Matokeo chanyA+ online




Tuesday, June 27, 2017

WANAWAKE WAWEKA REKODI YA KUCHEZA SOKA KATIKA KILELE CHA UHURU,MLIMA KILIMANJARO.

Timu za Gracier fc na Volcano fc zikijiandaa kwa mchezo wa kirafiki katika eneo la Kreta,kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakiweka pozi la picha katika Kreta ya Uhuru katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.

Kundi la Wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa zaidi ya 20 walioshiriki kuweka rekodi ya kucheza soka katika eneo la kreta lililopo katika kilele cha Uhuru.
Baadhi ya wachezaji walioshiriki mchezo wa soka katika Kilele cha uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrta Loibook akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini ,Devota Mdachi walipowapokea wachezaji wa timu za taifa za wanawake wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Mwika.
Mhifadhi Mkuu KINAPA,Betrita Loibook pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii,Geofrey Tengeneza wakifurahia mara baada ya wachezaji wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani kuweka rekodi ya kucheza mpira katika kilele cha Uhuru .
Wachezaji wa timu za Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya utalii pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.

Wachezaji 30 wa timu za soka za mataifa mbalimbali wameshiriki kuweka rekodi ya kwanza Duniani kwa kucheza mchezo wa kirafiki katika mlima Kilimanjaro ,umbali mita 5731 kutoka usawa wa bahari .

Rekodi nyingine iliyowekwa ni ile ya mwamuzi wa kike wa Tanzania anayetambulika na Shirikiho la Soka Duniani (FIFA) ,Jonesia Rukyaa  kuchezesha mchezo huo  wa dakika 90 uliomalizika kwa sare ya bila kufungana .

Thursday, June 15, 2017

MKOA WA DAR ES SALAAM KUFUNGWA KAMERA


MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH. PAUL MAKONDA AZINDUA MPANGO KABAMBE WA KUIMARISHA HALI YA JESHI LA POLISI MKOANI DAR ES SALAAM.

Na: Mwandishi wa Matokeo chanyA+
Katika awamu ya kwanza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paulo Makonda amezindua mpango wa kukarabati Magari ya Polisi yanayotumika katika doria. Amepokea magari Mabovu 26 ambayo yamesafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro kuundwa upya ili kuanza kufanya kazi ya Doria. Magari hayo yatakuwa na muundo unaowawezesha askari kukaa kidoria nasio kama abiria kama ilivyosasa.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paulo Makonda, ameahidi kukabidhi  polisi vifaa vya ulinzi kama silaha za kukamata kwa kupiga shoti ya umeme, kurunzi za mwanga mkali, bastola 500 na vikinga risasi.

Mkuu wa Mkoa wa Dae es salaam alipokuwa ziarani nchini Marekani, amepata vifaa vya patrol kwa ajili ya Jeshi la Polisi Mkoani Dar es Salaam ambavyo ni Baiskeli 500 na Pikipiki 200.

Katika awamu ya pili atakarabati na kuunda tena magari 30 na kufanya jumla yawe 56.

Amesema Katika magari hayo mara yatakapo kamilika yatafungwa Kamera za kufuatilia magari hayo na kutuma matukio yote ya barabarani Katika picha mwendo mojakwamoja makao makuu ya polisi.

Vilevile kutafungwa komputa 8 katika vituo 20 ambapo taarifa zote zinazoripotiwa zitasajiliwa kwenye computer na wahusika/watuhumiwa kuchukuliwa picha na alama mbalimbali ambazo zitahifadhiwa katika Data Centre ambayo raisi ameizindua.

Mkuu wa mkoa ameanza na vituo vya polisi 20 sasa, kutafungwa kamera ambazo zitakuwa na uwezo wa kutuma matukio mojakwa moja kwa OCD, RPC, Kamishina wa Jeshi la Polisi na kwa Mkuu wa Mkoa ambae ni Mwenyekiti wa Ulinzi na usalama wa Mkoa.


Kupitia kamera hizi wataona mubashara matukio yote yanayoendelea katika vituo vya polisi. Mtu akiiingia au akitoka polisi ataonekana.

Hatua hizi zitaondoa usumbufu kwa raia hasa wakati ndugu wanapomtafuta ndugu yao aliyekatika vituo vya polisi. Mfano ndugu aliyepotea au aliyekamatwa na kuwekwa mahabusu, hivyo hauta hangaika kumtafuta kila kituo bila mafanikio. Mwnanchi atakapo toa taarifa kituooni atataja jina na polisi watamtafuta kwa “search” tu kwenye mtandao wa jeshi la polisi kisha ataonekana kituo alipo ripoti.

