Matokeo chanyA+ online




Thursday, January 31, 2019

WAZIRI MBARAWA AZINDUA BODI YA MAJI YA TAIFA

048A01055
 Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akimkabidhi nyenzo za kutendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Taifa Profesa Hudson Hamis Ngotagu.
048A1073
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na Katibu Mkuu, Profesa Kitila Mkumbo pamoja na Wenyeviti wa Bodi za Maji Tanzania.

SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA KILITEX-ARUSHA

Serikali iliwalipa stahili zote Watumishi wa Kiwanda cha nguo cha KILITEX kilichopo mkoani Arusha baada ya kufungwa kutokana na tatizo la ukosefu wa mtaji na malimbikizo ya madeni.

Hayo yamebainishwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, alipokua akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalaum Mhe. Catherine Magige, aliyeuliza ni lini Serikali itawalipa wafanyakazi 545 wa KILITEX ambao bado wanadai pensheni baada ya kiwanda hicho kufungwa ilihali mwajiri wao hakuwasilisha michango yao kwenye Mfuko wa Kijamii wa PPF.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, kwa mujibu wa kumbukumbu na nyaraka za ufilisi, taratibu za ufilisi zilikamilika na wafanyakazi hao walilipwa stahiki zao kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni  namba 46 ya mwaka 1931. 

“Baadhi ya wafanyakazi walilipwa mafao ya kiinua mgongo kwa mkupuo na wengine walirejeshewa michango yao kwa kadiri walivyochangia baada ya Mfilisi kushindwa kulipa riba, adhabu na malimbikizo ya michango kwenye mfuko wa Pensheni wa PPF”, alisema Dkt. Kijaji.

Alisema Kiwanda hicho kilisimamisha shughuli za uzalishaji mwaka 1994 na kuwekwa chini ya ufilisi na PSRC mwaka 1995.

Aidha akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlimba, Mhe. Suzan Kiwanga, alietaka kufahamu ni lini wafanyakazi 11075 wa Shirila la Reli la Tanzania na Zambia- TAZARA waliostaafishwa kwa lazima miaka 55 mwaka 2005, watalipwa mafao yao.

Alisema Serikali imefuatilia madai hayo na takwimu sahihi ni wastaafu 271 walistaafishwa na madai yao yanashughulikiwa ili waweze kulipwa mafao yao.

KAMPUNI YA KENYA KUNUNUA TANI LAKI MOJA ZA KOROSHO GHAFI TANZANIA


1X2A1398
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Taifa ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Dkt. Hussein Mansoor (kushoto) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya INDO Power Solutions ya nchini Kenya, Bw. Brian Mutembei (kulia) wakisaini Mkataba wa mauziano ya korosho ghafi kiasi cha tani laki moja kwa malipo ya Shilingii bilioni 418. Wanaoshuhudia tukio hilo muhimu ni Prof. Palamagamba Kabudi (wa pili kushoto), Waziri wa Katiba na Sheria, Joseph Kakunda (kushoto), Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Innocent Bashungwa (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Kilimo na Dan Kazungu, Balozi wa Jamhuri ya Kenya nchini. Tukio hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa mikutano uliopo Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha tarehe 30 januari 2019. Mawaziri hao wapo jijini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
1X2A1414
Dkt. Mansoor na Bw. Mutembei wakibadilishana Mkataba huo mara baada ya kusaini 
1X2A1363Prof. Kabudi akizungumza kabla ya kuanza kwa tukio hilo la kihistoria la kusainiwa mkataba wa ununuzi wa tani laki moja za korosho ghafi 
1X2A1358
Kakunda nae akizungumza 
1X2A1348
Dkt. Bashungwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) 
1X2A1377
Balozi wa Kenya nchini, Kazungu akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya kusainiwa mkataba wa ununuzi wa tani laki moja za korosho kutoka Tanzania 
1X2A1382
Bw. Mutembei nae akieleza furaha yake katika kukamilisha ununuzi wa korosho kutoka Tanzania 
1X2A1333
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Joseph Buchweshaija akizungumza kwa ufupi kuhusu hafla hiyo ya uwekaji saini mkataba wa ununuzi wa korosho. Wengine katika picha ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,  Prof. Florens Luoga ( kulia walioketi) akifuatiwa na Prof. Sifuni Mchome, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria na Dkt. Evaristo Longopa, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali 
1X2A1328
Mkutano ukiendelea. Kushoto ni Mkurugenzi wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka
Serikali ya Tanzania kupitia Bodi ya Taifa ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko imesaini mkataba wa mauzo ya korosho ghafi kiasi cha tani laki moja kwa Kampuni ya Kenya ya INDO Power Solutions kwa malipo ya Shilingi bilioni 418.

