Matokeo chanyA+ online




Thursday, August 24, 2023

VIONGOZI WAKUU WA BRICS WAKIWA KWENYE MKUTANO WA 15 WA BRICS UNAOFANYIKA JIJINI JOHANNESBURG NCHINI AFRIKA KUSINI TAREHE 24 AGOSTI, 2023.








 

MSAJILI AKUTANA NA VIONGOZI WA CHADEMA KUJADILI KUIMARISHA DEMOKRASIA NCHINI

Mwenyekiti wa CHADEMA mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe (kushoto), akisisitiza jambo mbele ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, wakati wa kikao cha Msajili na viongozi waandamizi wa CHADEMA leo jijini Dar es Salaam. Kikao cha Msajili na CHADEMA ni juhudi za ofisi hiyo kuimarisha hali ya kisiasa hususan demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini. 

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (katikati) na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (kulia) wakimsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA, mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe (kwanza kushoto) wakati wa kikao cha Msajili na chama cha CHADEMA chenye lengo la kuimarisha demokrasia ya vyama vingi vya siasa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe (kulia) akiteta jambo na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (katikati), baada ya kumaliza kikao chenye lengo la kuimarisha demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu Mkuu wa CHADEMA ndugu John Myika. 




 

Tuesday, August 22, 2023

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AMPOKEA RAIS WA JAMHURI YA INDONESIA JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana  na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo wakati alipowasili katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuanza Ziara ya Kikazi hapa nchini tarehe 22 Agosti, 2023.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo wakati wakielekea kwenye Viwanja vya mapokezi ya Viongozi Ikulu Jijini Dar es salaam wakati wa Ziara ya Kikazi ya Rais huyo hapa nchini tarehe 22 Agosti, 2023.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Indonesia ukipigwa katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam kwenye mapokezi rasmi kwenye Ziara ya Kikazi ya Rais huyo hapa nchini tarehe 22 Agosti, 2023.





Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam kwa Mapokezi rasmi wakati wa Ziara yake ya Kikazi hapa nchini tarehe 22 Agosti, 2023.






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo Ikulu Jijini Dar es salaam wakati wa Ziara yake ya Kikazi hapa nchini tarehe 22 Agosti, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko  Widodo wakati wa Ziara yake ya Kikazi hapa nchini Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 22 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 22 Agosti, 2023.


 

Monday, August 14, 2023

VIONGOZI PAMOJA NA BAADHI YA WANACHAMA WA CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA (TLS) PAMOJA NA CHAMA CHA WANASHERIA ZANZIBAR (ZLS) WAKIWA KWENYE KIKAO NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Kikao na Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Harold Sungusia akizungumza mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokwenda pamoja na ujumbe wake Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Masoud Rukazibwa akizungumza mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati alipokwenda pamoja na ujumbe wake Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati alipokutana na Viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.







Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Harold Sungusia Hati ya Kiwanja kilichopo Arusha kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi zao mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Agosti 14, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Wanachama wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Wanasheria Wanawake wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) pamoja na Wanasheria Wanawake wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Agosti 14, 2023.