Matokeo chanyA+ online




Monday, February 26, 2018

TAASISI ZA MTANDAO WA WANAWAKE WAKUTANA KUJADILI UTUNGWAJI WA SHARIA MPYA YA VYAMA VYA SIASA ITAKAYOLENGA UJENZI WA USAWA WA JINSIA.


Mkutano Huo Ulioandaliwa Na Tanzania Women Cross Platform (Ulingo) Umehudhuriwa Na Mabaraza/Jumuiya Za Wanawake Kutoka Vyama Mbali Mbali Vya Siasa, Viongozi Wa Barazaa Vyama Vya Siasa, Tanzania Center For Democracy, Mtandao Wa Wanawake Wa Kikatiba Na Uongozi, Women Fund Tanzania, Tanzania Women Parliamentary Group Pamoja Na Umoja Wa Wanawake Wawakilishi Zanzibar

Baadhi Ya Maridhiano Ya Mkutano Ilikuwa Ni Pamoja Na;
1. Kutaka Sheria Mpya Kutoa Maelekezo Kwa Katiba Za Vyama Vya Siasa Kutambua Nafasi Za Usawa Wa Jinsi Katika Nafasi Na Vikao Muhimu.

2. Kutaka Sheria Mpya Iwatambue Kikatiba Nafasi Za Usawa Kwa Wanawake (Kuwe Na Deliberate Clause)

3. Wajumbe Wameomba Vyama Vya Siasa Vipunguziwe Nguvu Ili Kuwa Na Taasisi Imara Ambazo Sio Za Kisiasa

4. Wajumbe Pia Wamelaani Vikali Matumizi Ya Lugha Zisizo Na Staha Zinazoendelea Katika Majukwaa Ya Kisiasa Na Kusema Kwamba Huo Sio Utamaduni Wetu Wa Siasa

Mgeni rasmi wa mkutano huo Mhe Naibu Spika wa Baraza la wawakilishi Zanzibar amepokea mapendekezo na maridhiano ambayo yatafikishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kama maoni katika kuandaa sheria mpya ya vyama vya siasa.

Pamoja na wajumbe wengine muhimu waliohudhuria akiwemo Mhe John Cheyo, Mhe John Shibuda, Mhe Suzan Lymo, pamoja na wengine wengi wamekubaliana kuandaa kikao kupitia ULINGO ili kukutana na viongozi wote wa vyama vya siasa katika kueleza maoni yao.
















Wednesday, February 21, 2018

ZIARA  YA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN MKOANI SIMIYU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma maneno yalioandikwa kwenye jiwe la msingi mara baada ya kufungua jengo la upasuaji kwenye hospitali ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais akimsabahi Mtoto Mchanga pamoja na Mama yake Bi. Mariam Patrik mkazi wa Nyashimba ambaye amejifungua katika wodi ya wazazi ya hospitali ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kufungua jengo la Upasuaji lililopewa jina la Samia Suluhu Hassan Operating Theatre.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu kama ishara ya ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima lenye vyumba 43 vya kufanyia kazi.


MAKAMU WA RAIS  MKOANI SIMIYU







Sunday, February 11, 2018

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MUFINDI

Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Iringa ambapo leo alitembele wilaya ya Mufindi na kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ikiwa mmoja ni wa kujenga maabara ya kisasa na madarasa na kidato cha tano na cha sita katika Sekondari ya Mgololo na upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.
Akiwahutubia wananchi waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi  la Upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole , Makamu wa Rais alisema katika kila kituo cha afya kinachopanuliwa ama kujengwa Serikali imezingatia  huduma za mama na mtoto ili kupunguza vifo vya akinamama na watoto, kuborsha huduma za upasuaji .
Serikali imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho na kutumia mafundi wa kawaida kujenga ilikuweza kusaidia kutoa ajira kwa vijana zaidi wa eneo husika.
Makamu wa Rais amezitaka halmashauri zisimamie utoaji na matumizi ya fedha wanazotoa kwa Vijana asilimia 5 na Wanawake asilimia 5 ili kuleta tija kwenye shughuli za maendeleo.
Makamu wa Rais alisema  “tunapozungumzia uchumi wa viwanda lazima tuwaandae Vijana tangia wadogo, tuhakikishe wanafundishwa  yale yanayohitajika”.
Makamu wa Rais aliwaambia wakazi wa Mafinga, watakapokuja tena kwenye kampeni watawataka wananchi waseme Serikali yao imewafanyia nini.
Mapema leo Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara na madarasa  ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Mgololo, ujenzi ambao utagharimu  shilingi milioni  450 za kitanzania chini ya ufadhili wa kiwanda cha Mufindi Paper Mills.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa ujenzi wa kituo cha afya Ihongole Mafinga, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma maneno yalioandikwa kwenye jiwe la msingi la ujenzi wa maabara na madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Mgololo, Mufindi mkoani Iringa mara baada ya kulifungua ,pembeni yake ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Rai wanaomiliki kiwanda cha Mufindi Paper Mills Bw. Jaswant S. Rai na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza. 





 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwenye uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole

Saturday, February 10, 2018

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA ASEMA MWISHO WA KERO ZA ARDHI NA DHURUMA NYINGI KWA WANYONGE UMEFIKA