Mkataba huo umesainiwa jijini Arusha tarehe 30 Januari 2019 kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo Dkt. Hussein Mansoor kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Bw. Brian Mutembei, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya INDO Power Solutions ya nchini Kenya.

Tukio hilo la kihistoria lilishuhudiwa na Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria,  Joseph Kakunda, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Innocent Bashungwa, Naibu Waziri wa Kilimo, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, Dkt. Evaristo Longopa, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,

Viongozi wengine walioshuhudia ni Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu, Prof. Sifuni Mchome, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Joseph Buchweshaija, Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara, Prof. Siza Tumbo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Edwin Rutaberuka, Mkurugenzi wa TanTrade, Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini na Waandishi wa Habari.

Awali wakizungumza kabla ya kusainiwa kwa Mkataba huo Mawaziri hao wakiongozwa na Prof. Kabudi, kwa pamoja walipongeza kwa dhati uamuzi wa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali kununua korosho kutoka kwa wakulima ili kuepusha wakulima hao kuuza korosho zao kwa bei ya chini kwa watu wasio kuwa na nia njema kwa wakulima. Itakumbukwa kuwa, mwezi Novemba 2018, Rais Magufuli alitoa maelekezo kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo waratibu zoezi la ununuzi wa korosho kutoka kwa wakulima kwa shilingi 3,300 kwa kilo moja.

Kwa upande wake Prof. Kabudi alisema kuwa anampongeza Rais Magufuli kwa uamuzi huo wa Serikali kununua korosho yote ili wakulima wapate bei inayolingana na jasho lao ambao hatimaye umezaa matunda kwa faida na maendeleo ya nchi.

Naye Kakunda alieleza kuwa Bw. Mutembei ni mnunuzi wa kwanza kati ya wengi ambao walikuwa kwenye mazungumzo na Serikali kuhusu ununuzi wa korosho hizo. Kakunda alisema katika majadiliano Serikali iliangalia kufanya biashara ya faida ambayo itawezehsa kulipa gharama mbalimbali ikiwemo gharama za upakiaji na upakuaji, malipo kwenye Serikali za Mtaa na michango mingine ya kijamii kwa mujibu wa makubaliano. Hivyo aliwataka watanzania na wenye viwanda kutokuwa na wasiwasi kwani Serikali ina nia njema ya kuwaletea maendeleo wananchi hususan kupitia sekta ya kilimo cha korosho.

“Wakulima wa Korosho wanatakiwa kumshukuru Rais Magufuli kwa uamuzi wake ambao unalinda maslahi ya mkulima na umewawezesha kuuza korosho zao kwa faida. Nawakaribisha wafanyabiasha makini kuja nchini kwani Serikali ipo tayari kuwasikiliza watu wa aina hiyo na kufanya nao biashara” alisema Kakunda.

Kwa upande wake, Bashungwa alieleza kuwa katika msimu wa korosho wa mwaka 2018/2019 tayari zimekusanywa tani 213,159 ambazo kati ya hizo tani 126,194 zimehakikiwa na tayari wakulima wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani wamelipwa fedha zao kwa zaidi ya asilimia 95.5. Bashungwa aliongeza kuwa, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha Wakulima wote kulipwa fedha zao hadi kufikia tarehe 05 Februari 2019.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Balozi wa Kenya nchini, Kazungu alisema kuwa kusainiwa kwa mkataba huo ni faraja kubwa kwake katika historia ya mahusiano kati ya Tanzania na Kenya ambayo yanaendelea kuimarika siku hadi siku. Aidha, alieleza kuwa mkataba huo ni mfano mzuri wa kuimarika kwa mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hususan katika masuala ya kilimo na biashara.

