Matokeo chanyA+ online




Tuesday, March 31, 2020

PROF. KABUDI ATEMBELEA IDARA NA VITENGO WIZARANI AZUNGUMZA NA WATUMISHI



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof.  Palamagamba John Kabudi (wa kwanza kulia) akizungumza na watumishi wa Idara ya Ulaya na Amerika wakati alipowatembelea na kujadililiana nao masuala mbalimbali ya utendaji kazi wa Idara hiyo kwenye ofisi za Wizara zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma, tarehe 31 Machi 2020

Mhe. Waziri Prof. Kabudi akimsikiliza mmoja wa watumishi wa Idara ya  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakitoa ufafanuzi kuhusiana na utekelezaji wa majukumu ya idara.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof.  Palamagamba John Kabudi ametembelea Idara na vitengo vya wizarani na kuzungumza na watumishi walioko katika ofisi za wizara
kwenye majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma, tarehe 31 Machi 2020.

Prof. Kabudi ametumia nafasi hiyo kuzungumza na mtumishi mmoja mmoja ili kuwafahamu na kuona jinsi  wanavyoyafahamu na kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuona namna wanavyogeuza changamoto wanazokutana nazo kuwa fursa katika sehemu zao za kazi


Monday, March 30, 2020

MKUTANO WA BAJETI KUANZA LEO JIJINI DODOMA



 Spika wa  Bunge, Job Ndugai (Mb), akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ambayo yatafanyika katika  Utaratibu wa Uendeshaji wa Shughuli za Bunge wakati wa Mkutano wa Bunge wa Bajeti unaotarajiwa kuanza leo Jijini Dodoma. Spika ametangaza mabadiliko kadhaa ambayo yatafanyika wakati wa uendeshaji wa shughuli za Bunge ili kukabiliana na janga la Ugojwa wa Korona.  Wakwanza kulia ni  Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.
 Spika wa Bunge Job Ndugai (katikati) akizungumza wakati wa Kikao cha kamati ya Uongozi ambayo ilikutana ili kujadili na kupitisha shughuli zitakazofanyika wakati Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuanza kesho Jijini Dodoma. kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na  Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama.
   Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akizungumza wakati wa Kikao cha kamati ya Uongozi ambayo ilikutana ili kujadili na kupitisha shughuli zitakazofanyika wakati wa Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuanza kesho Jijini Dodoma. Katikati ni Spika wa Bunge Job Ndugai na Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Jenista Mhagama.

Wajumbe wa kamati ya Uongozi katika kikao cha Kamati kilichokutana ili kujadili na kupitisha shughuli zitakazofanyika wakati wa Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuanza kesho Jijini Dodoma.

PICHA NA BUNGE

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA HOSPITALI WILAYA YA KIBAHA ILIYOTENGWA KUWAHUDUMIA WAGONJWA WA CORONA

Waziri Mkuu, Kaasim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (wa tatu kulia) wakati alipokagua hospitali ya wilaya ya kibaha iliyopo eneo la Lulanzi  ambayo imetengwa kwa ajili ya kuwahuduma kwa wagonjwa wa Coroma, Machi 28, 2020.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo  na wa pili kushoto ni  Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Bakari.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua wodi za hospitali ya wilaya ya Kibaha  iliyopo eneo la Lulanzi  ambayo imetengwa  kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa Corona Mchi 28, 2020. Kushto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilio. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu 
 
Na.WAMJW-Kibaha

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea Hospitali mpya ya Halmashauri ya Wilaya Kibaha ambayo itatumika kulaza  watakaobainika kuwa na Virusi vya ugonjwa wa Corona (Covid19).

Mhe.Kassim Majaliwa amesema  hospitali hiyo itatumika kulaza watu walioambukizwa ugonjwa huo  na kwamba itatumika kwa muda na baada ya ugonjwa huo kwisha itaanza kutoa huduma nyingine za afya.

Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi wa Wilaya ya Kibaha kuwa watu wenye maambukizi ya VIRUSI vya  COVID 19 watalazwa katika hospitali hiyo kwa muda wa siku 14 na baada ya uchunguzi ikibainika hawana ugonjwa huo wataruhusiwa kurejea nyumbani.

Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya Corona na amezikumbusha familia kuwa na utaratibu wa kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji tiririka na sabuni au  kutumia vitakasa mikono (sanitizer).

