Matokeo chanyA+ online




Monday, June 27, 2022

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA KWENYE KILELE CHA SHEREHE YA MIAKA 25 YA MFUKO WA FURSA SAWA KWA WOTE (EOTF) JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika kilele cha Sherehe ya miaka 25 ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Juni, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko huo tarehe 27 Juni, 202

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa pamoja na Baadhi ya Wake wa Viongozi mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko huo tarehe 27 Juni, 2022


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kazi mbalimbali za kijasiriamali zinazofanywa na wanufaika wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) katika maadhimisho ya kilele cha Mfuko huo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC  Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Juni, 2022





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo kwa Baadhi ya Wafadhili waliojitolea kuunga mkono  Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) katika maadhimisho ya kilele cha Mfuko huo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC  Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Juni, 2022



Viongozi mbalimbali pamoja na Wanufaika wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko huo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Juni, 2022.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyekiti wa EOTF Mama Anna Mkapa katika picha ya pamoja na Wake wa Viongozi mara baada ya maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko huo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Convention Center Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Juni, 2022.



 

Monday, June 13, 2022

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan atembelea Kituo cha Saratani cha Dar Al Hanan, Muscat nchini Oman


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati alipotembelea Kituo cha Saratani cha Dar Al Hanan kilichopo Muscat nchini Oman tarehe 13 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Kituo cha Saratani cha Dar Al Hanan kilichopo Muscat nchini Oman wakati alipotembelea Kituo hicho tarehe 13 Juni, 2022.

 

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KIONGOZI MKUU WA TAIFA LA OMAN SULTAN HAITHAM BIN TARIQ AL SAID, MUSCAT NCHINI OMAN



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Kiongozi Mkuu wa Taifa la Oman Sultan Haitham bin Tariq Al Said mara baada kuwasili Al Alam Muscat kwa ajili ya mazungumzo yaliyofanyika tarehe 13 Juni, 2022. 

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Kiongozi Mkuu wa Taifa la Oman Sultan Haitham bin Tariq Al Said mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Al Alam Muscat nchini humo tarehe 13 Juni, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Mwenyeji wake Kiongozi Mkuu wa Taifa la Oman Sultan Haitham bin Tariq Al Said kwenye Kasri ya Al Alam Muscat nchini humo tarehe 13 Juni, 2022. 

 





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembelea na kuangalia shughuli mbalimbali za Utamaduni, pamoja na historia ya Oman katika Makumbusho ya Taifa hilo yaliyopo Muscat nchini humo tarehe 13 Juni, 2022.


 

CHAMA CHA USHIRIKA CHA MUUNGANO KIZIGUZIGU KAKONKO KIGOMA KUUZA TANI 400 ZA MAHARAGE WFP

Wakulima Agnes Christopher (kutoka kulia)  Esther Makere na Winfrida Mkwabi wakisambaza maharage ambayo yamefikishwa na wakulima kwenye Chama cha Ushirika Muungano Kiziguzigu wilayani Kakonko mkoani Kigoma.
  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa               akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya kilimo.

Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Muungano kata Kiziguzigu wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Jackson Bujege akitoa maelezo namna walivyonufaika na WFP
Ofisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kakonko, Mkoa wa Kigoma Khalfan Muhidin akielezea namna WFP na mashirika mengine yalivyoinua kilimo wilayani hapo.

 

Na Mwandishi Wetu, Kakonko

 

CHAMA cha Ushirika cha Muungano Kiziguzigu Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma kinatarajia kuuza tani 400 za zao la maharage kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wanunuzi wengine katika msimu huu wa 2021/2022.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Ushirika huo, Jackson Bujege wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao walitembelea chama hicho na kuona shughuli ambazo wanafanya.

Bujege alisema wakulima wa maharage wameongeza uzalishaji baada ya kupata Mradi wa Kigoma Pamoja Program (KJP), ambapo kwa upande wa kilimo  unatekelezwa na WFP, Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC), Shirika la Uendelezaji wa Mitaji la Umoja wa Mataifa (UNCDF) na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO).

Alisema mashirika hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza uzalishaji, ubora wa mazao na masoko hivyo watahakikisha manufaa hayo yanaendelea.

“WFP wamekuja kutukomboa ambapo baada ya mradi kuanza mwaka 2018 walinunua tani 100 za maharage, msimu wa pili tani 368 na msimu huu tunatarajia kuuza tani 400 kwa sh.1950 hadi 2,000,” alisema.

Bujege alisema katika misimu hiyo miwili wakulima ambao ni wanachama wa AMCOS waliweza kuingiza sh.milioni 717, fedha ambazo zimetumika kuchochea shughuli za maendeleo na kilimo.

“AMCOS hii ina wanachama 308 ambapo wanaume ni 200 na wanawake 108, ila tunaendelea kuhamasisha wanachama wanawake kujiunga ili kuweza kuwainua,” alisema.

