Matokeo chanyA+ online




Thursday, February 28, 2019

PROF MBALAWA AHIMIZA JAMII KUSHIRIKI KULIENDELEZA BONDE LA MTO ZAMBEZI


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa  Makame Mbarawa, amefungua Mkutano wa Saba wa Mawaziri wa Maji wa nchi nane  zilinazohusiana na Bonde la Mto Zambezi (Zambezi Watercourse Commission – ZAMCOM) na kuitaka jamii ya mataifa hayo kuona umuhimu wa kamisheni ya chombo hicho kuendelea kuimarika na kusimamia raslimali za ZAMCOM kwa manufaa yaliyokusudiwa.
Waziri Mbarawa alikuwa anafungua kikao cha Baraza la Mawaziri wa Maji katika Ukumbi  wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, vikao vikiwa ni Mkutano wa Sita wa Baraza la Mawaziri Februari 26 – 27 na Mkutano wa saba wa Kamati ya Wataalaam ya ZAMCOM, nchi husika zikiwa ni Angola, Botswana, Msumbiji, Malawi, Namibia, Zambia, Zimbambwe na Mwenyeji Tanzania.
Mkataba wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi ulianza rasmi mwaka 2011 kwa lengo la kusimamia raslimali za maji za Bonde la Mto Zambezi, Tanzania ambayo ni mwanachama maji yake toka Ziwa Nyasa, kwa wastani wa asilimai 16 ya maji yaingiayo Ziwa Zambezi kwa mito,  humwagika Ziwa Zambezi na Bonde hilo linahitaji hifadhi na zipo fursa za kuwepo miradi ya manufaa kwa nchi hizo.
Baraza limepokea Mpango kazi (Strategic Plan) na  Mfumo  wa kubadilishana, kutumia na kuhifadhi takwimu za raslimali za Maji kwa njia ya TEHAMA, ambapo Tanzania imemaliza muda wake wa Uenyekiti na nafasi hiyo kupewa Zambia.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS MTENDAJI MWANDAMIZI WA JICA KAZUHIKO KOSHIKAWA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa (wa tatu Kushoto) na ujumbe wake baada ya kukukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Februari, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa.
Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro na Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Shinichi Goto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa (wa tatu Kushoto) na ujumbe wake walipokutana  Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro
 
Mhe. Rais Magufuli ameishukuru JICA kwa kuwa mdau muhimu wa maendeleo ya Tanzania na amemhakikishia Bw. Kazuhiko Koshikawa kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano huo hususani katika ujenzi wa miundombinu.
Ameelezea kufurahishwa kwake na kutiwa saini kwa miradi miwili ya upanuzi wa barabara ya Mwenge – Morocco (kilometa 4.3) na Daraja la Gerezani Jijini Dar es Salaam ambayo ujenzi wake utaanza wakati wowote kuanzia sasa, pamoja na msaada wa shilingi Bilioni 57 kwa ajili ya uboreshaji wa bandari ya Kigoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya picha ya kuchora ya wanyama wakuu watano (Big Five)  Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019.
Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro


Kwa upande wake Bw. Kazuhiko Koshikawa amempongeza Mhe. Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano kwa juhudi kubwa za kukuza maendeleo ya Tanzania na kuendeleza ushirikiano mzuri na JICA uliowezesha miradi mingi ya maendeleo kutekelezwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro amesema ushirikiano mzuri wa Serikali ya Tanzania na JICA unathibitisha rekodi nzuri ya uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi mbalimbali ambao una manufaa makubwa katika uchumi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya kinyago ja UJAMAA  Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019.
Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro

Katika mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli ameagana na Mwakilishi Mkazi wa JICA hapa nchini aliyemaliza muda wake Bw. Toshio Nagase na kumkaribisha Mwakilishi Mkazi mpya wa JICA Bw. Naofumi Yamamura.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na  Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa (wa tatu Kushoto) na ujumbe wake baada ya kukukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro

Wednesday, February 27, 2019

WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU WAHAKIKISHIWA KUONGEZEWA MIKATABA

Rais wa Shirikisho la Viwanda vya Misitu Tanzania ( SHIVIMITA) Ben Sulus akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu kuhusu kuongezewa muda wa mikataba kutoka miaka miwili hadi miaka mitano ya kupewa vitalu vya miti katika Shamba la Miti la Sao Hill lililopo mkoani Iringa wakati Washirika hao walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.

Na Lusungu Helela-WMU

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii. Mhe. Constantine Kanyasu amewahakikishia wamiliki wa viwanda vya misitu Tanzania kuwa atashughulikia ombi lao la kutaka kuongezewa muda wa mikataba yao kutoka  miaka miwili hadi  mitano ya kupewa mgao wa vitalu vya miti
Pia ameahidi kuyafanyia kazi malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa ofisini kwake na wamiliki hao yakiwemo ya gharama za tozo ya ushuru wa mazao ya misitu  (Cess) inayotozwa na Halmashauri za wilaya ya Mufindi ambayo licha  Serikali kutoa maagizo ya kuzuia tozo hiyo bado wadau hao wanaendelea kutozwa.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akisalimia na baadhi ya Wanachama wa Shirikisho la Viwanda vya misitu Tanzania mara baada ya kufanya mazungumzo nao kuhusu ombi la kuongezewa muda wa mikataba kutoka miaka miwili hadi miaka mitano ya kupewa vitalu vya miti katika Shamba la Miti la Sao Hill lililopo mkoani Iringa wakati Washirika hao walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma

 Mhe. Kanyasu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Rais wa Shirikisho la Viwanda vya Misitu Tanzania (SHIVIMITA) na Wanachama wa Shirikisho hilo  waliomtembelea ofisini kwake  jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo,  Rais wa SHIVIMITA, Ben Sulus amemuomba Naibu Waziri  aangalie  namna ya kuwasaidia wadau hao waongezewe muda wa mikataba kutoka miaka miwili hadi mitano ya kupewa mgao wa vitalu vya misitu ili waweze kupata mikopo kutoka kwenye Taasisi za Kifedha kwa ajili ya kuendeshea viwanda vyao
Rais huyo ameeleza kuwa Taasisi za Kifedha  zimekuwa zikiwanyima  mikopo kwa kuhofia fedha zao kupotea kutokana na wadau hao kutokuwa na uhakika wa kuongezewa mikataba mara baada ya mikataba yao ya kuvuna magogo ya miaka miwili waliyopewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).
Amesema  endapo watapewa mikataba  ya miaka mitano watakuwa na uhakika wa kuweza kuendeleza viwanda vyao kwa vile Taasisi hizo za Kifedha zitaweza kuwapa mikopo watakayoomba na  zitakuwa na uhakika wa kurudishiwa  fedha hizo.
Katika hatua nyingine, Wadau hao wamemuomba awe mlezi wao katika jitihada wanazozichukua za kuhakikisha wanakuwa wazalishaji wa bidhaa za mwisho kama vile milango pamoja na meza   zitokanazo na mbao badala ya kujikita kuuza mbao tu.

BODI YA WAKURUGENZI YA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI TANZANIA – (TAWA)


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb.), amekamilisha uteuzi wa safu ya wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – (TAWA), kulingana na mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 3.1.1 cha amri ya uanzishwaji wa Mamlaka ya TAWA ( GN na. 135 ya mwaka 2014)  kwa kuwateua wajumbe wengine wawili.
Wajumbe walioteuliwa kukamilisha safu inayotakiwa ni;
  • Jane Claude Mihanji na
  • Bi Magdalena Joseph Kimaty
Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 26 Oktoba, 2018.
Wakati huo huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, amebatilisha uteuzi wa Dkt. Freddy S. Manongi kuwa mjumbe wa bodi ya TAWA.
Imetolewa na
Dorina G. Makaya
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
27 Februari, 2019

NDITIYE KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU SHULE ZA SEKONDARI LUDEWA


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa nne kulia) akimkabidhi Mbunge wa Ludewa, Deo Ngalawa kompyuta 25 kwa ajili ya sekondari za Wilaya ya Ludewa, Njombe wakati wa ziara yake Wilayani humo. Anayeshuhudia katikati yao ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amegawa kompyuta 25 kwa shule za sekondari za Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe zenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi kujifunzia na waalimu kufundishia, kuongeza uelewa na kupata maarifa kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa kuunganisha kompyuta hizo na mtandao wa intaneti ili kuwawezesha wanafunzi wa Wilaya hiyo kuongeza kiwango cha ufaulu
Nditiye amekabidhi kompyuta hizo kwa Mbunge wa Ludewa, Deo Ngalawa kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Ludewa ili ziweze kutumika kwenye shule mbali mbali zilizopo Wilayani humo
“Nimeleta kompyuta 25 ili zigawiwe kwenye shule mbalimbali ili watoto wajifunze kutumia TEHAMA pamoja na waalimu waliopewa mafunzo ya TEHAMA na taasisi yetu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)”, amesema Nditiye. Kompyuta hizo zimetolewa na UCSAF ambayo inahusika na ufikishaji wa huduma za mawasiliano vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara
Nditiye ameongeza kuwa Wilaya ya Ludewa inafahamika katika kipindi cha miaka ya nyuma kwa kuwa moja ya Wilaya saba nchini ambapo wanafunzi wake wana kipaji cha akili ukilinganisha na Wilaya nyingine zilizopo nchini ambapo ameona ni vema kuwapatia wanafunzi wa shule za Wilaya hiyo kompyuta hizo ili waweze kuongeza ufaulu, kujenga uelewa na kupata maarifa ili waweze kuwa wanafunzi vinara kama iliivyokuwa imezoeleka katika kipindi cha miaka ya nyuma. Pia, amesema kuwa Tanzania inaongoza katika matumizi ya TEHAMA katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mara baada ya kupokea kompyuta hizo kwa niaba ya wananchi, Mbunge wa Ludewa, Deo Ngalawa alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere kuwa, kuwe na kituo kimoja cha kutunga mitihani Ludewa ili waalimu watunge mtihani wa aina moja na waweze kumaliza kufundisha masomo ya kiada na ziada kama walivyopanga kwa muhula husika wa masomo ili waweze kuwapima wanafunzi wote kwa pamoja
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Andrea Tsere alimueleza Nditiye kuwa wataweka intaneti kwenye kompyuta hizo ili waalimu na wanafunzi waweze kupata notisi. Pia, amesema kuwa kompyuta hizo zitatumika kuinua kiwango cha elimu na zimefika muda muafaka
“Mmetusaidia sana, umeingia kwenye akili yangu ya kuinua kiwango cha elimu Ludewa,” amesisitiza Tsere wakati akimshukuru Nditiye kwa kuzipatia shule za Wilaya yake kompyuta 25. Tsere amewataka waalimu wakuu wa shule kuzitunza kompyuta hizo na kuzifanyia matengenezo pindi inapohitajika badala ya kuacha ziharibike na pasipo kuzipanga vizuri kwa sababu ni vifaa vya Serikali badala yake wanapanga lini wavichukue badala ya kuzitunza vizuri ili zisaidie wanafunzi wengi na kwa muda mrefu. Aidha, amesisitiza kwa waalimu hao kuwa kompyuta zikipotea na wao wapotee
Katika hatua nyingine, Nditiye amewaeleza wananchi hao kuwa, Wizara yake ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia UCSAF imetoa ruzuku kwa kampuni ya simu ya Halotel na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ili wajenge minara 11 kwenye maeneo ya mwambao kwa wananchi waishio Wilayani Ludewa kwa kuwa hawana mawasiliano.
“Tunahitaji Ludewa iwasiliane na dunia,” amesisitiza Nditye. Amefafanua kuwa minara tisa imejengwa na kampuni ya Halotel na miwili ni ya TTCL
Vile vile, ameongeza kuwa, ujenzi wa meli ya abiria waishio Ludewa kwa ajili ya usafiri wa Ziwa Nyasa umekamilika ambapo kwa sasa meli hiyo inafanyiwa majaribio kabla ya kuanza safari zake na Serikali inakamilisha ujenzi wa gati za kushusha na kupakia abiria kwenye mwambao wa ziwa hilo kwenye maeneo ya Manda, Lupingu, Nsele, Yiga na Nkanda ambapo meli hiyo inatarajiwa kuanza safari zake za kutoka Ludewa, Njombe hadi Kyela, Mbeya mwezi Aprili mwaka huu
“Tunataka Lupingu hadi Matema watu wapite kwa lami,” amefafanua Nditiye. Ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa Ludewa mjini na kuwaeleza kuwa  azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa barabara ya Lusitu – Mawengi yenye urefu wa kilomita 50 inajengwa kwa kiwango cha zege kwa gharama ya shilingi bilioni 159 ambapo tayari mkandarasi wa kutoka nchi ya Korea yupo na anaendelea na ujenzi wa barabara hiyo ili iweze kupitisha madini ya Mchuchuma na Liganga
Ngalawa amewaeleza wananchi kuwa anamshukuru Nditiye kwa kuwa alifanya ziara kutoka Lupingu hadi Manda mwaka jana mwezi wa tatu akiwa na miezi minne tu tangu alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri na kushuhudia ukosefu wa mawasiliano kwa wananchi waishio mwambao na sasa minara 11 imejengwa ambapo tayari minara mitatu ya Nkanda, Mawengi na Mahong’olo imewashawa na meli ya abiria pia itaanza safari zake
Tsere alimshukuru Ngalawa kwa kumleta Nditiye ambapo alisafiri na boti siku nzima Ziwani mwaka jana mwezi wa Machi na kushuhudia ukosefu wa mawasiliano kwa kuwa tangu dunia iumbwe wananchi wa mwambao hawajawahi kupata mawasiliano na sasa wanawasiliana
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

KATIBU MKUU CHAULA ATEMBELEA TAASISI YA JKCI

Wafanyakazi wa Taasisis ya Moyo Jakaya Kikwete wametakiwa kufanya kazi zao kwa umoja, kuwasaidia wahitaji na kuwatendea haki wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.

Rai hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula alipokuwa akizungumza  na wafanyakazi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Chaula alisema kazi ya kuwahudumia wagonjwa ni ngumu na ni ibada hivyo basi kutokana na matendo mema watakayowatendea wagonjwa ambao ni wahitaji Mwenyezi Mungu atawalipa kwa  kuwajalia afya njema ili waweze kuwahudumia kwa miaka mingi zaidi.

“Nawapongeza sana kwa kazi mnayoifanya ya kuwahudumia wagonjwa  wenye matatizo ya moyo, kazi hii ni  ngumu jambo la muhimu ni kuwa na upendo  baina yenu na wagonjwa mnaowahudumia. Hakika Mwenyezi Mungu atawalipa kwa huduma yenu mnayoitoa”, alisisitiza Dkt. Chaula.

Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi hao kufanya kazi zao  kwa bidii, wakati  na kutimiza wajibu  wao kwani hakuna  kisichowezekana katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa vitu  vyote vipo ndani ya uwezo wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kutembelea Taasisi hiyo na kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa.

Prof. Janabi  alisema idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na kutoa mfano wa wagonjwa wa nje 8557 waliotibiwa mwezi wa kwanza ukilinganisha na wagonjwa 7222 waliowaona mwezi wa Desemba mwaka jana.

Alisema   idadi ya wagonjwa wanaolazwa imeongezeka kutoka wagonjwa 282 kwa mwezi wa kumi na mbili mwaka jana hadi kufikia 312 waliolazwa mwezi wa kwanza mwaka huu.

“Tunaona wagonjwa kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani ila wagonjwa wetu wengi zaidi wanatoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, Arusha, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Pemba,Katavi, Kigoma Kilimanjaro, Lindi, Manyara, Mara, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida,Tanga na Unguja ”, alisema Prof. Janabi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimwelezea Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya, Dkt. Zainab Chaula jinsi duka la dawa linavyohudumia wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. 
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godfrey Mbawala akimwelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula jinsi wanavyofanya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa watoto kutumia mtambo wa Cathlab wakati katibu mkuu huyo alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiangalia moja ya chumba cha VIP kilichopo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. Kutoka kulia kwa Katibu mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.

KATIBU MKUU UJENZI ATEMBELEA TEMESA NA KUKAGUA VIFAA VIPYA VYA KARAKANA

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga wa kwanza kushoto akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe kuhusu vifaa vipya vya karakana vilivyonunuliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ajili ya kusambazwa kwenye karakana zake mikoani, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Sylvester Simfukwe kulia akimpa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga katikati kuhusu mashine mpya za karakana zilizonunuliwa na Wakala huo kwa ajili ya kusambazwa kwenye karakana zake mikoani. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga wa tatu kulia akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Sylvester Simfukwe kushoto kuhusu mashine mpya ya kukagua gari na kupima uwiano wa matairi ya magari (3D Wheel Allignment) iliyonunuliwa na kufungwa katika karakana ya Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle na Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga wa nne kulia akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Sylvester Simfukwe kushoto kuhusu mashine ya kukagua gari na kupima uwiano wa matairi ya magari (3D Wheel Allignment) iliyonunuliwa na kufungwa katika karakana ya Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam, wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle na Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga wa pili kulia akifurahia jambo na mafundi wa karakana ya Mt. Depot mara baada ya kumaliza kukagua karakana hiyo, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO - (TEMESA)

MKUTANO WA 11 WA KUTATHMINI SEKTA YA AFYA WAFANYIKA ZANZIBAR

 Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt,Jamala Adam Taibu akizungumza katika Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.
 Muakilishi wa W,H,O Zanzibar Dkt,Ghirmany Andermichael akizungumza katika Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.
 Katibu Mkuu Wizara ya  Afya Asha Ali Abdalla akitoahotuba yake katika Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akitoa hotuba ya ufunguzi katika Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufungua  Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud katikati akiwa na Naibu Waziri Wizara ya Afya Harusi Saidi Suleiman(kushoto yake)na Viongozi mbalimbali katika Picha ya pamoja katika hafla ya Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.
 Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt,Jamala Adam Taibu akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Ufunguzi wa Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.
 Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Afya waliohudhuria katika Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.
Mtaalamu wa masuala ya Afya ya Uzazi kutoka shirika la UNFPA Zanzibar Batula Abdi akitoa mchango wake katika Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.


RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AFUNGUA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LEO UKUMBI WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikagua gwaride maalum llililoandaliwa kwa ajili ya Ufunguzi wa Bunge la Afrika Mashariki katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga, alipowasili katika viwa vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.(Picha na IKULU)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga wakiingia katrika ukumbi wa Mkutano kwa ajili ya Ufunguzi.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Afrika Mashariki lililofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)
Baadhi ya wabunge wa bunge la Afrika Mashariki wakisikiliza hotuba  ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  amesema kuwa suala la kupambana na rushwa lina umuhimu mkubwa katika maendeleo ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa ikizingatiwa kwamba vitendo hivyo vinazorotesha uchumi na maendeleo.

Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Chukwani mjini Zanzibar wakati akizindua Mkutano wa Nne wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambapo kwa mwaka huu unafanyika hapa Zanzibar.

Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alieleza kuwa kuwepo kwa Mswada wa rushwa katika mkutano wa Bunge hilo mwaka huu kuna umuhimu mkubwa kwani utasaidia katika kupambana na vitendo vya rushwa ambavyo vimekuwa vikiathiri sana uchumi na maendeleo ya nchi na wananchi wake.

