Matokeo chanyA+ online




Tuesday, June 30, 2020

MWENYEKITI WA CCM RAIS MAGUFULI ARUDISHA FOMU YA MAOMBI YA KUOMBA RIDHAA YA KUTEULIWA KUWA MGOMBEA



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya Ukumbi wa NEC mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kurudisha Fomu ya Maombi ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya kuzijaza Fomu hizo na kupita wadhamini katika mikoa yote ya Tanzania.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilisha na kusaini Fomu za maombi ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya kuzijaza Fomu hizo na kupita wadhamini katika mikoa yote ya Tanzania.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilisha na kusaini Fomu za maombi ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya kuzijaza Fomu hizo na kupita wadhamini katika mikoa yote ya Tanzania.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilisha na kusaini Fomu za maombi ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya kuzijaza Fomu hizo na kupita wadhamini katika mikoa yote ya Tanzania.


Jumla ya wanachama Milioni 1,023, 911 wa  Chama cha Mapinduzi(CCM) wamejitokeza kumdhamini Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Magufuli katika fomu za kuwania kupitishwa na Chama hicho kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu 2020.



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Fomu zake alizopata wadhamini mara baada ya kuzikabidhi kwa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa katika Ukumbi wa NEC makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya  kuzipokea Fomu  hizo katika ukumbi wa CCM Makao Makuu Dodoma, Katibu Mkuu Bashiru Ally amesema kuwa wanachama hao wajitokeza kwa wingi na kuonyesha kuwa na imani na Dkt. Magufuli

Dk. Bashiru amesema, jumla ya wanachama Milioni 1,023, 911 walijitokeza kumdhamini  Rais Magufuli kutoka mikoa 32 na jumuiya zake tatu za Wazazi, Vijana na Wanawake.
 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Fomu zake alizopata wadhamini mara baada ya kuzikabidhi kwa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa katika Ukumbi wa NEC makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachama mbalimbali wa CCM waliokusanyika nje ya Ofisi za Makao Makuu ya CCM White House jijini Dodoma mara baada ya kurudisha Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachama mbalimbali wa CCM waliokusanyika nje ya Ofisi za Makao Makuu ya CCM White House jijini Dodoma mara baada ya kurudisha Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachama mbalimbali wa CCM waliokusanyika nje ya Ofisi za Makao Makuu ya CCM White House jijini Dodoma mara baada ya kurudisha Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachama mbalimbali wa CCM waliokusanyika nje ya Ofisi za Makao Makuu ya CCM White House jijini Dodoma mara baada ya kurudisha Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi wengine wa Chama cha Mapinduzi, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula, Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally Kakurwa mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa NEC katika Makao Makuu ya CCM White House jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Sekretariet ya Chama cha Mapinduzi mara baada ya kuzungumza katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.

 


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wanachama wa CCM mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama White House jijini Dodoma. PICHA NA IKULU

 


WAZIRI KIGWANGALLA AAGIZA KUUNDWA KWA KAMATI UANZISHWAJI WA PORI LA AKIBA NA WMA YA ZIWA NATRON.


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kuundwa kwa Kamati itakayopitia na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya namna bora ya kushughulikia mgogoro wa uanzishwaji wa Pori la Akiba na WMA ya Ziwa Natron.

Kamati hiyo itahusisha watalaam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wajumbe kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mkuu wa wilaya ya Longido, Ngorongoro,  Monduli na wajumbe kutoka katika vijiji vyenye mgogoro kuzunguka eneo la ziwa Natron.

Dkt. Kigwangalla ameunda Kamati hiyo leo jijini Arusha wakati wa kikao cha kujadili uanzishwaji wa Pori la Akiba na WMA ya Ziwa Natron, kikao kilichowahusisha wawakilishi wa wananchi kutoka kutoka katika maeneo yenye mgogoro wilayani Longido, viongozi wa mila wa kabila la Masai na viongozi wa serikali wa wilaya ya Longido.

Amesema Kamati hiyo itafanya kazi ya kupitia maeneo yote ya vijiji yenye mgogoro na kutoa mapendekezo yatakayoainisha matumizi bora ya ardhi kwa wananchi wanaoishi kuzunguka Ziwa Natron pamoja na kuzingatia maslahi mapana ya Taifa kwa kulinda uhifadhi na ikolojia ya ziwa Natron ambalo ni muhimu duniani kwa mazalia ya ndege aina ya Flamingo.