Alisema mikakati ya chama chao ni kuhakikisha uzalishaji unaongezeka hadi kufikia tani 1,000 za maharage.

Ofisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kakonko, Khalfan Muhidin alisema halmashauri hiyo inafurahi ujio wa WFP na mashirika mengine ambapo zaidi ya wakulima 1,800 wamepata elimu kuhusu uhifadhi mazao, mbinu za kulima, kupunguza upotevu wa mazao yakiwa shambani na masoko.

“Wananchi wengi wamehamasishwa kukusanya mazao katika eneo moja, kwani bei yake ni kubwa na wakulima wananufaika,” alisema.

Ofisa huyo alisema ujio wa mradi huo umeongeza mapato kwa halmashauri ambapo mwaka jana wamekusanya ushuru zaidi ya Sh.milioni 21.8 kutoka Sh.milioni tano zilizokuwa zikakusanywa awali.

Alisema wataendelea kutoa elimu kwa wakulima zaidi ya 200,000 walioko kwenye wilaya hiyo, ili kuhakikisha wanaongeza uzalishaji na kujiunga na vyama vya ushirika.

“Lengo ni kuongeza uzalishaji kupitia AMCOS zilizopo ambapo kwa sasa tuna Gwarama, Muungano, Kabingo, Kuchikeka na Kanyonza,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa alisema ujio wa mashirika hayo wilayani kwake umechangia shughuli za uchumi na maendeleo kukua kwa kasi.

Naye Mkuu wa Ofisi ya WFP Kibondo, Saidi Johari alisema katika msimu huu wanatarajia kununua tani 3,000 za maharage kutoka kwa wakulima mbalimbali nchini.

JAMII YA WAWINDAJI YA WAHADZABE SINGIDA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAPIMIA ARDHI

 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angeline Mabula akimpatia hatimliki ya kimila Bibi Agnes Mangashini kutoka Jamii ya Wawindaji ya Wahadzabe wa Kijiji cha Munguli Kata ya Mwangeza wilayani Mkalama wakati wa hafla ya kukabidhi hati hizo iliyofanyika jana.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo,

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angeline Mabula akizungumza katika hafla hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ,Sophia Kizigo akizungumza wakati wa zoezi la utoaji hatimiliki hizo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angeline Mabula na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo (kushoto)  wakiserebuka na Wanawake wa Kikundi cha Sanaa cha Jamii ya Wawindaji ya Wahadzabe wa Kijiji cha Munguli Kata ya Mwangeza wilayani Mkalama.
Watoto wakiwa kwenye hafla hiyo.

WAZIRI DKT MABULA AIPONGEZA JAMII YA WAHADZABE KWA KUKUBALI KUPIMIWA ARDHI

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameipongeza jamii ya wawindaji ya wahadzabe iliyopo wilaya ya Mkalama mkoani Singida kwa utayari iliyouonesha wa kutambua na kukubali kupimiwa maeneo yao na kupatiwa hatimiliki za kimila.

Jumla ya hatimiliki za kimila mia moja (100) zikiwemo 26 zinazomilikiwa kwa pamoja kati ya mke na mume zimetolewa kwa jamii ya wawindaji ya Wahadzabe ikiwa ni hatua kubwa kutokana na jamii hiyo kujishughulisha zaidi na uwindaji, utafutaji matunda, urinaji asali na uchimbaji mizizi.

Dkt Mabula alisema, hatua hiyo inaonesha nia na dhamira njema waliyonayo ya kutaka kuyalinda maeneo yao wenyewe na kwa kushirikiana na serikali.

‘’Hakika hizi ni salamu na ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa jamii ya wawindaji inaungana naye na mkoa tayari kwenda naye sambamba katika kuletea watu wote maendeleo’’ alisema Dkt Mabula.

Akizungumza na wananchi wa jamii ya wawindaji ya Wahadzabe katika kijiji cha Munguli kata ya Mwengeza wilaya ya Mkalama Juni 11, 2022 alisema, jamii hiyo ni miongoni mwa jamii ndogo nchini ambayo iko katika hali ya kupoteza ardhi wanayoimiliki kutokana na jamii nyingine kuingia na kufanya shughuli zisizoendana na tamaduni za jamii hiyo jambo alilolieleza linahatarisha ustawi na maisha na desturi za Wahadzabe.

 ‘’Katika miaka ya hivi karibuni jamii hii imekuwa ikikabiliwa na tishio la kutoweka na kupoteza uhalisia wa maisha yao baada ya jamii nyingine kuingia katika maeneo ya mapori ya asili yanayotumiwa na Wahadzabe kwa ajili ya kufanya  shughuli za ufugaji, ukulima na hata upasuaji wa mbao jambo alilolieleza limekuwa tishio kwa kiasi kikubwa kwenye jamii hii’’ alisema Dkt Mabula

Alitolea mfano wamatishio kwa jamii hiyo kuwa ni pamoja na kupotea kwa makazi ya asili yanayojengwa kwa nyasi kavu chini ya matawi ya miti, wanyama kutoweka, mizizi na matunda kupotea kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na shughuli nyingine ambazo hazilindi uoto wa asiili wa mapori hayo.

