Matokeo chanyA+ online




Saturday, August 13, 2022

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MKOANI IRINGA











Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wananchi wa Mkoa wa Iringa alipowasili katika Uwanja wa CCM Samora kwa ajili ya kuhutubia Mkutano wa Hadhara tarehe 12 Agosti, 2022. 

 





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Iringa kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa CCM Samora tarehe 12 Agosti, 2022.





 

OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI ZINGATIENI MASLAHI MAPANA YA NCHI

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb) akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (hawapo pichani) wakati wa kikao chake cha kujadili utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam


Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas D. Ndumbaro (aliyevaa miwani) wakati wa kikao cha Waziri huyo na Menejimenti ya Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb) (aliyesimama mbele katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kikao kazi na Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam


Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damasi Ndumbaro (aliyeketi mbele meza kuu) wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam



Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damasi Ndumbaro akiteta jambo na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt Luhende (kushoto) baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Serikali yaitaka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) izingatie maslahi mapana ya nchi katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku ya kusimamia, kuratibu na kuendesha mashauri ya madai na usuluhishi kwa niaba ya Serikali na taasisi zake ili kuhakikisha kuwa inatetea maslahi ya Serikali na wananchi ndani na nje ya nchi

Hayo yameelezwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) wakati wa kikao kazi baina yake na Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali iliyoongozwa na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Nalija Luhende kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwa na majadiliano na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo ili kujadili utekelezaji wa majukumu ambapo kikao hicho kilifanyika jijini Dar es Salaam.

Dkt. Ndumbaro alisema kuwa ni muhimu Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ihakikishe inaiwakilisha vema Serikali na taasisi zake kwenye mashauri ya madai na usuluhishi ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata inachostahili kwa maslahi mapana ya taifa na wananchi wake kwa ujumla ili kulinda hadhi ya Serikali 

“Wizara hii imeshikilia haki ya wananchi; amani na utulivu wa nchi; na uwekezaji nchini; hivyo ni muhimu kuhakikisha wananchi wanapata haki yao kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi zilizopo; nchi inavutia wawekezaji kwa kuwahakikisha amani na utulivu; pamoja na kuwa na miongozo stahiki inayohusu mikataba katika uwekezaji ili kulinda maslahi mapana ya taifa,” amefafanua Dkt. Ndumbaro

Pia, ameongeza kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inaendesha mashauri ya madai na usuluhushi kwa maslahi mapana ya taifa la Tanzania hivyo ni muhimu kwa watumishi kutekeleza majukumu kwa kuweka uzalendo mbele; kuzingatia taaluma; maadili ya kazi; weledi na uzoefu kwenye maeneo ya migogoro, usuluhishi, na majadiliano ikiwa ni pamoja na kushirikisha wadau ili kuhakikisha kuwa Serikali inashinda na kunufaika na uwepo wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Ofisi hiyo kwa niaba ya Menejimenti, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Nalija Luhende amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Ofisi hiyo mwaka 2018 hadi mwezi Juni mwaka 2022; Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeendesha jumla ya mashauri 5,905 ambapo kati ya hayo mashauri 5,768 ni ya madai na mashauri 137 ni ya usuluhishi.

Dkt. Luhende ameongeza kuwa ili kufikia azma ya kupanua wigo wa utendaji wa Ofisi hiyo na kuongeza ukaribu katika kuhudumia wananchi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ina Ofisi 17 ambazo zimefunguliwa kwenye mikoa yote yenye masjala za Mahakama Kuu ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na kwenye mikoa ya Dodoma; Mtwara; Iringa; Ruvuma; Tanga; Kilimanjaro; Arusha; Kigoma; Mara; Mwanza; Kagera; Shinyanga; Tabora; Rukwa; Mbeya; na Morogoro.

Dkt. Ndumbaro yuko Dar es Salaam kwenye ziara ya kikazi ambapo ataonana na kuzungumza na taasisi za Wizara hiyo ikiwemo Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali; Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Ofisi ya Mwendesha Mashtaka; Tume ya Haki za Binadamu; Wakala wa Vizazi na Vifo; na Taasisi ya Msaada wa Kisheria ili kujadili utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo kwa Serikali kwa niaba ya wananchi 

 

Rais Samia Suluhu Hassan aweka jiwe la Msingi Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kama ishara ya kuweka Jiwe la Msingi Mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege Iringa. Hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi imefanyika katika Mtaa wa Mapanda kata ya Nduli Mkoani Iringa tarehe 12, Agosti, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mtaa wa Mapanda mara baada ya kuweka jiwe la Msingi Mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa tarehe 12, Agosti, 2022.


 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akiongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha maandalizi ya Mkutano wa Kawaida wa 42 wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika Agosti 17 & 18,2022 Jijini Kinshasa,nchini DRC






 

WAZIRI JAFO AELEKEZA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UPANDAJI MITI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ‘STAMICO na
Mazingira At 50’ iliyoambatana na tukio la upandaji miti katika eneo la wazi
Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akizindua Kampeni ya ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana
na tukio la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo (katikati) akishiriki mazoezi ya viungo na viongozi wengine kulia
Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Doto Biteko na Mkuu wa Mkoa Dodoma Rosemary
Senyamule wakati wa uzinduzi wa ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana
na tukio la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).



Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa uzinduzi wa
‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana na tukio la upandaji miti katika eneo
la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akzungumza wakati wa wakati
wa uzinduzi wa ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana na tukio la upandaji
miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).