Awali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alimweleza Waziri Mkuu kwamba hospitali hiyo ilipokea kiasi cha shilingi milioni 394 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa hospitali hiyo.
 

Saturday, March 28, 2020

WATANZANIA ENDELEENI KUKABILIANA NA CORONA - WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  wakikagua jenereta lilitolewa na familia ya Karimjee  Jivanji ya jijini Dar es salam lenye thamani ya sh. milioni 75 wakati alipopokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali  kwa ajili  ya mapambano dhidi ya  ugonjwa wa CORONA, Machi 28, 2020, Magogoni jijini Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Azan Zungu.

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kukabiliana na ugonjwa wga  Corona ili Kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo na mheshimiwa Waziri Mkuu baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa kinga, fedha na dawa kutoka taasisi, kampuni na umoja wa mama ntilie nchini.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipima joto la mwili wakati alipowasili ofisini kwake  Magogoni jijini Dar es salaam kupokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali  kwa ajili ya mapambano dhidi ya  ugonjwa wa Corona, Machi 28, 2020.
 Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema Kuwa Watanzania wanapaswa kuzingatia kuchukua tahadhari kama vile kunawa mikono Mara kwa Mara kwa maji yanayotiririka na kuepuka misongamano ili kudhibiti janga hili kubwa lililozikumba pia mataifa makubwa.

“Wakati tunaendelea kukabiliana na janga hili la Corona pia tunapaswa kujua kwamba ugonjwa huu utaleta athari za kiuchumi,” amesema Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu amewashukuru Watanzania waliojitokeza kuchangia fedha, dawa na vifaa kinga kwa Kuwa msaada huo itasaidia watu WOTE waliokumbwa na COVID- 19 pamoja na kusaidia Watanzania kujikinga  ili Kuzuia kusambaa kwa homa kali ya mapafu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. milioni 230  ukiwa ni mchango wa Benki ya UBA wakati alipopokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali  kwa ajili ya mapambano dhidi ya  ugonjwa wa CORONA, Machi 28, 2020, Magogoni jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kushoto ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Usman Isaka na wa nne kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Farhiya Warsama. 

“Hivi vitu vyote tulivyopokea Leo ni gharama kubwa, tumeona Watanzania wenye moyo wamekuja hapa kuungana na Serikali kukabiliana na ugonjwa huu, hivyo hatuwezi kuacha hivi bila kutoa shukrani kwa wenzetu waliotoa msaada huu,” amesema Mhe. Waziri Mkuu.

Amesema Watanzania wanaopenda kuchangia jitihada za kukabiliana na ugonjwa huu, wachangie fedha Benki Kuu kupitia akaunti ya National Relief Fund Electronic, namba 9921159801 na kwamba wanaweza kuchangia kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitumika kitakasa mikono wakati alipowasili ofisini kwake  Magogoni jijini Dar es salaam kupokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali  kwa ajili ya mapambano dhidi ya  ugonjwa wa Corona, Machi 28, 2020.

Baadhi ya Kampuni zilizochangia Serikali katika kukabiliana na Corona ni Benki ya NMB milioni 100, CRDB  Milioni 150, Benki ya UBA  milioni 230,  umoja wa mama ntilie  Milioni 2, Ashton Media  Milioni 104 na Kampuni mbalimbali zimechangia  fedha na vifaa kinga kwa lengo la kukabiliana ugonjwa wa Corona.

Wakati huohuo Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa kwa kipindi cha masaa 24 tangu jana Alhamisi Machi 27,2020 jumla ya sampuli 26 zimewasilishwa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na zote zimethibitishwa hazina maambukizi'Negative', hivyo  mpaka sasa hapa nchini watu waliothibitika 'positive' kuwa na ugonjwa huo bado ni kumi na tatu(13).

RAIS MAGUFULI AWASILI CHATO MKOANI GEITA AKITOKEA DODOMA

Rais Dkt John Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Ndege Chato Mkoa wa Geita leo Jumamosi akitokea jijini Dodoma.

Rais Dkt John Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Ndege Chato Mkoa wa Geita leo Jumamosi akitokea jijini Dodoma.

Rais Dkt John Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Ndege Chato Mkoa wa Geita leo Jumamosi akitokea jijini Dodoma.








