Matokeo chanyA+ online




Sunday, May 31, 2020

WAZIRI KAIRUKI AWAPONGEZA VIONGOZI MKOA WA SINGIDA KWA KUHIMIZA UWEKEZAJI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kuchakata mafuta ya alizeti cha Yaza Investment kilichopo Wilaya ya Iramba mkoani hapa, Yusuph Nalompa, akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki (katikati), sababu ya kiwanda hicho kushindwa kuanza uzalishaji alipokitembelea wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea miradi ya uwekezaji mkoani hapa jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,  Dk. Rehema Nchimbi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida na viongozi wengine wa mkoa huo kwa kuhimiza uwekezaji hususani wa viwanda vya uzalishaji wa mafuta ya kula ya alizeti.

Kairuki alitoa pongezi hizo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea miradi ya uwekezaji mkoani hapa ambapo alikagua viwanda vitano vya  Yaza Investment, Kiwanda cha Singida Grains and Oil Mills au Singida Fresh, Kiwanda cha Meru Millers Ltd,  Kiwanda cha Biosustain Tz Ltd na Kiwanda cha Q-STEK Tz Ltd.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kula ya alizeti cha Singida Grains and Oil Mills au Singida Fresh, Khalid Ally (wa pili kushoto) akimuelekeza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki alipotembelea kiwanda hicho wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea miradi ya uwekezaji mkoani.

" Kipekee nikupongeze mkuu wa mkoa Dk. Rehema Nchimbi kwa namna unavyohimiza uwekezaji katika mkoa wa singida ambao mpaka sasa una viwanda 1800" alisema Kairuki.

Hata hivyo Kairuki alisikitishwa na Kiwanda cha kuchakata mafuta ya alizeti cha Yaza Investment kilichopo Wilaya ya Iramba mkoani hapa chenye uwekezaji mkubwa wa zaidi ya bilioni 10.2 kikiwa hakifanyi kazi licha ya miundombinu yake yote ikiwaimekamilika.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki, akitoka kuangalia mtambo wa kutengeneza mafuta ya alizeti katika Kiwanda cha  Meru Millers Ltd.

Kairuki alisema kiwanda hicho kilitegemea kutoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 50 huku ajira zisizo za moja kwa moja zaidi 1000, kuzalisha mbegu,  pamoja na wasafirishaji.

" Jambo ili linaumiza sana moyo na kusikitisha." alisema Kairuki.

Alisema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji imekuwa ikihimiza mara kwa mara kama juu ya uwekezaji kama ambavyo  Waziri Mkuu   mwenye wizara hiyo amekuwa akiweka mkazo katika kilimo cha mazao mkakati na hivi karibuni alionekana mkoani Kigoma akigawa miche ya mbegu za michikichi takriban milioni 1.8.
 Meneja wa Kiwanda cha Biosustain Tz Ltd, Salum Khalfan (katikati), akimuelekeza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki alipotembelea kiwanda hicho. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Sajjad Haider.
 Wafanyakazi wa Kiwanda cha Biosustain Tz Ltd wakiwa katika eneo la kiwanda.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki akiwa ameongoza na viongozi mbalimbali wakati akienda kukagua  Kiwanda cha Yaza Investment. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,  Dk. Rehema Nchimbi na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula.
 Wananchi Kijiji cha Ndago na viongozi wa Wilaya ya Iramba wakimsikiza Waziri Kairuki (hayupo pichani) wakati akizungumzia kuhusu Kiwanda cha Yaza Investment ambacho hakifanyi kazi.
 Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dk. Rehema Nchimbi, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ndago kuhusu kiwanda hicho.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki  akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ndago kuhusu kiwanda hicho.
 Askari Polisi wa Wilaya ya Iramba wakiimalisha ulinzi wakati wa ziara ya Waziri Kairuki katika Kiwanda cha Yaza Investment.
 Moja ya jengo la Kiwanda cha Yaza Investment.
 Makofi yakipigwa wakati  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki  alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ndago kuhusu kiwanda hicho.

