Matokeo chanyA+ online




Saturday, March 27, 2021

RAIS SAMIA AWANGOZA WATANZANIA KATIKA MAZISHI YA HAYATI RAIS MAGUFULI






 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akilihutubia Taifa Mara Baada ya kumalizika Misa Maalum kwa ajili ya aliyekuwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanyika March 26,2021 katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato wakati wa Maandalizi ya Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Familia Kijijini kwake Chato Kilimani Mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mama Janeth Magufuli Mjane wa  aliyekuwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika leo March 26,2021 katika Makaburi ya Familia Kijijini kwake Chato Kilimani Mkoani Geita


 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitia Udongo kwenye Kaburi wakati wa Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli yaliyofanyika leo March 26,2021 katika Makaburi ya Familia Kijijini kwake Chato Kilimani Mkoani Geita.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika  March 26,2021 katika Makaburi ya Familia Kijijini kwake Chato Kilimani Mkoani Geita.


 

MATUKIO: VIONGOZI MBALIMBALI WAKIWEKA MASHADA YA MAUA KWENYE KABURI LA HAYATI JPM























Wednesday, March 17, 2021

KAMPUNI MBILI KUTEKELEZA REA III, MZUNGUKO WA PILI, TABORA

 Zuena Msuya, Tabora

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezitambulisha kampuni mbili zitakazohusika na usambazaji umeme vijijini mkoani Tabora kupitia mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, utakaotekelezwa Kipindi cha miezi 18, kuanzia Sasa.

Dkt.Kalemani amezitambulisha kampuni hizo wakati wa ziara ya kukagua baadhi ya vijiji vya mkoa huo ambavyo bado havijafikiwa na Umeme vikiwemo Miyenze na Kanyenye wilayani Uyui, pamoja na Kijiji cha Kaselya wilayani Nzega Mkoani Tabora, iliyofanyika Machi 16, 2021.

Katika ziara hiyo Dkt. Kalemani aliambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, pamoja na viongozi wakuu waandamizi wa Wizara.

Pamoja na mambo mengine, Dkt.Kalemani aliwataka wakandarasi hao kufanya kazi usiku na mchana kwa kasi, ubunifu na Usahihi ili kukamilisha mradi huo ndani ya muda uliopangwa ama hata kabla ya muda huo.

Aliwasitiza wakandarasi hao kutumia vijana walio katika eneo la mradi kufanya kazi zisizohitaji taaluma maalum kama vile kuchimba mashimo, kuvuta nyaya na nyingine kama hizo ili kunufaika na uwepo wa mradi huo.

Zaidi ya shilingi Bilioni 108.2 zitatumika kutekeleza mradi wa usambazaji wa Umeme katika vijiji 299 vilivyosalia katika mkoa huo wenye jumla ya vijiji 725. 

Tayari vijiji 426 vimepata umeme katika wilaya zote za mkoa huo wenye wilaya Saba.

Wilaya hizo ni Tabora Mjini, Kaliua, Uyui, Nzega, Urambo, Sikonge na Igunga.

Kampuni zilizopata dhamana ya kutekeleza mradi huo mkoani humo ni Kampuni ya kizalendo ya Sillo pamoja na Kampuni ya kigeni ya Ceylex kutoka nchini Sri-lanka.

Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, alitilia mkazo maelekezo yaliyotolewa kwa wakandarasi hao na kuwaeleza kuwa, Serikali imewaamini na kuwapa dhamana kubwa kutekeleza mradi huo hivyo wakamilishe kazi hiyo kama mkataba unavyoelekeza.

Wakili Byabato alisema kuwa, wakandarasi hao wakikamilisha kwa wakati mradi huo kwa kumaliza kuunganisha vijiji vyote vilivyosalia, Tanzania itaandika historia mpya kwa bara la Afrika, licha ya kuwa ya kwanza kwa kuunganisha umeme kwenye vijiji vingi kwa nchi za Afrika.

Wakandarasi kutoka Kampuni ya kizalendo ya Sillo iliyopewa dhamana ya kutekeleza Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili, wakimsikiliza wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kutambulisha wakandarasi watakaotekeleza mradi huo, mkoani Tabora, iliyofanyika Machi 16, 2021.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kaselya( hawapo pichani) wilayani Nzega, wakati wa ziara ya kutambulisha wakandarasi watakaotekeleza Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu, mzunguko wa Pili mkoani Tabora, iliyofanyika Machi 16, 2021.