DKT. MPANGO: SIJARIDHISHWA NA ENEO LILIPOJENGWA SOKO LA KIMATAIFA KIGOMA


Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina, akifafanua jambo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (katikati), alipotembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Kimkakati  Mnanila, lililopo wilayani Buhigwe mkoani Kigoma


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, kutafuta eneo jipya, kubwa, lenye hadhi ya kujengwa soko la Kimataifa badala ya eneo linapojengwa Soko la Kimkakati la Kimataifa la Mnanila, lililoko katika mpaka wa Burundi na Tanzania.

Maagizo hayo ameyatoa wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa soko hilo la Kimkakati la Kimataifa akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayopatiwa fedha na Serikali.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isodor Mpango (Mb), akitoa maelekezo kwa uongozi wa Wilaya kuhusu soko la Mnanila lililopo wilayani Buhigwe mkoani Kigoma alipotembelea ujenzi wa mradi wa soko hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Rashid Mchata


Dkt. Mpango alisema kuwa hajaridhishwa na ubora wa ujenzi wa soko hilo ambalo linatarajiwa kuwa la kimataifa kutokana na kujengwa katika eneo dogo, na ujenzi wake uko chini ya kiwango ikilinganishwa na kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kilichotumika kujenga miundombinu ya mradi huo uliolenga kuchochea shughuli za biashara na kiuchumi kati ya wananchi wa Tanzania na Burundi.

Alisema kuwa atatuma timu ya wataalamu kuchunguza na kufanya ukaguzi maalaum ili kubaini watu waliohusika kushauri soko hilo lijengwe katika eneo lisilokuwa na hadhi pamoja na kuchunguza matumizi ya fedha za mradi huo zilivyotumika.

Mhandisi wa Wilaya ya Buhigwe Bw. Zakaria Cosmas, akielezea taarifa ya maendeleo ya mradi kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kushoto, alipotembelea na kukagua majengo ya Soko la Kimkakati Munanila, lililopo wilayani Buhigwe mkoani Kigoma. Wengine ni baadhi ya viongozi wa Wilaya na Mkoa wa Kigoma


Aidha, Dkt. Mpango alisema iwapo utabainika udanganyifu wa matumizi ya fedha hizo hatua kali zitachukuliwa na kwa kuanzia ataanza na ofisini kwake kujua vigezo vilivyotumiwa na wataalam wake walioishauri Wizara iidhinishe matumizi ya kiasi hicho cha fedha huku wakijua kuwa eneo linalojengwa mradi huo halina sifa ya kujengwa miundombinu

“Mtafute eneo lingine tofauti ambalo linaweza kweli  kubeba dhana ya Soko La kimataifa ili tukuze biashara  na wananchi wetu wapate kipato na Halmashauri iweze kulipa na kugharamia maendeleo ya nchi yetu lakini kwa mawazo madogo hivi hatuta sogea” alisema Dkt. Mpango.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Bw. Anosta Nyamwoga, (kushoto) na Mhandisi wa Wilaya ya Buhigwe Bw. Zakaria Cosmas, wakichukua kero mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Wakazi wa Kata ya Mnanila mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isodor Mpango (Mb), (hayupo pichani), alipotembelea eneo la ujenzi wa mradi wa Soko la Kimkakati Mnanila lililoko wilayani Buhigwe, mkoani Kigoma


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina, amesema atashughulikia kwa haraka dosari zilizobainika katika ujenzi wa Soko la Mnanila. Ambalo malengo yake ni kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza kipato cha Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe na mkoa wa Kigoma kwa ujumla ili iweze kujitegemea.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilayaya Buhigwe Bw. Anosta Nyamwoga, alimuahidi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwamba Halmashauri yake itatafuta eneo jipya kwa ajili ya ujenzi wa soko kubwa la kimataifa kwa haraka.

