Matokeo chanyA+ online




Friday, July 29, 2022

UZINDUZI WA NALA KENYA

 Tarehe 21 Julai ilikuwa hatua nyingine muhimu katika safari ya NALA.

NARA imetangaza idhini waliyopewa na Benki Kuu ya Kenya kwa ushirikiano na Benki ya Equity, na kusherehekea ufunguzi wa ofisi yetu mpya jijini Nairobi. 

NARA inajenga Mapinduzi kwa ajili ya Afrika. Zaidi ya 80% ya pesa zinazotumwa Afrika hufanywa na pesa taslimu. Asilimia 20 iliyobaki hufanywa kupitia chaneli za kidijitali lakini zinategemea safu nyingi za ada na makaratasi. 


NALA inatumia teknolojia ya kisasa zaidi na kufanya kazi na jumuiya za karibu kufanya malipo bila matatizo iwezekanavyo. 

Programu ya NARA iliyo rahisi kutumia inaruhusu mtu yeyote kutuma pesa kwa haraka kutoka Uingereza au Marekani (EU inakuja hivi karibuni!) kwenda Kenya, Uganda, Tanzania, Ghana (pamoja na nchi nyingine nyingi za Kiafrika na sarafu zinakuja hivi karibuni!) kwa viwango vya chini zaidi vinavyopatikana.
Ikumbukwe


- Kuna Waafrika bilioni 1.3 ulimwenguni na inasalia kuwa mahali ghali zaidi kutuma pesa (8-9% hupotea kwa ada)


- NARA inaziba pengo kati ya familia zinazoishi maelfu ya maili ambazo zinawajibika kifedha kwa kutumia teknolojia inayopunguza gharama ya kutuma pesa


- NARA inarahisisha biashara na Afrika kwa kujenga njia na mifumo ya malipo inayotegemewa kwa kutumia teknolojia ya kisasa zaidi


Benjamin Fernandes ,Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa NARA 

Utahitaji kusasisha programu yako hadi toleo jipya zaidi (katika App Store au Play Store) ili kufungua kipengele hiki!



Malipo barani Afrika yamejengwa kwa asilimia 1. NARA inaleta teknolojia ya malipo ya karne ya 21 barani Afrika ili kuunda njia za malipo za gharama nafuu na zinazotegemeka sana ambazo marafiki, familia na wafanyabiashara wanaweza kutumia. Wakati malipo ni rahisi, ya kuaminika, na yanapatikana kwa kugusa kitufe, chochote kinawezekana.

Monday, July 25, 2022

WIZARA YASAINI MAKUBALIANO NA KAMPUNI YA EXTENSIA YA UINGEREZA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (Kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakitia saini Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect, tukio lililofanyika  Julai 25, 2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (katikati) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakitia saini Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect. Anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara hiyo, Bi. Lugano Rwetaka. 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akibadilishana nyaraka na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakati wa tukio la utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect  Julai 25, 2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (Kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakionesha nyaraka zilizosainiwa za Makubaliano baina ya Wizara na Kampuni hiyo ya kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect  Julai 25, 2022 jijini Dodoma.

 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano na  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, Bw. Tariq Malik (kushoto) wenye lengo la kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect   Julai 25, 2022 jijini Dodoma.


Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, Bw. Tariq Malik akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano baina ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Tewknolojia ya Habari na Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza  Julai 25, 2022 jijini Dodoma 


Picha ya pamoja ya baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Jim Yonazi (wa nne kushoto mstari wa mbele) na watendaji kutoka Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Kampunihiyo, Bw. Tariq Malik (wanne kulia mstari wa mbele kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano baina ya Wizara na Kampuni hiyo wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect   Julai 25, 2022 jijini Dodoma.


 Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, lengo likiwa ni kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect.

 

Kongamano hilo pia linalenga kuzidi kukuza matumizi ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kufungua wigo wa mifumo, ubunifu na uwekezaji katika TEHAMA.

 

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano hayo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi amesema  Kongamano la Connect To Connect (C2C) litafanyika kwa siku mbili tarehe 7 na 8 Septemba, 2022 ambapo nchi nyingi zinatarajiwa kushiriki ikiwa ni pamoja na nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki.

 

Amesema kuwa Tanzania inaunganisha nchi saba za jirani ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na Msumbiji  kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hivyo kuwa na fursa kubwa ya kupeleka huduma na kuchichimua uchumi kupitia TEHAMA.

 

Dkt. Yonazi ameeleza kuwa Kongamano litatoa pia fursa kwa nchi zitakazoshiriki kufanya majadiliano, kujifunza na kuweka mikakati ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuchangia uchumi , kuongeza fursa za uwekezaji, ajira na elimu.