Alisema amekuwa akifanya hivyo sehemu mbalimbali lengo likiwa ni kuona Taifa linajitosheleza katika mafuta ya kula kwani kwa sasa tunaagiza mafuta hayo zaidi ya asilimia 60.

Kairuki alisema Mkoa wa Singida umejaaliwa na kuwa una baraka kwani zao la alizeti linastawi vizuri na kuwa Kiwanda cha Yaza Investment ni moja ya kiwanda kikubwa katika Wilaya ya Iramba na mwekezaji ni mzawa hivyo haitawezekana uwekezaji huo hupotee hivi hivi.
 Mwananchi wa Kata ya Ndago. Hassani akizungumzia kiwanda hicho.

Alisema wizara inahimiza kuwepo na viwanda vingi vya kuzalisha mafuta ya kula na kuwa kama Taifa zaidi ya sh.bilioni 443 tunapoteza kwa ajili ya kuagiza mafutà na ukiangalia katika zao la alizeti zaidi ya asilimia 70 kwenye mafuta yanatokana na zao hilo hivyo ni lazima likapewa kipaumbele.

Msimamizi wa Kiwanda cha Singida Grains and Oil Mills, Jamal Juma akitoa taarifa kwa Kairuki alisema tozo mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kushindwa kutoa leseni ya athari za mazingira zimesababisha 
kiwanda hicho kuchelewa kuanza kufanya kazi.
 Diwani wa Kata ya Ndago, Hewery Nkandi akizungumzia changamoto wanazopata wananchi kutokana na kiwanda hicho kutofanya kazi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kula ya alizeti cha Singida Grains and Oil Mills au Singida Fresh, Khalid Ally (katikati) akienda kumtembeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki kwenye kiwanda hicho.

 Wananchi wakimsikiza Waziri Kairuki (hayupo pichani) wakati alipofika kutembelea Kiwanda cha Singida Grains and Oil Mills

Alisema mpaka sasa wanatoa huduma hiyo kwa shule za msingi 45 Arusha zenye jumla ya wanafunzi 65,743 na shule moja Singida yenye wanafunzi 1,288 na kuwa katika baadhi ya maeneo ya wakulima wametoa mbegu bora ya alizeti ili wakulima wavune 
zaidi kwa ekari na kupata mafuta mengi kutoka kilo moja ya mavuno.

Meneja wa Kiwanda cha Mount Meru Millers Ltd, Nelson Mwakabuta (katikati) akimuonesha  Waziri Kairuki mafuta yanayozalishwa na kiwanda hicho. Kulia ni Operation Meneja wa kiwanda hicho, Sanjay Chourasya.



Na Dotto Mwaibale, Singida

Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda cha Mount Meru Millers Ltd, Nelson Mwakabuta alisema ili kuongeza hamasa ya wanafunzi kuzingatia masomo hususan wa shule za msingi na kwa nia ya kukuza mahusiano mema mema na jamii, kampuni ina utaratibu wa kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi tangu mwaka 2015.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MARAIS WASTAAFU WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI ZA IKULU YA CHAMWINO MKOANI DODOMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Ofisi ya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma

. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Marais Wastaafu, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere pamoja na viongozi wengine wakati wa wimbo wa Taifa.

Viongozi mbalimbali wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi wa Ofisi za Ikulu ya Chamwino

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Marais Wastaafu, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere mara baada ya chakula cha mchana katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Marais Wastaafu, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere  ikulu ya chamwino  Dodoma.

Saturday, May 30, 2020

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MARAIS WASTAAFU WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI ZA IKULU YA CHAMWINO MKOANI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 30 Mei 2020.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere kuashiria uzinduzi wa Mitambo na magari yatakayotumika katika ujenzi wa Ujenzi Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 30 Mei 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika Chepe ili kuweka zege na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi Ujenzi Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 30 Mei 2020.

. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo la Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere wakisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere wakielekea kwenye uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Ofisi za ikulu ya chamwino mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli awakabidhi Hati ya Makabidhiano ya zawadi ya Ndege aina ya Tausi 25 kwa marais wastaafu na Mama Maria Nyerere mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere hafla hiyo fupi ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma


.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika sherehe za  Makabidhiano ya zawadi ya Ndege aina ya Tausi 25 kwa  marais wastaafu na Mama Maria Nyerere mjane wa Baba wa Taifa  kwa ajili ya kuwafuga katika Makazi yake, hafla hiyo fupi ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Hati ya Makabidhiano ya zawadi ya Ndege aina ya Tausi 25 kwa Mama Maria Nyerere mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kuwafuga katika Makazi yake, hafla hiyo fupi ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Hati ya Makabidhiano ya zawadi ya Ndege aina ya Tausi 25 rais mstaafu Benjamin William Mkapa kwa ajili ya kuwafuga katika Makazi yake, hafla hiyo fupi ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Thursday, May 28, 2020

TAKUKURU MKOA WA SINGIDA YAMBURUZA KORTINI DAKTARI KWA TUHUMA YA RUSHWA


Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda, akizungumza na waandishi wa habari.
Na Godwin  Myovela,  Singida.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) Mkoa wa Singida imemburuza mahakamani Dkt. Abdul Sewando wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida (Mandewa) akituhumiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mgonjwa kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana kwenye ofisi za PCCB, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 5, 2020 majira ya saa 9 na nusu alasiri baada ya kuwekewa mtego na kujiridhisha uwepo wa tuhuma hizo.
Alisena mtuhumiwa alikamatwa na maafisa wa TAKUKURU baada ya kumaliza kumsafisha mgonjwa akiwa eneo la Hopitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Singida (Mandewa)
Elinipenda alisema awali uchunguzi wa TAKUKURU mkoani hapo ulibaini,  Mei 6, 2020 mtuhumiwa alipokea kiasi cha sh.60, 000 kutoka kwa mgonjwa ambaye jina lake limehifadhiwa ili ampe huduma ya kumsafisha baada ya kumfanyia vipimo vya ' Ultra Sound.'
Alisema uchunguzi wao pia  ulibaini kuwa mtuhumiwa alielekeza atumiwe fedha hizo kwa njia ya mtandao ambapo alizipokea kwa njia ya Mpesa kupitia simu yake.
Elinipenda alisema TAKUKURU Mkoa wa Singida inatoa rai kwa watumishi wa idara ya afya mkoani humo kufanyakazi kwa kuzingatia maadili na miiko ya taaluma zao hususani kipindi hiki ambacho jamii inawategemea sana kutokana na janga la Corona.
Aidha alisema Wananchi wasisite kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwa kufika ofisini, kupiga simu ya bure 113, kutuma ujumbe kwenye namba 113 na kupakua TAKUKURU App.

WAKULIMA WILAYA YA IKUNGI WAPONGEZA SERIKALI KWA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI

 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza kuhusu malipo ya wakulima wa Kata ya Iglanson kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.

Wakulima  Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wapongeza Serikali kwa kuelekeza ununuzi wa mazao yao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.

Pongezi hizo walizitoa mwishoni mwa wiki wakati wa ulipwaji wa fedha zao baada ya kuuza choroko kwa  njia ya stakabadhi ghalani katika Kata ya Iglanson.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza wakati wa utoaji wa malipo hayo alishukuru Serikali  kwa kuwajali wakulima.
 Afisa Ushirika wa Wilaya ya Ikungi, Gurisha Nsemo akizungumza na Wakulima wa Kata ya Iglanson wakati wa malipo hayo.

" Kipekee nishukuru Serikali kwa kuelekeza matumizi ya mfumo huu wa stakabadhi ghalani kwani umekuwa ni mkombozi kwa wakulima wetu." alisema Mpogolo.

Alisema katika wilaya hiyo wakulima zaidi ya 500 wamenufaika na mfumo huo ambapo wameweza kupata zaidi ya sh.milioni 139 na kuokoa zaidi ya sh.milioni 54 ambazo wangenyonywa wakulima.

Mpogolo alisema changamoto kubwa iliyokuwepo ni walanguzi hao kujikita kwenye maeneo ya vijiji na kuupinga mfumo huo kwa kuwa ulikuwa ukiwanufaisha kwa miaka mingi.
Mkulima, Isack Shango,  akimshukuru Rais Magufuli kwa niaba ya wenzake.   
Mkulima, Magreth Magamba, akizungumza. 