Hata hivyo, alisema kuwa, kwa kutambua athari iliyopo mbele ya jamii hiyo ya wahadzabe, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikitafuta njia bora ya kulinda jamii hiyo pamoja na jamii nyingine zinazofanana ili kuhakikisha inajenga jamii yenye usawa kwa watumiaji wote wa rasilimali za ardhi nchini.

Aidha, katika kuleta usawa Serikali imeendelea na program mbalimbali kuhakikisha kila kipande cha ardhi kinapimwa kwa lengo la kuruhusu usawa na ustawi  siyo tu wa binadamu bali wa viumbe vyote vyote hai nchini.

‘’Ukiachilia mbali ukuzaji na uhifadhi wa tamaduni za jamii ya uwindaji kiloichonifurahisha zadi ni kuona jinsi jamii ilivyostaarabika kwa kuona na kuelewa umuhimu wa baba na mama kumiliki ardhi kwa pamoja , kwa hili niwapongeze’’ alisema Dkt Mabula.

Mkuu wa wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo alisema, jamii ya Wahadzabe katika eneo hilo la kijiji cha Munguli kata ya Mwengeza imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya mgogoro wa mpaka unaosababisha maeneo wanayotegemea kwa shughuli zao kuharbiwa.

‘’Changamoto kubwa ya hapa, jamii ya Wahadzabe vyakula wanatoa porini, wanakula asali na nyama zakuwinda na misitu ikiharibiwa au maeneo wanayotegemea kupata vyakula yanapoharibiwa ni changamoto kubwa, hata hivyo niwapongeze kwa uvumilivu wao’’ alisema Kizigo.

Bosco Charles Samweli, Diwani wa Kata ya Mwengeza alimueleza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula kuwa, eneo hilo la jamii ya Wahadzabe kwa muda mrefu limekuwa na changamoto ya migogoro ya mpaka na wananchi wanaoishi wilaya za jirani za Karatu Arusha na Mbulu mkoa wa Manyara. Hata hivyo alisema kwa sasa changamoto zinaelekea kumalizika kutokana na juhudi kubwa za mkuu wa wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo katika kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na jamii ya wawindaji ya Wahdazabe katika kijiji cha Munguli kata ya Mwengeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida alipokwenda kutoa hatimiliki za kimila kwa wananchi wa jamii hiyo Juni 11, 2022. Wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo.

Mkuu wa wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida Sophia Kizigo akizungumza wakati wa zoezi la utoaji hatimiliki za kimila kwa jamii ya wawindaji ya Wahdazabe katika kijiji cha Munguli kata ya Mwengeza Juni 11, 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na Mkuu wa wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo wakiwapungia mkono wananchi wa jamii ya wawindaji ya Wahdazabe wakati wa zoezi la utoaji hatimiliki za kimila kwenye kijiji cha Munguli kata ya Mwengeza wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida Juni 11, 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimpatia hatimiliki ya kimila Chifu wa jamii ya wawindaji ya wahadzabe Edward Mkumbo kwenye kijiji cha Munguli kata ya Mwengeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida Juni 11, 2022. Wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo,




Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoka kwenye nyumba ya Chifu wa Jamii ya wawindaji ya Wahadzabe katika kijiji cha Munguli kata ya Mwengeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida Juni 11, 2022. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo.



Chifu wa jamii ya wawindaji ya wahadzabe Edward Mkumbo akiwa amesishikilia hatimiliki ya ardhi mara baadhi ya kukabidhiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula katika kijiji cha Munguli kata ya Mwengeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida Juni 11, 2022.


RAIS SAMIA AWASILI MUSCAT NCHINI OMAN KWA AJILI YA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU


Kikosi cha Jeshi la Oman kikiwasili katika viwanja vya Kasri ya Al Alam kwa ajili ya Mapokezi Rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Muscat nchini Oman tarehe 12 Juni, 2022. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Mwenyeji wake Kiongozi Mkuu wa Taifa la Omani Sultan Haitham bin Tariq Al Said wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa katika mapokezi Rasmi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kasri ya Al Alam Muscat nchini Oman tarehe 12 Juni, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Kiongozi Mkuu wa Taifa la Omani Sultan Oman Haitham bin Tariq Al Said kabla ya kuanza mazungumzo yaliyofanyika Kasri ya Al Alam Muscat nchini Oman tarehe 12 Juni, 2022. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Oman mara baada ya kuwasili Kasri ya Al Alam Muscat nchini humo tarehe 12 Juni, 2022.