 

Naye Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik amesema kuwa 

Kongamano hilo lilifanyika Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2013 hadi 2015 na kuleta mafanikio makubwa. Aidha, Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano kwa mara nyingine ambapo itapaisha zaidi Tanzania kama kitovu cha mawasiliano. 

 

Kwa upande wa Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo, Bw. Mulembwa Munaku amesema kuwa utiaji saini wa makubaliano hayo ni hatua ya awali ya kuanza maandalizi ya Kongamano kubwa litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi.

 

Naye Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari- MAELEZO,Bw. Gerson Msigwa ameipongeza Wizara kwa juhudi za kuweka mifumo imara ambayo itasaidia kutimiza malengo ya Serikali ya kuinua uchumi wa nchi kupitia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

MAKAMU WA RAIS MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA DORIS MOLLEL FOUNDATION JULAI 25

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) Bi. Doris William Mollel, Mazungumzo yaliofanyika Jijini Dar es salaam tarehe 25 Julai 2022.






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) Bi. Doris William Mollel, mara baada ya Mazungumzo yaliofanyika Jijini 

Dar es salaam  tarehe 25 Julai 2022.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango  tarehe 25 Julai 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) Bi. Doris William Mollel, Mazungumzo yaliofanyika Jijini Dar es salaam.

 

Makamu wa Rais amempongeza mkurugenzi huyo kwa jitihada anazofanya katika kuchangia vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwaajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti). Amesema taasisi hiyo inapaswa kuwekeza pia katika utoaji elimu ya afya ya uzazi ili kukabiliana na ongezeko la Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kwani maeneo mengi hasa ya vijijini wanashindwa kupata uelewa juu jambo hilo.

 

Makamu wa Rais amesema serikali imeendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kwa ujenzi wa hospitali za wilaya, vituo vya afya katika kata pamoja na zahanati katika vijiji ili kuendelea kukabiliana na changamoto za vifo vya mama na mtoto. Ametoa wito kwa wadau, taasisi za dini pamoja na wananchi kwa ujumla kulipa kipaumbele suala la kuwasaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati ili kukabiliana na changamoto ya vifo vinavyotokana na hali hiyo.

 

Katika Mazungumzo hayo Bi. Doris Mollel amempongeza Makamu wa Rais kwa jitihada alizofanya za kutambua changamoto zinazojitokeza katika malezi ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati  hapa nchini na kuamua kuchangia vifaa tiba kwaajili ya watoto hao katika hospitali ya taifa Muhimbili hivi karibuni. Aidha ameishukuru serikali kwa kuendelea kuiunga mkono taasisi hiyo husasani katika ajenda ya mtoto njiti na tayari wamewasilisha ombi la kuongezwa likizo kwa wanaojifungua kabla ya wakati pamoja na kuwasilisha maoni ya kuwekwa elimu ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika masomo ya sayansi kwa shule za msingi na baiolojia kwa shule za sekondari.

 

Amesema tayari serikali imetenga shilingi bilioni 23.36 katika bajeti ya Wizara ya afya kwa mwaka 2022/2023 pamoja na kutenga vyumba mia moja kwaajili ya watoto njiti ili kuweza kupunguza idadi ya watoto njiti wanaopoteza maisha kutokana na changamoto mbalimbali. Ameongeza kwamba taasisi hiyo ibeba ajenda ambayo imeridhiwa ya kuhakikisha huduma za mtoto njiti zinawekwa katika bima ya afya ya mama wa mtoto ili kuepusha gharama kubwa zinazojitokeza wakati wa kumhudumia mtoto anapozaliwa kabla ya wakati. 

 

 

WAZIRI NDALICHAKO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA


Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani). 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akimkaribisha Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot   tarehe 25 Julai, 2022 katika ofisi ndogo za Ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa na   Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot pamoja na ujumbe wake  leo tarehe 25 Julai, 2022, mara baada ya kukutana naye katika ofisi ndogo za Ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa  Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot  tarehe 25 Jula, 2022, alipomtembelea katika ofisi ndogo za Ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa na   Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot  tarehe 25 Julai, 2022, mara baada ya kukutana naye katika ofisi ndogo za ofisi hiyo Jijini Dar es salaam.

 

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA KWENYE SIKU YA MASHUJAA JIJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma kwa ajili ya kushiriki katika Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa tarehe 25 Julai, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kwa ajili ya Heshima ya Wimbo wa Taifa wakati ukipigwa kwenye Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka silaha za jadi (Ngao na Mkuki) kwenye mnara wa Mashujaa kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022.








Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi kwenye Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022.

 





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati akiondoka katika viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022.