Matokeo chanyA+ online




Monday, May 31, 2021

AJENDA KUU YA SERIKALI NI KUJITEGEMEA KATIKA UZALISHAJI MBEGU - WAZIRI MKENDA


Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akikagua vitendea kazi vya kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO wakati alipofanya ziara ya kikazi Jijini Arusha,  tarehe 30 Mei 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akikagua ghala la kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO wakati alipofanya ziara ya kikazi Jijini Arusha,  tarehe 30 Mei 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mbegu (TASTA) Ndg Bob Shuma akisisitiza jambo wakati akizungumza mbele ya Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO wakati alipofanya ziara ya kikazi Jijini Arusha,  tarehe 30 Mei 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO Tanzania Ndg Clive Mugadza wakati alipofanya ziara ya kikazi Jijini Arusha,  tarehe 30 Mei 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO Tanzania Ndg Clive Mugadza, Mkurugenzi Mtendaji wa jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mbegu (TASTA) Ndg Bob Shuma pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya SEED.CO wakati alipofanya ziara ya kikazi Jijini Arusha,  tarehe 30 Mei 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mkurugenzi wa kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO Tanzania Ndg Clive Mugadza wakati alipofanya ziara ya kikazi Jijini Arusha,  tarehe 30 Mei 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO Tanzania Ndg Clive Mugadza wakati alipofanya ziara ya kikazi Jijini Arusha,  tarehe 30 Mei 2021.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha

Katika kuendeleza ushirikiano na Sekta binafsi, ambalo ni jukumu la kisheria la Serikali kuhamasisha sekta binafsi katika uzalishaji wa Mbegu Bora, Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda katika ziara yake Jijini Arusha, leo tarehe 30 Mei 2021 ametembelea moja ya kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO

Waziri Mkenda pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao wa Wizara ya Kilimo Ndg Nyasebwa Chimagu wamepata fursa ya kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kampuni hiyo binafsi hasa katika suala zima la uchakataji na utunzaji wa Mbegu Bora unavyofanywa na kampuni hiyo kutoka hatua za awali Mbegu zinapotoka shambani, zinapopokelewa, kuchakatwa, kupimwa na kupakiwa tayari kwa kumfikia mkulima.

Katika ziara hiyo Waziri Mkenda amesema kuwa moja ya ajenda kuu ya Wizara ya Kilimo ni kuhakikisha nchi inazalisha mbegu za kutosha za kilimo kupitia sekta binafsi kadhalika Mamlaka ya Mbegu ya Serikali (ASA) ili kufikia hatua ya kujitosheleza katika uzalishaji mbegu na kuanza kuuza nje ya nchi.

Amesema kuwa serikali inahimiza Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) pamoja na Taasisi zote zinazojihusisha na utafiti hususani wa mbegu kuhakikisha kuwa zinazendelea kufanya utafiti wa mbegu bora na zitakazo ongeza tija katika kilimo.

“Tunataka mtu aweze kuzalisha kiasi kikubwa zaidi kwa Hekari moja ili nguvu ya mkulima iwe inazaa matunda makubwa na vilevile itatusaidia sana kwenye masoko kwa sababu ukizalisha kwa wingi hata kama bei ya mazao imeshuka lakini kipato kinakuwa kikubwa” Amekaririwa Prof Mkenda

Waziri Mkenda amesema kuwa pamoja na juhudi za serikali za kutumia taasisi ya utafiti (TARI) na mamlaka ya Mbegu (ASA) ambayo ina kazi ya kuchukua mbegu bora na kuzalisha kwa wingi ili kuzipeleka kwa mkulima lakini pia serikali inafanya kazi kwa karibu na sekta binafsi ikiwemo kampuni ya mbegu ya SEED.CO

Prof Mkenda ameipongeza kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO kutokana na uzalishaji wa mbegu bora ambazo zimekuwa na matokeo mazuri kwa wakulima ambapo amewahakikishia hitaji lao kubwa la kukodi mashamba ya serikali kwa ajili ya uzalishaji mbegu bora linafanyiwa kazi kwa haraka iwezekanavyo.

