Matokeo chanyA+ online




Thursday, April 27, 2023

WATANZANIA WALIOKWAMA SUDAN WAREJEA NCHINI SALAMA






Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akisalimiana na mmoja wa Watanzania waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan ambako kuna mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Jeshi la Sudan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF). Mtanzania huyo amepata changamoto za kiafya kwa kupata mshituko kufuatia matukio ya mapigano hayo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiongea na Marubani waliorusha ndege ilyowabeba Watanzania waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Jeshi la Sudan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF)


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Sudan, Mhe. Silima Kombo Haji baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kutoka Sudan ambako kuna mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Jeshi la Sudan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) wa pili kulia; Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo (kulia); Balozi wa Tanzania nchini Sudan, Mhe. Silima Kombo Haji na Mkurugenzi wa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kuwapokea Watanzania waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan ambako kuna mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Jeshi la Sudan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF).

Watanzania waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan ambako kuna mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Jeshi la Sudan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF) wakiwa wanakamilisha taratibu za uhamiaji ili waweze kukutana na familia zao zilizokuwa zinawasubiri uwanjani hapo

Watanzania waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan ambako kuna mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Jeshi la Sudan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF) wakiwa wanakamilisha taratibu za uhamiaji ili waweze kukutana na familia zao zilizokuwa zinawasubiri uwanjani hapo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiongea na baadhi ya wazazi waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuwapokea vijana wao waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiongea na vyombo vya habari vilivyofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kushuhudia tukio la kuwapokea Watanzania waliorejeshwa na Serikali kutoka Sudan.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiongea na familia zilizofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuwapokea wapendwa wao walirejeshwa na Serikali kutoka Sudan. 







 

Wednesday, April 26, 2023

Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mkazi wa Nyakanazi Mkoani Kagera, mwenye matatizo ya ngozi

.





Mtoto huyo alifika Ikulu kwa ajili ya kumshukuru Rais Samia kwa msaada wa matibabu aliompatia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. Rais alimuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza wakati wa ziara yake Nyakanazi Mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2022 na kuagiza apatiwe matibabu baada ya kuhangaika kwa muda mrefu.

Tuesday, April 25, 2023

KLINIKI YA AGA KHAN, MKOA WA MJINI MAGHARIBI.



Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi amesema Shirika la maaendeleo la Aga Khan (AKDN) limekuwa likijitahidi kuimarisha afya na ustawi wa jamii ulimwenguni kote pamoja na Zanzibar. Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 25 Aprili 2023 katika uzinduzi wa kituo cha afya cha Kliniki cha Aga Khan ambacho kitatoa huduma za dharura, huduma za kibingwa pia wagonjwa watapata huduma za afya zilizounganishwa dijitali na Hospitali ya Aga Khan iliyopo Dar es Salaam. Serikali ya Zanzibar inatambua umuhimu wa huduma bora za afya hivyo sekta hiyo imepata mageuzi makubwa ambayo yanajumuisha huduma za afya kwa ngazi ya shehia, wilaya hadi mkoa kupitia Hospitali za rufaa ikiwa na jumla ya vituo vya afya 172 ambavyo vipo katika wilaya 11 Zanzibar. Naye Binti Mfalme Zahra Aga Khan alisema uwekezaji kupitia Shirika la maendeleo la Aga Khan kupitia miundombinu ya huduma za afya ya Zanzibar inaonyesha dhamira yake ya kuendelea kuboresha afya na ustawi wa jamii ulimwenguni kote.

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Balozi wa Muungano wa Umoja wa Falme za Kiarabu Nchini Tanzania (UAE), Ikulu Ndogo Tunguu Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa (UAE) Nchini Tanzania Mhe. Khalifa Abdulrahman Almarzouqi alipofika Ikulu Ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 25 Aprili 2023. 

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Muungano wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Zayed Al Nahyan uliowasilishwa na Balozi wa (UAE) Nchini Tanzania Mhe. Khalifa Abdulrahman Almarzouqi Ikulu Ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 25 Aprili 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na  Balozi wa (UAE) Nchini Tanzania Mhe. Khalifa Abdulrahman Almarzouqi mara baada ya kukabidhi Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Muungano wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Zayed Al Nahyan Ikulu Ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 25 April 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa (UAE) Nchini Tanzania Mhe. Khalifa Abdulrahman Almarzouqi alipofika Ikulu Ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 25 April 2023. 