Friday, March 27, 2020

KINONDONI YA PAMBANA NA CORONA KWA KUPULIZIA DAWA KWENYE MAENEO YA MIKUSANYIKO



Mratibu wa kudhibiti Malaria mkoa wa Dar es Salaam, Dokta Ford Chisongela akiangalia wataalamu wa Afya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wakati wakikagua mtambo unaotumika kupulizia dawa kwa ajili ya kuuwa wadudu wanaoambukiza homa inayosababishwa na Virusi vya Corona.
Wataalamu wa Afya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wakipuliza dawa katika vituo vya mabasi ya endayo haraka katika eneo la Kinondoni Mkwajuni. 

Halmashauri ya Manispa ya Kinondoni kwa kushirikiana na wataalamu wa Afya wa Halmashauri hiyo na mkoa wa Dar es Salaam wameendesha zoezi la upuliziaji dawa katika vituo vya mabasi yaendayo haraka pamoja na vituo vya daladala ikiwa ni katika mkakati wa kudhibiti  maambukizi ya Vizuri vya Corona.
 Zoezi hilo  limefanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo makazi ya wananchi , maeneo ya kutolea huduma mbalimbali ikiwemo masoko sambamba na kwenye mikusanyiko ya watu hususani  Kanisani na Msikitini.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo, Mhe. Benjamini Sitta amesema kuwa zoezi hilo linafanyika kwa lengo la kuuwa wadudu wanaosababisha maambukizi ya Vizuri vya Corona (COVID 19) na kwamba maeneo yote katika Halmashauri hiyo yatapuliziwa dawa.
Meya Sitta amefafanua kuwa ugonjwa huo ambao umekuwa tishio kubwa duniani Halmashauri hiyo imejipanga kikamilifu katika kuukabili ugonjwa huo usisambae ikiwa ni pamoja na kusambaza wataalamu wa kupulizia dawa hiyo kwenye kata zote za Halmashauri hiyo.
“Kwa ujumla tunashiriki ipasavyo katika kupambana na maambukizi ya virusi hivi, kwa pamoja tunaunganisha nguvu kutoka kwenye ngazi ya mkoa,  Kinondoni ni Halmashauri moja wapo ambayo imeanza zoezi hili  kwenye maeneo yote na leo tumeanzia Kata ya Msasani ambapo ndio kuna wataalii wengi” amesema Mhe. Meya Sitta.
Mhe. Meya Sitta ameongeza kuwa “ ni jambo la muhimu kuchukua hatua kabla ya kupata madhara , nakinga ni muhimu kuliko tiba , Kinondoni hatujasubiri janga hili litufikie, tulianza kuchukua hatua mapema, tulijiandaa vizuri ndio mana hata sasa tunaendelea kuchukua hatua kwakupiga dawa kwenye maeneo ya wananchi wetu.
Aidha Mhe. Meya Sitta amesisitiza kuwa Kinondoni imejipanga na hivyo kuishukuru Serikali ya awamu ya tano kwakudhibiti na kupambana dhidi ya kutokomeza ugonjwa huo sambamba na kuwaelimisha wananchi jambo ambalo limepokelewa kwa asilimia 100.
Kwa upande wake Mratibu wa Malaria mkoa wa Dar es Salaam, Dokta Ford Chisongela amesema kuwa  mkoa unashirikiana na Halmashauri katika kuhakikisha kuwa unatokomeza ugonjwa huo unaosababishwa na Vizuri vya COVID 19 ( Virusi vya Corona) kwa kupulizia dawa hizo katika maeneo yote ya mkoa huo.
Amefafanua kuwa katika kuongeza nguvu ya kupulizia dawa hiyo, mkoa umeamua kutumia magari ya zimamoto pamoja na yale ya Polisi kikosi Cha kutuliza ghasia (FFU) kwa lengo la kuongeza nguvu katika zoezi hilo kwa kuwa magari hayo yanauwezo mkubwa wa kufanya kazi  kwa haraka na hivyo kuwatoa hofu wananchi wasishtuke pindi watakapo yaona mitaani.

WAZIRI MKUU MAJALIWA - KAMATI ZA MAAFA KATIKA NGAZI ZA MIKOA NA WILAYA ZIUNGANE NA WARATIBU WENGINE KUKABILIANA NA CORONA (COVID-19)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na ugonjwa wa Corona, ambayo yeye ni Mwenyekiti wake, katika kikao kilichofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Machi 25, 2020. (Picha na OIfisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza kamati za Maafa katika ngazi za mikoa na wilaya ziungane na waratibu wa kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) waliopo katika maeneo yao.

