Thursday, April 30, 2020
RC MAKONDA ATOA MSAADA WA MABATI YENYE THAMANI YA MILIONI 476 KWAAJILI YA KUEZEKA NYUMBA 1,000 ZA WAJANE WALIOKUMBWA NA MAFURIKO DAR
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza |
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa msaada wa Mabati
yenye Thamani ya shilingi Milioni 476 kwaajili ya Kuezeka Nyumba 1,000
za Wajane mkoani humo ambao nyumba zao zimeathiriwa na mafuriko
yanayotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha ambapo amewataka Wananchi
waliojenga mabondeni kuondoka.
RC Makonda amesema hayo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani baada ya kukosa makazi ya kuishi hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya pole kwa adha waliyoipata.
RC Makonda amesema hayo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani baada ya kukosa makazi ya kuishi hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya pole kwa adha waliyoipata.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza |
Aidha
RC Makonda amewapa siku 10 Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanapitia maeneo
ya Mito na Mabonde kukagua athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa
kuwashirikisha viongozi wa mitaa ili kwa pamoja watoe mapendekezo ya
nini kifanyike kisha wampatie ripoti ya kuonyesha hatua za kukabiliana
na Mafuriko ya Mara kwa Mara.
Aidha RC Makonda amesema athari zinazoonekana kwa sasa ni matokeo ya Jamii kuwafumbia macho watu wanovunja sheria kwa kujenga mabondeni, kuchimba mchanga na kuziba mikondo ya maji jambo linalopelekea Mafuriko hivyo ametaka kila mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake.

Nyumba mbalimbali zilizoathiriwa na Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar na Kwingineko nchini |
Pamoja na hayo RC Makonda amesema kwa sasa serikali inaendelea kurejesha miundombinu na madaraja yaliyochukuliwa na Mafuriko ikiwemo ujenzi wa madaraja ya muda mfupi ili kuwezesha shughuli za kijamii kuendelea.
RC Makonda pia amewaelekeza wakandarasi kutumia kipindi hiki cha mvua kuangalia kama Design ya madaraja wanayojenga yanakidhi kuhimili na kupitisha maji ya mvua ili wabuni design mpya zinazokidhi viwango.
BENKI YA CRDB YAICHANGIA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE MILIONI 50 KWA AJILI YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto)
akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI), Prof. Mohamed Janabi mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 kwa
ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo,
ikiwa ni kukamilisha ahadi yake ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni
100 ili ziweze kufanikisha upasuaji wa moyo kwa watoto, makabidhaino
hayo yamefanyika leo kwenye Taasisi hiyo, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto)
akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI), Prof. Mohamed Janabi mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 kwa
ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo,
ikiwa ni kukamilisha ahadi yake ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni
100 ili ziweze kufanikisha upasuaji wa moyo kwa watoto, makabidhaino
hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi
akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully
Esther Mwambapa, kabla ya makabidhiano ya mfano wa hundi ya shilingi
milioni 50 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotibiwa katika
Taasisi hiyo, ikiwa ni kukamilisha ahadi yake ya kuchangia kiasi cha
shilingi milioni 100.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto)
akizungumza wakati alipofika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 kwa
ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo,
ikiwa ni kukamilisha ahadi yake ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni
100. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI), Prof. Mohamed Janabi.
Wednesday, April 29, 2020
WAZIRI MKUU AKABIDHI MAGARI 10 YA KUBEBEA WAGONJWA KWA WABUNGE
Mbunge wa Nyasa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,
Mhandisi Stellla Manyanya akilala chini (kugalauka) ikiwa ni ishara ya
shukurani na furaha iliyokithiri kwa mujibu wa mila za wangoni na
wamatengo, wakati alipokabidhiwa ufunguo wa gari la kubebea wagonjwa kwa
ajili ya Kituo cha Afya cha Mbamba Bay. Mheshimiwa Majaliwa alikabidhi
magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi
bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja
vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amekabidhi magari 10 ya kubebea wagonjwa kwa
wabunge ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za dhati za Serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuhakikisha
Watanzania wanapata huduma bora za afya karibu na makazi yao.
Magari hayo 10 ni kati ya magari 50 ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya sh. bilioni sita yaliyonunuliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Global Fund. Kati ya magari hayo, 18 yatapelekwa kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa na 32 ni kwa ajili ya hospitali za Halmashauri pamoja na vituo vya afya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Dodoma Mjini
ambaye pia ni Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde
wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye
thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo
yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini
Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wa tatu kulia ni Mbunge wa Nyasa ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi, Stella Manyanya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) wakifurahia wakati Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta (kulia) alikionyesha ufunguo wa gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhiwa wakati Waziri Mkuu alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto (kulia) wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea shukurani kutoka kwa Mbunge wa Mbulu Vijijini Fratei Massay wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo leo (Jumatano, Aprili 29, 2020) kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Ambapo amesema mbali na magari hayo kutolewa kwa ajili ya kuboresha huduma za mama na mtoto pia yatatumika kuwahudumia wagonjwa wa corona ili kuokoa maisha ya wananchi.

“Eneo hili tumeliwekea nguvu za kutosha na Watanzania wote ni mashahidi kwa namna ambavyo Serikali imejitahidi sana katika kupunguza vifo vya mama na mtoto kwenye jamii zetu. Magari haya yatakwenda kutumika kwa ajili ya mama na mtoto lakini kwa kuwa gari litakuwepo kituoni litawahudumia na wagonjwa wengine.” Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Mbunge wa Nyasa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandishi, Stella Manyanya. Waziri Mkuu amewashukuru wabunge wote kwa namna wanavyoishauri Serikali katika kufanya maboresho ya sekta mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na sekta ya afya ambapo leo wameshuhudia matunda ya ushauri wanaoutoa.
“Magari haya yatakwenda kufanya kazi ya kuokoa maisha ya Watanzania wengi kwa kuwasafirisha wagonjwa wa rufaa kutoka kituo cha afya kwenda hospitali ya wilaya na hospitali ya wilaya kwenda hospitali ya rufaa.”
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema ununuzi wa magari hayo ni utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuboresha zaidi huduma afya kwa wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum,
Amina Makilagi wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa
wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020.
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu,
Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu akiwa na baadhi ya wabunge waliokabidhiwa funguo za magari ya
kubebea wagonjwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye viwanja vya
Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 29, 2020. Magari 50
ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya shilingi bilioni 6 yalikabidhiwa
kwa wabunge. Waziri
Ummy amesema Wizara imenunua magari hayo ili kuimarisha huduma za rufaa
kwa wagonjwa hususani kwa akina mama wajawazito hata hivyo kutokana na
changamoto ya ugonjwa wa corona pia magari hayo yatatumika kwa ajili ya
kubebea wagonjwa wa corona.
“Watanzania wameshuhuduia kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli, wameshuhudia upatikanaji wa dawa, wameshuhudia maboresho makubwa katika upatikanaji wa vifaa tiba, ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa hosptali za halmashauri pamoja na hospitali za rufaa za mikoa na uboreshwaji wa miundombinu ya kutolea huduma za afya.”
Akizungumza kwa niaba ya wabunge waliopokea magari hayo, Mbunge wa Ileje, Janneth Mbenne amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kitendo hicho cha kihistoria.
“Watanzania wameshuhuduia kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli, wameshuhudia upatikanaji wa dawa, wameshuhudia maboresho makubwa katika upatikanaji wa vifaa tiba, ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa hosptali za halmashauri pamoja na hospitali za rufaa za mikoa na uboreshwaji wa miundombinu ya kutolea huduma za afya.”
Akizungumza kwa niaba ya wabunge waliopokea magari hayo, Mbunge wa Ileje, Janneth Mbenne amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kitendo hicho cha kihistoria.
Mbunge wa Nyasa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,
Stella Manyanya akitazama gari la kubebea wagonjwa la Kituo cha Afya cha
Mbamba Bay wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokabidhi magari 50
ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6,
Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi
ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa mawazo na maono makubwa ya maendeleo
ya Taifa. Magari haya yatakwenda kuboresha huduma za afya katika majimbo
yetu.”
Naye Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2015-2020 kwa vitendo. “…moyo usio na shukurani hukausha mema yote na heri wale wanaowajali wagonjwa kwa maana ufalme wa Mungu ni wao.”
Pia, Mbunge wa Nyasa na Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Stella Manyanya amesema kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Nyasa wanamshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa msaada huo kwani walikuwa na changamoto kubwa na gari la kubebea wagonjwa.

WATANZANIA WAJITOKEZA KUPIMWA USIKIVU MLOGANZILA
NAIBU WAZIRI MGALU AMTAKA MKANDARASI KUMALIZA KAZI KWA WAKATI
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye ushungi), akikagua Yadi ya Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, wilayani Gairo, akiwa katika ziara ya kazi hivi karibuni. |
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amefanya ziara mkoani Morogoro na kumwagiza
Mkandarasi, Kampuni ya State Grid, anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, mkoani
humo kumaliza kazi kwa wakati.
Mgalu
alilazimika kufanya ziara hiyo baada ya kupokea malalamiko ya kusuasua kwa
Mradi husika ambapo aliwaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kumsimamia Mkandarasi huyo ili kuhakikisha
anakamilisha kazi kwa muda ulioainishwa kwenye Mkataba.
Wakati
wa ziara hiyo iliyofanyika Aprili 25 mwaka huu, Naibu Waziri alitembelea baadhi
ya vijiji vya Wilaya za Gairo na Mvomero kujionea maendeleo ya kazi husika.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati-mwenye ushungi), akikagua kazi ya kuunganisha umeme vijijini inayoendelea katika eneo la Ukwamani, wilayani Gairo hivi karibuni. |
Vijiji
vilivyotembelewa ni Ukwamani na Nguyami (Gairo) pamoja na Komtanga (Mvomero).
Kadhalika, Naibu Waziri alitembelea Yadi ya Mkandarasi iliyopo Gairo Mjini.
Naibu
Waziri aliwaasa viongozi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kuchukua
tahadhari juu ya ugonjwa wa Covid – 19 unaosababishwa na virusi vya Corona huku
wakiendelea kufanya shughuli zao.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye ushungi), akikagua Yadi ya Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, wilayani Gairo, akiwa katika ziara ya kazi hivi karibuni. |
Pia,
aliwataka TANESCO Mkoa wa Morogoro kuhakikisha wananchi wote wanaolipia ili
kuunganishiwa umeme, wanapatiwa huduma hiyo kwa wakati.
WAZIRI HASUNGA - UZALISHAJI WA KAHAWA WAONGEZEKA WAFIKIA TANI 214,962
Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema kuwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya Tano ya Dkt. John Magufuli zao la Kahawa limeweza kufikia uzalishaji wa tani 214,962 .
Ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya Kahawa katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya tano na kusema kuwa kwa wastani kila mwaka imekuwa ikizalisha tani 51,777 ya kahawa nzuri ambapo uzalishaji huo uliwezesha taifa kuingiza fedha nyingi za ndani na za kigeni.
Amebainisha kuwa kwa upande wa wakulima katika kipindi cha miaka minne wameweza kujipatia jumla ya Trilioni 1.195 ambazo zimeenda kuwanufaisha wakulima wa zao hilo. “Lakini kama Taifa pia tumeweza kupata dola za marekani milioni 427.9 ambazo ni fedha za kigeni katika kipindi hiki kitu ambacho ni mafaniko makubwa kwa wizara,” Amesema
Alifafanua kuwa kwa wastani baada ya kuanza kwa zoezi la uandikishaji wa wakulima kwa lengo la kuweza kuwatambua ili kuwahudumia mpaka sasa wakulima 286,397wamesajiliwa.
Alisema hao ndio wakulima wadogo wadogo ambao wanajishughulisha na zao la kahawa katika mikoa 16 ambayo ameitaja na kueleza kuwa kuna wakulima wakuba ambao wana mashamba 101 ambao wanazalisha kwa kiwango kikubwa zao hilo.
