Matokeo chanyA+ online




Thursday, September 20, 2018

BARABARA MPYA ZA LAMI ZA MITAA YA MIKOCHENI NA MSASANI ZAONGEZA KASI YA KUKUZA UCHUMI JIJINI DSM.






Monday, September 17, 2018

NCHI YETU INASONGA MBELE... TUNACHAPA KAZI!



Maana #SisiNiTanzaniaMpyA+ yenye kupata Matokeo ChanyA+ 110% kwenye kila nyanja ya kukuza uchumi imara na madhubuti 








MFUGALE FLYOVER Yakamilika kwa asilimia 100


MFUGALE Flyover ahadi ya Rais Dkt. Magufuli ya tarehe 17 Oktoba 2015 Ime...


Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 17 Octoba 2015 katika kampeni za uchaguzi mkuu 2015, Dk Magufuli alifanya kampeni katika jimbo la Segerea, aliwaomba wakazi wa Dar es Salaam wampatie kura Oktoba 25 ili aweze kutekeleza miradi hiyo mikubwa itakayoenda sanjari na ujenzi wa barabara za juu zitakazopunguza foleni.
LEO AHADI IMETIMIA BAADA YA KUANZA RASMI KUTUMIKA KWA FLYOVER MPYA YA Eng. Patrick MFUGULE

Thursday, September 13, 2018

Tanzania ilivyoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara nchini Msumbiji


Mheshimiwa Balozi Rajabu Luhwavi, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji (katikati), wengine kutoka kushoto ni ndugu Albert Philipo, Afisa wa Wizara kutoka Idara ya Diaspora (kushoto) na ndugu Nelson Nkini, Mwenyekiti wa Watanzania (Diaspora) wanaoishi nchini Msumbiji  akikaribishwa katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 54 yanayojulikana kwa jina la FACIM yaliyofanyika tarehe 27 Agosti hadi 2 Septemba 2018 Maputo nchini Msumbiji. Ushiriki wa wafanyabiashara kutoka Tanzania uliratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
                                                                                                                 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Carlos Agostinho do Rosário wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 54 ya FACIM alipotembelea banda la Tanzania na kukaribishwa na Bi. Getrude Ngweshemi, Kaimu Meneja - Masoko ya Ndani wa TanTrade na Bw. Albert Philipo, Afisa Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje ambapo alipatiwa maelezo kuhusu bidhaa za viwandani pamoja na vivutio vya utalii wa Tanzania. 
Balozi Rajabu Luhwavi akipokea maelezo kutoka kwa Afiisa wa Wizara, Bw. Albert Philipo kuhusu bidhaa za Tanzania zilizoletwa na wafanyabiashara mbambali kutoka Tanzania wakati wa maonesho ya biashara ya kimataifa ya 54 ya FACIM Maputo, Msumbiji. Wengine katika picha hiyo ni wafanyabiashara kutoka Kampuni mbalimbali nchini Tanzania.

Mheshimiwa Balozi Luhwavi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania walioshiriki katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 54 ya FACIM mjini Maputo.
Gavana wa Nampula, Mheshimiwa Victor Borges akiwa na Mheshimiwa Balozi Rajabu Luhwavi kushoto kwake wakikata utepe wakati wa kufungua Maonyesho ya Biashara Nampula tarehe 20 Agosti 2018. Maonesho hayo yalihusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na wenyeji wa Msumbiji. 
Mheshimiwa Balozi Rajabu Luhwavi akitoa maelezo mafupi wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Biashara Nampula yaliyohusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania. Kwa upande wake Balozi Luhwavi, alieleza kuwa maonesho haya ni ya kimkakati kwa ajili ya kukuza na kuimarisha umoja, mshikamano na mahusiano ya kiuchumi yaliyojengwa na waasisi wetu hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; hayati Sheikh Abeid Amani Karume, aliyekuwa rais wa kwanza wa Zanzibar na hayati Samora Moises Machel, aliyekuwa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Msumbiji. Maonesho haya yalifungua fursa za masoko kwa bidhaa za viwanda vya Tanzania pamoja na kuendeleza juhudi za utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kwa vitendo na kukuza uchumi, hususan uchumi wa viwanda.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kilele cha maonesho ya bidhaa za Tanzania mjini Nampula akiwa pamoja na Balozi Rajabu Luhwavi na Katibu Mkuu wa Jimbo la Nampula, Bi. Veronica Langa wakipata maelezo kuhusu teknolojia ya kisasa ya ufugaji samaki kutoka kampuni ya Dokaman ya nchini Tanzania.
Kutoka kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mheshimiwa Rajabu Luhwavi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ndugu Juma Ali Juma, Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara TanTrade, Bi. Anna Bulondo wakipata maelezo kutoka kwa wawakilishi wa kampuni ya A- Z Textile Mills inayojishughulisha na utengenezaji nguo, vifaa vya plastiki, mifuko ya kuhifadhia mazao na bidhaa nyingine.

Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mheshimiwa Rajabu Luhwavi akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi 

Friday, September 7, 2018

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA MRADI WA UFUGAJI SAMAKI KWENYE MABWAWA NA VIZIMBA KATIKA KAMBI YA JESHI 27KJ MAKOKO-MUSOMA MKOANI MARA .SEPTEMBA 6,2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashira uzinduzi rasmi wa Mabwawa 9 na Vizimba vya kufugia samaki aina ya Sato katika Kambi ya Jeshi YA 27 KJ Makoko Mkoani Mara.Wengine ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luaga Mpina,Katibu mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt.Frolence Turuka ,Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima,Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo,Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.Modestus Kimbilimba.Septemba 6,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya kukata utepe kuashira uzinduzi rasmi wa Mabwawa 9 na Vizimba vya kufugia samaki aina ya Sato katika Kambi ya Jeshi YA 27 KJ Makoko Mkoani Mara.Wengine ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luaga Mpina,Katibu mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt.Frolence Turuka , Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima,Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo,Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.Modestus Kimbilimba.Septemba 6,2018.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa kuashira uzinduzi rasmi wa Mabwawa 9 na Vizimba vya kufugia samaki aina ya Sato katika Kambi ya Jeshi YA 27 KJ Makoko Mkoani Mara.Wengine ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luaga Mpina,Katibu mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt.Frolence Turuka ,Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima,Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo,Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.Modestus Kimbilimba.Septemba 6,2018.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima mara baada ya kukata kuzindua rasmi mradi wa ufugaji wa Samaki wa kwenye mabwawa katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mradi wa ufugaji wa Samaki wa kwenye mabwawa wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mradi huo katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.

Askari wa Jeshi la kujenga Taifa wakiwawekea samaki chakula katika Mabwawa ya kufugia samaki hao wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.
Askari wa Jeshi la kujenga Taifa wakiwvua samaki katika Mabwawa ya kufugia samaki hao wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA BUNDA WAKATI AKIWA NJIANI KUELEKEA MUSOMA MKOANI MARA.SEPTEMBA 5,2018


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Bunda mjini wakati akiwa njiani kuelekea Musoma mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Bunda mjini wakati akiwa njiani kuelekea Musoma mkoani Mara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Bunda mjini wakati akiwa njiani kuelekea Musoma mkoani Mara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Bunda mjini wakati akiwa njiani kuelekea Musoma mkoani Mara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kwa njia ya Simu kuhusu mgogoro wa ardhi uliopelekea Bibi Nyasasi Masige mwenye kilemba aliyekaa kudai kunyang’anywa Kiwanja chake Wilayani Bunda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Bibi Nyasasi Masige kiasi cha Shilingi laki tano ili zimsaidie mara baada ya kusikiliza kero yake ya madai ya kunyanga’nywa kiwanja chake. Rais Dkt. Magufuli ameagiza uchunguzi ufanyike haraka ili haki ya bibi huyo iweze kupatikana.

RAIS DKT.JOHN MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA BARABARA YA NYAMUSWA-BUNDA-KISORYA-NANSIO KM 121 SEHEMU YA BULAMBA –KISORYA KM 51 PIA AHUTUBIA WANANCHI WA NANSIO UKEREWE MKOANI MWANZA.SEPTEMBA 4,2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Magu mara baada ya kufungua viwanda vya Lakairo Industries Ltd vilivyopo Magu mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe kuashiria uzinduzi wa Barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya-Nansio km 121 katika sehemu ya Barabara ya Bulamba Kisorya km 51 katika sherehe zilizofanyika Kisorya Bunda mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika mkasi na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa barabara Barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya-Nansio km 121 katika sehemu ya Barabara ya Bulamba Kisorya km 51 katika sherehe zilizofanyika Kisorya Bunda mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara Barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya-Nansio km 121 katika sehemu ya Barabara ya Bulamba Kisorya km 51 katika sherehe zilizofanyika Kisorya Bunda mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kisorya kabla ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya-Nansio km 121 katika sehemu ya Barabara ya Bulamba Kisorya km 51 katika sherehe zilizofanyika Kisorya Bunda mkoani Mara.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati akipokuwa akisikiliza maelezo ya mradi wa maji wa Nansio Ukerewe mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati akitoka kukagua pampu za kusukuma maji katika mradi wa maji uliopo Nansio Ukerewe mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako ili kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Ualimu Murutunguru kilichopo Nasio Ukerewe mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Nansio hawaonekani pichani katika eneo la chuo cha Ualimu cha Murutunguru kilichopo Nasio Ukerewe mkoani Mwanza.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ukerewe mara baada ya kuwasili akitokea Kisorya mkoani Mara.
Sehemu ya Wananchi wa Nansio Ukerewe waliohudhuria katika mkutano wa hadhara Septemba 4,2018
Sehemu ya barabara ya ya Bulamba Kisorya km 51 iliyoanza kujengwa kwa kiwango cha lami.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MBALIMBALI IKIWEMO UJENZI WA MELI MPYA, CHELEZO, UKARABATI WA MELI YA MV VICTORIA NA MV BUTIAMA KATIKA ZIWA VICTORIA MKOANI MWANZA.SEPTEMBA 3,2018


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia zoezi la utiaji saini Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika Bandari ya Mwanza Kusini mara baada ya kushudia utiaji saini wa Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika Bandari ya Mwanza Kusini mara baada ya kushudia utiaji saini wa Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika Bandari ya Mwanza Kusini mara baada ya kushudia utiaji saini wa Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd.
Mfano wa Meli mpya itakayojengwa ambayo Mkataba wake umesainiwa. Meli hiyo itakuwa na Urefu wa Mita 90, Kimo mita 10, uwezo wa kubeba abiria 1200 magari madogo 20, mizigo tani 400 na itakuwa ikisafiri kwa muda wa masaa sita tu kutoka Mwanza mpaka mkoa wa Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Song Geum Yong watatu kutoka kushoto waliokaa,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella wakwanza kulia waliokaa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe watatu kutoka kulia pamoja na wabunge mbalimbali wa mikoa ya Kanda ya ziwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika eneo la kupigia picha mara baada ya kushudia zoezi la utiaji saini ujenzi wa Meli mpya katika Ziwa Victoria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Song Geum Yong wakati kikundi cha ngoma za asili cha Bujora kilipokuwa kikitumbuiza.
Kikundi cha ngoma za asili cha Bujora cha mkoani Mwanza kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali ikiwemo Wabunge wakiwa wamesimama kimya kutoa heshma kwa wananchi waliopoteza maisha katika Meli ya MV Bukoba iliyozama katika ziwa Victoria mwaka 1996.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati akiwasili katika eneo la Bandari la Mwanza South.
Baadhi ya wananchi waliofika katika eneo la Bandari la Mwanza South kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Song Geum Yong watatu kutoka kushoto waliokaa,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella wakwanza kulia waliokaa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe watatu kutoka kulia pamoja na wandishi wa Habari mbalimbali waliokuwa wakihabarisha umma kuhusu tukio hilo la utiaji saini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Song Geum Yong mara baada ya tukio hilo la utiaji saini ujenzi wa Meli, Chelezo, pamoja na Ukarabati wa Meli.