“Lakini nimewaahidi endapo watajenga maabara kubwa ya kisasa kwa ajili ya shughuli za mbegu hapa Tanzania, nitajitahidi kuhakikisha kuwa wanapata mashamba makubwa angalau mawili kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mbegu” Amesema Mkenda

Amewasihi kuongeza zaidi uzalishaji wa mbegu ikiwa ni pamoja na kuanzisha uzalishaji wa mbegu bora za mazao mbalimbali badala ya Nafaka na Mbogamboga pekee, Kwa kufanya hivyo kutakuwa na uwezekano wa kuongeza mbegu bora na zenye tija kwa wakulima nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mbegu (TASTA) Ndg Bob Shuma amepongeza Serikali kwa kuamua kulichukulia kwa msisitizo swala la uzalishaji wa mbegu bora nchini ambapo ameeleza furaha yake na kumuhakikishia Waziri wa Kilimo kuwa umoja huo unaendelea na mkakati madhubuti katika uzalishaji wa mbegu bora na kwa wingi.

Hata hivyo amerejea msisitizo wa Waziri wa Kilimo kuyaomba mashirika mengine nchini na nje ya nchi kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya mbegu ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa karibu na serikali kupitia taasisi ya TARI na ASA ili kuongeza ufanisi katika sekta ya mbegu.

Sunday, May 30, 2021

WAWEKEZAJI WAIOMBA SERIKALI KUDHIBITI UVAMIZI RANCHI ZA TAIFA


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (kulia) akiongea na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fredy Lowassa (kushoto) walipokutana katika kikao kilichoandaliwa na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kilichofanyika jijini Dodoma jana. Mbunge huyo alikuwa ni miongoni  mwa Wawekezaji waliohudhuria kikao hicho.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Sehemu ya Wawekezaji waliohudhuria kikao kilichoandaliwa na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) jijini Dodoma jana. 
 



Na Mbaraka Kambona,

 

Wawekezaji wa muda mrefu katika Vitalu vya Ranchi za Taifa wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kudhibiti uvamizi unaofanywa na baadhi ya Wananchi katika maeneo hayo kwani vitendo hivyo vimekuwa kikwazo kikubwa katika kuendeleza Sekta ya Mifugo nchini. 

Wawekezaji walisema  hayo kwa Waziri wa Mifugo na  Uvuvi, Mashimba  Ndaki alipokutana nao katika kikao kilichoandaliwa na Kampuni za Ranchi za Taifa (NARCO)  kilichofanyika jijini Dodoma jana. 

Wakieleza changamoto wanazozipata katika uwekezaji wao walisema kuwa pamoja na mambo mengine, suala la Wananchi kuvamia maeneo yao waliyowekeza linakwamisha kufanya shughuli zao za kuendeleza ufugaji wa kisasa. 

Mwenyekiti wa Wawekezaji hao, Jackson Mwasonga alisema kuwa wavamizi wanakwamisha shughuli zao na kuna wakati wanalazimika kutoa hela kwa wavamizi hao ili waweze kuchunga mifugo yao katika maeneo wanayomiliki kihalali. 

"Mhe. Waziri inafika wakati tunatoa hela ili tuweze kuchunga na kunusuru mifugo yetu,uvamizi unatishia maisha yetu na mali zetu, tunaomba mtangaze wavamizi waondoke ili tuweze kufanya ufugaji unaohitajika kwa amani," alisema Mwasonga. 

Projestus Gamasho, Mwekezaji katika Ranchi ya Kitengule, Mkoani Kagera alisema ranchi hiyo kwa sasa imevamiwa na tembo zaidi ya Mia Sita (600) na wameharibu miundombinu yote huku akiiomba Serikali kutoa msaada wa haraka kuwaondoa tembo hao. 

Mwekezaj wa Ranchi ya Uvinza, Kigoma, Benard Katamba  alisema wavamizi katika Ranchi hiyo sio tu wamechukua maeneo yao,  wanaiba mifugo yao kila wakati jambo ambalo linawakatisha tamaa ya kuendelea na ufugaji. 

Sisi Wawekezaji wa Ranchi ya Uvinza tumevamiwa haswa, mpaka sasa nimeshaibiwa ng'ombe 25 na mbuzi 150 na sina matumaini yoyote ya kuwapata, kwa kweli tunaomba msaada wa Serikali," alisema Katamba. 

Kufuatia hali hiyo, Mwekezaji katika Ranchi ya Misenyi, Mkoani Kagera, Nestory Lugakingira akitoa ushauri kwa Serikali alisema kuwa ili waweze kuishi kwa amani Serikali ione uwezekano katika yale maeneo yaliyovamiwa yagawiwe kwa wavamizi hao na sehemu itakayobaki waitumie kuendeleza mifugo yao na kuepuka migogoro na wananchi hao. 

Akitoa ufafanuzi wa hoja za Wawekezaji hao, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki alisema kuwa Serikali ipo pamoja na Wawekezaji hao na itachukua hatua kali kwa wale wote wanaovamia maeneo ya ranchi kinyume na Sheria. 

"Ninaelewa kwamba kuna maeneo ambayo Wananchi wanakaa na kuwaondoa itakuwa ni uvunjifu wa haki za binadamu, maeneo hayo tutayainisha na ili tuone kama tunataka kuendelea nayo au tukubali  maeneo hayo yawe na matumizi mengine," alisema Ndaki. 

Aidha, Ndaki alitumia fursa hiyo kuwahimiza Wawekezaji hao kuyatumia maeneo waliyowekeza kwa malengo yaliyokusudiwa huku akisema kuna baadhi ya Wawekezaji wamekuwa hawayatumii vizuri maeneo hayo jambo lililopelekea kuvamiwa. 

"Niwaombe kuanzia sasa mkayatumie maeneo hayo kwa malengo yaliyokusudiwa, mkafanye ufugaji wa kibiashara, mkifanya hivyo mtaweza kuainisha vizuri gharama za matumizi na faida mnayopata," alisisitiza Ndaki. 

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya NARCO, Paul Kimiti  alisema uvamizi unaoendelea unawaumiza Wawekezaji  na kuwakatisha tamaa huku akiiomba Serikali kuchukua hatua kudhibiti vitendo hivyo. 

Naiomba Serikali kuangalia uwezekano wa NARCO kuwa na Askari kama TANAPA, naamini watasaidia kudhibiti uvamizi huu kabla haujashamiri, na vitendo hivyo vitakoma," alisema Kimiti 

Lengo la kikao hicho kilichoandaliwa na NARCO ni kuongea na Wawekezaji hao kuhusu Tozo mpya ya pango ya kitalu itakayoanza kufanyakazi Julai 1, 2021 na kuwahimiza kuhuisha mikataba yao.


Saturday, May 29, 2021

WANANCHI WA MAFIA WAPATA HUDUMA ZA MADAKTAR BINGWA KUTOKA JAMII BORA



 0G8A4319.MOV.04_32_29_10.Still001.jpg

Mtaalam wa Afya kutoka Jamii Bora Dr Hanifa  akitoa malekezo kwa wanachi waliofika kupata huduma 

0G8A4335.MOV.04_35_47_06.Still001.jpg

Sehemu ya wananchi wa Kisiwa cha Mafia wakisubiri Kuonana na Madaktari Bingwa kutoka Mtandao wa Jamii Bora

Mbunge wa Jimbo la Mafia Mkoani Pwani ambae pia  NAIBU Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia Omary Kipanga ameupongeza Uongozi wa matandao wa Wataalam  wa Afya wa jamii bora kwa kuwezesha wananchi wa jimbo hilo kupata matibabu bure kutoka kwa madaktari Bingwa

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge Huyo, katika Ufunguzi wa kambi ya siku mbili ya matibabu bure kutoka madaktari Bingwa wa Mtandao wa JamiiBora ya Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mafia Juma Salum amesema kuwa ni jambo la faraja kwa wananchi kupata huduma hiyo

 Aidha ametoa wito  kwa wadau wengine wa afya kuiga mfano huo kwa lengo la kuwasaidia wananchi ambao wemekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kiafya

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Mtandao wa Jamiibora Dakta Abbas Mussa amesema lengo la kufanya hivyo ni kutekeleze malengo ya mtandao huo la kuhakikisha jamii inapata huduma kutoka kwa madaktari bingwa katika maeneo yao  ambayo yamekuwa hayafikiwi na wataalam hao

Aidha amesema kuwa katika mtandao huo kuna madaktari bingwa wa aina mbalimbali ikiwemo macho,afya ya akili,magonjwa ya akina mama na watoto pamoja na magonjwa mengine ambapo wataalam hao wa afya takribani 45 watakuwa kisiwani Mafia kwa lengo la kuwahudumia wananchi bure

Nae Amiri wa Jumuiya ya JAI Yahya Masao ameitaka jamii kuwa na muamko katika kuchangia damu kwa lengo la kusaidia makundi yenye uhitaji.

Wananchi wa Kisiwa cha Mafia wametoa shukrani zao kwa Mtandao wa wataalam wa Afya  Jamii Bora kwa huduma hizo ambapo zimewasaidia kutokusafiri hadi Jijini Dar es salaam ili kuonana na Madkari hao bingwa

WAZEE SINGIDA WAMPOKEA RASMI RC MAHENGE, WAAHIDI KUMPA USHIRIKIANO


Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge, akizungumza na Wazee wa Manispaa ya Singida   kwa mara ya kwanza tangu ahamishiwe akitokea mkoani Dodoma katika kikao kilicho fanyika leo. Kulia ni .Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Wilaya  ya Singida, Ramadhan Maughu na kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi,akizungumza kwenye kikao hicho.


Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Wilaya  ya Singida, Ramadhan Maughu akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Shabani Mkata, akizungumza kwenye kikao hicho. 
Kikao kikiendelea.
Baadhi ya Watumishi wa Manispaa ya Singida wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Mzee Shabani Mwangi, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mzee aliye jitambulisha kwa jina moja la Duki, akichangia jambo kwenye kikao hicho.



 Godwin Myovela na Dotto Mwaibale, Singida.

Baraza la Wazee Mkoa wa Singida limempokea rasmi Mkuu mpya wa Mkoa, Dkt. Binilith Mahenge na kuahidi kumpa kila aina ya ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.

Dkt. Mahenge ambaye kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliteuliwa na kuapishwa hivi karibuni kushika wadhifa huo kuchukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amestaafu.

Akizungumza na baraza hilo mkoani hapa, Dkt. Mahenge aliwaomba wazee hao kumpa ushirikiano ili kwa pamoja aweze kuongoza kwa ufanisi jahazi hilo lenye shabaha ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta mageuzi ya kiuchumi ndani ya mkoa.

"Singida ina kila kitu chema. Tuna Hali ya hewa nzuri inayokubali kila aina ya mazao...alizeti, ufuta, dengu, korosho na tunafuga sana, lakini zaidi tuna viwanda vya kutosha vya kukamua mafuta ya zao la alizeti," alisema Mkuu wa Mkoa.

Alihimiza kila mtu kwa nafasi yake likiwemo kundi la vijana, watendaji na wananchi wote kuwajibika kwa kuchapa kazi ili kupunguza au kuondoa kabisa adha ya umasikini.

Dkt. Mahenge pamoja na kumshukuru Rais Samia kwa kumuamini na kumkabidhi mkoa huo kikubwa alisisitiza ushirikiano hususani kwenye nyanja ya kuinua sekta ya kilimo-na hasa zao la alizeti.

Alisema anatarajia kuona mtazamo chanya katika mageuzi makubwa ya kilimo cha alizeti katika muktadha wa kuleta utajiri kwa kila mtu, kaya, jamii,  lakini pia kuigeuza Singida kuwa kimbilio la soko kama sehemu ya jitihada zilizopo katika kukabiliana na changamoto ya kitaifa ya uhaba wa mafuta ya kula.

Akieleza hali halisi ya zao hilo mkoani hapa kwa sasa, alisema changamoto kubwa inayokwamisha ustawi wake kwanza ni uhaba wa mbegu bora, lakini pia wakulima wengi wamekosa utaalamu stahiki kujua kanuni za kilimo chake.

Mahenge alisema kwa ushirikiano na watendaji wake waliopo watahakikisha wanaongeza nguvu katika eneo hilo na lingine la kutoa utambuzi kwa mkulima kumuwezesha kufanya Uchaguzi sahihi wa mbegu zinazotoa kiwango cha juu cha mafuta na zinazohimili magonjwa yatokanayo na visumbufu vya wadudu.

Katika hilo, mkakati mwingine uliopo ndani ya ofisi yake kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali za kilimo ni kuhakikisha mbegu hizo zinaanza kupatikana kwa wingi na kuwafikia wakulima kwa gharama nafuu.

"Tatizo lililopo ukilinganisha na mazao mengine alizeti haina Bodi ya uratibu na usimamizi ndio mana hata kasi ya ukuaji wake haiendi kwa ufanisi," alisema Dkt. Mahenge na akaongeza;

"Wakulima wengi wanapopeleka zao hili sokoni wanaonekana kama wamepunjwa sababu kubwa ni mbegu kukosa sifa na ubora wa kutoa mafuta mengi." 

Alisema, mathalani, mbegu bora ya alizeti ijulikanayo kama Hysun 33 ambayo hukomaa kati ya siku 90 na 110 kwa uwezo wa kutoa gunia 16 hadi 22 kwa heka, sawa na uwiano wa lita 29 hadi 31 bei yake bado ipo juu na wakulima wengi wanashindwa kumudu.

Awali, akizungumza kwenye mkutano huo uliobeba hotuba hiyo iliyoashiria mikakati, matarajio na mwelekeo wa vipaumbele kadhaa kwa niaba ya wazee, Mwenyekiti wa Baraza hilo Ramadhan Maughu alimhakikishia Mkuu wa Mkoa ushirikiano wa hali ya juu katika azma iliyopo ya kubadilii sura ya kiuchumi ya mkoa.

""Karibu sana Singida wazee wote mbele yako wamekukubali na wamekupokea tutakupa kila aina ya ushirikiano, mana hatukuzoea wala kuwahi kuitwa na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa yeyote..kwa utambuzi huu inaonyesha umelelewa vizuri," alisema Mwenyekiti huyo.

WAZIRI JAFO AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo (wa tatu kushoto) pamoja na viongozi mbalimbali akiongoza matembezi ya hiyari kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021 ambapo alimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akizungumza na wananchi katika eneo la Medeli kabla ya kuongoza zoezi la upandaji miti kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akipanda mti katika eneo la Medeli kabla ya kuongoza zoezi la upandaji miti kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.


  

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Medeli akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akiwa na Naibu Waziri Mhe. Hamad Chande na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Medeli ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akitoa neno la utangulizi wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Medeli ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.

Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na wananchi katika eneo la Medeli kabla ya kuongoza zoezi la upandaji miti kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akizungumza katika eneo la Medeli kabla ya kuongoza zoezi la upandaji miti kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.

DKT. MAHENGE AKUTANA NA VIONGOZI WOTE WA DINI MKOA WA SINGIDA, AJA NA MIKAKATI MIZITO KUPAISHA KILIMO CHA ALIZETI


 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge, akizungumza na viongozi wa dini mkoani hapa  kwa mara ya kwanza tangu ahamishiwe akitokea mkoani Dodoma katika kikao kilicho fanyika leo Kulia ni .Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi  Pascas Muragili na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.
Padre Thomas Mangi wa Kanisa Katoliki (RC)
Viongozi wa dini wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea..
Kikao kikiendelea.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waisalaamu (BAKWATA)  Manispaa ya Singida, Hamisi Kisuke, akizungumza kwenye kikao hicho.


Kaimu Sheikhe wa  Mkoa wa Singida, Issa Nassoro, akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu wa Baraza Kuu la Waisalaamu (BAKWATA)  Mkoa wa Singida, Sheikhe, Burhani Mlau, akizungumza kwenye kikao hicho.