  
Wakulima wa Kata ya Iglanson wakisubiri kulipwa.
Alisema wachuuzi walikuwa wanatumia vipimo feki kwani utakuta katika kilo 50 zitazopimwa na mkulima utaona kilo tatu zilikuwa zikikatwa kiujanja na walanguzi hao.  Huku wachuuzi wakinunua kilo moja kati ya sh.400 hadi 600 lakini kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani waliweza kuuza kwa sh.1075 kwa kilo kwenye mnada wa tarehe 14 mwezi Mei 2020.

Mpogolo alitaja changamoto nyingine kuwa ni walanguzi hao kuwalaghai wakulima kuwa vyama vya ushirika vilikiwa havina uwezo wa kuwalipa fedha zao siku hiyo hiyo wakati sio agizo la mfumo.

Wakulima wa Kata ya Iglanson wakisubiri kulipwa. 
 Meneja wa Benki ya NMB, Wilaya ya Ikungi, Osward Kayuni, akizungumzia umuhimu wa wakulima hao kufungua akaunti ili malipo yao yalipwe kwa njia ya simu. 

Akimuongelea mkulima Joyce Nzela ambaye alitoa malalamiko kwa Rais Magufuli wakati alipo simama kwa muda na kuongea na wananchi wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma akitokea Chato, ambaye alilalamikia mfumo wa ununuzi wa zao hilo alisema walipofuatilia hakuonekana katika orodha ya wakulima waliopeleka choroko  kwenye AMCOS ya Kijiji cha Mayaha kama alivyodai. Hata hivyo kumbukumbu zilionyesha kwenye mkutano wa kutoa elimu ya mfumo uliofanyika Mei Mosi 2020 Kijiji cha Mtavila kuwa Joyce, alikuwa miongoni mwa wachuuzi walioupinga mfumo na kuwataka wakulima wasiukubali.

" Tulifuatilia tuligundua jina lake halikuwepo kwenye orodha ya wakulima ambao walipaswa kulipwa lakini wenzake, Zuhura na Amina walikuwepo kwenye orodha ya AMCOS ya Iglanson na malipo yao yalikuwepo." alisema Mpogolo.
 Choroko zikiwa kwenye mnada.

Mkulima, Isack Shango,  alimshukuru Rais Magufuli kwa niaba ya wenzake na kusema walanguzi walikuwa wakiwanyonya kwa kutumia vyombo vikubwa huku bei ikiwa ndogo.

Alisema walanguzi hao walikuwa wakitumia ndoo maarufu kwa jina la Mozambiki yenye ukubwa wa kuingiza kilo 25 ambayo ikiwa na malighafi walinunua kwa sh.60,00 na bila malighafi walikuwa wakilipia sh.70,000
Mkulima, Francis Magesa (kushoto) akitafsiri lugha ya kisukuma wakati mama huyo (kulia) alipokuwa akimshukuru Rais Magufuli kwa kuwapelekea mfumo huo.

Na Dotto Mwaibale, Singida
Wakulima wengine waliompongeza Rais Magufuli kwa kuwawezesha kulipwa fedha zao kupitia Benki ya NMB ni pamoja na  Magreth Magamba, Emmanuel Ncheyi na Francis Magesa.

Meneja wa Benki ya NMB, Wilaya ya Ikungi, Osward Kayuni aliwataka wakulima hao kufungua akaunti katika benki hiyo ili malipo yao yaweze kufanyika kwa haraka kupitia  simu zao badala ya utaratibu wa kuwapelekea fedha mkononi ambao sio salama.

Wakulima hao wameshukuru mfumo huo kwanza wanapata pesa zaidi  kuliko mwanzo, pili kutumika kwa vipimo vya uhakika na tatu pia kuimarishwa kwa vyama vya ushirika ambapo wamemuomba Rais Magufuli mazao mengine ya mpunga na alizeti yaingizwe kwenye mfumo kwani wananyonywa sana kipindi hichi cha mavuno.