Matokeo chanyA+ online




Friday, February 28, 2020

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MSIKITI WA BAKWATA KINONDONI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akisindikizwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamiz wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa 28, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki katika dua na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) alipofanya ziara ya kustukiza
kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa 28, 2020
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Februari, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti mkubwa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Msikiti huo unajengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco baada ya kuombwa na Mhe. Rais Magufuli alipofanya ziara rasmi hapa nchini Oktoba 2016.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) akitembezwa kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa 28, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea machache na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamiz wa Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA) baada ya kufanya ziara ya kustukiza kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo
Ijumaa 28, 2020

Akiongozwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally, Mhe. Rais Magufuli amejionea kazi za ukamilishaji wa jengo jipya la Msikiti na jengo la ofisi ya Taasisi ya Mfalme Mohammed VI wa Morocco zikiendelea kukamilishwa, na ameelezea kufurahishwa kwake na ubora na uzuri wa Msikiti huo.
Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mfalme Mohammed VI wa Morocco kwa kutekeleza ombi alilomuomba la kuwajengea Waislamu Msikiti mkubwa kuliko yote hapa nchini, na amempongeza Mufti wa Tanzania na Waislamu wote kwa kujengewa nyumba nzuri ya Ibada.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) akitembezwa kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa 28, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) akitembezwa kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa 28, 2020

Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwajali Waislamu na kuwaombea msaada wa kujengewa Msikiti huo ambao ujenzi wake umefikia asilimia 97.
Akiwa na viongozi wenzake wa BAKWATA, Sheikh Mkuu Aboubakar Zubeir bin Ally ameongoza Dua ya kumuombea Mhe. Rais Magufuli na kuliombea Taifa ili Mwenyezi Mungu aiepushe Tanzania dhidi ya maradhi ya homa ya virusi vya corona, kudumisha amani na utulivu na kuombea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu ufanyike vizuri na kwa amani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) akitembezwa kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa 28, 2020


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akisindikizwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamiz wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa 28, 2020

MASENETA KUTOKA UFARANSA KUFANYA ZIARA NCHINI


Ujumbe wa maseneta sita (6) kutoka Ufaransa unatarajiwa kufanya ziara nchini kuanzia tarehe 01 hadi 08 Machi, 2020.  

Ujumbe huo utawasili nchini tarehe 29 Februari, 2020 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar utaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Ufaransa inayoshughulikia masuala ya Maendeleo Endelevu na Naibu Rais wa Kikundi cha Kirafiki na nchi za Bahari ya Hindi Seneta Harve Maurey.


SERIKALI YADHAMIRIA KUPELEKA UMEME WA GRIDI MKOA WOTE WA KAGERA

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (aliyeinua mkono), akitoa maelekezo mbalimbali kwa uongozi wa TANESCO, yanayohusu kuboresha huduma ya upatikanaji umeme kwa wananchi, alipotembelea Kituo cha kupoza umeme Kyaka, kilichopo wilayani Misenyi, Mkoa wa Kagera, Februari 27 mwaka huu. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali Dennis Mwila.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amesema Serikali imedhamiria kupeleka umeme wa gridi ya Taifa katika Mkoa wote wa Kagera, awamu kwa awamu ikianza na Wilaya za Bukoba Vijijini, Muleba na Misenyi.

Amesema Wilaya hizo za awali zitaungwa kwenye gridi ya Taifa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kutoka sasa.

Waziri ameeleza hayo Februari 27 mwaka huu wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Generali Marco Gaguti, akiwa katika ziara ya kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Generali Marco Gaguti (kushoto), akimweleza jambo Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kulia). Waziri na Ujumbe wake walifika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kumweleza dhamira ya ziara yake mkoani humo, Februari 27 mwaka huu. 
“Wataalamu wetu kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wataanza kujenga njia ya kusafirisha umeme wa kilovoti 33 kutoka Kanazi mpaka Itako na kutoka Itako mpaka Misenyi,” amefafanua.

Akieleza zaidi, amesema maeneo hayo yataanza kutumia umeme wa gridi ya Taifa inayotoka Geita mpaka maeneo ya Ngara, Biharamulo na baadaye Misenyi.

