upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe Ummy Mwalimu amemshukuru Makamu wa Rais kwa kuzindua mradi huo
ambao utakua msaada mkubwa katika mapambano dhidi ya ukatili wa
kijinsia.
" Mhe
Makamu wa Rais kama Wizara tumejipanga katika kuhakikisha tunaongeza
elimu zaidi kwa wananchi iki tuzidi kupunguza wimbi la vitendo hivi,
lengo letu ni kutokomeza kabisa vitendo hivi ili kuwa na Taifa imara
ambalo litakua na mshikamano na amani baina yetu bila kujali huyu ni
Mwanaume au Mwanamke," amesema Waziri Ummy.
Nae
Mwenyekiti wa ALAT Mhe Gulamhafeez Mukadam amesema kuna changamoto
kwenye dira ya pamoja juu ya utokomezaji wa vitendo vya ukatili wa
kijinsia jambo ambalo linaleta athari ya maendeleo ya wanawake na hivyo
kuzorotesha uchumi wa Nchi.
"
Nimpongeze Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Mhe Godwin Kunambi kwa namna
ambavyo amekua msaada kwa akina Mama wa Jiji hili kwa kuwapatia mikopo
inayowawezesha kufanya biashara zao. Serikali za Mitaa jukumu lao ni
kuwawezesha wananchi wao kuzipata fursa.
"
Lakini pia kuna changamoto ya masoko, lugha chafu kwa wanawake sokoni
hizi changamoto zinapaswa kushughulikiwa na kutokomezwa kabisa.
Tukiwawezesha wanawake na kuwaepusha na vitendo vya unyanyasaji tutakua
tunatengeneza Taifa imara na madhubuti na kuweza kufikia azma ya Mhe
Rais ya uchumi wa kati kupitia viwanda," amesema Mhe Mukadam.
Makamu
wa Rais Mhe Mama Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi
wa mradi wa kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya
wanawake na watoto katika maeneo ya masoko. Uzinduzi huo umefnyika
jijini Dodoma.
Wananchi
waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa kutokomeza vitendo vya kikatili
dhidi ya wanawake wakimsikiliza mgeni rasmi ambaye ni Makamu wa Rais Mhe
Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) jijini Dodoma.
Maafisa
Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wakiwa na
pikipiki walizokabidhiwa na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan
jijini Dodoma. Pikipiki hizo zimelenga kuwasaidia katika kuwafikia kundi
kubwa la wanawake ambao wanafanyiwa unyanyasaji wa kijinsia.
RAIS MAGUFULI ATOA POLE KWA FAMILIA KIFO CHA MEJA JEN MSTAAFU ALBERT LAMECK MBOWE
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisalimiana
na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa marehemu Meja
Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam, mara baada ya
kuwasili nyumbani kwa Marehemu Salasala kwa ajili ya kutoa pole kwa
Familia Julai 30,2019.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa pole
kwa Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe
aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Jijini Dar es Salaam ikiongozwa na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni
kaka wa Marehemu nyumbani kwao Salasala Dsm. Julai 30,2019.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza
na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemu mara
baada ya kutoa pole kwa Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert
Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza
na Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe
aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Jijini Dar es Salaam ikiongozwa na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni
kaka wa Marehemu nyumbani kwao Salasala Dsm. Julai 30,2019.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiomba dua
maalumu na Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe
aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Jijini Dar es Salaam iliyoongozwa na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni
kaka wa Marehemu nyumbani kwao Salasala Dsm. Julai 30,2019.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza
baada ya kuomba dua maalumu na Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu
Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam iliyoongozwa na Mhe. Freeman Mbowe
Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemu nyumbani kwao Salasala Dsm.
Julai 30,2019.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza
na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemu pole
kwa Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe
aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Jijini Dar es Salaam alipowatembelea nyumbani kwao Salasala Dsm kwaajili
ya kutoa pole kufuatia msiba huo. Julai 30,2019.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiagana na
Waombolezaji wengine akiwa ameambatana na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa
Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye
pia ni kaka wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe
aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutoa pole kufuatia msiba huo
nyumbani kwao Salasala Dsm. Julai 30,2019.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiagana na
Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemu Meja Jenerali
Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutoa
pole kufuatia msiba huo nyumbani kwao Salasala Dsm. Julai 30,2019.