Wananchi wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Kimkakati Mnanila, lililopo wilayani Buhigwe mkoani Kigoma

 

Taswira ya baadhi ya majengo ya Soko la Kimkakati Mnanila, lililopo wilayani Buhigwe mkoani Kigoma yanavyoonekana kwa sasa ambayo yote kwa pamoja yamegharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.3. Soko hilo linatarajiwa kuimarisha biashara kati ya Tanzania na Burundi


Awali, baadhi ya wakazi wa Kata ya Mnanila, akiwemo Bw. Amon Ndabita, walieleza kutoridhishwa na ujenzi wa soko hilo na kwamba hawajashirikishwa katika kupendekeza eneo linalofaa kwa ujenzi wa soko hilo la kimkakati la kimataifa ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni 2.3 zinazotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango chini ya radi wa kuziwezesha Halmashauri kujitegemea kimapato.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza na Wananchi wa Mnanila, alipotembelea na kukagua maendeleo ya  Ujenzi  wa Soko la Kimkakati Mnanila, lililopo wilayani Buhigwe mkoani Kigoma


Katika hatua nyingine, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alimpa muda wa siku 15 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Bw. Anosta Nyamwoga, kuwalipa mamalishe, vibarua, mafundi waliojenga Soko hilo la Kimkakati la Kimataifa Munanila ambao wamelalamika mbele yake kutolipwa fedha zao tangu mwezi Julai mwaka 2019.

Mkazi wa Mnanila wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, Bi. Letisia Kidugwa, ambaye ni mama lishe katika Soko la Kimkakati la Kimataifa Mnanila, akimweleza Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu kutolipwa zaidi ya shilingi milioni 2.5 na wakandarasi wanaojenga soko hilo tangu mwaka 2019, ambapo Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Bw. Anosta Nyamwoga, kulipa madai ya mama huyu, mafundi pamoja na vibarua ndani ya siku 15

 

(Picha na Josephine Majura – KIGOMA)



Na Josephine Majura, Peter Haule-KIGOMA


“Nakuagiza uwalipe fedha zao zote wanazodai na utajua utakako zitoa fedha hizo, uwalipe na wewe utawadai wakandarasi wakulipe fedha zako kwani ulitakiwa kuhakikisha wananchi hawa wanapata haki zao” alisisitiza Dkt. Mpango

Dkt. Mpango yuko katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma kukagua miradi ya maendeleo inayopewa fedha na Serikali ambapo ametembelea Miradi ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Munzeze, Ujenzi wa Jengo la Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe na Ujenzi wa Soko la Kimkakati la Kimataifa Mnanila.


JAJI NDIKA - SHERIA YA WANAWAKE NA WATOTO ZITAFSIRIWE ZIENDANE NA WAKATI

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt. Jaji Gerald Ndika amewataka Majaji na Mahakimu kutafsiri sheria zinaohusu masuala ya wanawake na watoto ili ziendane na mazingira ya sasa katika kuendesha mashauri yanayohusu masuala la unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.

Akizunguza wakati wa Mafunzo ya Haki za Binadamu na Unyanyasaji hususani kwa  wanawake na watoto, yanayofanyika Mjini Bagamoyo Mkoa wa  Pwani Jaji Ndika   alisema  kuwa sheria zilizopo kwa kiwago kikubwa zinajitosheleza kinachotakiwa jinsi ya kuzitafasiri,  hivyo Majaji na Mahakimu watoe tafsiri ambayo inaendana na mazingira ya matukio yalivyo.


Washiriki wa Mafunzo ya Mafunzo ya Haki za Binadamu , unyanyasaji  na ukatili wa kijinsia  hususan kwa  wanawake na watoto  (wa kwanza kulia) ni Jaji wa Mahakama ya Rufani  Tanzania, Mhe.Rehema   Kerefu na (wa pili kulia) ni Jaji wa Mahakama ya Rufani  Tanzania, Mhe. Dkt. Gerald Ndika wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.(wa tatu kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Joaquine De Mello.


Jaji Ndika ambaye ni mshiriki katika mafunzo hayo,  alisema kuwa moja ya faida zake ni kuwaandaa wawezeshaji katika eneo hilo ili kusaidia Mahakama ya Tanzania, Majaji wa Mahakama ya Rufani,Majaji wa Mahakama Kuu, Mahakimu,watumishi mbalimbali ambao wanatoa maamuzi juu ya  vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa wanawake na watoto kuwa na umahiri.

