Matokeo chanyA+ online




Saturday, August 21, 2021

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan apokea Ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020.







 

 


Mkuu wa Mkoa Singida, Dkt.Binilith Mahenge akisisitiza jambo wakati Wajumbe wa Kamati ya Siasa  Mkoa  wa Singida walipo kuwa wakikagua mradi wa Chuo cha Ufundi VETA jana unaojengwa wilayani Ikungi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Alhaji Juma Kilimba (wa tatu kushoto) akiongoza kamati hiyo kukagua mradi wa vyoo Zahanati ya Puma. Kulia ni Muuguzi Mkuu wa Zahanati hiyo Lucy Tathi.


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akizungumzia mradi wa ujenzi wa vyoo Zahanati ya Puma.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Puma, Samuel Mdimu akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo.
Wananchi wa Puma wakishuhudia ukaguzi wa mradi huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Denis Nyiraha akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa  vyoo vya Zahanati ya Puma. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita, akichangia jambo kwenye ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa vyoo  vya Zahanati ya Puma. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Singida, Dkt.Binilith Mahenge.


Muonekano wa baadhi ya majengo ya Zahanati ya Puma.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, Iddi Maalim akichangia jambo wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa vyoo  vya Zahanati ya Puma.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida Diana Chilolo akichangia jambo kwenye ukaguzi wa miradi hiyo.
Ukaguzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Kipumbuiko ukiendelea.Mradi huo umegharimu Sh. 359 Milioni na wananchi wameanza kunufaika nao.
Kaimu Afisa Tarafa Ikungi, Yahaya Njiku (kulia) akiwaelekeza jambo Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kipumbuiko, Debora Malali (kushoto) na Afisa Tawala  Wilaya ya Ikungi Dijo Ndangeki wakati wa Ukaguzi wa mradi wa maji wa Kijiji hicho.

Ukaguzi wa mradi wa maji Kijiji cha Kipumbuiko ukiendelea. Kulia ni Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Wilaya ya Ikungi Mhandisi Hapeness Liundi.
Wananchi wa Kijiji cha Kipumbuiko wakishuhudia ukaguzi wa mradi wao wa maji.


Ukaguzi wa madarasa Shule ya Sekondari Ikungi ukiendelea.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Shee, akihimiza umuhimu wa kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona wakati wa ukaguzi ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Issuna.
Ukaguzi wa maabara Shule ya Sekondari Ikungi ukiendelea.
Ukaguzi wa madarasa Shule ya Msingi Ikungi ukiendelea.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ikungi akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa madarasa.
Ukaguzi ujenzi wa Chuo cha Ufundi  VETA  ukiendelea.
  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Gutete Mahava akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi ujenzi wa Zahanati Kata ya Issuna.
Fundi rangi akiwajibika kwenye mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Issuna.
Ukaguzi ujenzi wa ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Issuna  ukiendelea.
Wananchi wa Kata ya Issuna,watumishi wa Wilaya ya Ikungi na wajumbe wa kamati ya siasa wakiwa kwenye ukaguzi wa mradi ujenzi wa Zahanati ya kata hiyo.
        Mwenyekiti wa Kikundi cha Ufugaji Nyuki cha Save The Bee cha Issuna, Mrisho Amiry akisoma taarifa ya mradi huo mbele ya kamati hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akizungumzia mradi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo mbele ya wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa kabla ya ukaguzi wa ujenzi wa hospitali hiyo.


Na Dotto Mwaibale, Singida


KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida imekagua miradi ya maendeleo wilayani Ikungi na kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo hususani eneo la maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika chini ya Serikali ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya afya.

Pia kupitia ukaguzi wa utekelezaji wa miradi hiyo CCM kwa namna ya kipekee imeguswa na mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Issuna iliyopo Wilaya ya Ikungi ambao unakwenda kutatua changamoto za wananchi wa eneo hilo za kusafiri umbali mrefu kwenda kata zingine kufuata huduma za afya.

Akizungumza jana wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa maagizo ya ilani ya CCM, Mwenyekiti wa kamati hiyo Alhaji Juma Kilimba alihimiza sekta hiyo na nyingine kuhakikisha inakamilisha miradi yote kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa.

"Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo nchini kote hivyo nawaomba wasimamizi wa ujenzi wa miradi hii kuwa wazalendo katika matumizi ya fedha hizo,". alisema Kilimba.

Katika hilo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Gutete Mahava akitoa taarifa ya ujenzi wa Zahanati hiyo alisema mradi huo ulibuniwa mwaka 2014 na upo Kijiji cha Issuna 'A'

Alisema zahanati hiyo ikikamilika itatoa huduma kwa wananchi wa vijiji vitano vya Issuna 'A, Issuna 'B', Ng'ongosoro, Nkuhi na Tumaini na kuwa ujenzi wake upo katika hatua za mwisho kukamilika.