Hata hivyo, Waziri amesema maeneo ambayo hayatafikiwa katika awamu ya kwanza kikiwemo kiwanda cha sukari cha Kagera na mengine yote yatakayosalia, yataendelea kutumia umeme kutoka nchi jirani ya Uganda wakati wakisubiri awamu nyingine ya utekelezaji wa mpango huo.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (aliyeinua mkono), akitoa maelekezo mbalimbali kwa uongozi wa TANESCO, yanayohusu kuboresha huduma ya upatikanaji umeme kwa wananchi, alipotembelea Kituo cha kupoza umeme Kyaka, kilichopo wilayani Misenyi, Mkoa wa Kagera, Februari 27 mwaka huu. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali Dennis Mwila. 

Akielezea kuhusu kuyaunga maeneo hayo yatakayosalia, Waziri amesema zoezi hilo litafanyika baada tu ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya umeme ya Kakono, Rusumo na Nyakanazi.

“Miradi hiyo ikikamilika, taratibu tutaweza kuwaondoa wale waliosalia kutoka kwenye gridi ya Taifa upande wa Uganda na kuwaunga kwenye gridi ya Taifa ya hapa nchini.”

Aidha, Waziri amebainisha kuwa, utekelezaji wa mpango huo ni sehemu ya mkakati wa serikali unaoendelea ukilenga kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo yote ya nchi yetu.
Akielezea kuhusu kuyaunga maeneo hayo yatakayosalia, Waziri amesema zoezi hilo litafanyika baada tu ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya umeme ya Kakono, Rusumo na Nyakanazi.

“Miradi hiyo ikikamilika, taratibu tutaweza kuwaondoa wale waliosalia kutoka kwenye gridi ya Taifa upande wa Uganda na kuwaunga kwenye gridi ya Taifa ya hapa nchini.”

Aidha, Waziri amebainisha kuwa, utekelezaji wa mpango huo ni sehemu ya mkakati wa serikali unaoendelea ukilenga kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo yote ya nchi yetu.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Ujumbe wake, wakikagua kituo cha kupoza umeme Kyaka, kilichopo wilayani Misenyi, Mkoa wa Kagera, alipokuwa katika ziara ya kazi Februari 27 mwaka huu.


Veronica Simba – Kagera  

Ameeleza zaidi kuwa, mbali ya kuimarisha hali ya upatikanji umeme nchini, serikali pia inapanga kuwa na umeme mwingi utakaotosheleza mahitaji ya ndani na kuuza ziada kwa nchi jirani za Ukanda wa Afrika Mashariki.

“Leo sisi tunanunua umeme kutoka kwa jirani zetu. Tunataka nasi tuwauzie umeme hapo baadaye. Uhakika wa kufanya hivyo tunao kutokana na miradi mikubwa tunayoitekeleza ukiwemo ule wa kuzalisha umeme (megawati 2,115) wa Julius Nyerere huko Rufiji.”

Kwa upande wake, Brigedia Gaguti amepongeza uamuzi huo wa serikali kuunganisha umeme wa gridi ya Taifa katika Mkoa wote wa Kagera na kuahidi kutoa ushirikiano kadri utakavyohitajika katika kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kikamilifu.

Katika ziara hiyo ya siku moja, Waziri na Ujumbe wake walitembelea maeneo mbalimbali ambayo yatahusika katika utekelezaji wa Mradi huo kikiwemo kituo cha kupoza umeme cha Kyaka kilichopo wilayani Misenyi.

