Matokeo chanyA+ online




Thursday, March 28, 2024

 RAIS SAMIA AKIPOKEA RIPOTI YA (CAG) NA TAARIFA YA UTENDAJI KAZI WA (TAKUKURU) KWA MWAKA 2022/2023


"Ripoti hizi zilizotolewa hapa zinasaidia katika maboresho ya serikali kwa watumishi wa umma kwasababu ripoti zilizotolewa hapa tutakwenda kuangalia kwenye dosari na kufanya marekebisho na mwakani pengine hizi hazitajirudia na tutakuwa tumesogea.

Tunawashukuru sana CAG na TAKUKURU kwakuwa kazi hii inaimarisha utendaji ndani ya mashirika ya umma na kupunguza hasara...itafika pahali mashirika yetu hayatakuwa kwenye hasara na badala yale yataleta faida.

 

Tumesikia ongezeko la hati safi na hii ni kwasababu CAG anatoa hati hapa na watu wakipata wanakwenda kurekebisha na matokeo yake tuna 99% ya hati safi na 1% ndio hati chafu kwahiyo tunasinga mbele ripoti hizi zinatusaidia sana.

 

Ripoti hizi zinatusaidia kwenye kungeza ukusanyaji wa mapato na tumeona vipengele mbalimbali vya CAG na TAKUKURU kwamba wanasaidia kuziba ile mianya ya kupotea kwa fedha na rushwa na mapato kurudi serikali na hii inasiaida kuimarisha nidhamu katika matumizi ya serikali na utendaji kazi wetu.

 

Naipongeza TAKUKURU kwa ubunifu mpya wa uibuaji wa kero kwa kushirikiana na wananchi kwamba wanakwenda kule chini wanakaa na wananchi na wananchi wanasema na wao wanazichukua kero wnazipeleka taasisi husika zinafanyiwa kazi na hii inatusaidia kupunguza kero kwa wananchi na kutufanya serikali iwajibike ipasvyo.

Nimpongeze CAG kwa uibuaji wa mambo kadhaa na kupendekeza hatua za kuchukiliwa ingawa ametuhimiza kwamba utekelezaji uende kwa haraka na kwa kiwango kikubwa lakini yote hayo yanatusaidia kwenda kutekeleza yale maelekezo ambayo CAG na TAKUKURU wanayaibua huko wanapofanya kazi kuyaleta Serikalini.

 

Kwa ujumla nishukuru kazi kubwa sana inayofanywa na Taasisi hizi mbili na kwa mujibu wa katiba kazi yangu leo hapa ni kupokea ripoti ya CAG lakini safari haijaisha, katiba inanitaka ninapozipokea ndani ya muda fulani niwe nimezikabidhisha Bungeni nami nakuahidi nitafanya hivyo CAG.

 

Kwa upande wa taarifa za TAKUKURU tutazifanyia kazi ndani ya Serikali na maeneo yote yaliyoibuliwa tutayafanyia kazi ipasavyo.

 

Wakati taarifa zinawasilisha nilikuwa natizama sura za watu tumechoka kwelikweli nadhani kwasababu Alhmis lakini pia yaliyokuwa yakisemwa ni makubwa pia, lakini kuna swahum na kwaresma, sasa wale wa kwaresma karibu mnafunguka mnamaliza niwatakie Pasaka njema, twendeni tusherehekee Pasaka kwa usalama...wale wa swahum tuendelee hatupo mbali inatelemka kwa kasi...tunakwenda vizuri."


Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


#Na Haya Ndiyo Matokeo Chanya+

Tuesday, March 26, 2024

TPA NA EACOP WAFIKIA MAKUBALIANO KUIMARISHA BANDARI YA TANGA KWA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA AFRIKA MASHARIKI


Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeingia mikataba mitatu na East African Crude Oil Pipeline ( EACOP) Limited kwa ajili ya kuridhia kutumika kwa Bandari ya Tanga katika kutekeleza mradi wa kimkakati wa ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani, Tanga Tanzania.
Mikataba hiyo mitatu inahusisha kukodisha eneo la kujenga miundombinu ya kuhifadhi mafuta, kutumia eneo la maji katika Bandari ya Tanga na mkataba wa kufanya shughuli za Bandari ambapo TPA imetoa sehemu ya gati mita 200 kwa Mkandarasi wa mradi Kampuni ya BBN Ltd kwa ajili ya kuegesha vyombo vinavyotumika kupokea na kupeleka vifaa na mahitaji mbalimbali ya ujenzi wa Gati Maalum (Jetty) la kupokelea mafuta ghafi.
Mikataba hii ni ya muhimu katika utekelezaji wa mradi wa EACOP hususani katika sekta ya usafirishaji majini kwa kuzingatia kuwa TPA kwa mujibu wa Sheria imepewa jukumu la kusimamia maeneo yote ya fukwe na mwambao kwa ajili ya shughuli za kibandari.
Sherehe hizo zimefanyika katika Kata ya Sojo iliyopo Jimbo la Bukene, Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora na kuhudhuriwa na Wananchi na Viongozi wa Nchi za Tanzania na Uganda.

#NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+

NDEGE MPYA AINA YA BOENG 737 MAX 9, KUONGEZA UFANISI KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI WA ANGA- TANZANIA


Uwezo wa Abiria

Boeing 737 MAX 9 ina uwezo wa kubeba abiria kati ya 178 hadi 220, ingawa idadi halisi inaweza kutofautiana kulingana na usanidi wa ndege.

 

Ufanisi wa Mafuta

Moja ya sifa kuu za Boeing 737 MAX 9 ni ufanisi wake wa mafuta. Ndege hii hutumia teknolojia ya hali ya juu kama vile injini za kizazi kipya na kubuni la kukata asili la mabawa ili kupunguza matumizi ya mafuta. Hii inamaanisha gharama za uendeshaji zinapungua na pia inapunguza athari kwa mazingira.

 

Kiwango cha Upeo wa Ndege

Boeing 737 MAX 9 ina uwezo wa kufikia viwango vya juu vya ndege kwa umbali mrefu. Hii inamaanisha inaweza kufanya safari za muda mrefu bila kupata matatizo mengi.

 

Utendaji wa Juu

Ndege hii ina utendaji wa juu wa kushughulikia mazingira tofauti ya hewa na hali ya hewa. Hii ni muhimu kwa kuhakikisha usalama na faraja ya abiria wakati wa safari.

 

Tehama ya Juu

Boeing 737 MAX 9 inajumuisha vifaa vya kisasa vya teknolojia ya mawasiliano na vifaa vya burudani vya hali ya juu, kuhakikisha kuwa abiria wanapata uzoefu bora wa safari.

 

Usalama Ulioimarishwa

Baada ya matatizo ya usalama yaliyogunduliwa katika awamu ya awali ya Boeing 737 MAX, Boeing ilifanya marekebisho na uboreshaji kwenye mfumo wa udhibiti wa ndege na mafunzo ya marubani ili kuhakikisha usalama wa hali ya juu kwa abiria. Hii imeweka Boeing 737 MAX 9 katika viwango vya juu vya usalama.

 

Hizi ni baadhi tu ya sifa na uwezo wa Boeing 737 MAX 9, ndege ambayo inachukuliwa kama moja ya chaguo bora kwa mashirika ya ndege yanayotafuta ufanisi, utendaji, na usalama.


#NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+ 

 MAKAMU WA RAIS AMTEMBELEA WAZIRI MKUU MSTAAFU MSUYA






Thursday, March 21, 2024

 MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MRADI WA MAJI SAME MWANGA KOROGWE







Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo eneo la la Nyumba yaMungu Wilaya ya Mwanga wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024.

 





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika eneo la Nyumba ya Mungu Wilaya ya Mwanga kwaajiliya kutembelea na kukagua chanzo cha maji cha mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameagiza uongozi wa Wizara ya Maji pamoja na watendaji wa Wizara hiyo kuhakikisha miji ya Same na Mwanga inapatiwa huduma ya maji safi na salama kupitia mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe ifikapo mwezi juni mwaka huu 2024.

 

Makamu wa Rais amesema hayo wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo kilichopo eneo la Nyumba ya Mungu Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro. Amewataka watendaji wa Wizara ya Maji kujipanga vizuri kuwasimamia wakandarasi kwa kufanya kazi usiku na mchana ili adhma na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa juu ya mradi huo yaweze kutekelezwa.

 

Makamu wa Rais amesema wananchi wa maeneo hayo wamesubiri mradi huo kwa miaka 19 tangu ulipoahidiwa mara ya kwanza hivyo ni wakati wa kuhakikisha mradi huo unakamilika. Amemtaka Waziri wa Maji kutembelea mradi huo mara kwa mara ili kutambua changamoto na kuzitatua haraka iwezekanavyo.