Amesema kuwa Mkutano huo ambao katika Miswada yake ambapo miongoni mwao kutakuwepo Mswada huo ambao utajadiliwa unakwenda sambamba na juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na nchi wanachama katika kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa na uhujumu wa uchumi.

Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika jitihada zake za kukomesha vitendo vya rushwa imeunda Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kwa lengo la kushughulikia suala zima la kupambana na rushwa.

Alisema kuwa juhudi hizo zinaendelea kwa mashirikiano ya pamoja na wananchi hatua ambayo imepelekea Mamlaka hiyo kuweza kupiga hatua kubwa.

Aliongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli imeongeza juhudi zaidi katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa kwa kuweka mikakati mbali mbali.

Alisema kuwa Serikali zote mbili ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeimarisha usimamizi wa sheria na kuongeza Bajeti katika sekta ya sheria sambamba na kuongeza wataalamu ili kusimamia kesi zinazohusiana na rushwa.

Hivyo, Rais Dk. Shein alisema kuwa juhudi hizo zitasaidia sana pamoja na zile sheria zitakazotungwa na Bunge hilo ambazo zote kwa pamoja zinaweza kufikia lengo lililokusudiwa.

Aidha, Rais Dk. Shein alisisitiza suala zima la kuzingatia umhimu wa maadili na tabia njema katika kutekeleza majukumu ya viongozi hao hasa katika wakati huu ambao teknolojia na mifumo ya maisha imebadilika na baadhi ya wakati hupelekea Wabunge kufanya vitendo ambavyo vinahitaji umakini na maamuzi ya busara ili waweze kulinda hadhi yao.

Alisema kwamba inatia moyo kuona kwamba Ukanda wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa Kanda zinazoongoza katika ukuaji mzuri wa uchumi duniani ambapo katika mwaka wa 2017 uchumi ulikuwa kwa asilimia 4.6 ikilinganishwa na mwaka 2016 ambapo uchumi ulikuwa asilimia 4.4.

Alieleza kuwa hayo ni mafanikio makubwa ambayo yanapaswa kuendelezwa  huku akisisitiza kuwa kutokana na Afrika ya Mashariki kuwa na zaidi ya watu milioni 162 hali hiyo inapelekea kuwepo kwa soko kubwa la bidha mbali mbali pamoja na huduma muhimu.

Pia, alieleza kuwa Afrika Mashariki ina ardhi kubwa yenye kilomita za mraba 1.82 milioni ambayo ni vyema rasilimali hiyo ikatumika vizuri ili iweze kuleta tija kwa nchi wanachama.

Vile vile, Rais Dk. Shein alipongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na nchi wanachama katika kuhakikisha kwamba Jumuiya hiyo inafikia malengo yake hasa katika suala zima la kukuza uchumi, uimarishaji wa utawala Bora, uismarishaji wa sheria pamoja na uimarishaji wa amani na utulivu.

Rais Dk. Shein ameeleza kutiwa moyo sana na juhudi za Umoja huo za kuimarisha lugha ya Kiswahili ambayo hivi sasa imekuwa ni lugha inayounanisha wanachama katika shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii.

Alieleza kuwa Zanzibar inathamini sana fursa iliyopewa ya kuwa Makamo Makuu ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki na kuahidi kuwa fursa hiyo itaitumia vizuri ili kuhakikisha malengo yaliokusudiwa yanafikiwa.

Dk. Shein alimuhakikishia Spika wa Bunge hilo Martin Ngonga kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza na kuitangaza lugha ya Kiswahili na kufahamisha kwamba kupitia Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) imekuwa ikiandaa makongamano mbali mbali ya Kiwahili ambayo yanajumuisha wataalamu kutoka sehemu mbali mbali duniani.