Mchungaji Wilson Mkoma kuoka Kanisa la EAGT, akizungumza kwenye kikao hicho.
Jaji Mstaafu, Fatuma Masengi,akizungumza kwenye kikao hicho.
Kasisi Joseph Kense wa Kanisa la Anglikana, akizungumza kwenye kikao hicho.
Abdurahaman Hassan Naibu Amri wa Mkoa Jamaat Ansaari Sunna, akizungumza kwenye kikao hicho.


 
Godwin Myovela na Dotto Mwaibale, Singida.



Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Dini mbalimbali, ambapo pamoja na kuwaomba ushirikiano, alitumia jukwaa hilo kueleza mipango, mikakati na mwelekeo wa singida mpya katika muktadha chanya wa maendeleo.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika ofisini kwake mkoani hapa, Dkt. Mahenge pamoja na mambo mengine, aliwataka viongozi hao wa dini kumpa ushirikiano wa kutosha hususani kwenye eneo la kuongeza tija ya kilimo cha alizeti ili kuokoa fedha nyingi zinazotumiwa na serikali kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi.

"Nadhani tuanze na mkakati wa haraka wa kushusha gharama ya mbegu ya alizeti. Mbegu zinazozaa vizuri na kutoa mafuta mengi bei yake haikamatiki ipo juu sana," alisema Mkuu wa Mkoa.

Akifafanua hilo, alisema kama serikali na wadau watashirikiana katika kushusha gharama ya mbegu hiyo basi ni dhahiri mkoa huo ambao jiografia yake ni rafiki kwa zao hilo itakuwa ni jawabu la kupunguza au kumaliza kabisa changamoto iliyopo ya upungufu wa mafuta ya kula.

Alisema kwa sasa nchi inaagiza takribani Tani laki 5 za mafuta ya kula kila mwaka jambo linalogharimu na kuleta mtikisiko wa uchumi, na alisisitiza katika kuepusha hilo lisiendelee mkoa wa Singida haukwepeki.

"Naomba viongozi wangu wa dini mtuunge mkono nguvu kubwa ielekezwe kwenye ongezeko la uzalishaji wa alizeti,..sababu soko la mafuta ya kula ni la uhakika, na viwanda tunavyo vya kutosha. Suala la hii changamoto ya mbegu na agronomia tunaendelea kushughulika nayo kama mkoa ili kuwezesha viwanda kuwa na malighafi ya kutosha," alisema Dkt. Mahenge.

Hata hivyo alipongeza juhudi kubwa za aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Rehema Nchimbi kwa namna alivyosimamia uzalishaji wa zao la korosho na ameahidi kuendeleza zaidi zao hilo kwa ustawi wa uchumi wa wana-singida.

Katika hilo, Mkuu huyo wa Mkoa alihamasisha jamii kujenga utamaduni wa kula vyakula vinavyozalishwa ndani ya nchi ikiwemo korosho, dengu na ufuta ili kupanua zaidi wigo wa soko la ndani kuliko kutegemea soko la nje.

Awali, wakichangia hotuba yake kwa nyakati tofauti, mbali ya kupongeza mkakati mzuri wa serikali uliopo, hususani kwenye eneo la ongezeko la tija ya zao la alizeti, jukwaa hilo lilimsihi Dkt. Mahenge kuweka mkazo katika kuimarisha huduma za afya, ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, ukosefu wa dawa hospitalini, sanjari na kupandisha zaidi ufaulu kwenye sekta ya elimu.

Aidha, walimtaka aharakishe umaliziaji wa miradi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa iliyopo, Stendi Kuu ya abiria, umeme, maji na miundombinu ya barabara ambayo kasi yake sio ya kuridhisha na imegeuka kero kwa wananchi.

Pamoja na mambo mengine, walimtaka afuatilie serikalini kujua nini hasa kimekwamisha ujenzi wa Uwanja wa Ndege Singida, mkoa ambao ni wa kimkakati na upo jirani zaidi na makao makuu ya nchi huku tayari hatua za usanifu na upembuzi yakinifu kabla ya kuanza ujenzi wa Uwanja huo vilikwishafanyika.