 

 


 

Saturday, April 22, 2023

NASAHA ZA MUFTI WA TANZANIA, SHEIKH ABUBAKAR ZUBEIR KWA WATANZANIA KATIK...

RAIS SAMIA AHUTUBIA BARAZA LA EID EL-FITR KITAIFA LILILOFANYIKA JNICC JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu kwenye Baraza la Eid El-Fitr ambalo Kitaifa limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Aprili, 2023.
Mwenyekiti wa Chadema Mhe Freeman Mbowe akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakimsikiliza Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Baraza la Eid El-Fitr ambalo Kitaifa limefanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Aprili, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt. Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria Baraza la Eid El-Fitr tarehe 22 Aprili, 2023. Wengine katika picha ni Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Omar pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Mama Shamim Khan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kwenye Baraza la Eid El-Fitr ambalo Kitaifa limefanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Aprili, 2023.







 

Tuesday, April 18, 2023

JK AKUTANA NA WANARIADHA GABRIEL GEAY NA WENCE TARIMO MJINI BOSTON, MAREKANI

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wanariadha Gabriel Geay (kushoto kwake) na Wence Tarimo (kulia kwake) ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi - wa Zanzibar na kushoto ni mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo.


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya jezi toka kwa mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo wakati alipoonana na wanariadha Gabriel Geay (kushoto kwake) na Wence Tarimo (kulia kwake) ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi - wa Zanzibar.



Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha mwanariadha Gabriel Geay mjini Boston Marekani, siku moja baada ya shujaa huyo kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon.


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kitabu mwanariadha Gabriel Geay mjini Boston Marekani, siku moja baada ya shujaa huyo kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon.



Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wanariadha Gabriel Geay (kushoto kwake) na Wence Tarimo (kulia kwake) ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi - wa Zanzibar.


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  na Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi - wa Zanzibar wakiwa na Watanzania waishio Marekani pamoja na wanariadha Gabriel Geay  na Wence Tarimo ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo na kushoto ni mtoto wa Bongo Zozo.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo aliyeongozana na  mwanariadha Gabriel Geay alipokutana nao mjini Boston Marekani, siku moja baada ya shujaa huyo kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon.





 

KAMATI KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA DIPLOMASIA YA UCHUMI YAANZA KAZI RASMI

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Kamati ya Kutathmini Utendaji wa Wizara alipokutana nayo jijini Dodoma tarehe 18 Aprili 2023 kama ishara ya kuanza rasmi kwa kazi ya Kamati hiyo. Kamati hiyo ambayo iliundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 28 Machi, 2023 inao wajumbe saba (7) na inaongozwa na Balozi Msatafu, Mhe. Hassan Simba Yahya (wa kwanza kushoto)
Kikao na Kamati kikiendelea
Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathmini utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianio wa Afrika Mashariki, Balozi Mstaafu, Mhe. Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa kikao kati ya Kamati hiyo na Mhe. Dkt. Tax
Mjumbe wa Kamati, Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar akiwa kwenye Kikao kati ya Kamati hiyo na Mhe. Dkt. Tax. Kushoto ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati hiyo
Wajumbe wengine wa Kamati ambao ni Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (kulia) na Balozi Peter Kalaghe wakati wa kikao kati ya kamati hiyo na Mhe. Dkt. Tax

Mjumbe wa Kamati, Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka (kulia) akiwa na Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati (kushoto)
Wajumbe wengine wa Kamati ambao ni Balozi Tuvako Manongi (kushoto) na Mhe. Balozi George Madafa wakati wa kikao kati ya Kamati na Mhe. Waziri Tax
Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati wakifuatilia kikao

Kikao kikiendelea

Mhe. Dkt. Tax (katikati mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja  na Mwenyekiti wa Kamati Kutathmini utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Simba (wa pili kushoto mstari wa kwanza) pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo

Mhe. Dkt. Tax (katikati mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja  na Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathmini utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Simba (wa pili kushoto mstari wa kwanza), Wajumbe wa Kamati pamoja na Sekretarieti ya Kamati hiyo