Kwa upande wake, mnunuzi wa korosho hizo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Indo Power Solutions, Bw. Mutembei alisema amekuja kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kumwinua mkulima wa Tanzania na kwamba anawataka wale wote wanaobeza jitihada hizo za Rais Magufuli kuacha mara moja huku akilaani kitendo cha baadhi ya wafanyabiashara kuendelea kuwakandamiza wakulima kwa kununua mazao yao kwa bei ndogo wanazopanga wao huku wakijua wazi kuwa wakulima hao wametumia gharama kubwa katika uzalishaji wa mazao hayo.

Pia aliwataka wafanyabiashara kufuata taratibu na sheria katika kufanya biashara kama Serikali zinavyoelekeza na kuacha kuchanganya biashara na siasa.

Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Nafaka, Dkt. Mansoor alieleza kufurahishwa na tukio hilo ambalo limekuja wakati mwafaka wakati nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zikijiandaa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi utakaofanyika jijini humo hivi karibuni. Aidha alisema kuwa, kwa kiasi kikubwa tukio hilo limeiinua Bodi yake na kwamba anatoa wito kwa wafanyabiasha wengine wa ndani na nje ya Tanzania kuja nchini na kushirikiana na Bodi hiyo ili kuwakomboa wakulima wengi Zaidi.

Mkataba huo umesainiwa wakati baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Tanzania wakiwa jijini Arusha kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 1 Februari 2019.

TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI - RC MWANGELA

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (rtd) Nicodemus Elias Mwangela amewataka Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) kukamilisha miradi ya ujenzi wanayo pewa ndani ya muda wa makubaliano ya mikataba.

Brig. Jen. (rtd) Mwangela ameyasema hayo jana wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa na ya Katibu ya Katibu Tawala Mkoa kati ya TBA na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.

“TBA mna sifa nzuri ya kujenga majengo ya serikali kwa kuzingatia ubora unaotakiwa na kwa gharama nafuu lakini kuna wakati kunakuwa na kusita katika kuwapa kazi kutokana na historia yenu ya kuchelewesha kukamilisha miradi mnayopewa ya ujenzi”, ameeleza Brig. Jen. (rtd) Mwangela.

Ameongeza kuwa TBA wamechelewesha ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ujenzi wa Hospitali ya Mji wa Tunduma hivyo ucheleweshaji huo usirudie katika mikataba hiyo miwili waliyopewa kwani hatasita kuvunja mikataba hiyo endapo wataonyesha ucheleweshaji.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila ameishukuru serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuupatia Mkoa wa Songwe kiasi cha shilingi bilioni 26.8 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali mkoani hapa.

Kafulila amesema serikali imekuwa ikitoa fedha za miradi mbalimbali lakini kasi ya utoaji wa fedha na matumizi ya fedha hizo kwenye miradi husika imekuwa haiendani na hivyo kusababisha kuchelewa kukamilika kwa miradi hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwa amini na kuwapa miradi hiyo miwili yenye thamani ya shilingi bilioni moja na kuahidi kuikamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Mhandisi Cosmas amesema hapo awali walikuwa na changamoto kama vile ukosefu wa maji, umeme na baadhi ya vifaa lakini wamesha zifanyia kazi changamoto hizo hivyo watamaliza miradi hiyo Juni 30, 2019 kama walivyokubaliana katika Mikataba.
IMG_4592
 Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila akisaini mikataba ya Ujenzi wa nyumba za Mkuu wa Mkoa na ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, ambapo Wakala wa Majengo (TBA) wamekubali kukamilisha ujenzi huo kwa muda wa miezi mitano na kwa gharama ya shilingi bilioni moja.
IMG_4597
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila na Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas wakisaini mkataba wa ujenzi wa nyumba za Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala Mkoa, wa Kwanza Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Rtd) Nicodemus Mwangela.

MTENDAJI MKUU TEMESA AKAGUA MASHINE YA KISASA YA KUKAGUA MAGARI KARAKANA YA MT. DEPOT

PIC%2B1
 Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe (wa pili kushoto) akimpa maelezo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kushoto) wakati alipotembelea karakana ya Mt. Depot kukagua mashine ya kisasa ya kukagulia magari iliyofungwa katika karakana hiyo. Kushoto ni Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.
PIC%2B2
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe  (wa pili kushoto) wakati alipotembelea karakana ya Mt. Depot kukagua mashine ya kisasa ya kukagulia magari iliyofungwa katika karakana hiyo ili kurahisisha utendaji kazi. Kushoto ni Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.
PIC%2B3
 Pichani, gari linaonekana likiwa limenyanyuliwa juu na mashine ya kisasa (3D Wheel Allignment) tayari kwa kuanza kukaguliwa, mashine hiyo ya kisasa imefungwa katika karakana ya TEMESA Mt. Depot Keko Jijini Dar es Salaam. Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA una mpango wa kufunga mashine nyingine kama hizo katika karakana za mkoa wa Mwanza na Dodoma.
PIC%2B4
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akikagua maboksi maalumu ya kuhifadhia mtambo wa kuongozea taa za magari (traffic light controller) katika karakana ya Mt. Depot kikosi cha Umeme. Kushoto ni Kaimu meneja wa kikosi hicho Mhandisi Pongeza Semakuwa na wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO - (TEMESA)

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)

V25A9199
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani alipomtembelea tarehe 31 Januari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Katikati ni Meneja Masoko na Utafiti Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndg. Itandula Kambalagi.
V25A9220
V25A9273
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani alipomtembelea tarehe 31 Januari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
V25A9351
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulid Banyani (wa pili kulia) walipomtembelea tarehe 31 Januari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

BODI YA USHAURI NFRA YATEMBELEA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA MKOANI MANYARA, YAMTAKA MKANDARASI KUONGEZA KASI YA UJENZI

Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imetembelea eneo la Mradi wa ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa Mkoani Manyara na kuipongeza kampuni ya Unia Araj Realizacje Sp.o.o) chini ya msimamizi wa utekelezaji wa mradi huo ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kasi waliyoanza nayo ya ujenzi.

Kampuni hiyo ambayo imeanza ujenzi huo tarehe 15 Disemba 2018 katika Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara katika kipindi hicho imetekeleza mradi huo kwa kasi nzuri, Imesema Bodi hiyo.

Mradi huo katika Kanda ya Arusha (Babati), pamoja na Dodoma, Makambako, Mbozi, Shinyanga, Songea, Sumbawanga na Mpanda. utagharimu Dola za Kimarekani Milioni 55, ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ikiwa ni sehemu ya kiasi cha milioni 110 kilichotolewa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza na mkandari wa mradi huo Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mhandisi Eustance Kangole alisema kuwa kampuni hiyo inapaswa kuongeza kasi zaidi ya ujenzi ili kukamilisha kwa muda uliopangwa.


Alisema kuwa Hifadhi ya Chakula inayohitajika kukidhi mahitaji ya dharula kwa miezi mitatu ni zaidi ya tani 500,000 ukilinganisha na tani 150,000 iliyokuwa inahitajika miaka ya 1992 Wakala ulipoanzishwa.



Pia, technologia ya vihenge itawezesha Wakala kutumia teknolojia ya kisasa na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji, Itawezesha Wakala kuhifadhi chakula kwa muda mrefu Zaidi, itasaidia kupunguza upotevu wa zao la mahindi baada ya kuvuna (posthaverst loss) na kuongeza soko la mahindi nchini na kuimarisha usalama wa nafaka inayohifadhiwa kwa kudhibiti sumukuvu (Aflatoxin) kwa mahindi yaliyohifadhiwa.


Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Eustance Kangole na katibu wake ambaye pia ni Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba imefanya ziara hiyo mara baada ya kikao kazi cha 33 cha Bodi hiyo Jijini Dodoma kilichofanyika kwa lengo la kujadili masuala muhimu ya Wakala ikiwemo utekelezaji wa mkataba wa mauzo ya mahindi Tani 36,000 kwa Shirika la Chakula Duniani (WFP) sambamba na kujadili maendeleo ya Mradi wa Vihenge na Maghala ya kisasa.

