Matokeo chanyA+ online




Tuesday, November 28, 2017

DIRISHA LA KODI KIELEKTRONIKI LAMPAISHA RAIS MAGUFULI MUAROBAINI ALIOUSEMA UMETIMIA

Tangu kuzinduliwa Dirisha la Ukusanyaji Kodi kidigitali June mosi 2017 (Electronic Revenue Collection System - eRCS) ambalo lilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Makamu wa Rais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassani pamoja na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mohamad Shein,  mawaziri kadhaa wa serikali za Muungano na serikali ya Mapinduzi; Kwa mara ya kwanza serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipatia bila bugudha Ushuru mkubwa wa bidhaa na kodi ya Ongezeko la Thamani zitokanazo na makampuni ya simu.

Mfumo huu uliosukwa na vijana wa Kitanzania wazalendo, umefanikisha kuongeza mapato litokanalo na mtandao (Ciber Space) kwa Zanzibar kwa 51% kwa robo ya tatu ya mwaka 2017 ukilinganisha na miezi kama hiyo 2016.
Uchunguzi uliofanyika katika robo hiyo (tatu) ya mwaka 2017 (Julai,August na Septemba 2017), umebaini Zanzibar imelipwa kupitia mfumo wa eRCS Tsh Bil 7.2 ambayo imeongezeka kwa 51% ukilinganisha na miezi kama hiyo mwaka 2016 ambapo makusanyo ya jumla ya kodi yalikuwa  Tsh Bil 3.5 pekee.



Kwa mujibu wa vielelezo vya makusanyo wa TRA, miezi mitatu kabla ya mfumo huu kuzinduliwa rasmi (April,May na June); Makampuni ya simu yalilipa jumla ya kodi ya  Tsh Bil 101.7 lakini baada ya kuzinduliwa rasimi kwa mfumo huu wa eRCS na makampuni ya simu (TTCL,HALOTEL,AIRTEL,VODACOM,ZANTEL,SMART na TIGO) kuugwa ndani ya mfumo; Kwa kipindi cha miezi mitatu pekee ( Julai,Agost na Septemba 2017), yameweza kulipa kwa njia ya kielektroniki Tsh Bil 128.9 kukiwa na ongezeko la Sh Bil 27.2 sawa na 21% huku ongezeko la kodi ya thamani ikipanda kwa 9% yaani Tsh. Bil 4.7 sambamba na ongezeko la Ushuru wa Bidhaa 29% yaani Tsh. Bil 22.




Taarifa za kiuchunguzi zimebaini serikali inafuatilia kwa kina udanganyifu wowote utakao ama uliojitokeza kabla na baada ya mfumo hasa taarifa za makampuni ya simu katika matumizi yaoya kila mwezi.

Mpaka sasa, benk kadhaa nchini zimekamilisha taratibu za kuungwa katika mfumo huu na kuanza kulipa kodi kielectroniki.  Huu ni ushindi mkubwa kwa mkakati wa Rais Magufuli katika kupata njia bora za kukusanya mapato nchini. 
Ikumbukwe wajenzi wa mfumo huu ni vijana wazalendo walioaminiwa na serikali ili kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zingetumika katika ujenzi wa mfumo huo kutumia wataalamu na makampuni ya kigeni.


Hivi ndivyo mapato yanavyoonekana katika Dashibodi ambazo viongozi wakuu wa nchi wanaona mapato yanavyokusanywa kielectroniki kwa kutumia mfumo  wa eRCS kila sekunde.



Jedwali hili linaonyesha  Mabenk yaanza kulipa baada ya yale yaliyokamisha kujiunga na ERCS ambyo ni BANK M na AMANA BANK Tanzania ina Mabenk zaidi  ya 20






Wednesday, November 22, 2017

MBUNGE AWASAIDIA WANAWAKE VYEREHANI 370 NJOMBE



CHAPA KAZI Mhe. NEEMA MGAYA
• Ni mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe Mhe. NEEMA MGAYA

• Msaada huo wa Vyerehani 370 una thamani zaidi ya shilingi Milioni 90

• Lengo ni kina Mama wajikwamue kiuchumi huku akiunga mkono juhudi za Mhe. Rais na Serikali kuhimiza uchumi wa viwanda na kuwataka Watanzania kufanyakazi kwa bidii

ili Nchi yetu... izidi kupata
Matokeo chanyA+
Ku


Friday, November 10, 2017

MIRADI MIKUBWA YA MAJI 2017/2018








MIAKA 10 YA MTANDAO WA POLISI WANAWAKE,MITANDAO KWA HABARI NJEMA



MIKOPO NA ONGEZEKO LA MAHITAJI KWA ELIMU YA JUU NCHINI




UPANUZI WA VIWANJA VIKUBWA VYA NDEGE NCHINI


RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE.DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI CHA KAGERA KILICHOPO WILAYANI MISENYI MKOANI KAGERA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI NA WAFANYAKAZI WA KIWANDA HICHO NOVEMBA 8,2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Misenyi wakati wakitoa kero zao mbalimbali mara baada ya kuwasili wilayani Misenyi akitokea Bukoba mjini Novemba 8,2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Misenyi wakati wakitoa kero zao mbalimbali mara baada ya kuwasili katika kiwanda cha sukari cha Kagera akitokea kwenye mashamba ya miwa ya kiwanda cha Kagera Novemba 8,2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli  wakimsikiliza mtaalamu wa Kilimo aliyekuwa akielezea mambo mbalimbali katika mashamba ya miwa katika Kiwanda hicho cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Misenyi mkoani Kagera

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Mitambo ya kuchujia na kuvutia maji kwa ajili ya Mashamba ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar, mitambo hiyo ipo pembezoni mwa Mto Kagera katika Wilaya ya Misenyi Novemba 8,2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza mtaalamu wa Kilimo aliyekuwa akielezea namna mbegu za miwa zinavyoandaliwa katika mashamba ya miwa katika Kiwanda  cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Misenyi mkoani Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Charles Mwijage Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji paoja na viongozi na wataalamu wa kilimo cha miwa katika mashamba ya miwa alipotembelea Kiwanda  cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Misenyi mkoani Kagera Novemba 8,2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Shamba la miwa la Kiwanda hicho cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Misenyi mkoani Kagera Novemba 8,2017.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia namna uharibifu wa mazingira uliofanywa katika moja ya mito iliyopo kiwandani mara baada ya kukagua Shamba la miwa la Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Misenyi mkoani Kagera Novemba 8,2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi kwa nyimbo nzuri ya mapokezi kutoka watoto wa chekechea mara baada ya kutembelea Shamba la miwa la Kiwanda cha Sukari cha Kagera kilichopo Misenyi mkoani Kagera Novemba 8,2017.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sukari kabla ya kufungwa kwenye mifuko yake alipotembelea kiwanda cha sukari cha Kagera kilichopo wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera Novemba 8, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishika moja ya mfuko wa sukari ambayo ipo tayari kwa kusafirishwa alipotembelea Kiwanda cha Sukari cha Kagera kilichopo Misenyi mkoani Kagera Novemba 8,2017.