Mkuu wa mkoa ametoa wito kwa wananchi kwamba siku mfumo utakapozinduliwa ni lazima taarifa ziandikwe kwenye computer na wala zisiwekwe kwenye makaratasi ambayo yalikuwa yanaleta usumbufu kwa wananchi.

Ili Kukomesha biasha za magendo, Mkuu wa mkoa amesema kwamba kutawekwa kamera hasa Katika bandari bubu, na stendi za mabasi.

Vilevile Mkuu wa mkoa amesema tayari ameanza kusimamia ufungaji wa kamera Katika jiji lote la Dar es salaam, hasa maeneo ya taa za barabarani ambazo zitasaidia sana kudhibiti makosa ya barabarani, Hivyo kutambua mienendo ya waendesha magari.



Vilevile Kamera Zitadhibiti mambo yafuatayo:-

•       Kupunguza kazi kwa askari wanaohangaika kusumbuana na waendesha magari wanaovunja sharia za barabarani.

•       Zitakomesha wizi wa kukwapuliwa pochi, mabegi, vifaa vya magari, matairi ya magari, kuvunjiwa vioo. Hivyo Vijiwe vyote vinavyouza vifaa vya magari vitasajiliwa na waeleze kwamba bidhaa wanazipata wapi?

•       Kwa kushirikiana na TTCL Kutakuwa na application (APP) maalumu ya kukuonyesha hali ya msongamano wa jiji la Dar es salaam Kiganjani mwako, Hivyo itawasaidia sana madereva kuchagua njia za kupita ili kuepusha msongamano wa magari Katika njia moja.


Pia Imeandikwa 
https://africa.cgtn.com/2017/06/15/tanzania-to-install-street-cameras-in-its-biggest-city-dar-es-salaam/

Wananchi 7 kati ya 10 wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli

Wananchi 7 kati ya 10 wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli/7 out of 10 citizens approve of the performance of President Magufuli


Rais anakubalika zaidi miongoni mwa makundi ya wazee na wenye kiwango kidogo cha elimu

15 Juni 2017, Dar es Salaam: Asilimia 71 ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani. Kiwango hiki kimeshuka kutoka asilimia 96 mwezi Juni 2016.  Viwango vya kukubalika kwa Rais vinatofautiana katika makundi mbalimbali:
  • Asilimia 68 wenye umri chini ya miaka 30 wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 82 wenye umri zaidi ya miaka 50
  • Asilimia 75 ya wananchi wenye elimu ya msingi au chini yake wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 63 ya wale wenye elimu ya sekondari au zaidi
  • Asilimia 75 ya wananchi masikini wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 66 ya wananchi matajiri.

Viwango vya kukubalika kwa viongozi wengine navyo pia vimeshuka katika kipindi hicho hicho.
  • Wabunge:  Kukubalika kwa utendaji wa wabunge kumeshuka kutoka asilimia 79 (Juni 2016) hadi asilimia 58 (Aprili 2017).
  • Madiwani: Kukubalika kwa utendaji wa madiwani kumeshuka kutoka asilimia 74 (Juni 2016) hadi asilimia 59 (Aprili 2017).
  • Wenyeviti wa vijiji/mitaa: Kukubalika kwa utendaji wa wenyeviti wa vijiji/mitaa kumeshuka kutoka asilimia 78 (Juni 2016) hadi asilimia 66 (Aprili 2017).
Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika utafiti wake uitwao Matarajio na matokeo; Vipaumbele, utendaji na siasa nchini Tanzania. Utafiti huo unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi. Matokeo hayo yanatokana na takwimu zilizokusanywa mwezi Aprili mwaka 2017 kutoka kwa wahojiwa 1,805 kutoka maeneo mbalimbali Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye matokeo haya).

Kukubalika kwa vyama vya siasa kunatoa taswira mchanganyiko. Kukubalika kwa CCM kumeendelea kuimarika, ikiwa ni kati ya asilimia 54 na asilimia 65 kati ya mwaka 2012 na 2017, Baada ya kushuka mwaka 2013 na 2014 ambapo kiwango cha kukubalika kilifikia asilimia 54 kutoka asilimia 65 ya 2012. Kukubalika kwa CCM kumeendelea kubaki katika kiwango hicho hicho cha asilimia 62 tangu uchaguzi wa mwaka 2015 na asilimia 63 mwaka 2017. Kukubalika kwa Chadema kumeshuka hadi asilimia 17 mwaka 2017 kutoka asilimia 32 mwaka 2013.