Wakazi wa Kijiji cha Kaselya wilayani Nzega, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kutambulisha wakandarasi watakaotekeleza Mradi wa Usambazaji wa Umeme vijijini Awamu ya Tatu, mzunguko wa Pili mkoani Tabora, iliyofanyika Machi 16, 2021.

WIZARA YA KILIMO YAWEKA MKAKATI KUONGEZA USHINDANI SOKO LA DUNIA

Waziri wa Kilimo Prof. adolf Mkenda akizindua mfumo wa kilimo ujulikanao “Kizimba Business Model ” unalenga kuwaunganisha vijana kufanya kilimo biashara chini ya taasisi ya SUGECO leo mjini Morogoro.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO Bw.Revocatus Kimario.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Sokoine Prof. Raphael Chibunda akizungumza kwenye uzinduzi wa Kizimba Business Model leo Morogoro amesema mfumo huo chini ya SUGECO unalenga kusukuma na kubadili kilimo kuwa cha kibiashara na kuvutia vijana wengi zaidi kushiriki.
Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akisalimiana na Makamu  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda (kulia) leo wakati alipozindua mfumo wa Kizimba Business Model unaolenga kuwaunganisha vijana kufanya kilimo biashara chini ya taasisi ya SUGECO.

Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda akitazama bidhaa inayotengezwa na mjasiliamali Fatma Mbaga (kushoto) chini ya usimamizi wa SUGECO ikiwa ni mkakati wa kukuza biashara ya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji SUGECO Revocatus Kimario.

 

Na Farida Saidy, Morogoro.

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali kupitia Wizara ya Kilimo itaendelea kushirikiana na wadau wa kilimo ili kuhakikisha kunakuwa na mageuzi mapya katika sekta ya Kilimo kwa kufanya utafiti wa mbegu bora za Kilimo ili kuleta tija katika Kilimo kwa ajili ya kuongeza ushindani katika soko la dunia

Waziri wa Wilimo Prof Mkenda alisema hayo katika ziara yake mkoani morogoro wakati wa kuzindua mkakati mpya wa kilimo  kwa utaratibu wa kizimba ulioandaliwa na sokoine university graduate entrepreneurs cooperative [SUGECO] tukio ambalo limewashirikisha wadau mbalimbali wenye nia ya kuleta mageuzi kwenye kilimo

Alisema kuwa kilimo kinachangia chini ya theluthi moja ya pato la Taifa licha ya wakulima kukumbana na changamoto kwenye kilimo hivyo wakulima wanahitaji fedha kwa ajili ya kuinua hali zao za maisha katika kuleta mageuzi ya kilimo

Alisema kuwa suala la kuongeza tija katika kilimo litasaidia kuongeza pato la wakulima na Taifa kwa ujumla, kuna haja ya kuongeza tija kwenye kilimo ili kuwa na ushindani duniani pamoja na kusimamamia mauzo ya mazao ili kuongeza faida kwa wakulima

“Bila mbegu nzuri huwezi kuzalisha vizuri, tunahitaji matumizi bora ya pembejeo na teknolojia ikiwa ni pamoja na umwagiliaji na namna ya kuwafikia watu tunahitaji mfumo huu wa kizimba tuliozindua leo kuharakisha namna ya kwenda haraka kuwafikia wakulima na kuleta matokeo chanya ambayo itasambaa kwa watu na kuchukua kama mfano” alisema prof mkenda 

Alisema kuwa mkakati wa kizimba ulipaswa kuanza mapema zaidi ili kusonga mbele katika maendeleo ya kilimo, hivyo amesema kuwa vijana wanapaswa kupewa kipaumbele katika uzalishaji wa mazao endapo kama watawezeshwa kupata ardhi pamoja na mitaji

Katika mpango mpya wa kizimba wanapaswa kupeana uzoefu na ushirikiano wa kutosha ili kuzalisha zaidi ambapo wananchi wanahitaji fedha katika kukuza uzalishaji huku akiwaomba wadau wa bank kutoa mikopo kuwezesha wakulima kuzalisha mazao na kutengeneza kwa wakulima wanapozalisha mazao yao na uhakika wa kupata masoko

Alisema kuwa sekta ya kilimo ni miongoni mwa sekta zinazoajiri watu wengi zaidi ni muhimu kupewa kipaumbele kutumika kama nguvu kazi ya taifa huku akieleza changamoto kubwa inayokwamisha vijana ikiwa ni kukosa mitaji pamoja na ardhi kwa ajili ya uzalishaji wa mazao

Aidha prof mkenda alisema kuwa katika maeneo ya vijini hasa katika maeneo yenye changamoto ya hali ya hela na uhaba wa mvua, inaonesha hali halisi ya maisha ya wakulima hivyo utaratibu wa vizimba utasaidia kuongeza tija katika kilimo

Wakati huohuo ametoa wito kwa Halmashauri zote hapa nchini wasaidie namna ya kusogeza kilimo kwa kuwa wakulima wengi wanalima bila kuwa na uhakika wa masoko na kuuza mazao yao hivyo wajenge mazingira ya kutengeza hela ili kupata faida

“Nawapongeza halmashauri ya nzega kutoka hekta 40, kibiti hekta 1000, mvomero hekta 1500,na halmashauri ya liwale wametoa hekta 300 huu ni uthubutu wa pekee sana kuongeza tija kupitia ardhi hii” alisema prof mkenda

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya SUGECO Dkt Anna Temu amewapongeza SUGECO  kubuni mbinu ya kukuza kilimo na kuwaomba waishi katika jamii ya wakulima na wafugaji ili kujikita na mbinu za kuondoa umaskini ambayo ndio kipaumbele cha sugeco katika mkakati wao kubuni mpango huo

Nao wanufaika wa SUGECO Bwana Yohana Itayo na Fedrick Jonathan wameiomba serikali kupanua wigo kusaidia vijana ili kupata ujuzi kwa vitendo kushirikiana na wakulima wenye uzoefu hivyo wameshauri vijana wanaomaliza vyuo wapelekwe kupata uzoefu wa kuanzisha mashamba yao wenye

joseph Masimba ni Afisa Meneja uendeshaji wa SUGECO amesema kuwa kizimba ni mfumo wa kuzalisha kwa pamoja ambao unaziweka rasilimali zote kwa pamoja kujumuisha mabank, wadau wa maendeleo kilimo lengo ikiwa ni kushughulikia changamoto zinazoikumba sekta ya kilimo hasa tatizo la tija, vijana kukosa ardhi na mitaji katika uzalishaji mazao ya kilimo

WAZIRI NDALICHAKO AKIPONGEZA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA KWA KUKARABATI MAJENGO YA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kwa kusimamia vizuri ukarabati wa majengo ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Msinga (FDC) kilichopo Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro.


Waziri Ndalichako ametoa pongezi hizo mara baada ya kukagua ukarabati wa majengo katika Chuo hicho ambapo amesema ameridhishwa na ubora kazi iliyofanyika na kuwataka wanafunzi kusoma kwa bidii kwa kuwa Serikali yao inawajali na imeboresha mazingira ya kujifunzia.


Amesema Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Msinga ni moja kati ya Vyuo 54 vilivyofanyiwa ukarabati kupitia Mradi wa Mukuza Ujuzi na Stadi za Kazi unaosimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.


Akizungumzia masuala ya nidhamu kwa wanafunzi, Waziri Ndalichako amewataka walimu pamoja na kufundisha masomo ya darasani  kuhakikisha  mafunzo juu ya uraia na uzalendo yanakuwa endelevu ili kuwa na vijana wenye nidhamu na  wazalendo  wanaothamini tunu zilizoachwa na waasisi wa nchi hii.  

 

“Hii kazi nzuri ambayo tumeifanya hapa muienzi na vifaa ambavyo mmeomba  naahidi kuwa nitavifanyia kazi, itakuwa  haina maana yoyote kama ninyi mtakuwa hamna uzalendo kwa sababu vifaa vinaweza vikaja na mkaviaharibu ni lazima vijana mlinde rasilimali za nchi yenu,”alisema Waziri Ndalichako.


Amewapongeza wanafunzi wa fani ya uashi katika Chuo hicho kwa kujenga jengo la  mlinzi na kusistiza kuwa hayo ndio mafunzo yanayotakiwa kwa kuwa vijana wanamaliza wakiwa na ujuzi.


“Mafunzo na mitaala yetu ni mizuri lakini wakati mwingine vijana mnakuwa hamzingatii na kufuatilia kwa ukaribu masomo, kwa hiyo walimu niwasii kama ambavyo nimeona kazi nzuri mmeifanya muendelee kuwafundisha vijana wetu na msisahau kuwajengea maadili mema kwa ajili ya taifa letu,”amesisitiza  Waziri Ndalichako


Waziri Ndalichako ameahidi kufanyia kazi changamoto za baadhi ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi ili wanafunzi waweze kusoma vizuri.


Nae Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Msinga Miriam Msomvu amesema ukarabati uliofanyika umetumia zaidi ya Sh milioni 560 na kwamba umewezesha kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 130 mwaka 2019 kufikia wanafunzi 312 mwaka 2021.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Msinga wameishukuru Serikali kwa kufanya ukarabati mkubwa katika Chuo chao na kumuaomba Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kuwaondolea changamoto ya upungufu wa baadhi ya vifaa vya kujifunzia.

Muonekano wa moja ya majengo ya Chuo cha Maendeleo wananchi Msinga kilichopo wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro baada ya ukarabati.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na  wanafunzi   wa  Chuo cha Maendeleo ya wananchi Msinga kilichopo wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani kilimanjaro mara baada ya kukagua ukarabati uliofanyika chuoni hapo .
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiangalia wanafunzi wa fani ya Uashi   katika Chuo cha Maendeleo ya wananchi Msinga  kilichopo wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani kilimanjaro wakijifunza kwa vitendo.

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiangalia moja ya barakoa iliyoshonwa na wanafunzi katika Chuo cha Maendeleo ya wananchi Msinga kilichopo wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani kilimanjaro

KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI YATEMBELEA CHUO CHA MZUMBE, MOROGORO KUKAGUA UJENZI WA HOSTELI NA MADARASA

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (aliyetangulia mbele) wakikagua jengo jipya  la Madarasa ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro wakati walipotembelea Chuoni hapo leo Machi 16, 2021. PICHA NA BUNGE
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakikagua jengo jipya  la Hosteli Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro wakati walipotembelea Chuoni hapo leo Machi 16, 2021.
Makamu Mweyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro kukagua ujenzi wa Hosteli na Madarasa leo Machi 16, 2021.

 

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (katikati) akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro kukagua ujenzi wa Hosteli na Madarasa leo Machi 16, 2021. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof. Mathew Luhanga na kulia ni Makamu Mweyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Japhet Hasunga.

BILIONI 2.5 KUKAMILISHA UJENZI CHUO CHA VETA RUKWA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga akifafanua jambo alipotembelea kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mkoani Rukwa hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga (katikati) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Veta mkoani Rukwa. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Veta wa wizara hiyo, Margaret Mussai na Msimamaizi Mkuu wa Ujenzi wa chuo hicho, Jeremiah Longido.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga amesema Serikali imetenga jumla ya Shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) cha mkoa wa Rukwa.

Amesema utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya kwanza ulifadhiliwa kwa mkopo kutoka  benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na kujengwa na Mkandarasi ambapo mradi ulifikia asilimia 52.

Mhe Kipanga ameeleza kuwa kwa sasa  ujenzi utakamilishwa kwa fedha za Serikali kwa kutumia utaratibu wa force akaunti na unatarajia kukamilika ili kuwezesha kuanza udahili Mwezi Julai 2021.

"Napenda kuwatoa wasiwasi wana Rukwa kwani Serikali sasa imetenga Shilingi bilioni 2.5 za kukamilisha ujenzi wa chuo hiki na kwamba tunatarajia ndani ya muda mfupi fedha hizi zitalipwa ili ujenzi uweze kukamilika ifikapo Julai, 2020," amesema Kipanga.

Awali, akitoa taarifa ya mradi huo,  Msimamizi Mkuu wa mradi, Jeremiah Longido amesema awamu ya kwanza ya ujenzi ilianza mwaka 2018 na mpaka sasa umefikia asilimia 52 ambapo umegharimu jumla ya Shilingi bilioni 3.6.

Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Carolius Misungwi ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya kumaliza ujenzi wa chuo hicho na kuahidi ofisi yake kutoa ushirikiano katika  kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.