Monday, July 29, 2019
Saturday, July 27, 2019
WAZIRI MKUU ATAKA RUVUMA IONDOE VIKWAZO VYA UWEKEZAJI
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Ruvuma uendelee
kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo na kuondoa vikwazo vyote ili
kuvutia wawekezaji zaidi.
“Mkoa
wa Ruvuma kama ilivyo mikoa mingine, unazo fursa ambazo zikiendelezwa,
zitaleta tija na kusaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa
letu. Nitoe rai kwa mkoa uendelee kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo
sambamba na kuondoa vikwazo vyovyote vya uwekezaji na biashara ili
kuvutia zaidi wawekezaji wa ndani na nje,” amesema.
Ametoa
wito huo leo mchana (Alhamisi, Julai 25, 2019) wakati akifungua
Kongamano la Biashara na Uwekezaji mkoani Ruvuma linaloendelea kwenye
uwanja wa Majimaji, Manispaa ya Songea. Pia amezindua Mwongozo wa
Uwekezaji wa mkoa huo.
Amesema
katika ustawi wa uchumi, nchi nyingi hapa duniani zimeweza kukuza
uchumi wao kupitia ujenzi wa viwanda na zikafanikiwa kupunguza umasikini
katika jamii zao. Amezitaja nchi hizo kuwa ni Marekani, China, Japani,
Korea ya Kusini na Ujerumani.
“Tunapaswa
kuiga kutoka wa wenzetu. Ndiyo maana Tanzania pia tunahamasisha ujenzi
wa viwanda kuanzia ngazi ya vijiji mpaka mikoa ili tulete mageuzi ya
kiuchumi yatakayowezesha upatikanaji wa ajira na hatimaye kuondoa
umaskini,” amesema Waziri Mkuu na kuongeza:
“Kongamano
hili ambalo kaulimbiu yake ni “Ruvuma itavuma kwa uchumi wa viwanda,
wekeza sasa,” imelenga kutangaza fursa za uwekezaji na biashara zilizopo
mkoani humu, na inajipambanua vema na kuendana na azma ya Serikali ya
awamu ya tano ya kujenga uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo
2025.”
Amesema
mchango wa sekta ya viwanda kiuchumi na kijamii nchini ni pamoja na
kuongeza pato la Taifa na kupandisha hali ya maisha ya wananchi;
kusaidia nchi isiyumbe kiuchumi ikizingatiwa kuwa viwanda vingi
havitegemei hali ya hewa kama kilimo; kuboresha urari wa biashara
(improve balance of trade) kwa sababu tija yake ni kubwa na hasa
zikiuzwa bidhaa nyingi nje ya nchi na kupunguza uagizaji wa bidhaa
kutoka nje ya nchi.
Amezitaja
faida nyingine kuwa ni kuchangia maendeleo ya sekta nyingine kama za
kilimo, uvuvi, elimu na madini; kutengeneza ajira kwa wananchi;
kuchagiza na kuharakisha maendeleo ya teknolojia na rasilimali watu na
kuwezesha matumizi mazuri ya maliasili zilizopo kwa faida zaidi.
Nyingine
ni kuleta uhakika wa soko la mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na
madini kwa sababu hutumika kama malighafi na kuwepo kwa uhakika wa
kuingiza fedha za kigeni nchini kupitia mauzo ya bidhaa nje ambapo
husaidia kuagiza mitambo, malighafi na bidhaa nyingine ambazo
hazizalishwi nchini.
Mapema,
akitoa salamu kwa niaba mabalozi wengine, Mwakilishi wa Balozi wa
China, Bw. Xian Bing alisema ana uhakika kuwa kongamano hilo
litafanikiwa kuleta mabadiliko mkoani humo kwa sababu wana bidii ya
kazi.
“Ninaahidi
kuleta wawekezaji kutoka China kwa sababu tunataka waje kuleta
teknolojia mpya, wafanye kazi pamoja na Watanzania na wawafundishe
teknolojia hizo mpya. Tunataka hapa Ruvuma iwe model (mfano) kwa mikoa
mingine,” alisema.
Akielezea
kwa kifupi kuhusu mwongozo uliozinduliwa na Waziri Mkuu, mtafiti kutoka
Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Hoseana Lunogelo
alisema walitumia mfumo shirikishi ili kupata mwongozo unahusisha
wawekezaji wa ndani.
“Mwongozo
huu umezingatia Dira ya Taifa ya 2025 katika kutimiza azma ya Serikali
ya kuwa nchi ya uchumi na viwanda, tumeshirikisha wananchi wa mkoa wa
Ruvuma ili wasibakie kuwa watazamaji,” alisema.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kufungua
maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai
25.2019.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa
China Tanzania, Bwana Xian Ding, wakati alipoipongeza Serikali ya awamu
ya tano katika kuwaletea wananchi wake maendeleo, kwenye maonesho ya
viwanda na kongamano la uwekezaji,yaliyofanyika katika Mkoa wa Ruvuma,
Julai 25.2019.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kitabu cha muongozo wa uwekezaji katika
Mkoa wa Ruvuma, kwenye maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji
mkoani Ruvuma. Julai 25.2019. Tokea kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje John Ndumbalo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa amebeba mkaa wa mawe, wakati akikagua
mabanda kwenye banda la TANCOAL, katika maonesho ya viwanda na
kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019. Tokea kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme na kulia ni Mkuu wa Jiolojia
TANCOAL.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mkaa wa mawe, uliyotengenezwa kwa
ajili ya matumizi ya nyumbani na wajasiriamali wa kikundi cha Mbalawala
Women Group, wakati akikagua mabanda kwenye maonesho ya viwanda na
kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019. Tokea kulia ni
Meneja wa Fedha wa kikundi hicho, Esta Silas na Msimamizi wa Mradi,
Hajra Yakub.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Christina Mndeme (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya
Mbinga Coffee Curing Company, kabla ya kufungua maonesho ya viwanda na
kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Christina Mndeme, akiangalia na vikundi vya ngoma, kwenye maonesho ya
viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019.(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.SHEIN AWASILI ZANZIBAR AKITOKEA NCHINI UINGEREZA KWA ZIARA MAALUM
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi
Seif Ali Iddi, alipowasili Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume
Zanzibar akitokea Nchini Uingereza kwa ziara Maalum.(Picha na Ikulu)
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar,
alipowasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar
akitokea Nchini Uingereza, alipokuwa na ziara Maalum.,(Picha na Ikulu)
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,, akisalimiana na Wananchi
waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar
kumpokea akitokea Nchini Uingereza kwa ziara Maalum.(Picha na Ikulu)
Friday, July 26, 2019
HIFADHI MPYA YA MWL.NYERERE KUKUZA UTALII SELOUS.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka wizara ya Maliasili na Utalii
kutenganisha eneo la uwindaji Selou (Hunting block) kwa kutengeneza
Hifadhi ya Taifa ambayo itaitwa Hifadhi ya taifa ya Mwalimu Julius
Nyerere.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji
mkoani Pwani utakaozalisha megawatt 2,115, Rais Magufuli amesema kuwa
eneo la uwindaji la Selou ni eneo ambalo limezunguka mradi huo mkubwa wa
umeme na lina urefu wa kilomita za mraba elfu 57.
“Eneo
la Selou ni eneo kubwa ambalo linachukua takribani kilomita 50, hivyo ni
lazima Wizara itenge eneo ambalo litatengenezwa na kuwa Hifadhi kuweza
kukidhi mahitaji ya utalii na kukisaidia kizazi kijacho kuendelea kuenzi
mambo ambayo ameyafanya baba wa Taifa,” amesema Rais Magufuli.
Amesema
maeneo ya uwindaji wa wanyama yanafikia 47 katika mbuga ya wanayama
Selou hivyo Wizara ya Maliasili lazima itenge eneo la hifadhi na la
uwindaji, ili kuimarisha utalii na kuvutia watalii wengi katika mbuga
hiyo
Rais
Magufuli alisisitiza kuwepo kwa utaratibu kwa Wizara ya Maliasili na
Utalii kuangalia maeneno ambayo yanavitalu wa uwindaji ili kuhakikisha
kuwa Serikali inafaidika na maeneno hayo, pia aliagiza barabara ya
kutoka Fuga kilomita 60 kwenda mahari ambapo mradi unajengwa ianze
kutengenezwa kwa rami ili kufungua sekta ya utalii katika Mbuga ya
wanayama Selous.
Aidha,
Rais Magufuli amesema kuwa mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji ni mradi
ambao unaweza kudumu kwa muda wa miaka 60 ambapo utasaidia kuzalisha
umeme wa kutosha na kusaidia Tanzania kuweza kutekeleza malengo ya
milenia ya maendeleo endelevu.
