Matokeo chanyA+ online




Tuesday, May 23, 2023

MAKAMU WA RAIS KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA AfDB MISIRI











 

NAIBU WAZIRI PINDA ATAKA UWAJIBAKAJI UNAOZINGATIA SHERIA SEKTA YA ARDHI

 

 Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika tarehe 22 Mei 2023 mkoani Dodoma.


Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati wa kikoa cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara yake tarehe 22 Mei 2023 mkoani Dodoma

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara yake tarehe 22 Mei 2023 jijini Dodoma.

Naibu waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amesema watumishi wa sekta ya ardhi nchini wanao wajibu katika utendaji kazi na dhana nzima ya kuongeza ufanisi na tija kwa kuzingatia sheria.

"Tunahitaji nidhamu na miongozo mbalimbali ili kutoa huduma stahiki kwa watanzania.

 

Pinda aliyekuwa akimuwakilisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleio ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema hayo tarehe 22 Mei 2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendekeo ya Makazi.

 

Aidha, amesema mwajiri naye anao wajibu wa kuweka mazingira mazuri mahali pa kazi sambamba na kuwaheshimu watumishi na kuwaendeleza ili kuwezesha kutekeleza majukumu yao  ipasavyo.

 

Akigeukia suala la urasimishaji makazi holela, Naibu Waziri Pinda alisema mpango wa urasimishaji unafikia kikomo mwaka huu wa 2023 na makazi holela yanaendelea kushamiri huku miji ikikua kwa kasi.

 

Kwa mujibu wa Pinda aliyekuwa akimuwakilisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, kazi ya Baraza la Wafanyakazi ni kutumia mkutano huo wa Baraza kuishauri serikali juu ya mkakati mpya wa kuondoa makazi holela.

 

Amelitaka Baraza la Wafanyakazi kujadili kwa kina makadirio ya mipango ya matumizi  kwa mwaka 2023/2024  na kuweka mipango inayotekelezeka.

 

Pamoja na mambo mengine ametaka kuwekwa mikakati madhubuti kwenye masuala ya makusanyo ya kodi ya ardhi ambapo amesema wizara imekusanya bil 129 sawa asilimia 51.6 ya lengo jambo alilolieleza  halikubalikia.

 

Ameelekeza kila mkoa kuongeza kasi ya makusanyo ili kutimiza lengo lililowekwa na kuchukua hatua kwa wadaiwa wote sugu kutokana na muda wa msamaha wa rais kupita.

UHUSIANO WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI UKO IMARA

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akiongea na watumishi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi.Fatma Hamad Rajab.


Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi.   Fatma Hamad Rajab (kushoto) katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mei 22, 2023 jijini Pritoria

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (wa sita kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

 


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi.        Fatma Hamad Rajab (wa pili kulia) akiangali baadhi ya nyaraka zinazohusu Tanzania zilizopo katika Makumbusho ya Afrika Kusuni wakati wa ziara kwenye makumbusho hayo Mei 22, 2023 jijini Pritoria nchini Afrika Kusini.

 

.

 


 Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema uhusiano wa Tanzania na Afrika Kusini uko imara na unaendelea kukua siku hadi siku katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya Utamaduni.

Balozi Milanzi amesema hayo Mei 22, 2023 jijini Pritoria nchini Afrika Kusini wakati akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo ambao walifika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini humo kujitambulisha kuwa watakuwa kwenye ziara ya mafunzo yenye lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu na Afrika Kusini katika masuala ya Utamaduni na Sanaa.

 

“Ugeni huu sasa ni wa pande mbili za Muungano hasa kwenye eneo hili muhimu la Utamaduni. Utamaduni ni dhana pana zaidi, kuna suala la lugha, vyakula, mavazi. Mimi nimependa sana mwelekeo huu wa Serikali na wizara zetu za Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, sasa zinafanya vizuri kwenye masuala ya michezo, masuala na Utamaduni, karibuni sana hapa Afrika Kusini” amesema Balozi Milanzi.

  

Uhusiano huo mwema umedhihirishwa kwa mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili ambapo baadhi ya wajumbe kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wapo Afrika Kusini kwa ziara ya mafunzo yenye lengo la kubadilishana uzoefu katika kuendesha sekta za Wizara hiyo.

 

Kwa upande wake Mkuu wa msafara ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi.          Fatma Hamad Rajab amesema kuwa nchi zetu zinahitaji kushirikiana ili kutunza urithi wake kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

 

Aidha, mafunzo hayo pamoja na mambo mengine yanalenga kubadilishana ujuzi na kuboresha namna ya kuendesha Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika ili kuhifadhi, kulinda na kuendeleza historia ya nchi hizo mbili za Tanzania na Afrika Kusini. 

 

Monday, May 22, 2023

DK.MWINYI AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA QATAR KUJA ZANZIBAR









Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi  baada ya kuwasili jana usiku jijini Doha, Qatar  akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano mkubwa wa Jukwaa la Kimataifa la tatu la Uchumi utakaofunguliwa kesho. 

Katika ziara yake Rais Dk. Mwinyi leo asubuhi amekutana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Qatar Mhe. Muhamed Bin Ahmed Al-Kuwari na  wadau kutoka sekta binafsi ya Viwanda.