Mahava alisema kuwa walipokea Sh.50 Milioni kutoka Serikali kuu na ununuzi wa vifaa vyote umefanyika na tayari Wizara ya Fedha imetenga Sh.8 Milioni kwa ajili ya dawa na vitendanishi.

Hata hivyo kamati hiyo imeomba hatua za haraka zichukuliwe ili kuharakisha ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo ambao bado mradi wake unasuasua kutokana na changamoto za kifedha -kutokana na umuhimu wake mkubwa kwa idadi kubwa ya watu wanaozunguka wilaya hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza baada ya kukamilika kwa ziara hiyo aliwashukuru wakurugenzi na wakuu wote wa wilaya zote kwa kusimamia miradi hiyo.

"Niwashukuru wakurugenzi wote na wakuu wa wilaya kwa umoja wenu na kusimamia miradi hii ambayo inatumia fedha nyingi kutoka Serikalini,".  alisema Mahenge.

Akizungumzia mradi wa maji wa Kipumbuiko Dkt. Mahenge aliwata wahusika kutoangalia faida zaidi badala yake wazingatie utoaji wa huduma kwa wananchi na kuutunza.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro aliishukuru kamati hiyo na akatumia nafasi hiyo kuelezea mikakati ya maendeleo ya wilaya hiyo hususani katika sekta ya kilimo hasa cha zao alizeti na mpunga ambao unalimwa kwa wingi maeneo ya Iyumbu.

Alitaja eneo lingine watakalo liangalia ili kupata mapato ni kwenye madini, ufugaji wa nyuki na miradi mingine.

Kamati hiyo katika wilaya hiyo ilikagua mradi wa ujenzi wa madarasa mawili na ofisi moja Shule ya Sekondari Ikungi, ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Msingi Ikungi, ukamilishaji wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo, ujenzi wa mradi wa maji Kipumbuiko, ujenzi wa matundu saba ya vyoo Zahanati ya Puma, ufugaji wa nyuki  (Kikundi cha Save The Bee Issuna, ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Issuna, ujenzi wa Chuo cha Ufundi cha VETA na ukamilishaji wa ujenzi wa maabara Shule ya Sekondari Ikungi.

Friday, August 20, 2021

VYAMA VYA SIASA 11 VYATOA MSIMAMO KATIBA MPYA, VYAUNGANA NA RAIS SAMIA

 

Na Said Mwishehe

Viongozi wa Umoja wa Vyama vya Siasa ambavyo havina wawakilishi Bungeni wamesema wataendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu kuhusu kuwataka wananchi kuwa na subira katika mchakato wa Katiba Mpya.


Umoja huo umesema wao msimamo wao katika mchakato wa Katiba mpya mbali ya kumuunga mkono wanappendekeza mchakato uanzie ulipoishia awali kwa wananchi kupiga kura ya maoni kwani mapendekezo ya Katiba mpya yalishafanyika ,hivyo hawaoni sababu ya kuanza upya kwani ni matumizi mabaya ya fedha za umma.


Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha DP Abdul Mluya amesema msimamo wao wanaunga mkono kauli ya Rais lakini hawaoni sababu mchakato wa Katiba Mpya kuanza upya na badala yake uanzie ulipoishia.


"Kuna uwezekano wa kuendeleza pale walipoishia katika mchakato wa katiba mpya kuliko kuanza upya uandishi wa katiba kwa maana utaweza kupoteza gharama kubwa fedha ambazo zingeweza kuendeleza miradi mingine nchini.


“kwenye mchakato wa katiba tuliishia kwenye kura ya maoni (katiba pendekezwa) kwahiyo msimamo wetu tunasema kwamba kutokana na Dunia kuingia kwenye wimbi la ugonjwa wa korona uliopelekea kuyumba kwa uchumi hatuoni tija na afya kwa watanzania kama tutakwenda kuwaingiza kwenye suala uandishi wa katiba mpya kama ile iliyotumia zaidi ya bilioni 200.


"Kuna haja ya msingi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutuleta kura ya maoni tupige kura ili kupata katiba ambayo imeshatumia fedha za wananchi kuliko kuanza uppya mchakato wa kuandika katiba mpya.Haya sisi ndio maoni yetu na yaheshimiwe kama nasi tunavyoheshimu mawazo ya wengine,"amesema.