Pia, Waziri Mkuu amewasisitiza Watanzania waendelee kujikinga na ugonjwa huo kwa kuhakikisha wanajiepusha na misongamano isiyokuwa ya lazima na hata wakienda kwenye maeneo ya kutolea huduma kama sokoni, vituo vya mabasi wapeane nafasi kati ya mtu mmoja na mwingine.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Machi 26, 2020) wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Kitaifa cha Kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma. Kikao hicho kimehusisha wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ipeleke wataalamu katika maeneo yenye mahitaji makubwa kama kwenye viwanja vya ndege, vituo vya mabasi na bandarini.

“Lengo letu ni kuhakikisha nchi inabaki salama hivyo Watanzania tuendelee kuwa na tahadhari ya kutosambaa kwa ugonjwa huu na pale tunapokwenda kwenye maeneo ya kutolea huduma tujipe nafasi kati ya mtu mmoja na mwingine.”

Waziri Mkuu amesema kamati hiyo inatakiwa ifuatilie na isimamie vizuri ili kuhakikisha watu wote wanaoingia nchini wanapimwa na wanafuatilia ili kujua historia zao za safari katika kipindi cha siku 14, lengo likiwa ni kuzuia maambukizi hayo yasisambae kwa jamii.

Amesema watu wote waliopewa dhamana ya kuratibu zoezi la kupeleka watu walioko kwenye karantini, wahakikishe wahusika wanafika kwenye hoteli walizozichagua. Pia Serikali inafanya utaratibu wa kutenga maeneo ambayo watu watakuwa wanakaa bila gharama na yatakuwa na huduma zote muhimu.

Pia, Waziri Mkuu amevishukuru vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Serikali katika kuelimisha umma namna ya kujikinga na virusi vya corona, ambapo amevitaka viendelee na utaratibu huo kwani utasaidia wananchi kupata elimu na kuweza kujikinga na maabukizi hayo.

Machi 23, 2020, Waziri Mkuu aliunda kamati tatu kwa ajili ya kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi ya corona (COVID-19).

Kamati hizo ni ya Kitaifa ambayo inaongozwa na Waziri Mkuu na itahusisha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Wengine ni Waziri Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Pia, Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Msemaji Mkuu wa Serikali, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Katika kikao cha leo, Waziri Mkuu ameongeza wajumbe wawili ili waongeze nguvu katika kukabiliana na virusi vua corona ambao ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Thursday, March 26, 2020

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI PAMOJA NA TAARIFA YA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipima joto la mwili kabla ya kuingia katika ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kupokea Taarifa ya CAG kwa Mwaka 2018/2019 pamoja na Taarifa ya TAKUKURU leo tarehe 26/03/2020.

 Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipima joto la mwili kabla ya kuingia katika ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
 Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipima joto la mwili kabla ya kuingia katika ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

 Spika wa Bunge Job Ndugai akipima joto la mwili kabla ya kuingia katika ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kutoka kwenye ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo alipokea Ripoti mbili za Mwaka 2018/2019 kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa PCCB pamoja na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu, pamoja Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakitoka kwenye ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Spika wa Bunge Job Ndugai wakwanza kushoto waliokaa, akifatiwa na CAG Charles Kichere, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo wapili kutoka kulia waliokaa pamoja na Wafanyakazi wa Ofisi ya TAKUKURU na CAG, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Spika wa Bunge Job Ndugai wakwanza kushoto waliokaa, akifatiwa na CAG Charles Kichere, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo wapili kutoka kulia waliokaa pamoja na Wafanyakazi wa Ofisi ya TAKUKURU na CAG, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ripoti ya Mwaka 2018-2019 kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 26/03/2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ripoti ya Mwaka 2018-2019 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, wakionyesha ripoti 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea Ripoti mbili za Mwaka 2018/19, moja kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea Ripoti mbili za Mwaka 2018/19, moja kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Makabrasha ya Taarifa Mbalimbali alizokabidhiwa na CAG katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma Muhtasari wa Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ya Mwaka 2018-2019 iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 26/03/2020.
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere akisoma Muhtasari wa Taarifa yake ya Mwaka 2018/2019 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU