Matokeo chanyA+ online




Thursday, April 28, 2022

WAZIRI UMMY MWALIMU AMUAGA MWAKILISHI MKAZI WA WHO ALIYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI

 Na WAF - Dodoma.


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo ameagana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Tigest Ketsela Mengestu aliyemaliza muda wake kutumikia nafasi hiyo hapa nchini.

Dkt. Tigest ambaye amedumu katika nafasi hiyo kwa muda wa miaka minne hapa nchini ameagwa rasmi na Waziri Ummy Mwalimu pamoja na Menejimenti ya Wizara katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma.

Waziri Ummy ameishukuru WHO kwa kuendelea kuwa karibu na Serikali na kutoa ushauri wa kitaalam, maoni na msaada kwenye masuala mbalimbali ya kupambana na magonjwa ambukizi na yasiyoambukiza.

"Mchango wa WHO katika kipindi chako hapa nchini unaonekana wazi, mmeweza kutusaidia Serikali kuboresha sekta ya afya na utekelezaji wa afua mbali mbalimbali za mapambano dhidi ya magonjwa" amesifu Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi na WHO pamoja na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi kuhakikisha kuwa inaboresha mifumo ya afya na Sekta ya afya kwa ujumla ili kujengea uwezo nchi na wataalam wetu kutambua na kudhibiti magonjwa

Kwa upande wake Dkt. Tigest ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Afya nchini na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mashirika ya kimataifa ikiwemo WHO kufanya kazi nchini.

"Ninashukuru sana kwa ushirikiano wenu mliotoa kwangu na kwa WHO, Mwenyezi Mungu awabariki wote na nashukuru sana kunipa nafasi ya kufanya kazi na Tanzania" ameshukuru Dkt. Tigest.







MAMLAKA YA MJI WA BUSAN KUISADIA TANZANIA KUENDELEZA UCHUMI WA BLUU

 Mamlaka ya mji wa Busan imeonesha utayari wa kuisadia Tanzania katika kuendeleza uchumi wa buluu na uvuvi.


Haya yamejili wakati wa mazumgumzo yaliyofanyika baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mstahiki Meya Mhe. Park Heong Joon alipomtembelea ofisini kwake katika Mji wa Busan, Jamhuri ya Korea.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Park ameeleza kuwa mamlaka ya Mji wake imekuwa ikifuatilia kwa ukaribu juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza uchumi wa buluu na uvuvi na hivyo wameona ni wakati muafaka kwao wa kushirikiana na kuisaidia Serikali katika kuendeleza sekta hiyo. Mhe. Park aliainisha baadhi ya maeneo ambayo wanakusudia kusaidia ili kuiinua sekta hiyo ikiwemo kutoa nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wadau na wataalam wa sekta ya uchumi wa buluu na vifaa vya kisasa vya uvuvi.

“Kwa muda mrefu tumekuwa tukifuatilia na kuvutiwa na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza sekta ya uchumi wa bluu na uvuvi, tupotayari kutoa mchango wetu katika kuendeleza sekta hii muhimu kwa maendeleo ya wananchi na Serikali ya Tanzania” alisema Mstahiki Meya Mheshimiwa Park.

Kwa upande wake Waziri Mulamula alieleza kuwa Serikali ya Tanzania inatambua mafanikio makubwa ambayo Mamlaka ya mji wa Busan imeyapata kutokana na jitihada zao za kuendeleza sekta ya uchumi wa bluu, hivyo imekuwa ni nafasi hadhimu kwa Tanzania kupata fursa ya kushirikiana na kusaidiwa na mamlaka ya mji huo katika kundeleza uchumi wa buluu na uvuvi.

“Kwa miaka 30 sasa tumeendelea kufurahia na kunufaika na matunda ya uhusiano mzuri wa kidiplomasia, leo hii ninayofuraha kubwa kuona uhusiano huu unafungua mlango mwingine mpya wa ushirikiano ambao utaleta manufaa makuwa kwa wananchi na Serikali yetu, nafurahi zaidi kuona hili linafanyika baina yetu na mamlaka ya Mji wa Busia ambao umepiga hatua kubwa katika sekta hii, kitu ambacho kinanipa matumaini kuwa tukitumia vyema uzoefu na maarifa tutakayopata kutoka kwenu tutapiga hatua kubwa ya maendeleo ndani ya muda mfupi” alieleza Balozi Mulamula.

Sambamba na hayo Mstahiki Meya alieleza nia yake kushirikiana na Tanzania katika maeneo mengine mbalimbali ya kiuchumi na kijamii. Miongoni mwa vitu alivyovitaja katika maeneo hayo ni pamoja na kununua zao la kahawa ya Tanzania, kuanzisha ushirikiano na urafiki na mji mojawapo wa Tanzania, kuhimiza makampuni na wafanyabiashara wa Mji wake kuwekeza Tanzania na ushirikiano katika Utamaduni na Sanaa.

Wakati huohuo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa mji wa Busan, Korea.

Mazungumzo hayo yamefanyika sambamba na kongamano la biashara lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania kwa kushirikiana na mamlaka ya Mji huo. Kongamano hilo lililenga kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji na vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa wafanyabiasha hao.

Akizungumza na wafanyabiashara hao Waziri Mulamula amewashawishi kuja nchini kuwekeza kwenye fursa zinazotokana na uchumi wa buluu, ambapo amewaeleza kuwa Tanzania ni sehemu salama kwa uwekezaji wao, vilevile, utashi na utayari wa kisiasa katika masuala ya uwekezaji kwa sasa umekuwa wa hali ya juu kuliko wakati mwingine wowote. Aliongeza kusema Serikali imefanya maboresho muhimu ya sera, sheria na kanuni za uwekezaji.

“Tanzania tupo tayari na tunashauku kubwa ya kufanyakazi na sekta binafsi ya Busan katika kuendeleza sekta yetu ya uchumi wa buluu ambayo bado ipo chini kimaendeleo” Waziri Mulamula.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao wameonesha kuvutiwa na fursa walizoelezwa kupatikana katika sekta ya uchumi wa buluu na wameeleza nia na utayari wao wa kuwekeza katika sekta hiyo hapa nchini.

Katika tukio jingine Waziri Mulamula amekutana na kufanyamazungumzo na Mwenyekiti na Rais wa Eximbank ya Korea Bw. Moon Kyu, Bang katika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Seoul, Korea.

Waziri Mulamula yupo nchini Korea kwa ziara ya siku tano (5) kufuatia mwaliliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wanchi hiyo Mhe. Chung Eui-yong, ambapo pia atashiriki hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea itayofanyika jijini Seoul tarehe 29 Aprili 2022. Tanzania na Korea zilianzisha uhusiano wa Kidiplomasia Aprili 29,1992.




RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA FILAMU YA TANZANIA THE ROYAL TOUR

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vyakula pamoja na mafuta kwa vituo mbalimbali 27 vya Watoto hao tarehe 28, Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akitoa misaada ya Vyakula mbalimbali pamoja na mafuta kwa vikundi 27 vya Watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi Mkoani Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwandishi wa Habari Maarufu wa Marekani ambaye ndiye mtayarishaji wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour Peter Greenberg mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa Filamu hiyo tarehe 28, Aprili, 2022.


Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.

 








Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.



Sunday, April 24, 2022

MAMA MARIA NYERERE NA MAMA JANETH MAGUFULI WASHIRIKI MISA MAALUMU YA KUADHIMISHA MIAKA 100 YA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE KANISA LA ST. PETERS JIJINI DAR




Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere akiwa na Mama Janeth Magufuli Mjane wa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli  na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Jenista Mhagama wakishiriki katika Misa Maalumu ya kuadhimisha Miaka 100 ya Kuzaliwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam Jumamosi Aprili 23, 2022

 

RAIS MWINYI ASHIRIKI KUMBUKIZI YA MIAKA 100 KUZALIWA MWALIMU NYERERE

 

Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassimu Majaliwa mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya nyumba ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Msasani  Aprili 23,2022 Jijini Dar es Salaam katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere ambapo Rais Mwinyi alikuwa Mgeni rasmi.


Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwasili kwenye viwanja vya nyumba ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Msasani  Aprili 23,2022 Jijini Dar es Salaam katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere ambapo Rais Mwinyi alikuwa Mgeni rasmi.Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa pamoja na mkewe wakitazama baadhi ya picha za Hayati Mwalimu Nyerere kwenye viwanja vya nyumba ya Mwalimu Nyerere Msasani  Aprili 23,2022 Jijini Dar es Salaam katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere ambapo Rais Mwinyi alikuwa Mgeni rasmi.


Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika viwanja vya Hayati Mwalimu Nyerere, Msasani  Aprili 23,2022 Jijini Dar es Salaam.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassimu Majaliwa akizungumza katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika viwanja vya Hayati Mwalimu Nyerere, Msasani  Aprili 23,2022 Jijini Dar es SalaamMakamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akizungumza katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika viwanja vya Hayati Mwalimu Nyerere, Msasani  Aprili 23,2022 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika viwanja vya Hayati Mwalimu Nyerere, Msasani  Aprili 23,2022 Jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Amos Makalla akizungumza katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika viwanja vya Hayati Mwalimu Nyerere, Msasani Aprili 23,2022 Jijini Dar es SalaamWaziri Mkuu Mstaafu Jaji Mstaafu Joseph Warioba akizungumza katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika viwanja vya Hayati Mwalimu Nyerere, Msasani  Aprili 23,2022 Jijini Dar es SalaamMeza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi wakipata picha ya pamoja na watoto na wajukuu wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa kwake Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika viwanja vya Hayati Mwalimu Nyerere, Msasani  Aprili 23,2022 Jijini Dar es SalaamMeza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi wakipata picha ya pamoja na wake wa viongozi wastaafu katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa kwake Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika viwanja vya Hayati Mwalimu Nyerere, Msasani  Aprili 23,2022 Jijini Dar es Salaam.Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi wakipata picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa kwake Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika viwanja vya Hayati Mwalimu Nyerere, Msasani  Aprili 23,2022 Jijini Dar es SalaamMeza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi wakipata picha ya pamoja na viongozi wa Dini katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya Kuzaliwa kwake Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika viwanja vya Hayati Mwalimu Nyerere, Msasani  Aprili 23,2022 Jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE KWA HISANI YA EMMANUEL MBATILO)

RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA WATANZANA WANAOISHI NCHINI MAREKANI JIJINI WASHINGTON DC


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Watanzania wanaoishi Nchini Marekani Jijini Washington DC.