Kuhusu suala la ajira ameeleza kuwa kwenye upande wa ajira zao hilo la kahawa limechangia ongezeko la ajira za watu kutoka millioni 2.3 hadi milioni 2.7 ambapo hao wote wamejiajiri au wameajiriwa na sekta hiyo na wanashiriki kwenye uzalishaji na mnyororo wa thamani.
Amefafanua kuwa mchango wa zao hilo katika uchumi wa Taifa kwenye upande wa sekta ya viwanda lina viwanda takribani 554 ambavyo vinajishughulisha katika uchakataji wa kahawa kutoka katika ngazi ya uzalishaji mpaka ulaji.
Waziri Hasunga amesema kuwa viwanda hivyo vipo katika madaraja tofauti hivyo kuchukua nafasi hiyo kumpongeza Rais na viongozi wengine wakuu kwa kazi kubwa waliyofanya katika kuhamasisha uzalishaji, kuongeza tija, na uzalishaji wa zao hilo.
Amesema katika jitihada hizo, wakati Serikali inaendelea na jitihada nyingine za kuongeza uzalishaji kilichofanyika ni kuamua kupunguza kodi mbalimbali ambazo zilikuwa zinapunguza mapato kwa mkulima.
“Tumefuta zaidi ya kodi na tozo 19 kwenye zao la Kahawa kwa hiyo sasa kodi hizo zimepungua na sasa hivi mkulima anaweza akanufaika zaidi na akapata fedha nzuri.
Sambamba na hilo, amesema kuwa uwekezaji umeongezeka katika utafiti ili kuweza kupata mbegu zilizo bora, zinazofaa kwenye kilimo cha zao hilo, zinazotumia maji kidogo, zenye kustahimili ukame na zenye kukinzana na magonjwa ya kila namna.
Waziri Hasunga ameeleza kuwa kuna aina nyingi za magonjwa yaliyokuwa yanalikabili zao hilo ambapo kwa sasa Taasisi ya utafiti cha Kahawa (TaCRI) kilichopo kwenye kanda nane kimefanya utafiti na kuja na mbegu 19 za kahawa aina ya Arabika ambayo ina onyesha mafanikio makubwa.
Amesisitiza kuwa pia kuna mbegu nyingine tano aina ya Robusta ambazo zote kwa pamoja ukizijumlisha zinapatikana aina 23 za mbegu zilizo bora zilizofanyiwa utafiti wa kina na kuweza kutumika.
Ameeleza kuwa baada ya uzalishaji huo kukamilika kazi kubwa ambayo serikali imefanya ni pamoja na kuongeza uzalishaji na ubora wa kahawa ndio maana inaendelea kusisitiza wakulima wakivuna kahawa wapeleke kwenye CPU ili kusimamia ubora ili ukiimarika zilete fedha nzuri.
Ameongeza kuwa sambamba na hayo kumekuwa na changamoto ya masoko lakini jitihada za serikali ya awamu ya tano zilizofanyika na maagizo ya viongozi wa juu wameifanya wizara kuanzisha utaratibu mpya wa namna ya kuuza kahawa.
Waziri Hasunga amebainisha kuwa awali kulikuwa na aina mbili za masoko ambazo ni soko la moja kwa moja ambapo wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika wanaingia mkataba na wanunuzi wa nje ya nchi na kuuza moja kwa moja hivyo kujipatia fedha nzuri.
“Pia, kulikuwa na soko ambapo kahawa nyingine inauzwa katika minada ambapo utaratibu wa nyuma ni kuwa minada yote ilikuwa inafanyika mkoani Kilimanjaro kwenye bodi ya kahawa lakini toka mwaka jana tulifanya maamuzi kwamba vianzishwe vituo vya minada” Alikaririwa Waziri Hasunga na kuongeza kuwa
“Kama sote tunavyojua kwamba kahawa ni moja ya mazao ya kimkakati ambayo yanalimwa katika mikoa zaidi ya 16 hapa nchini ambayo ni pamoja na Songwe, Mbeya, Ruvuma, Kagera, Kilimanjaro, Arusha, Mara, Kigoma, Tanga, Morogoro, Njombe, Katavi, na Mwanza”
Zao la Kahawa linashika nafasi ya tatu katika kuchangia mapato ya Taifa ambapo zao la kwanza ni Korosho likifuatiwa na zao la Tumbaku.
WAGONJWA 167 WAPONA CORONA NCHINI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa |
Na.WAMJW, Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa taarifa ya mwenendo wa Ugonjwa wa Corona nchini ambapo amesema kuwa kuna maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa watanzania 196 ambapo kati yao; kutoka Bara ni 174, Zanzibar 22 na kufanya jumla ya watu waliopata maambukizi kuwa ni 480.
Aidha,Waziri Majaliwa amesema kuwa idadi ya wagonjwa waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 167, (Zanzibar wako 36, Bara ni 83).
Hali kadhalika vifo 6 vimetokea na kufanya jumla ya waliofariki kwa ugonjwa wa Corona kufikia 16 hadi sasa.
Waziri Mkuu ametoa rai kwa Watanzania kuacha kutoa taarifa za uzushi za vifo kuwa kila Kifo kinachotokea hakisababishwi na Ugonjwa wa Corona.
NFRA WATAKIWA KUONGEZA WIGO WA MAPATO - KATIBU MKUU KUSAYA
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (aliyeshika sahani) akikagua ubora wa mahindi yaliyohifadhiwa katika ghala la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Shinyanga leo
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Kituo cha Afya ya Mimea Kanda ya Shinyanga wakati alipotembelea kuongea na watumishi wa taasisi hiyo iliyo chini ya wizara ya Kilimo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (aliyevaa koti la bluu) akiongea na watumishi wa NFRA Kanda ya Shinyanga wakati alipokagua ghala la hifadhi ya mahindi leo mjini Shinyanga,
Picha na Habari na Wizara ya Kilimo.
Wizara ya Kilimo imeiagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kubuni njia muafaka ya kuongeza mapato kwa kuhifadhi nafaka zaidi na kufanya biashara ya mazao ya kilimo.
Agizo hilo limetolewa leo (28.04.2020) mjini Shinyanga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya wakati alipofanya ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na wakala kanda ya Shinyanga.
“Kuanzia sasa nataka kuona NFRA inafanya kazi kwa kujitegemea zaidi bila kutegemea fedha za serikali kwa kubuni mikakati ya kutumia uwepo wa vihenge vya kisasa na ghala vinavyojengwa na serikali hapa Shinyanga” alisema Kusaya.
Alibainisha kuwa serikali inatekeleza mradi mkubwa wa shilingi Bilioni 15.24 wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi kwa kujenga vihenge (silos) sita zenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 na ghala moja kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi tani 10,000 za nafaka katika eneo la Ibadakuli mkoani Shinyanga.
Alieleza kuwa mradi huo ni wa mafanikio kwani utawezesha uhifadhi wa mazao toka kwa wakulima kuongezeka toka tani 14,500 za sasa hadi tani 44,500 kwa mwaka utakapokamilika mwezi Juni mwaka huu.
“Tafuteni mbinu itakayoifanya NFRA mhifadhi nafaka nyingi zaidi kama mahindi,choroko,maharage ,mpunga na ziada muweze kuuza na kupata fedha za kujiendesha kibiashara ikiwemo kutumia fursa ya mahitaji makubwa ya nafaka hususan chakula kwenye nchi za jirani na Tanzania” alisitiza Kusaya.
Katika hatua nyingine Kaimu Meneja wa Kanda ya Shinyanga Meriana Yateri ameishukuru serikali kwa uamuzi wake wa kujenga vihenge vya kisasa na ghala kwani vitasidia kuongeza uwezo wa kanda na nchi kuhifadhi mazao mengi yatakayotumika wakati wa dharura na majanga.