Amesema
mradi wa mto Rufiji utasaidia kuchochea maendeleo katika sekta ya
viwanda ambapo wewekezaji wataweza kupata umeme wa uhakika na kwa bei
nafuu na wenye kuaminika ili kuweza kuzarisha bidhaa zenye ubora.
“Mradi
huu wa umeme wa mto Rufiji unaweza kudumu kwa muda wa miaka 60 na
kusaidia watanzania kupata umeme wa uhakika na wenye gharama nafuu ambao
utasaidia wawekezaji kupata huduma ya umeme kwa uhakika bila mgao ili
kuweza kuzarisha bidhaa zenye ubora na kuweza ushindano kwenye masoko
mbalimbali ya kimataifa,” amesema Rais Magufuli.
Rais
Magufuli alisisitiza kuwa katika utekelezaji wa mradi huo, mkandarasi
anatakiwa kutumia wafanyakazi walioko karibu kwa kazi ambazo siyo za
kitaalamu, akasisitiza ajira zitolewe kwa wenyeji wa maeneo ya mradi kwa
mikoa ya Morogoro na Pwani, na amewataka wananchi kuchangamkia fursa
kwa miezi hiyo 36 ya ujenzi.
Kwa
upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema kuwa Ndoto
ya Rais Magufuli ya kuenzi mambo makubwa ya Baba wa Taifa, Mwl.Julias
Nyerere ikiwemo utekelezaji wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme katika
maporomoko ya maji ya mto Rufiji.
“Mhe.
Rais, ndoto yako leo imeanza kupata mafanikio, ndoto yako ni kupeleka
umeme hadi kule kijijini kwa wananchi wa kawaida na umetoa agizo kuwa
kila nyumba ya mtanzania iwe ya bati, nyasi au tembe lazima iwake umeme,
kwa hiyo umeme huu ambao ujenzi wake umezinduliwa leo ni kukamilisha
azma yako bila kujali maisha ya watanzania”, Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa.
Waziri
Mkuu alisema kuwa kampuni zinazojenga mradi huo mkubwa wa kufua umeme
Tanzania, Els weldey na Arab Contructors, zinafanya kazi nzuri kwa hiyo
zitatekeleza mradi huo kwa weledi mkubwa, kama zinavyofanya kule Misri.
Naye
Waziri wa Nishati amesema mradi huo unabainisha mambo mawili ya kumuenzi
Rais wa kwanza Tanzania, hayati Julius Nyerere, ambayo Rais Magufuli
anatekeleza likiwemo kuhamisha makao makuu ya nchi kwenda Dododma,
ambayo tayari yanatekelezwa, likiwemo la ujenzi wa Bwawa la Rufiji.
“Naomba
niwakumbushe watanzania Mhe. Rais ametengeneza mambo makubwa mawili ya
ndoto ya baba wa Taifa ikiwemo kuhamisha makao makuu ya nchi kwenda
Dododma na utekelezaji wa mradi mahususi wa bwawa la kufua umeme, mradi
mkubwa wa kwanza Tanzania, Afrika Mashariki na wa nne barani Afrika,
huku ukiingia kwenye mabwawa 70 makubwa duniani yakuzarisha umeme,”
Waziri Kalemani.
Aidha
Waziri Kalemani amesema kuwa mradi huu utekelezaji wake utachukua miezi
42 ambapo hadi sasa miezi sita imeshapita na kubaki miezi 36 kukamilisha
ujenzi wa mradi huo ambao unategemewa kukamilika Juni 13, 2022.
Waziri
Kalemani aliongeza kuwa katika ujenzi wa mradi huo kazi kubwa ya
mkandarasi ni pamoja na ujenzi wa bwawa kubwa litakaloweza kuhifadhi
maji ya mita za ujazo billioni 33.2, ujenzi wa Power house itakayokuwa
na mashine tisa zenye kuzalisha megawati 235 kwa kila mashine na kazi ya
mwisho ni kujenga substation yenye kilovolt 400, ambapo ni umeme mkubwa
utakaotumika kwenye uchumi wa viwanda.
Umeme
huo utasafirishwa kutoka Rufiji kwenda Chalinze umbali wa kilomita 127
kwa dola za kimarekani 188 Chalinze mpaka Dar es Salaam na Dodoma na
ndio umeme utakao tumika kuendesha Treni ya kisasa (SGR), lengo la
Serikali ni kufikisha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025 kwahiyo mradi
huu mkubwa ni kichocheo kikubwa sana kuelekea uzarishaji wa hizo
megawati.
Kwa
upande wake Waziri wa nishati na umeme kutoka Misri Dkt. Mohamed Shaker
amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo unaimarisha mahusiano ya Tanzania
na Misri katika sekta mbalimbali, ikiwemo ya nishati.
“Ujenzi
wa mradi huu mkubwa ni moja ya hatua kubwa katika mahusiano ya nchi
mbili ambayo itahamasisha zaidi utekelezaji wa miradi mingine ya undugu
kati ya Tanzania na Misri, hususani kwenye nyanja ya umeme, nipende
kusisistiza kwamba mradi huu wa umeme Rufiji unaungwa mkono na Rais wa
Misri, Abdel Fattah El-Sisi” Waziri Shaker.
Nchi
ya Misri itaendelea kushirikiana na Tanzania katika utoaji wa mafunzo ya
teknolojia ya kuzalisha umeme, kwani ina vituo 22 vya kutolea mafunzo
hayo na imetoa nafasi 50 kwa wataalamu kutoka Tanzania kwenda kujifunza
masuala ya ufuaji na uzalishaji umeme.
RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MRADI WA KUFUA UMEME WA MAJI KATIKA MTO RUFIJI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati wa Misri Dkt.
Mohamed Shaker wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi mradi
wa Ujenzi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji
katikati ya Morogoro na Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimpongeza Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker mara baada ya
kuweka Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115
katika eneo la mto Rufiji katikati ya Morogoro na Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akifurahia pamoja na viongozi wengine mara baada ya tukio hilo la
uwekaji wa Jiwe la Msingi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri
wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker, Waziri wa Nishati Medard
Kalemani pamoja na viongozi wengine akisikiliza namna mradi wa Kuzalisha
umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji utakavyokuwa ukifanya
kazi mara baada ya kukamilika.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiangalia michoro ya ujenzi huo mkubwa wa kufua umeme.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa
Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker wakati
wakielekea kwenda kuweka jiwe hilo la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo itakayotumika
katika mradi huo mkubwa wa kufua umeme.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiangalia eneo la bonde katika mto Rufiji mara baada ya kuweka jiwe la
msingi la mradi huo wa umeme.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la Mradi.
Eneo la mto Rufiji ambalo litatumika katika ujenzi huo wa kufua umeme kama linavyoonekana. PICHA NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Julai, 2019
ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji
Mkoani Pwani ambao utakamilika Juni 2022 na kuzalisha megawati 2,115.
Sherehe za uwekaji
wa jiwe la msingi la mradi huo zimefanyika kando ya eneo litakapojengwa bwawa
la maji na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nishati wa Misri Mhe. Dkt. Mohamed Shaker,
Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Tanzania, Wabunge, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya
Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, Viongozi wa Dini, Viongozi
wa vyama vya siasa na viongozi wa taasisi mbalimbali za Serikali.
Ujenzi wa mradi
huo utagharimu shilingi za Kitanzania Trilioni 6.5 na bwawa litakalojengwa
litakuwa la kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki na la nne kwa ukubwa Barani
Afrika, na Mhe. Rais Magufuli amependekeza bwana hilo liitwe Bwawa la Nyerere
ikiwa ni kutambua na kuenzi maono ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage
Nyerere aliyetaka kujenga bwawa hilo wakati wa uongozi wake.
Katika hotuba
yake, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kusimamia
utekelezaji mradi huo na ameeleza kuwa Serikali imechukua hatua za kujenga
bwawa hilo ili kuongeza uzalishaji wa umeme nchini kutoka megawati 1,601 zinazozalishwa
hivi sasa, hadi kufikia megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.
Mhe. Rais Magufuli
amesema pamoja na kutekeleza mradi huo, Serikali itajenga mradi wa kuzalisha
umeme katika mto Ruhudji utakaozalisha megawati 359, mradi wa Lumakali megawati
222, mradi wa kakono megawati 87, Rusumo megawati 80 na mingine itakayotumia
nishati ya gesi, makaa ya mawe, jua, jotoardhi, upepo na urani.
Amewataka
wakandarasi wanaojenga mradi (Arab Contractors na Elsewedy Electric za Misri)
kukamilisha mradi huo kabla ya Juni 2022 hasa ikizingatiwa hakuna tatizo la
fedha ili Watanzania waanze kunufaika mapema.