Alisema kuwa hatua hiyo ina lengo la kukiimarisha na kukuza matumizi sahihi ya Kiswahili fasaha kwa kuangalia kwamba Zanzibar ndio chimbuko la Kswahili sanifu.
Rais Dk. Shein alisema anaamini kwamba Jumuiya hiyo inaweza kuwa eneo muhimu la kiuchumi duniani, hivyo jitihada zaidi zinahitajika katika utekelezaji wa malengo makuu yaliopangwa na Jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kushajiisha uekezaji, kuendeleza sekta ya utalii, viwanda, elimu na kutilia mkazo  suala zima la kuongeza ajira na kuimarisha miundombinu.

Pamoja na hayo, Rais Dk. Shein aliitaka Jumuiya ya Afrika Masharik kupitia Bunge lake hilo kuchukua jitihada katika kupambana na vitendo mbali mbali vyenye kuathiri uchumi ikiwemo suala zima la utakasishaji wa fedha.

Vile vile, Rais Dk. Shein alieleza haja ya kuendeleza teknolojia ya Habari na Mawasiliano huku akiwasisitiza Wabunge wa Bunge hilo kufanya kazi kwa mashirikiano mazuri na Mabunge mwengine ya nchi wanachama ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi mzuri zaidi.

Aidha, Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kulipongeza Bunge hilo kwa kufanya mkutano wake huo hapa Zanzibar na yeye kupata fursa kwa mara ya pili kuufungua mkutano huo na kutoa shukurani zake kwa kuweza kukaa pamoja na chombo hicho muhimu cha kutunga Sheria.

Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumpongeza Spika wa Bunge hilo kwa  kuchaguliwa kuwa Spika wa tano na kuweza kukiongoza chombo hicho huku akiwapongeza Wajumbe wote wa Bunge hilo kwa kuchaguliwa kukiongoza chombo hicho muhimu katika Afrika Mashariki.

Pamoja na hayo, alisifu utaratibu wa Bunge wa kufanya mikutano katika miji ya nchi wanachama jambo ambalo linapelekea wananch kufahamu majukumu ya chombo hicho ambapo alisema utaratibu huo unaenda sambamba na falsafa ya kuweka umoja na mshikamano kwa watu wa Afrika Mashariki.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein ameleza kufurahishwa kwake na moja ya Miswada ambayo itajadiliwa katika Bunge hilo ambayo ni pamoja na Mswada wa vita dhidi ya rushwa, masuala ya kijinsia,ulemavu pamoja na mada nyengine zitakazojadili vitendo vya ugaidi vilivyojitokeza nchini Kenya.

Nao Wabunge hao walitoa shukurani kwa Rais Dk. Shein kwa heshima kuwa aaliyowapa ya kwenda kuzindua mkutano wao huo na kueleza kufurahishwa kwa kiasi kikubwa na hotua aliyoitoa ambayo imewapa matumaini makubwa.

Nae Spika wa Bunge hilo Martin Ngoga alitoa shukurani kwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na uongozi wake chini ya Spika wa Baraza hilo Zubeir Ali Maulid kwa mashirikiano mazuri wanayoyapata ambayo ni chachu katika utekelezaji wao wa kazi.

Aidha, Spika huyo alieleza umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika Umoja huo pamoja na Wajumbe wa Bunge hilo na kueleza mikakati waliyoiweka katika kuhakikisha lugha hiyo inatumika vyema ndani ya Bunge hilo pamja na nchi zote za Jumuiya hiyo.

Nae Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid alieleza mashirikiano mazuri yaliopo kati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Bunge hilo Afrika Mashariki na kueleza mafanikio makubwa yaliopatikana katika mashirikiano hayo.
Katika uzinduzi huo wa Mkutano wa (EALA) ambao unatarajiwa kuwa wa siku 10 moja, viongozi mbali mbali walihudhuria akiemo Spika wa Bunge hilo Martin Ngoga, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Wenyeviti na Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulid, Spika Mstaafu Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wajumbe wa Bunge hilo la Afrika Mashariki.