Vihenge 8 vinatarajiwa kujenzgwa Kanda ya Arusha katika eneo la (Babati) vyenye uwezo wa kuhifadhi nafaka Tani 25,000 ambapo pia yatajengwa maghala 2 yenye uwezo wa kuhifadhi nafaka Tani 15,000 hivyo kuwa na jumla ya Tani 40,000.

Baada ya mradi kukamilika Wakala utakuwa umeongeza uwezo wa kuhifahi kwa Tani 250,000 zaidi (vihenge vya kisasa 190,000 MT na maghala 60,000 MT) jambo ambalo litakuwa chachu na mafanikio yenye tija katika kuunga mkono Juhudi za utendaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.

Kupatikana kwa Mradi huo nchini ni jitihada za Serikali ambazo zitapelekea ukuaji wa uchumi nchini na kuchangia kuwezesha Tanzania ya viwanda ambapo kutawezesha maghala ya Wakala kuweza kuhifadhi akiba ya Chakula ambayo itaendana na mahitaji halisi ya dharura kulinganisha na ongezeko la watu nchini.

1R6A1184
Wajumbe wa Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakikagua eneo la Mradi wa ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa Mkoani Manyara unaojengwa na kampuni ya Unia Araj Realizacje Sp.o.o) chini ya msimamizi wa utekelezaji wa mradi huo ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
1R6A1179

1R6A1190

1R6A1195


1R6A1198

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MABALOZI WATATU WAPYA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 31 Januari, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi kutoka nchi 3 ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Balozi wa kwanza kukutana na Makamu wa Rais, alikuwa Mhe. Gaber Mohamed Abulwafa Balozi mpya wa Misri hapa nchini ambaye alifika kwa lengo la kujitambulisha na pia kuzungumzia mambo mbali mbali ya kuimarisha uhusiano baina ya nchini  mbili ambao ulianzishwa na waliokuwa marais wa nchi hizi, Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais Gamal Abdel Nasser Hussein wa Misri.

“Misri itaendelea kutoa ushirikiano katika masuala ya Elimu, Afya na masuala ya teknolojia ya ujenzi wa miundombinu yenye tija kwa mataifa haya mawili” alisema Balozi huyo.

Mwisho Balozi huyo mpya wa Misri aliahidi kusimamia miradi yote ambayo ipo kwenye makubaliano baina ya Serikali hizi.

Kwa upande wake Makamu wa Rais alimpongeza na kumkaribisha Tanzania pamoja na kumhakikishia ushirikiano mzuri katika kazi zake akiwa hapa nchini na kumueleza kuwa kwa miaka mingi uhusiano kati ya Misri na Tanzania umezidi kuimarika.

Balozi wa Pili kukutana na kuzungumza na Makamu wa Rais alikuwa Mhe. Francisca Pedros, Balozi mpya wa Spain hapa nchini ambaye Makamu wa Rais alimpongeza kwa kuwa Balozi wa kwanza mwanamke kuteuliwa kuja kuitumikia nchi yake hapa nchini.

Balozi wa Tatu kukutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Makamu wa Rais ni Balozi wa Ethiopia nchini Mhe. Yonas Yosef Sanbe ambaye alimueleza Makamu wa Rais furaha yake ya kuwa hapa na kuona namna mahusiano ya nchi hizi mbili yameboreka ambapo alisema kuwa

“nafarijika kuona namna ambavyo wanawake wanapewa nafasi za juu katika uongozi katika nchi hizi mbili”

Makamu wa Rais pamoja na mambo mengine alimpongeza Balozi huyo wa Ethiopia kwa kuwa Balozi wa kwanza mwenye makazi yake hapa Tanzania.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Mohamed Abulwafa (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi mpya wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Mohamed Abulwafa (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Spain nchini Mhe. Francisca (kushoto) aliyefika kujitambulisha ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi mpya wa Spain nchini Mhe. Francisca Pedros (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi mpya wa Spain nchini Mhe. Francisca Pedros(kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Ethiopia nchini Mhe. Yonas Yosef Sanbe aliyefika kujitambulisha leo Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi mpya wa Ethiopia nchini Mhe. Yonas Yosef Sanbe aliyefika kujitambulisha leo Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Wednesday, January 30, 2019

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI, BALOZI WA SWEDEN JIJINI DODOMA

V25A8961
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg alipomtembelea leo tarehe 30 Januari, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
V25A8993
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo leo tarehe 30 Januari, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
V25A9015
V25A9019
pika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg baada ya kumtembelea na kufanya nae mazungumzo leo tarehe 30 Januari, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. 
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI WA DSFA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Islam Seif Salum Mchenga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority – DSFA).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Mchenga umeanza tarehe 01 Desemba, 2018 na kwamba kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi - Zanzibar.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Emmanuel Andrew Sweke kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).
Uteuzi wa Dkt. Sweke umeanza tarehe 01 Desemba, 2018 na kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Utafiti wa Uvuvi Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tanzania Livestock Research Institute - TAFIRI) – Kigoma.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Sebastian W. Chenyambuga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI).
Uteuzi wa Prof. Chenyambuga umeanza tarehe 26 Januari, 2019.
Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Justinian Rwezaula Ikingura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania - GST).
Uteuzi wa Prof. Ikingura umeanza tarehe 18 Januari, 2019.

WAKENYA WAJA NCHINI TANZANIA KUJIFUNZA KUHUSU MIRADI MAJI TAKA

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Tim Ndezi akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA). Ujumbe huo ulilenga kutembelea na kujionea miradi ya majitaka maeneo ya Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi maalum ya Maji Taka inayotekelezwa katika maeneo yasiyopimwa na yenye msongamano. Wageni hao ni maofisa wa Serikali ya Kenya kutoka Kampuni ya majisafi na majitaka Nairobi (NCWSC) na Huduma za jamii, Mashirika binafsi na viongozi wa vikundi vya jamii wapo nchini kwa siku 5 wakitembelea Dar es Salaam na Mwanza.  
Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya, Kata ya Vingunguti Rahimu Seif Gassi (kulia) kiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka. Wageni hao ni maofisa wa Serikali ya Kenya kutokea upande wa Maji na Huduma za jamii, Mashirika binafsi na viongozi wa vikundu vya jami wapo nchini kwa siku 5 wakitembelea Dar es Salaam na Mwanza.
Mhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI), Festo Dominick Makoba ambaye ndiye msimamizi wa eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Moja ya Choo cha kisasa vinavyojenga na Shirika la CCI kwa kusaidiana na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) ili kuwawezesha wananchi wanaoishi katika maeneo yasiyo rasmi.
Moja ya chemba za vyoo vya kisasa.
Muonekano wa Choo cha zamani ambacho wakazi wa Vingunguti walivyokuwa wakitumia.
Mhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI), Festo Dominick Makoba ambaye ndiye msimamizi wa eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam akionyesha namna mabomba ya vyoo yalivyopita.
Wageni wakiendelea na ziara.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya, Kata ya Vingunguti jijini Dar es Salaam, Rahimu Seif Gassi (kulia) kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Tim Ndezi akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Wananchi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Wananchi wakimsikiliza mwenyekiti.
Bi Kellen Muchira kutoka Shirika la Caritas Switzerland lililopo nchini Kenya akizungumza machache juu ya jinsi walivyoweza kufika Tanzania kujifunza namna ya Shirika la CCI na DAWASA wanavyoweza kushirikiana kuwasaidia wakazi wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi kukusanya Maji Taka.
Afisa Miradi wa Akiba Mahirani Trust ya nchini Kenya, Patriki Njoroge akieleza machache mbele ya wakazi wa Vinguti jijini Dar es Salaam wakati walipofika Tanzania kujifunza namna ya Shirika la CCI na DAWASA wanavyoweza kushirikiana kuwasaidia wakazi wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi kukusanya Maji Taka.
Makazi wa Vingunguti akisoma risara mbele ya wageni.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA)  Mhandisi Charles Makoye akiwaelezea juu ya mradi wa kuchakata maji Taka uliopo Toangoma wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) (mwenye shati jeupe) akiwaonyesha chemba ya mradi wa kuchataka Maji Taka iliopo Toangoma jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Mhandisi Charles Makoye (Kulia) akiendelea kutoa maelezo.
Wageni wakiwa katika picha ya pamoja.