MWL NYERERE MEMORIAL HOSPITAL KUANZA KUTOA HUDUMA KWA BAADHI YA SEHEMU KATI KATI YA MWEZI UJAO – NAIBU WAZIRI MABULA


Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa  iliyopo  Musoma mkoa wa Mara 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba la Tiafa (NHC) kuongeza kasi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa  iliyopo  Musoma mkoa wa Mara ili kukamilika kwa muda uliopangwa.
Hospitali hiyo ya Kwangwa ni ya ghorofa tano yenye shemu tatu (Wing A, B na C) na inarajiwa kuanza kutoa Huduma kwa baadhi ya sehemu kati kati ya mwezi ujao
Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana tarehe 25 Februari mjini Musoma mkoa wa Mara wakati wa ukaguzi wa  maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo unaofanywa na NHC  akiwa katika ziara yake ya siku moja.
Alisema, pamoja na NHC kufanya vizuri katika ujenzi wa jengo la hospitali hiyo ukilinganisha na wakandarasi waliotangulia lakini inapaswa kuongeza kasi ili likamilike katika muda uliopangwa na kuanza kutoa huduma.

Kwa mujibu wa Mabula, Hospitali ya Kwangwa itakayojulikana kwa jina la Mwl Nyerere Memorial Hospital ina historia ndefu kwa kuwa pamoja na kuasisiwa na Rais wa Kwanza Mwalimu Julius Nyerere lakini utekelezaji wake unakamilishwa na serikali ya awamu ya tano. ‘’Ni vyema NHC mkaongeza bidii katika ujenzi wa hospitali hii ili ikamilike kwa haraka kwa kuwa hospitali hii ina historia ndefu na Rais John Pombe Magufuli ameamua ujenzi huu ukamilike kwa kutoa bilioni 15’’ alisema Mabula.

 



Katika kuhakikisha ujenzi wa hospitali hiyo unakamilika kwa wakati, Naibu Waziri Mabula alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa NHC Dkt Maulid Banyani kusimamia kwa karibu maendeleo ya ujenzi huo sambamba na kupatiwa ratiba ya mpango wa ujenzi na maendeleo yake kila baada ya siku mbili kwa nia ya kufuatilia kwa karibu. 

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani alimuahakikishia Naibu Waziri Mabula kuwa, ujenzi wa hospitali hiyo sasa utakamilika kwa wakati baada ya changamoto kadhaa ikiwemo ya Mshauri Mwelekezi kupatiwa ufumbuzi. 

Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima mbali na kuisifu NHC kwa kufanya mabadiliko makubwa ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa hospitali ya Kwangwa alioueleza kuwa ilikwamwa kwa mara kadhaa. 

‘’Toka Shirika la Nyumba la Taifa lianze ujenzi wa hospitali hii mwezi Agosti mwaka jana kuna mabadiliko makubwa ya kasi ya ujenzi na tunataka mjenge kwa wakati na viwango na Machi mwaka huu Huduma ya Mama na Mtoto ianze kutolewa ‘’ alisema Malima. 

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, hospitali hiyo itatoa huduma kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya ziwa pamoja na nchi jirani sambamba na kutumika kama sehemu ya utalii kutokana na mazingira ya hospitali. 

Historia ya Ujenzi wa Hospitali ya Kwangwa iliyopo Musoma mkoa wa Mara inaanzia mwaka 1977 pale Rais wa kwanza wa Mwl Nyerere alipotoa wazo la kujengwa kwake lakini ujenzi huo umekuwa ukikwama kwa nyakati tofauti hadi Rais John Pombe Magufuli alipotoa Shilingi Bilioni 15 kwa lengo la kukamilishwa mradi huo ambapo sasa unatarajiwa kukamilika mwaka huu.

Thursday, February 27, 2020

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAPITIA RASIMU YA KANUNI ZA USAJILI WA WATAALAMU ELEKEZI WA MAZINGIRA

Wajumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Baraza la Taifa la Hifadhi ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na wataalamu elekezi wakiwa katika kikao cha kufanya mapitio ya Rasimu ya Kanuni za Usajili wa Wataalamu Elekezi wa Mazingira kilichofanyika ukumbi wa NHIF jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Donald Chidowu akiongoza Kikao cha Wadau cha kufanya mapitio ya Rasimu ya Kanuni za Usajili wa Wataalamu Elekezi wa Mazingira kilichofanyika ukumbi wa NHIF jijini Dodoma.