Aidha amesema wanamuunga mkono Rais Samia katika chanjo ya COVID-19 ambayo ni hiyari sio lazima,lakini vyama hivyo vinawahamasisha wananchi kupata chanjo hiyo kwa lengo la kukabiliana na janga la ugonjwa huo.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha ADC, Bw.Doyo Almas amewataka viongozi na wananchi kwa ujumla kuacha tabia ya kuikosoa chanjo ya kujikinga na Uviko -19 kwani chanjo hiyo inatolewa kwa hiari na haina madhara yoyote.


Doyo amesema  Rais kwa busara zake ameruhusu kutoa mwanya kwa Watanzania wanaotaka na wasiotaka lakini yeye alikuwa ni miongoni mwa waliotaka na wakachanja na sisi viongozi tumemuunga mkono Rais katika chanjo ya Uviko kwasababu suala la afya linamuhusu mtu mmoja mmoja lakini kama taifa ukipoteza nguvu kazi ya taifa lazima upoteze harakati za kukuza uchumi.


Kuhusu Katiba mpya, Doyo amesisiti vyama hivyo 11 wanataka mchakato wa  Katiba uanze ulipoishia ili kuokoa fedha, maana wanaodai Katiba sasa wengine walikuwepo wakati wa mchakato wa awali  wa  Katiba inayopendekezwa ambayo ipo.


"Nchi imeingia gharama kubwa katika mchakato umekwenda na umefikia hapo.Kama wananchi wanataka Katiba basi twendeni tukaanzie hapo.Sisi vyama 12 tunaomba serikali sikivu ombi letu tuendelee na mchakato ambao awali ulikuwa umeishia,"amesema Doyo.


Katibu Mkuu wa Chama cha ADC, Doyo Almas akizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dar es Salaam kuhusiana na mchakato wa katiba mpya na mwenendo wa utoaji chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa corona
Katibu Mkuu wa Chama Cha DP, Abdul Mluya akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusiana na mchakato wa katiba mpya na mwenendo wa utoaji chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa Corona
Viongozi wa Vyama vya Siasa visivyo na uwakilishi Bungeni wakizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dar es Salaam kuhusiana na mchakato wa katiba mpya na mwenendo wa utoaji chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa korona

Wednesday, August 18, 2021

CCM SINGIDA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI MKALAMA


  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba (katikati) akizungumza na wajumbe wake wakati wakikagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama jana. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko na kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo ya Mkalama Sophia Kizigo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Lucy Shee akizungumza kwenye ukaguzi huo.
Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakikagua Hospitali ya Wilaya ya Mkalama.
Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakikagua ujenzi wa nyumba za wakuu wa idara.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akizungumza kwenye ukaguzi huo.
Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ukiendelea.

Mjumbe wa Halmashauri  Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita akizungumza kwenye ukaguzi huo.

Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakikagua ujenzi wa mradi wa maji.
Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakikagua ujenzi wa mradi wa maji.
Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakipokea taarifa ya ukarabati wa vyumba vya  maabara Shule ya Sekondari ya Gumanga.
Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakikagua ukarabati wa vyumba vya maabara Shule ya Sekondari ya Gumanga.
Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakikagua ujenzi wa  vyoo.
 


Na Dotto Mwaibale, Mkalama.

Kamati  ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida imefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama  na kukagua utekelezaji wa Ilani kwenye miradi ya maendeleo.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Alhaji Juma Kilimba  akiwa ameambatana na wajumbe wake aliipongeza Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa utekelezaji wa miradi.

Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba sita za wakuu wa idara, ujenzi wa uzio kuzunguka ofisi za Halmashauri urefu wa mita 750, ujenzi wa madarasa mawili na vyoo ,matundu 12 Shule ya Sekondari Gumanga, ukamilishaji wa vyumba viwili vya maabara Sekondari ya Mpambala, mradi wa maji Kijiji cha Nkungi.

Mradi mingine iliyotembelewa na kamati hiyo ni upanuzi wa wodi ya watoto kwa gharama ya Sh.180 milioni, wodi ya wanawake 160 milioni na wodi ya wanaume 160 milioni katika Hospitali ya Wilaya.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisikitishwa na ukarabati wa vyumba vya maabara katika Shule ya Sekondari Chemchemi ambavyo vimejengwa chini ya kiwango ukilinganisha na vile vilivyokarabatiwa kwa Sh.25 milioni  katika Shule ya Sekondari ya Gumanga licha ya kutolewa Sh.35 milioni kwa kila shule kwa ajili ya ukarabati huo.

Alisema Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo hivyo kuna kila sababu ya kuzitumia vizuri kwa manufaa ya wananchi.

Katika ziara hiyo viongozi mbalimbali walikuwepo wakiwemo wakuu wa idara wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo ya Mkalama Sophia Kizigo.

Leo  kamati hiyo itafanya ziara ya namna hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida

UPANUZI WA HOSPITALI TEULE YA MAKIUNGU MKOANI SINGIDA KUGHARIMU SH.10 BILIONI


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) akipata taarifa wakati wa ziara yake ya kukagua Hospitali Teule ya Makiungu ambayo ipo Wilaya ya Ikungi na Mkoa wa Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge, akizungumza katika ziara hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Jerry Muro, akizungumza katika ziara hiyo.
Hapa ukaguzi wa Chuo cha Ufundi cha VETA kinachojengwa wilayani Ikungi ukifanyika.
Ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA kinachojengwa wilayani Ikungi ukifanyika.
Ukaguzi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi ukifanyika.
Moja ya jengo la Hospitali ya Wilaya ya Ikungi likiwa katika hatua za kukamilika.

Na Dotto Mwaibale, Singida


Upanuzi  wa Miundombinu ya  Hospitali Teule ya Makiungu ambayo ni msaada mkubwa kwa wananchi wa Wilaya ya Ikungi na Mkoa wa Singida kwa ujumla mkoani hapa ambao unaendelea unatarajia kugharimu zaidi ya Sh.10. Bilioni.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Stephen Samanii, wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge wakati wa ziara yake ya kukagua hospitali hiyo iliyoanzishwa Novemba 6,1954, na Askofu Patrick Winters, Mmisionari Mpalotini. 

Alitaja baadhi ya majengo yanayotarajiwa kujengwa kuwa ni pamoja na jengo la hudumu za nje (OPD),wodi nane zenye uwezo wa kuwa na vitanda 350, jengo kubwa la upasuaji lenye vyumba sita vya upasuaji kwa wakati mmoja, ukumbi wa mikutano na ofisi za utawala.

Alisema ujenzi huo unatarajiwa kufanyika kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa.

Katika taarifa yake hiyo Dk.Samanii aliiomba Serikali kuisaidia hospitali hiyo msaada wa dharura wa ‘oxygen concentrator’ 10 zisizopungua zenye uwezo wa kuhudumia watu wawili kila moja kwa wakati mmoja.

Pia ameomba msaada wa mitungi ya gesi 20, kwa maelezo kwamba wagonjwa wenye changamoto za kupumua wanaongezeka kila siku hivyo bila ya kupata mitungi hiyo watashindwa kuwahudumia wagonjwa.

“Tunaomba ofisi yako kupitia kwa mganga mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ya Ikungi, mtusaidie upatikanaji wa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia kunusuru maisha ya wananchi”. alisema.

Aidha,ameomba wapatiwe misamaha ya kodi na kuondolewa kodi ya ongezeko la thamani (VAT), na ushuru wa forodha katika vifaa vya ujenzi, mashine na vifaa tiba.

“Pia vifaa vya usafi (sanitary equipment) vikiwemo vyoo vya kukalia na masinki yake,beseni za pekee,vifaa vya bafuni. na marumaru za square metres 23,000 kwa ajili ya ujenzi unaoendelea. Huo utakuwa mchango mkubwa sana wa serikali yetu katika ujenzi huu wa huduma za afya kwa wananchi wetu”,alisema.

Vile vile Dk.Samanii ameiomba Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) iruhusu mapema  mashine,vifaa tiba na vya ujenzi vilivyokwama bandarini hapo ili kazi hiyo ya ujenzi iweze kuendelea.

“Tunawashukuru kwa namna ya kipekee wafadhili wa nje ya nchi kupitia kwa PD Alessandro Nava na Dk.Manuela Buzzi,.kwa kukubali maombi ya Askofu kufanya kazi hii ya kihistoria,”.alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Binilith Mahenge akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo aliwashukru wafadhili wanaofanya upanuzi wa hospitali hiyo na kuwataka washirikiane na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ikungi jambo litakalosaidia kupunguza hama kumaliza kero zitakapokuwa zikijitokeza.

“Jambo jingine nawaomba kabla ya kuagiza vifaa au kitu cho chote kutoka nje ya nchi hakikisheni mnaishirikisha ofisi ya mkuu wa wilaya ili waweze kupewa taratibu za kupata  msamaha wa kodi au mwingine wowote. Ninawapongeza  kwa uamuzi wenu mzuri wa kuiunga mkono serikali katika kuboresha sekta ya afya”,alisema Dk.Mahenge.

Wakati huo huo,Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Jerry Muro,alisema milango ya ofisi yake itakuwa wazi kwa ajili ya kushirikiana na wafadhili na wadau wa maendeleo ndani ya wilaya hiyo. 

Katika ziara hiyo wilayani Ikungi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge alikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, Hospitali Teule ya Makiungu na Chuo cha Ufundi VETA.