Dk. Mwinyi aliwakaribisha wafanyabiashara hao wakubwa kuwekeza zanzibar kutokana na fursa zilizopo pia aligusia eneo jipya la uwekezaji ambalo ni utalii wa kumbi za mikutano.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa ZIPA Shariff Ali Shariff alieleza umuhimu wa kukutana kwa Mabaraza ya uwekezaji ya Zanzibar na Qatar ili kuimarisha uhusiano zaidi.

Pia alielezea fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar  zaidi kwa upande wa utalii kwani ujenzi wa hoteli kubwa za kifahari unahitajika kutokana na soko la utalii kuongezeka.


Fursa nyingine alizowakaribisha kuwekeza ni ukodishaji wa visiwa vidogo.

Halikadhalika aliwafahamisha kwa undani fursa zilizopo katika sera ya uchumi wa Buluu ambayo imewagusa zaidi wawekezaji hao hasa suala la uchimbaji wa gesi na mafuta.

Eneo jingine ni shamba la Makurunge Bagamoyo ambalo ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar linalofaa kwa utalii na hata kilimo.


📆 22 Mei 2023


📍Doha, Qatar

Monday, May 15, 2023

KELELE NA MITETEMO INAUWA WATOTO NJITI 12,000 KWA MWAKA ULAYA PEKE YAKE

Shirika la Afya Duniani (WHO) limebainisha kelele kuwa ni mojawapo ya

kisababishi cha madhara katika maisha ya binadamu. Aidha, kwa mujibu

wa “European Environmental Agency” (EEA, 2018) kelele zimeainishwa kuwa

mojawapo ya visababishi vya vifo vya mapema vya watoto “Pre-mature death”

ambapo takwimu zinaonyesha takribani watoto 12,000 hufariki kila Mwaka

katika Bara la Ulaya”.

Katika nchi yetu changamoto ya kelele zinazozidi viwango vilivyoainishwa

na TBS zinatokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo

matumizi yasiyo sahihi ya teknolojia. Kwa siku za hivi karibuni, kelele

zimeongezeka kwenye maeneo ya kazi na hivyo kusababisha matatizo ya

kiafya ikiwemo kupoteza uwezo wa kusikia, matatizo ya uzazi, kupunguza

umakini katika mafunzo, ajali na kupungua uwezo wa kusikilizana.


Vyanzo vikuu vya kelele hizi ni kumbi za starehe hasa biashara za vileo (baa),

vyombo ya usafiri na usafirishaji (kama magari, ndege na treni), matumizi

ya teknolojia zilizopitwa na wakati kwenye viwanda vikubwa na vidogo

(Karakana za kuchomelea, ufyatuaji matofali, mashine za kusaga na kukoboa

nafaka), majenereta, matangazo ya biashara mitaani, shughuli za ujenzi, nyumba za ibada n.k.



SHERIA NA SERA ZINAZOONGOZA UDHIBITI WA

KELELE NA MITETEMO

Udhibiti wa kelele na mitetemo nchini unasimamiwa na Sheria mbalimbali

zikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 pamoja na

Kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Udhibiti wa Kelele na Mitetemo) za

Mwaka 2015; Sheria ya Usalama Kazini ya Mwaka 2003; Sheria ya Afya ya

Jamii ya Mwaka 2009; Sheria ya Jumuiya [Sura ya 337 Marejeo ya 2002];

Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa [Sura 204 Marejeo ya 2002] na Kanuni za

Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018; Sheria ya Ardhi [sura 113 Marejeo ya

Mwaka 2019] na Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007 pamoja na Kanuni

zake za Mwaka 2018.

Sheria na Kanuni hizi zimeelekeza shughuli zote zenye madhara zifanyike

mbali na makazi ya watu na hivyo shughuli zenye kelele kufanyika mbali na

makazi ya watu ili kupunguza madhara kwa afya ya binadamu na mazingira.




BARAZA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA (NEMC)

Katika kuhakikisha kelele na mitetemo zitokanazo na shughuli mbalimbali

zinadhibitiwa, Baraza litafanya yafuatayo:

a. Kuendelea na ukaguzi wa maeneo ya biashara na kutoa

maelekezo mbalimbali ikiwemo Amri na Ilani za kudhibiti kelele.

b. Kuanisha na kutangaza maeneo ambayo kelele haziruhusiwi

(Noise Control Zone).

c. Kusimamia uanishaji wa ramani za maeneo yenye kelele

zilizopitiliza na kuandaa Mkakati wa udhibiti.

Mwongozo wa Kitaifa wa Udhibiti Kelele na Mitetemo

d. Kufanya tafiti za mara kwa mara kubaini hali ya uchafuzi wa

mazingira utokanao na kelele na mitetemo.

e. Kutoa elimu kwa jamii na maafisa mazingira kuhusu majukumu

yao katika udhibiti wa kelele na mitetemo.

f. Kupokea taarifa za malalamiko yanayohusu kelele na mitetemo.




Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan aongoza Viongozi pamoja na Waombolezaji kuaga Mwili wa Marehemu Bernard Kamilius Membe, Karimjee Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2023

 




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2023

 




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa pole kwa Familia ya aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2023








Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Viongozi mbalimbali pamoja na Waombolezaji wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam kabla ya kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe tarehe 14 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na waombolezaji kabla ya kuwaongoza kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe katika viwanja vya Karimjee tarehe 14 Mei, 2023.