Tuesday, April 28, 2020
TANZANIA NA KUWAIT ZAAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO
Mazungumzo yakiendelea. |
ARIFU ABRI ATOA MSAADA KWA WAHANGA WA MAFURIKO MBINGAMA PAWAGA
Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kupitia Wilaya ya Iringa Vijijini Arifu Abri akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi msaada kwa ajili ya wahanga wa kitongoji cha Mbingama tarafa ya Pawaga.
NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM
Taifa kupitia Wilaya ya Iringa Vijijini Arifu Abri ametoa msaada wa chakula
tani tatu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko wa kijiji cha
Isele kilichoko tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa vijijini mkoanbi
Iringa kwa kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya chakula.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, Arifu Abri alisema
kuwa changamoto wanayokabiliana nayo
wananchi wa kijiji hicho imepelekea kujitoa kuwasaidia watu wenye mahitaji
muhimu ili kuokoa maisha yao madhara waliyopata kutokana na mafuriko hayo.
Alisema alipata taarifa ya
wananchi wa kitongoji cha Mbingama kijiji cha Isele kuwa wamepatwa na mafuriko
kutokana na kunyesha kwa mvua nyingi msimu huu wa kilimo na kusabaisha hasara
kubwa kwa wananchi waliokuwa wanaishi katika eneo hilo lililotokea mafuriko na
kutegemea zaidi kilimo kwa ajili ya maisha.
Alisema kuwa moja ya mahitaji
ambayo wahanga wa mafuriko wa kitongoji cha Mbingama ni wananchi asilimia kubwa
kukosa chakula cha kila siku hivyo ndio maana msaada wangu nimejielekeza kwenye
kutoa chakula zaidi ambapo utawasaidia kwa kipindi hiki cha mafuriko.
“Najua kuna wadau wengine
wameshatoa baadhi ya msaada kulingana na mahitaji hata hivyo kwa upande wangu
mimi nimeamua kutoa chakula kulingana na mahitaji ambayo nimeona wanahitaji
wahanga wa mafuriko wa kitongoji cha Mbingama kijiji cha Isele Tarafa ya Pawaga”
alisema
Abri alitoa wito kwa wadau
wengine kuendelea kujitokeza kuwasaidia wahanga hao wa mafuriko katika
kitongoji cha Mbingama ili kuwasaidia kurudi kwenye maisha ambayo walikuwa
wameyazoe hapo awali kulingana na shughuli ambazo walikuwa wanazifanya kupa riziki
zao.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya
ya Iringa, Richard Kasesela mara baada ya kupokea msaada huo alimshukuru mjumbe
wa mkutano mkuu ccm taifaArifu kwa msaada huo kwa kuwa umekuja katika wakati
mwafaka kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo wananchi hao.
Aidha Kasesela alitoa wito kwa
wadau kujitokeza zaidi kuwasaidia wananchi hao ambao licha ya changamoto ya
chakula wanakabiliwa na changamoto ya nguo, makazi, madawa kwa lengo la kuweza
kuondokana na hali hiyo.
Naye mwenyekiti wa umoja wa
vijana Wilaya ya Iringa Makala Mapesah alisema kuwa wadau kama arifu Abri
wanatakiwa kuigwa katika jamii zetu kwa watu wenye uwezo kuwasidia watu ambao
wanakuwa wanamahitaji ili waendelee kuishi kama wananchi wengine wanaopata
mahitaji mengine.
“Mimi kama mwenyekiti niwaombe
wadau wengine waendelee kujitolea kama mdau huyu Arifu Abri ambaye amekuwa
msaada sana kwa wananchi wa wilaya ya Iringa vijijini kuwasiadia wananchi
mbalimbali hivyo lazima nimpongeze sana kwa kazi yake” alisema Makala
Katibu wa mbunge wa jimbo la
Isimani Thom Malenga alisema wahanga wa mafuriko ya kitongoji cha Mbingama bado
wanahitaji msaada zaidi hivyo anampongeza mdau Arifu Abri na kuwaomba wadau
wengine kujitokeza kutoa msaada kwa wahanga hao.
WAZIRI LUKUVI AKABIDHI NDOO 270 KUWAKINGA NA CORONA WANANCHI JIMBO LA ISIMANI
Kushoto ni katibu wa mbunge wa Jimbo la Isimani Thom Malenga akimkabidhi ndoo maalum za kujikinga na Corona mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela zilizotolewa na Mbunge William Lukuvi kwa ajili ya wananchi wa jimbo hilo
Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo
ya makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Isimani Mkoani Iringa Mh. William
Lukuvi amekabidhi kwa wananchi wa jimbo hilo jumla ya ndoo 270 maalum za kunawia mikono kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya
virusi vya Corona vinavyosababisha Ugonjwa wa Covid 19.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
ndoo hizo Katibu wa mbunge huyo Thom Malenga alisema kuwa vifaa hivyo
vimetolewa kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa jimbo la Isimani kutekeleza kwa
vitendo ushauri wa wizara ya afya nchini inayomtaka kila mwananchi kunawa mara
kwa mara ili kujiepusha na maambukizi ya Corona
Katibu huyo aliwahimiza
wananchi kuzingatia ushauri wa wataalam wa afya na kuzitumia ndoo hizo kwa kutakasa
mikono kila wakati kwa kuwa ndio moja ya kinga ambayo inaweza kuepuka kukumbwa
na maambukizi ya virusi hivyo ambavyo vimekuwa hatari kwa maisha ya Binadam
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ndoo hizo maalum kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Corona
Malenga alisema kuwa mbunge ametoa ndoo maalumu nne kwa kila kijiji ambacho kipo katika jimbo la Isimani kwa lengo la kusaidia katika maeneo yenye mikusanyiko na maeneo maalum kama ofisi za kijiji,virabu vya pombe na sehemu za kuabudia.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya
Iringa Richard Kasesela alisema mbunge wa jimbo la Isimani William Lukuvi
amekuwa mstari wa Mbele kuhakikisha anawasaidia wananchi wake kwa kila jambo
linapotokea huku akiwahimiza wabunge na viongozi wengine kuiga mfano wa
kujitolewa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.
Malenga alisema kuwa mbunge ametoa ndoo maalumu nne kwa kila kijiji ambacho kipo katika jimbo la Isimani kwa lengo la kusaidia katika maeneo yenye mikusanyiko na maeneo maalum kama ofisi za kijiji,virabu vya pombe na sehemu za kuabudia.
“Leo tumekabidhi ndoo maalum
zenye uwezo wa kubeba lita Ishirini kwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard
Kasesela kwa lengo la kusaidia kujikinga na virusi vya Corona,kinga bora kuliko
tiba hii ndio sababu ya mbunge kutoa msaada huu” alisema Malenga
mwenyekiti wa umoja wa vijana Wilaya ya Iringa vijijini Makala Mapessah akiwaonyesha waandishi wa ha bari ndoo maalum za kujikinga na Corona zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Isimani William Lukuvi
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
“Jukumu letu ni kuhakikisha
tunawatafutia sabuni wananchi ambao hawawezi kununua ili kuwasaidia kujikinga
na virusi vya Corona” alisema Kasesela
Kasesela alisema kuwa ndoo hizo
maalum zinaghama kubwa hivyo wananchi wanapaswa kuzitunza na kuendelea kumheshimu
mbunge huyo kwa juhudi ambazo amekuwa akizitoa kuhakikisha wananchi wanapata
mahitaji muhimu kwa maendeleo.
Hadi kufikia hii leo wilaya ya
Iringa haijapata mgonjwa yeyote yule mwenye maambukizi ya virusi vya Corona
hivyo bado wananchi wapo salama na wanapaswa kuendelea kujikinga na virusi
hivyo.
Naye mwenyekiti wa umoja wa
vijana Wilaya ya Iringa vijijini Makala Mapessah alimpongeza mbunge huyo kwa
kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha wananchi wa jimbo la Isimani wanakuwa salama
kwa kujikinga na virusi vya Corona.
Subscribe to:
Posts (Atom)