CCM inakubalika zaidi miongoni mwa wazee (asilimia 80), ukilinganisha na asilimia 55 ya vijana. Wanawake (asilimia 68) wanaikubali CCM kuliko wanaume (asilimia 58), maeneo ya vijijini (asilimia 66) kuliko maeneo ya mijini (asilimia 57), na wananchi masikini (asilimia 69) kuliko matajiri (asilimia 53). Wananchi wenye elimu ya sekondari, elimu ya ufundi au elimu ya juu wanaikubali CCM kwa asilimia 46.

Kukubalika kwa Chadema kwa ujumla unafuata mtiririko tofauti: ni mkubwa miongoni mwa vijana, wanaume, watu matajiri na wenye kiwango kikubwa cha elimu.

Ndani ya kipindi cha miaka miwili tu, vipaumbele vya wananchi vimebadilika sana. Mwaka 2015, asilimia 34 ya wananchi walitaja umasikini na uchumi duni kama moja ya vipaumbele vyao vikubwa ikilinganishwa na asilimia 60 waliotaja masuala hayo mwaka 2017. Mwaka 2015, ni asilimia 9 waliotaja upungufu wa chakula au njaa kama kipaumbele chao ikilinganishwa na asilimia 57 mwaka 2017.

Katika kipindi hicho hicho, wasiwasi wa wananchi juu ya huduma za umma na rushwa umepungua.

Asilimia ya wananchi wanaotaja masuala yafuatayo kuwa miongoni mwa changamoto kuu tatu zinazoikabili nchi:
  • Afya: asilimia 40 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 59 mwaka 2015.
  • Elimu: asilimia 22 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 44 mwaka 2015.
  • Miundombinu: asilimia 21 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 32 mwaka 2015.
  • Huduma ya maji: asilimia 19 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 46 mwaka 2015.
  • Rushwa: asilimia 10 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 28 mwaka 2015.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze, anasema: “Idadi kubwa ya wananchi inaendelea kuukubali utendaji wa Rais Magufuli. Lakini kushuka kwa viwango vya kukubalika kwake, pamoja na vile vya wabunge, madiwani na wenyeviti wa mitaa, ni ujumbe mzito kutoka kwa wananchi wanaohisi kuwa, tofauti na matarajio yao, wameangushwa na utendaji wa serikali katika kuzitatua shida zao moja kwa moja. Wananchi wana hofu na vitu vya msingi – kipato na chakula - na wanatuma ujumbe mzito kwa viongozi wao."

"Lakini utafiti unabainisha ujumbe mwingine kutoka kwa wananchi. Katika orodha ya matatizo makubwa matatu yanayowakabili, afya, elimu na maji zimeshuka ngazi. Sekta hizi kwa miaka mitatu mfululizo zilichukua nafasi za juu kama changamoto kuu zilizotajwa na wananchi. Utafiti huu unaashiria kuwa wananchi wanayaona mabadiliko katika upatikanaji wa huduma za jamii."


---- Mwisho ----

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Risha Chande, Mshauri Mwandamizi wa Mawasiliano, Twaweza
Barua pepe: rchande@twaweza.org | Simu: (+255) (0) 656 657 559

Maelezo kwa Wahariri
  1. Muhtasari huu na takwimu zake zinapatikana kupitia www.twaweza.org, au www.twaweza.org/sauti
  2. Twaweza inafanya kazi ya kupima uwezo wa watoto kujifunza, wananchi kuwa na utayari wa kuleta mabadiliko na serikali kuwa wazi na sikivu zaidi katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Twaweza ina programu, wafanyakazi na ofisi katika nchi zote tatu, na utaratibu unaoheshimika kimataifa wa kujifunza, ufuatiliaji na tathmini. Programu zetu muhimu ni pamoja na Uwezo, ambayo ni tathmini kubwa ya kila mwaka ya wananchi barani Afrika inayopima viwango vya watoto vya kujifunza kwenye maelfu ya kaya, na Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika kwa njia ya simu ya mkononi. Pia tunashiriki kwenye masuala ya umma na sera, kupitia ubia wetu na vyombo vya habari, juhudi za kimataifa zinazoshughulikia masuala ya uongozi kama vile mpango wa Ushirikiano na Serikali wazi (OGP).
  3. Tovuti: www.twaweza.org Facebook: Twaweza Tanzania Twita: @Twaweza_NiSisi
*****
Approval of the President is higher among older citizens and those with lower education levels

15 June 2017, Dar es Salaam: 
Seven out of citizens (71%) approve of the performance of President Magufuli since taking office. This is down from 96% in June 2016. Approval ratings for the President vary between groups.
  • 68% of those under age 30 approve of the President compared to 82% of those over 50
  • 75% of citizens with no education or some primary approve of the President compared to 63% of those with secondary education or higher
  • And approval is slightly higher among poorer citizens (75%) than among the richest (66%).
Approval ratings for other political leaders have also fallen over the same period.
  • MPs: 58% approval rating (April 2017) compared to 68% (June 2016)
  • Councilors: 59% approval rating (April 2017) compared to 74% (June 2016)
  • Village / street chair-people: 66% approval rating (April 2017) compared to 78% (June 2016)

These findings were released by Twaweza in a research brief titled The end of the beginning? Priorities, performance and politics in Tanzania. The brief is based on data from Sauti za Wananchi, Africa’s first nationally representative high-frequency mobile phone survey. The findings are based on data collected from 1,805 respondents across Mainland Tanzania (Zanzibar is not covered in these results) in April 2017.

Support for political parties paints a mixed picture. Support for CCM has remained steady, ranging between 54% and 65% between 2012 and 2017. After a slump in 2013 and 2014 during which the party’s approval rating fell to 54% (2013 and 2014) from 65% (2012), support has remained consistent since the election at 62% in 2015 and 63% in 2017. Support for Chadema, however, has seen declined to 17% in 2017 since it peaked at 32% in 2013.

Support for CCM is highest among older people (80%), compared to 55% among younger citizens. It is also higher among women (68%) than men (58%), in rural areas (66%) than urban areas (57%), among poorer citizens (69%) than among the relatively rich (53%). Fewer  than half (46%) of those with secondary, technical or higher education support CCM. Support for Chadema generally follows the opposite pattern, higher among the young, men, the relatively wealthy and those with more education.

Over the past two years, however, citizens’ priorities have shifted substantially. In 2015, 34% of citizens cited poverty or economic challenges as one of their top three priority areas for the country compared to 60% mentioning this in 2017. Even more notable, in 2015 fewer than one in ten citizens (9%) mentioned food shortages or famine as a priority issue compared to 57% in 2017.

During the same period, citizens’ concerns about public services and corruption appear to have diminished.

Percentages of citizens citing the following issues as among the top three challenges for the country:
  • Health: 40% in 2017 compared to 59% in 2015
  • Education: 22% in 2017 compared to 44% in 2015
  • Infrastructure: 21% in 2017 compared to 32% in 2015
  • Water supply: 19% in 2017 compared to 46% in 2015
  • Corruption: 10% in 2017 compared to 28% in 2015

Aidan Eyakuze, Executive Director of Twaweza, said: “A majority of citizens continue to approve of the performance of the President. But the sharp drop in ratings, combined with the drop in approval ratings for all politicians, sends a sobering message. Citizens are fast losing trust in their political leaders"

“But beyond the headline approval ratings” he continued, “a more interesting trend is visible. First, the sharp drop in people mentioning public services as priority areas is noteworthy. These sectors have consistently topped the ranks for citizens’ main challenges over the past three years. This poll suggests that citizens are signaling improvements in terms of public service delivery. But, the steep rise in the number of citizens expressing concerns about poverty and about food shortages should not be ignored. Citizens are deeply worried about the most basic of issues - food - and they are sending a strong message to their leaders. Who is listening?”