Sehemu ya Wajumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Baraza la Taifa la Hifadhi ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na wataalamu elekezi wakiwa katika kikao cha kufanya mapitio ya Rasimu ya Kanuni za Usajili wa Wataalamu Elekezi wa Mazingira kilichofanyika ukumbi wa NHIF jijini Dodoma.


WAFANYABIASHARA 1,950 WAPATIWA ELIMU YA KODI MKOANI IRINGA

Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwaelimisha wauzaji wa duka la vileo wa Mkoa wa Iringa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mkoani humo leo.

Jumla ya wafanyabiashara 1,950 wa Mkoa wa Iringa wamefikiwa na kupatiwa elimu ya kodi wakati wakampeni ya elimu kwa mlipakodi iliyofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 27 Februari,2020. 

Kampeni hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kuwafikia na kuwaelimisha baadhi ya wafanyabiashara wa Wilaya za Kilolo, Manispaa ya Iringa na Mufindi.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri David William (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati walipoingia wilayani humo kwa ajili ya kufanya kampeni ya elimu kwa mlipakodi. Wa nne kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Mhe. Mendrad Kigola na wa tatu kulia ni Meneja wa TRA Wilaya ya Mufindi Bw. Ernest Kagali.

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha kampeni hiyo mkoani humo, Afisa Msimamizi wa Kodi Mwandamizi wa TRA Bi. Catherine Mwakilagala amesema kuwa, zoezi hilo limekuwa na mafanikio makubwa kwani wamefanikiwa kuwaelimisha jumla ya walipakodi 1,950. 

“Mamlaka ya Mapato Tanzania tumehitimisha kampeni ya elimu kwa mlipakodi katika mkoa huu wa Iringa na zoezi hili limekuwa na mafanikio makubwa kwa sababu tumeweza kuwafikia jumla ya walipakodi 1,950 ambao wote tumewapatia elimu ya kodi na wamepata nafasi ya kutoa maoni na changamoto zao ambazo tumezipokea na nyingine tumezipatia ufumbuzi,” alisema Bi. Mwakilagala.
Afisa Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Chama Siriwa akifurahia jambo na mfanyabiashara wa Mkoa wa Iringa alipokuwa akimuelimisha kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mkoani humo leo.

Kwa upande wake Meneja wa TRA mkoani humo Bw. Lamson Tulyanje ametoa wito kwa wafanyabiashara wote waliotembelewa na maafisa wa TRA kwenye maduka yao na wale waliopata elimu kupitia semina wakati wa kampeni hiyo, kutumia elimu walioipata kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati na hiari.

“Elimu ambayo wameipata wafanyabishara mbalimbali kwenye kampeni hii ya elimu kwa mlipakodi, ni vizuri waitumie katika kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati ili Serikali iweze kutimiza majukumu yake ya kuwapatia huduma mbalimbali wananchi,” alieleza Bw. Tulyanje.
Afisa Msimamizi wa Kodi Mwandamizi Bi. Catherine Mwakilagala kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akitoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara wa Kijiji cha Igowelo kilichopo Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mkoani humo leo. 
Na Veronica Kazimoto
Bw. Richard Kilawa ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi kutoka Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoani humo ambaye ameishukuru TRA kwa kumfikishia elimu ya kodi dukani kwake na ameahidi kuendelea kulipa kodi kwa hiari.

“Ninashukuru sana TRA kunitembelea dukani kwangu na elimu yao imenifundisha kulipa kodi kwa hiari. Hivyo, nitawashawishi wafanyabiashara wenzangu walipe kodi kwa hiari ili tujenge nchi yetu,” alisema Bw. Kilawa.  


Naye, mfanyabiashara wa mbao wa Halmashauri hiyo, Bi. Maura Ng’umbi amesema kuwa, kupitia elimu iliyotolewa na maafisa wa TRA wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi, imewasaidia kujua umuhimu wa kulipa kodi stahiki kwa manufaa ya Taifa.

Kampeni ya elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mkoani Iringa ni mwendelezo wa kampeni zilizofanyika katika Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam kwa lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara kuhusu masuala mbalimbali ya kikodi, kupokea maoni na mapendekezo yao pamoja na kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi.