Matokeo chanyA+ online




Friday, May 31, 2019

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KATIKA SHEREHE ZA KUMWAPISHA RAIS WA MALAWI PROFESA ARTHUR MUTHARIKA

PMO_5532
 Waziri Mkuu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na , Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi, Ben Botolo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Chileka uliopo Blantyre Malawi kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi, Profesa  Arthur Peter Mutharika, Mei 31, 2019.
PMO_5541
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi,  Bw. Ben Botolo wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Chileka uliopo Blantyre nchini Malawi kuwakilisha, Rais Dkt John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi, Profesa, Arthur Peter Mutharika, Mei 31, 2019. 
PMO_5552
  Waziri Mkuu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na , Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi, Ben Botolo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Chileka uliopo Blantyre Malawi kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi, Profesa  Arthur Peter Mutharika, Mei 31, 2019. 
PMO_5563

PMO_5602

PMO_5609
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika wakati Rais huyo alipohutubia baada ya  alipoapishwa kwenye Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, Mei 31, 2019. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais huyo.
PMO_5660
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa zamani wa Malawi, Bakili Muluzi katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi Profesa Arthur Peter Mutharika zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, Mei 31, 2019.

MAONESHO YA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YAFANYIKA KWA MARA YA KWANZA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akiwasili aktika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma leo kwa ajili ya hafla ya kufunga Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yaliyoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Avemaria Semakafu na Mwenyekiti wa Bodi ya NACTE, Profesa John Kondoro (kulia).
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Vyuo na Taasisi za Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mara ya kwanza limeandaa Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ambayo yamefanyika Jijini Dodoma tarehe 27 hadi 30 Mei, katika uwanja wa Jamhuri.
Maonesho hayo yaliyofanyika kwa takribani siku tano na kufungwa leo na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ambapo kabla ya hotuba ya kufunga maonesho hayo, Ole Nasha aliweza kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Vyuo na Taasisi za Elimu na Mafunzo.

Thursday, May 30, 2019

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA NCHINI AKITOKEA AFRIKA KUSINI, NAMIBIA NA ZIMBABWE

aa8%2B%25282%2529
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Brigedia Jenerali Abdallah M. Alphonce na wafanyakazi wa ubalozi huo Bi. Alice Madele na Bi Joyce Makoye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare, kabla ya kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kurejea nyumbani akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.
aa2a
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitelemka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.
aa%2B%25283%2529
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi Diwani Athumani baada ya kutelemka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.
aa%2B%25284%2529
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda.
aa6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019 baada ya kuhitimisha ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi. 
a%2B%25281%2529
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare kabla ya kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kurejea nyumbani akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.
a%2B%25282%2529
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Majenerali wa Jeshi akiwa na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019 baada ya kuhitimisha ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.
a%2B%25283%2529
 Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa akipeana mikono na kuagana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhanga Mpina aliyeongozana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019 .
a%2B%25284%2529
Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa akipeana mikono na Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Bi. Joyce Makoye wakati wa kumsindikiza Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipohitimisha ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019. Wengine ni Bi Alice Madele pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini humo Brigedia jenerali Abdallah M. Alphonce 
a%2B%25286%2529
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019 baada ya kuhitimisha ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi PICHA NA IKULU

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAWASILISHA BAJETI BUNGENI

001
Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao hapa Nchini Tanzania wakifuatilia uwasilishaji wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa na Waziri Profesa Palamagamba John Kabudi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. May 30, 2019
01
002
Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia uwasilishaji wa hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo iliyowasilishwa na Waziri Profesa Palamagamba John Kabudi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. May 30, 2019
003
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akipongezana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro mara baada ya kuwasilisha bajeti ya Wizara hiyo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. May 30, 2019.
004
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe akiwa na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje, Zanzibar Balozi Mohamed Hamza(kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi. May 30, 2019.
005
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (kushoto) wakijadiliana jambo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro (katikati) pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Augustine Mahiga(kulia). May 30, 2019
006
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi  akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro wakisikiliza hoja za Wabunge wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma. May 30, 2019.
007
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi  akiwa katika picha ya pamoja nje ya Bunge na baadhi ya Mabalozi wanaoziwasilisha Nchi zao hapa Nchini. May 30, 2019.
008
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe akipongezwa na Mwakilishi wa Ubalozi wa China hapa Nchini Bw Lin Liang. May 30, 2019.
009
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akipongezwa na Dkt. Detlef Wrätcher Balozi wa Ujerumani hapa Nchini mara baada ya Waziri kuwasilisha hotuba ya Bjaeti ya Wizara yake. May 30, 2019.
10
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe akibadilishana mawazo na baadhi ya Mabalozi wanaoziwasilisha Nchi zao hapa Nchini mara baada ya kuwasilishwa hotuba ya bajeti ya wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma. May 30, 2019.
11
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akiwa pamoja na baadhi ya wazazi na watoto walioshinda katika mashindano ya uandishi wa insha kwa nchi za Afrika ya Mashariki,watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraji Mnyepe,May 30, 2019