For more information:
Risha Chande, Senior Communications Advisor, Twaweza
e: rchande@twaweza.org | t: (+255) (0) 656 657 559

Notes to Editors
  1. This brief and the data contained can be accessed at www.twaweza.org, or www.twaweza.org/sauti
  2. Twaweza works on enabling children to learn, citizens to exercise agency and governments to be more open and responsive in Tanzania, Kenya and Uganda. We have programs, staff and offices across all three countries, and a globally respected practice of learning, monitoring and evaluation. Our flagship programs include Uwezo, Africa’s largest annual citizen assessment to assess children’s learning levels across hundreds of thousands of households, and Sauti za Wananchi, Africa’s first nationally representative mobile phone survey.  We undertake effective public and policy engagement, through powerful media partnerships and global leadership of initiatives such as the Open Government Partnership
  3. You can follow Twaweza’s work
  4. Web: www.twaweza.org     Facebook: Twaweza Tanzania     Twitter: @Twaweza_NiSisi

Viongozi wa Dini Watangaza Siku Saba za Kumwombea Rais Magufuli


Viongozi wa dini wametangaza maombi ya siku saba nchi nzima kumwombea Rais John Pombe Magufuli ili aendelee na juhudi zake za kulinda raslimali za watanzania kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii ya dini zote, Askofu William Mwamalanga kwa niaba ya viongozi wa dini.

“Tumeamua kufanya maombi ya siku saba kwa kumtaka kila mtanzania popote alipo kutembea hatua saba kila siku akimwombea Mhe. Rais Magufuli ili Mungu amlinde pamoja na anaofanyanao kazi kwa usahihi (uaminifu)”, alisema Askofu Mwamalanga.

Ndani ya siku hizo saba kila mtanzania atakuwa ametembea jumla ya hatua 49 akimwombea Rais Magufuli na wazalendo wenzake.

Kwa mujibu wa Kiongozi huyo wa Dini, maombi hayo yataanza leo Alhamisi Juni 15 nchi nzima na yatajumuisha watu wa dini zote nchini, yaani madhehebu ya Kiislam, Kikristo, Kihindu, Budha na madhehebu mengine.


Maombi haya yanafanyika baada ya kuona kuwa Mhe. Rais Magufuli anachukua hatua madhubuti za kutaka waliohusika kwa namna yoyote kuiba raslimali za Taifa hususani madini, wanachukuliwa hatua na kuitaka kampuni ya ACCASIA kulipa kile ambacho walichukua kinyume cha sheria.

Askofu Mwamalanga alisema kuwa Kamati yake inamwomba Rais Magufuli achukue hatua za haraka kudhibiti raslimali za nchi kwa upande wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambako mali nyingi zinatoroshwa na wajanja wachache.

Kamati hiyo ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii ya dini zote imemwomba Mhe. Rais aziunganishe Wizara za Nishati na Madini na Maliasili na Utalii na kuunda wizara moja ambayo itasimamia kwa karibu raslimali za watanzania.

“Tunamwomba Rais Magufuli amchague mtu makini na mzalendo mwenye uchungu na nchi hii ili asimamie wizara hiyo, na nina hakika wizara hiyo ikisimamiwa vizuri, ndoto ya Rais ya kuifanya Tanzania kuwa nchi mhisani itatimia kwa kuwa hapa Mungu ametujalia kila kitu”,alisema Askofu Mwamalanga.

Viongozi hao wamempongeza Rais Magufuli kwa Uzalendo na Ujasri alionao katika kulinda raslimali za Taifa na kupambana na maovu. Wamesema ni kiongozi wa kuigwa na Marais au viongozi Duniani kote.

Kuhusu suala la walioachishwa kazi kutokana na kuwa na vyeti feki, Askofu Mwamalanga alisema kuwa Kamati inamwomba Mhe Rais kuwasamehe wale ambao wameitumikia nchi hii kati ya miaka mitano na 30 ili walau wapatiwe kifuta jasho licha ya kwamba walitumika bila kuwa na vyeti halali vya Kidato cha nne.

“Msamaha tunaoomba si wa kuwarudisha kazini bali tunaomba kwa ajili ya kupata kiinua mgongo kwani wengine walitumika kwa uaminifu na hata kupewa tuzo za ufanyakazi hodari (bora) hasa katika sekta za Afya,wauguzi, Elimu na maeneo mengine”, alisema Askofu Mwamalanga.

Mapema wiki hii, Rais Magufuli alipokea ripoti ya pili ya uchunguzi wa makinikia ambayo iliwajumuisha wanasheria na wachumi. Katika ripoti hiyo ilibainika kuwa kiasi kikubwa cha madini kilichukuliwa bila watanzania kupata chochote. Takriban madini yenye thamani ya shilingi trilioni 108 yalisafirishwa nje ya nchi bila Tanzania kupata faida kutokana na madini hayo.