‘‘Matukio haya yanatokana na mambo mengi ikiwemo mila potofu pamoja na  uelewa wao mdogo, wanaona kumpiga mke au mtoto ni jambo la kawaida na ana haki ya kufanya hivyo. Lakini ubora wa mafunzo haya yatasaidia kupata wakufunzi ambao wataenda kuwapa wengine elimu juu ya kuweza kupambana na ukatili na unyanyasaji wa wanawake na watoto,’’ alisisitiza Jaji Ndika. mafunzo hayo, alisema  ni ya mara ya tatu kufanyika yakiwa  ni endelevu katika kutoa elimu hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Joaquine De Mello akifungua rasmi mafunzo hayo, alisema kuwa  yana lengo la  kuwawezesha watoa maamuzi kuwa na uweledi zaidi  wa kutoa  haki na pia kuielimisha jamii  juu ya haki zao za msingi na tatizo la unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ambalo limekithiri.



Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Sehel, na (kushoto) ni Mwenyekiti wa TAWJA Mhe. . Joaquine De Mello na baadhi ya washiriki  wakifuatilia kwa karibu mafunzo hayo.

Aliongeza kwamba kumekuwa taarifa nyingi zinazotolewa na vyombo vya habari pamoja na wanajamii ambao wamejitokeza wazi kutoa matukio mbalimbali   juu ya suala hilo. Pia tafiti mbalimbali ambazo zimefanywa hivyo wamegundua kuwa matukio mengi ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia yanafanywa wahusika  wanaotuhumiwa kuwa  ni familia au ndugu wa karibu.

Alisema kuna mapungufu katika jamii kama vile utamaduni wa kutokuwa na utayari wa kusimamia na kuyapigia kelele  tatizo hilo,  ikiwa  ni sababu mojawapo ya unyanyasaji na ukatili huo.

‘‘Kupitia mafunzo haya kama watoa maamuzi tunataka wapate jicho la kipekee shauri linapokuja mbele yako mara moja unapata picha kuwa hili ni la kikatili na unalipa nafasi yake na hii itasaidia katika kuandaa taarifa ya matukio haya kwa usahihi, ikiwemo kuna takwimu ambazo tunazihitaji ili kujua nguiu gani ya ziada inahitajika katika kusimamia jambo hili,’’ alisema Jaji De Mello.

Mshiriki mwingine wa mafunzo hayo, ambaye Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine,iliyopo Jijini Dar es Salaam Mhe,  Hanifa Mwingira alisema jamii inapaswa kuona kuwa vitendo hivyo ni vibaya na kila mtu anapaswa kusema ‘ukatili sasa basi na mtoto wa mwenzako kuwa ni mtoto wako na hupaswi kumfanyia ukatili,’.



Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakijadiliana kwa pamoja mambo yanayohusu mafunzo hayo.

Mwingira alifafanua kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa viongozi wa dini ambao  watawaelimisha  waumini wao, wakiwemo  Wenyeviti wa vijiji, kata pamoja na mitaa na Maafisa wa Ustawi wa Jamii, Polisi, Magereza na wadau wengine wa  sharia.

Mafunzo hayo yanayoendelea Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani yalihudhuriwa na Majaji Wataafu kama vile Mh. Jaji Salum Massati ambaye anashiriki kama mtoa mada,

Jumla ya washiriki 26 wanapatiwa   mafunzo juu ya masuala ya unyanyasaji na ukatili kijinsi. Mafunzo hayo yameanza Juni 27, mwaka huu na yatamalizika Julai Mosi,  mwaka huu.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AANZA ZIARA YA KICHAMA KUSINI UNGUJA


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya Mkoa wa Kusini Unguja alipowasili katika ukumbi mdogo wa SUZA Tunguu leo Juni 30,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa kusini Unguja.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya Mkoa wa Kusini Unguja katika ukumbi mdogo wa SUZA Tunguu leo Juni 30,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa kusini Unguja.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM MKoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akizungumza nao katika ukumbi mdogo wa SUZA Tunguu leo Juni 30,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa kusini Unguja.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya Mkoa wa Kusini Unguja katika ukumbi mdogo wa SUZA Tunguu leo Juni 30,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa kusini Unguja.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM MKoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akizungumza nao katika ukumbi mdogo wa SUZA Tunguu leo Juni 30,2020. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya Kichama Mkoa wa kusini Unguja.

KAMPUNI YA VEGRAB ORGANIC FARMING LTD YAZINDUA SOKO LA PILIPILI KICHAA SINGIDA



 Mkurugenzi wa Kampuni ya Vegrab Organic Farming LTD,Gladness Nyange,akizungumzia kilimo cha pilipili kichaa wakati wa uzinduzi wa zao hilo uliofanyika Kitongoji cha Kipunda,Kjiji cha Mtunduru,wilaya ya Ikungi, mkoani Singida mwishoni mwa wiki.

Kampuni ya  Vegrab Organic Farming LTD kwa kushirikiana na kampuni inayouza matrekta ya AGRI-COM wamezindua soko la zao la pilipili kichaa litakaloweza kuwaongezea kipato wananchi wa Kitongoji cha Kipunda,Kjiji cha Mtunduru,wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo,Gladness Nyange alifafanua kwamba masoko ya zao la pilipili kichaa ni makubwa sana isipokuwa kinachotakiwa ni uzalishaji mkubwa na wenye ubora zaidi.

“Mimi nina imani na zao hili nyie mnaliona hivi lakini ni zao ambalo litatupeleka mbali sana kupitia juhudi ile tuliyoanzanayo tuendelee nayo,kwani masoko ni makubwa sana lakini yanataka uzalishaji mkubwa lakini pia wenye ubora.”alisisitiza Mkurugenzi huyo.
 Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,Gurisha Msemo akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa Kipunda AMCOS, Omari Nyuda, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Zao la pilipili baada ya kuvunwa.


Kwa mujibu wa Nyange Mkoa wa Singida unaweza kuwa kituo kikubwa sana cha uzalishaji wa zao la pilipili kichaa na siyo kwa Tanzania tu bali hata kwa Afrika Mashariki na kwamba endapo wataweka jitihada wanaweza kuongoza katika Afrika katika uzalishaji wa zao hilo.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa mazingira pamoja na ardhi iliyopo katika Mkoa wa Singida inadhihirisha wazi kabisa kwamba pilipili itakayozalishwa kwenye maeneo yote ya Mkoa wa Singida itakuwa nzuri kuliko inayotoka sehemu yeyote ile ya Tanzania na hata Afrika Mashariki.
 Zao la pilipili baada ya kuvunwa.

 Wakulima wa zao la pilipili wakiwa shambani.
 Mkulima Mohemed Salehe,  akizungumzia kilimo hicho.


Akizindua mnada wa soko hilo la pilipili kichaa,Afisa ushirika wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Gurisha Msemo alisema Kampuni inayonunua zao hilo imesaini mkataba wa miaka mitatu na kwa msimu wa 2019/2020 kampuni hiyo itanunua pilipili kichaa iliyoiva kwa bei ya shilingi 4,500/=kwa kilo moja na shilingi 5,000/= kwa pilipili mbichi kwa kilo moja.

Aidha Msemo alitoa sababu za soko la zao hilo kuzinduliwa katika Kata ya Mtunduru kuwa ni kutokana na idadi kubwa iliyopo ya wakulima wa zao hilo ambapo kati ya wakulima 159 waliolima pilipili kichaa Mkoani Singida,110 ni wakulima kutoka wilaya ya Ikungi.
Mkulima Mwanaidi Iddi, akizungumzia kilimo hicho.

Na Jumbe Ismailly,  Ikungi

Akimkaribisha kuzindua soko hilo,Mwenyekiuti wa Kipunda Amcos,Omari Nyuda huku akitumia kauli mbiu isemayo ongeza tija pilipili inalipa,alisisitiza juu ya uzalishaji bora wa zao hilo ili waweze kuendelea kupata fedha nyingi zaidi.

“Zao hili ambalo limekuwa na tija kwetu na kauli mbiu tunasema ongeza tija pilipili inalipa mradi na msimu umeshazinduliwa,kwa hiyo yetu ni mapesa,tupate pesa tuongeze uzalishaji tuongeze zao ubora zaidi tuweze kusonga mbele zaidi.”alifafanua Nyuda ambaye ni mwenyekiti wa Kipunda Amcos.