NAIBU WAZIRI KANYASU-"SERIKALI HAINA MPANGO WA KUNYANG'ANYA ARDHII"


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewatoa hofu wananchi kufuatia zoezi linaloendelea la kupanga matumizi bora ya ardhi katika wilaya kumi nchini hasa katika maeneo yanayopakana na Hifadhi za Taifa kuwa zoezi hilo halina mpango wowote wa kunyang'anya ardhi ya wananchi kwa ajili ya kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori.

Rai hiyo imetolewa leo na Mhe. Constantine Kanyasu kufuatia hofu kubwa iliyokuwa imetanda miongoni mwa wananchi wa vijiji 8 vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, wilayani Bunda mkoani Mara ambapo moja ya madai yao ni kwamba zoezi hilo limelenga kuchukua maeneo yao ya malisho kwa ajili ya kuanzisha Hifadhi ya Jumuiya ya Wanyamapori jambo ambalo sio kweli.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Sarakwa kinachotenganishwa kati ya mto Rubana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti , Mhe.Kanyasu amewaeleza wakazi hao kuwa zoezi la kupanga matumizi bora ya ardhi katika maeneo hayo lina faida kubwa ikiwemo kuepusha migogoro wa ardhi inayotokea mara kwa mara miongoni mwao.

Amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi ni zoezi la kitaifa ambalo limelenga kutenga maeneo maalum kwa ajili ya malisho, kilimo pamoja na shughuli za maendeleo kwa malengo yakuepusha migongano inayotokea sehemu mbalimbali nchini na si kunyang'anya ardhi mpya kama inavyodaiwa.

"Nataka niwahakikishie Wizara yangu haina mpango wa kuanzisha msitu wa Hifadhi wala Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori katika kijiji chenu, Huu ni uzushi upuuzeni" Alisisitiza Kanyasu.

Aidha, Mhe.Kanyasu amewaeleza wananchi hao kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi utasaidia kuepusha watu wachache kujimilikishia eneo kubwa,"kinachofanyika kwa sasa ni kuweka rekodi na nyaraka kwa ajili ya vizazi vyenu" Alisisitiza.

Amesema katika zoezi hilo la mpango wa matumizi bora ya ardhi wanachoweza kufanya ni kutenga eneo la msitu asili wa kijiji kwa ajili ya manufaa yao ikiwemo kuokota kumi na eneo litakuwa chini ya umiliki wa kijiji na sio serikali kuu.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewatoa wasiwasi wananchi hao kuwa licha ya kijiji hicho kuingia katika zoezi la mpango wa matumizi bora ya ardhi mifugo yao haitazuiliwa kwenda kunyweshwa maji katika mto Rubana.

"Nimesikia baadhi ya watu wakieneza uzushi kuwa baada ya mpango wa matumizi bora ya ardhi kukamilika hakuna mtu yeyote kupeleka mifugo katika mto Rubana, huu ni uwongo" alisema Kanyasu

Hata hivyo amewaeleza kuwa mita 500 kutoka katika mto huo ni eneo la kijiji kwa ajili ya malisho ya mifugo isipokuwa vitu ambavyo havitaruhusiwa kufanywa na mtu yeyote ni kulima pamoja na kujenga nyumba kwa vile eneo hilo ni shirikishi kwa Wanyamapori pamoja na mifugo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Bunda vijijini, Boniface Getere amewataka wananchi kuwa watulivu kwani serikali haina mpango wowote wa kunyang'anya ardhi badala yake mpango huo utakuwa mkombozi kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha badae.

" Mimi ni Mbunge wenu nisingeweza kukubali hata kidogo kama mpango huu wa matumizi bora ya ardhi umelenga kunyang'anya ardhi yenu." Alisisitiza Getere.

Naye, Mwenyekiti wa kijiji cha Sara, Samson Kapeta amekiri mbele ya Naibu Waziri kuwa mpango wa matumizi bora ni mpango mzuri isipokuwa kumejitokeza vikundi vya watu vilivyolenga kupotosha malengo mazuri ya serikali kwa ajili ya ardhi yao.

Mpango wa matumizi bora ya Ardhi ni mpango unaotekelezwa katika wilaya kumi nchini kwa ushirikiano katika ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi kwa kugharamiwa na Hifadhi ya Taifa ( TANAPA) NA LUSUNGU HELELA-MARA
1
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sarakwa kuhusu umuhimu wa zoezi la mpango wa matumizi bora wa ardhi unaofanywa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Ardhi katika wilaya kumi katika wilaya kumi nchini kuwa haujikiti kupokonya maeneo mapya ya wananchi kwa ajili ya kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori kama inavyodaiwa.
2
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Sarakwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe, Constantine Kanyasu akiwaeleza kuwa serikali inaendesha zoezi la mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya manufaa ya wananchi.
3
 Mbunge wa Bunda vijijini, Mhe, Boniface Getere akizungumza na wananchi wa Sarakwa kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu kuzungumza na wananchi hao kuhusu nia ya serikali ya kuendesha zoezi la mpango wa matumizi bora ya ardhi katika kijiji hicho.
4
Mratibu wa mipango wa matumizi bora ya ardhi, Rose Mdendemi akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa kijiji cha Sarakwa wilayani Bunda mkoani Mara kuhusu zoezi linaloendelea la mpango wa matumizi bora ya ardhi (Picha na Lusungu Helela-Wizara ya Maliasili na Utalii)

NEC YATANGAZA NAFASI ZA AJIRA ZA MUDA ZA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


Mwandishi wetu, NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi za kazi za muda kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura.

Kwa mujibu wa tangazo la maombi ya ajira hizo lililosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Mabamba Rajabu Moses, Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na wasiozidi miaka 45 wametakiwa kuomba.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, sifa zingine za waombaji ni kuwa na elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

“Awe na uwezo wa kutambua matatizo ya kompyuta ya hardware na software  na kuyatatua” ilisema sehemu ya tangazo hilo na kuongeza kuwa:.
“Awe na uwezo wa ku-istall programu za kompyuta na kutoa msaada wa kiuifundi wa TEHAMA kwa watumiaji.”

“Awe hajawahi kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai an awe na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yenye usimamizi mdogo”
Sifa nyingine za ziada za kazi hiyo zimetajwa kwenye tangazo hilo linalopatikana kwenye Tovuti ya NEC ya www.nec.go.tz na mitandao ya kijamii ya NEC.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA UONGOZI WA BUNGE LA VIJANA OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA


V25A1949
  Spika wa Bunge, Job ndugai (kushoto) akisalimiana na Spika wa Bunge la Vijana 2018/2019, Ndg. Zephania Sane pale uongozi wa Bunge hilo ulipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge hilo, Ndg. Ashiruna Muhunzi  na katibu wa Bunge, Ndg. Alphonsina Ambrosi
V25A1952
Spika wa Bunge, Job ndugai (kushoto) akikabidhiwa ripoti ya Bunge la Vijana 2018/2019 na Spika wa Bunge hilo, Ndg. Zephania Sane alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
V25A01943
Spika wa Bunge, Job ndugai (Mwenye joho) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Bunge la Vijana 2018/2019 ulipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Walioongozwa na Spika wa Bunge hilo, Ndg. Zephania Sane (wa nne kulia). (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Wednesday, May 29, 2019

VIONGOZI NA WATUMISHI WA WIZARA YA MADINI WATAKIWA KUWA WAADILIFU KATIKA UTENDAJI KAZI WAO

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akifungua mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupopichani) katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akikabidhi cheti cha ufanyakazi bora kwa mmoja wa wafanyakazi bora wa Wizara ya Madini, Bi. Asteria Muhozya baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Madini, Dotto Biteko (Mb) (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Madini  Bw. Issa Nchasi (kulia).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) na Waziri wa Madini, Dotto Biteko (Mb) wakifurahia jambo baada ya ufunguzi mafunzo kwa viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Madini  Bw. Issa Nchasi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) amewataka viongozi na watumishi wa Wizara ya Madini kuwa waadilifu katika utendaji kazi wao ili Tanzania iweze kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. 
Mhe. Mkuchika ametoa wito huo alipokuwa akifungua mafunzo kwa viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.

Mhe. Mkuchika amesema kuwa, katika kulenga dira ya pamoja ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 ni lazima viongozi na watumishi wa Wizara ya Madini kufuata misingi ya maadili kama inavyoelezwa katika Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma za mwaka 2005.
Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, kutozingatia viapo vya maadili ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Mhe. Mkuchika amewataka viongozi wa Wizara ya Madini kuwa mfano wa kuigwa katika kutekeleza kiapo cha uadillifu. 

“Kiongozi unapaswa kuwa mfano katika kutekeleza kiapo chako cha uadilifu, na kama utakuwa umesahau kiapo chako, si vibaya ukaichukua nakala ya kiapo ofisini kwako na kujikumbusha mara kwa mara,” Mhe. Mkuchika amesisitiza.

Mhe. Mkuchika amesema kuwa ni vema watumishi wa Wizara ya Madini hasa wanaofanya shughuli zao katika maeneo ya uchimbaji madini wawe waadilifu pia ili kuongeza tija na utendaji kazi mzuri.
“Watumishi mlioko kwenye maeneo yenye shughuli za uchimbaji, muwe waadilifu na mtangulize uzalendo wa nchi mnapotekeleza majukumu yenu” Mhe. Mkuchika amesema.

Aidha, Mhe. Mkuchika amewataka viongozi na watumishi wa Wizara ya Madini kuepuka vitendo vya rushwa huku akinukuu maneno ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Hayati Koffi Annan.

“Rushwa ni ugonjwa ambao unatafuna taratibu na wenye kuleta madhara katika jamii. Unadhoofisha demokrasia na utawala wa sheria, unaleta uvunjifu wa haki za binadamu, unaharibu hali ya maisha, na kusababisha kuwepo kwa mauaji na mambo mengine yanayotishia usalama wa binadamu” Mhe. Mkuchika amesema.

Katika tukio la ufunguzi wa mafunzo hayo, Mhe. Mkuchika amekabidhi vyeti vya ufanyakazi bora kwa watumishi 12 wa Wizara ya Madini.
Mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini yamefanyika lengo ikiwa ni kukumbushana stadi muhimu za kazi, kuwajengea uwezo wa utendaji kazi na kuongeza ari ya utekelezaji wa majukumu yao.

IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 29 MEI, 2019

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MWANAMWEMA SHEIN, AJUMUIKA NA WATOTO YATIMA WA MAZIZINI ZANZIBAR KATIKA FUTARI ALIYOWAANDALIA

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuka na Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar katika Futari Maalum aliyowaandalia jana 28-5-2019, katika makazi yao mazizini, akiwa na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi.
Watoto wanaoishi katika Nyumba ya Serikali ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar wakipata futari walioandaliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, iliofanyika katika makazi yao mazizini jana 28-5-2019.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa katika futari aliyowaandalia Watoto wa Nyumba ya Serikali ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar, kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman Iddi na kushoto Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Mauydline Castico, wakijumuika na Watoto hao katika futari hiyo iliofanyika katika makazi yao mazizini jana 28-5-2019.

Watoto wa Nyumba ya Watoto Mazizuini Zanzibar wakiwa katika futari ilioandaliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, iliofanyika katika makazi yao mazizini Zanzibar.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Mtoto anayelelewa katika Nyumba ya Watoto Mazizini Zanzibar Mtoto Nadir Abdalla mwenye umri wa mwaka moja na miezi mitano,baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya futari maalum aliyowaandalia katika makazi yao mazizini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na kuagana na Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar baada ya kumalizika kwa hafla ya futari aliyowaandalia katika makazi yao Mazizini akiwa na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi.(Picha na Ikulu, Zanzibar)