 

Aidha Makamu wa Rais ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha wanalinda mazingira na chanzo cha maji ya mradi huo ili kuwa endelevu.

 

Wakandarasi wa Mradi huo wameahidi kufikia malengo yaliyowekwa ya kuhakikisha mradi huo unakamilika ifikapo mwezi juni mwaka huu 2024.

Tuesday, March 12, 2024

 TATHMINI YA MIRADI MIKUBWA YA KIMKAKATI TANZANIA CHINI YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

 

Miradi ya kimkakati nchini Tanzania, chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, inaleta mabadiliko makubwa na matokeo chanya katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hapa ni tathmini fupi ya maendeleo ya miradi hiyo:

 

Daraja la Kigongo – Busisi

Mafanikio, Mradi umefikia asilimia 75 ya utekelezaji, ukionyesha maendeleo makubwa.

Ujenzi wa daraja unachochea uchumi, kuongeza usafiri wa watu na bidhaa, na kuunda ajira.

Matarajio

Kukamilika kwake kutapunguza muda wa kuvuka Ziwa Victoria, kuboresha usafiri, na kupunguza msongamano wa magari.

Reli ya Kisasa (SGR)

Mafanikio, Asilimia 97.65 ya ujenzi umekamilika, na mkoa wa Pwani unapokea uwekezaji mkubwa.

Kuimarisha usafiri wa mizigo, kuunganisha na bandari kavu, na kukuza miundombinu ya reli.

Matarajio

Kupunguza msongamano wa mizigo, kusaidia uanzishwaji wa viwanda, na kuboresha soko la ndani.

 

Julius Nyerere Hydroelectric Power Plant (JNHPP)

Mafanikio, JNHPP inachangia asilimia 85 ya upatikanaji wa umeme, na kuongeza Megawati zaidi inatarajiwa.

Kutoa umeme wa uhakika, kuongeza upatikanaji wa umeme, na kuboresha huduma za nishati.

Matarajio

Kupunguza uchafuzi wa mazingira, kuimarisha usalama wa nishati, na kuwa na ziada ya Megawati.

Miradi hii inaonyesha dhamira ya serikali katika kuendeleza miundombinu na kutoa fursa za kiuchumi na kijamii. Huku ikiendelea, miradi hii inategemewa kuwa na athari Chanya  kwa maisha ya wananchi na uchumi wa nchi.


#NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+

Saturday, March 2, 2024

 MAFANIKIO YA SEKTA YA UJENZI KATIKA MKOA WA ARUSHA 


 Sekta ya Ujenzi imepata mafanikio makubwa katika Mkoa wa Arusha. Kupitia juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia TANROADS, kumekuwa na maboresho makubwa katika miundombinu ya barabara na madaraja.

 

Kulingana na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Mha. Reginald R. Massawe, kumekuwa na ongezeko la kilometa 53 za barabara za lami, ambapo mtandao wa barabara za lami umefikia kilometa 478.78 mwaka 2024. Barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami ni pamoja na Wasso-Sale, T/Packers-Bypass, na Kijenge-Usariver.


 

Mbali na hilo, zaidi ya kilometa 152 za barabara ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi kwa kiwango cha lami. Miradi mingine inayoendelea ni pamoja na Mianzini-Ngaramtoni Juu, Karatu-Kilimapunda, T/Packgers-Losinyai, Mbaunda-Losinyai, Mto wa Mbu-Selela, na Wasso-Loliondo.

 

Serikali imeanzisha pia mchakato wa ujenzi wa barabara mpya kama vile Arusha-Kibaya-Kongwa na Karatu-Mbulu-Haydom-Sibiti River-Lalago-Maswa. Ujenzi wa barabara ya Ngaresh-Enguik (Monduli Juu) km 11.66 kwa kiwango cha lami uko katika hatua za mwisho za kutangaza zabuni ya mkandarasi.


Miradi ya madaraja pia imekamilika ikiwa ni pamoja na Daraja la Nduruma na Daraja la Kimosonu. Zaidi ya taa 991 zimewekwa katika barabara mbalimbali za Arusha-Namanga, Arusha-Minjingu, Kijenga-Usariver, Makuyuni-Ngorongoro, Arusha Bypass, na T/packers-Losinyai.

 

Hizi ni hatua muhimu za maendeleo katika Sekta ya Ujenzi ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Mkoa wa Arusha.




#NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+