Waziri wa Nishati,
Mhe. Dkt Medard Kalemani amesema tayari wakandarasi wanaojenga mradi huo
wamelipwa asilimia 15 ya fedha zote za mradi huo ambayo ni sawa na shilingi
Trilioni 1.007 na kwamba ujenzi utahusisha bwawa la maji lenye uwezo wa
kukusanya mita za ujazo Bilioni 33.2, Jengo la mitambo ya kuzalisha umeme
litakalokuwa na mitambo 9, kituo cha umeme na njia ya kusafirishia umeme yenye
urefu wa kilometa 135 hadi kufika Chalinze.
Naibu Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema
Wabunge wanampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa utekelezaji wa mradi huo na
wanaamini kuwa umeme utakaozalishwa utawasaidia Watanzania na pia kufanikisha
miradi mikubwa inayotekelezwa katika awamu hii ikiwemo ujenzi wa reli na ujenzi
wa viwanda.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amesema kuanza
kwa ujenzi wa mradi huo ni mafanikio makubwa ya Mhe. Rais Magufuli ambaye amedhamiria
kuhakikisha kila nyumba ya Mtanzania inapatiwa umeme.
Waziri wa Nishati
wa Misri amewasilisha salamu za Rais wa Misri, Mhe. Abdel Fattah El- Sisi
ambaye ameahidi kufuatilia ujenzi wa mradi huo unaofanywa na kampuni za Misri
na pia ameahidi kuwa nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja
mbalimbali ikiwemo kutoa udhamini wa masomo ya nishati jadidifu kwa wanafunzi
50 ambao watasaidia juhudi za kuongeza uzalishaji wa umeme hapa nchini.
Aidha, Mhe. Rais
Magufuli amewataka Watanzania kujivunia mafanikio haya makubwa ya kuongeza
uzalishaji wa umeme nchini na kutoyumbishwa na wanaopinga utekelezaji wa mradi
huo kwa kigezo cha uharibifu wa mazingira kwani mradi huo utasaidia zaidi
kutunza mazingira kwa watu kutumia umeme badala ya kuni na mkaa zinazotokana na
ukataji wa miti, na pia utasaidia kuwepo uvuvi, kilimo cha umwagiliaji na
kuinua utalii kutokana na Wanyama wengi kupata maji ya uhakika.
“Kwenye hili pori la Selous
kuna hoteli za kitalii za gharama kubwa, kuna vitalu vya utalii 47 na kuna
uwindaji unaendelea, sasa haiwezekani sisi tukitaka kujenga bwawa la kuzalisha
umeme tuambiwe tunaharibu mazingira wakati eneo tunalotumia ni chini ya
asilimia 3 ya pori la Selous.
Mradi huu umekumbana na
upinzani mkali wa ndani na nje ya nchi, lakini kwa kuwa sisi ni Taifa huru na
sio masikini kama watu wanavyodhani, tumeamua kutekeleza mradi huu”
amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli
ameagiza kumegwa kwa sehemu ya Pori la Akiba la Selous ili iwe Hifadhi ya Taifa
na amependekeza iitwe Hifadhi ya Nyerere na sehemu yenye vitalu vya uwindaji
iendelee, lengo likiwa kuimarisha zaidi uhifadhi wa maliasili katika eneo hilo
na kupata manufaa zaidi.
Ameagiza barabara
ya kuunganisha eneo la mradi huo mpaka Fuga ianze kujengwa kwa kiwango cha lami
hatua kwa hatua ili kurahisisha mawasiliano ya eneo hilo.Pamoja na kutaka
wananchi wa Morogoro na Pwani wapewe kipaumbele katika ajira wakati wa mradi
huo, Mhe. Rais Magufuli ameagiza mradi huo kukatiwa bima ya Taifa, utoaji wa
vibali vya kazi kwa wafanyakazi wa kutoka nje ya nchi ufanyike haraka na vyombo
vya ulinzi na usalama vya Morogoro na Pwani vishirikiane kuulinda.
Pia amewataka
viongozi na wananchi wa Mikoa yote yenye vyanzo vya maji vinavyomwaga maji yake
katika mto Rufiji kuhakikisha wanavitunza vyanzo hivyo ili viendelee kuchangia
maji mengi katika mto Rufiji.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Rufiji
26 Julai,
2019
Subscribe to:
Posts (Atom)