Matokeo chanyA+ online




Sunday, March 31, 2019

RAIS MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) 146 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

1
2
3
 Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa na Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kabla ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya 146 wa kundi la 65 la mwaka 2018 katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
4

5
 Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania 146 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
6

7
 Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Wakivalishana vyeo mara baada ya kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika tukio lililofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
8
 Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakila kiapo cha Utii mbele ya Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutunukiwa Kamisheni Ikulu jijini Dar es Salaam.
9
  Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoka katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
10
  Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Brigedia Jenerali Steven Mnkande wakati wakielekea kwenda kupiga picha za kumbukumbu Ikulu jijini Dar es Salaam.
11
 Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Brigedia Jenerali Steven Mnkande wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Maafisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania mara baada ya kutunukiwa Kamisheni Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Friday, March 29, 2019

UTOAJI WA ELIMU BORA NI KIPAUMBELE CHA NCHI - MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema utoaji wa elimu bora kwa Watanzania ni moja ya vipaumbele vya nchi katika kuleta maendeleo na kufikia malengo ya Milenia 2025, Elimu kwa wote (EFA) na Mkakati wa Kupambana na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA). 
Amesema ili kuweza kufanikisha malengo hayo wanahitaji sekta hiyo kuwa bora, imara, inayokidhi mahitaji ya jamii kwa kuwapa vijana maarifa na ujuzi wa kukabiliana na matatizo ya kijamii, kitaifa na kimataifa.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 29, 2019) wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Parokia ya Ikwiriri, mkoani Pwani. Ameipongeza Parokia hiyo kwa kubuni mradi wa ujenzi wa shule.
Amesema sekta ya elimu ni wakala wa mabadiliko katika jamii kiuchumi, kiteknolojia na kiutamaduni katika kuleta maendeleo ya nchi na wadau muhimu wa sekta hiyo ni pamoja na Serikali, washirika wa maendeleo, mashirika ya kiraia na ya kidini, sekta binafsi na jamii kwa ujumla. 
Waziri Mkuu amesema kuwa wadau wote hao wamekuwa wakichangia kwa njia mbalimbali katika kuboresha utendaji wa sekta hiyo na kusababisha Serikali kupata mafanikio makubwa sana katika upatikanaji wa huduma za Jamii zikiwemo za elimu, afya na maji. 
”Hivi sasa kila Kijiji nchini kina shule ya msingi na ongezeko limefikia idadi ya shule 17,659 zikiwemo zilizo chini ya Kanisa katoliki 204. Pia tumeweza kujenga shule za sekondari katika kila kata ambapo ongezeko limefikia shule za sekondari 4,883 nchi nzima zikiwemo zilizo chini ya kanisa katoliki 266”. 
Waziri Mkuu amesema idadi hiyo ya shule imesaidia kutoa fursa kwa wanafunzi wengi kupata elimu nchini katika ngazi mbalimbali.  ”Hivi sasa kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015/2010 tunatekeleza mpango wa elimu bila ada kwa kutoa sh. Bilioni 24.4 kila mwezi”.
Amesema lengo la Serikali la kutoa kiasi hicho cha fedha kila mwezi ni kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapata fursa bila vikwazo na  Wilaya ya Rufiji nayo inanufaika, ambapo imetengewa kiasi cha milioni 394.5 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Lengo la Serikali kutoa Elimumsingi Bila Ada ni kuleta ujumuishi kwa kuhakikisha watoto wote hususan wale ambao wanatoka katika familia zisizo na uwezo wanapata haki ya msingi ya kupata elimu. 
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuongezeka kwa ufaulu wa darasa la saba kumeleta changamoto ya uwepo wa miundombinu ya shule za sekondari hususan kwa kidato cha kwanza ambayo ni kielelezo cha mafanikio ya utekelezaji wa sera ya Elimumsingi Bila Ada. 
Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengoalitumia fursa hiyo kuishikuru Serikalikwa kurejesha hali ya usalama na utulivu katika eneo la Rufiji na Kibiti.

Kardinali Pengoalisema kurejea kwa hali ya utulivu na usalama katika maeneo hayo kumemuondolea mzigo wa kiutendaji uliokuwa ukimuumiza kwa kuwa mapadri aliokuwa akiwapangia katika parokia za huko walikuwa wakisema ‘tumekosa nini’.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Askofu wa Jimbo la Ifakara, Salutaris Libena wakiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. Wa pili kulia ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Fancis wa Asiz Ikwiriri, Padre Disma Kimboi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza wakati alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri  mkoani Pwani, Machi 29, 2019.  Wengine kutoka kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Jimbo la Ifakara, Salutaris Libena na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Francis wa Asiz Ikwiriri, Padre Dismas Kimboi.
Wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya wasichana ya  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa ambaye alipewa nafasi ya kusalimia wakati Waziri Mkuu alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri Mkoani Pwani Rufiji, Machi 29, 2019.  Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na wa nne kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani na  Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Askofu wa Jimbo la Ifakra,  Salutarisi Libena baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. Katikati ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi  baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri Mkoani Pwani, Machi 29, 2019. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)

MKUCHIKA AMTEMBELEA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI NA MAMA MARIA NYERERE

IMG_2459
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiagana na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
IMG_2236
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akimsikiliza Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
IMG_2328
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), wa pili kushoto ni Mama Siti Mwinyi na wa kwanza kushoto ni Afisa anayesimamia Dawati la Viongozi Wastaafu wa Kitaifa, Bi. Nyasinde Mukono.

IMG_2334
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiteta jambo na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
IMG_2355
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akifafanua jambo kwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
IMG_2380
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akizungumza na watoto wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipomtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Wa kwanza kulia ni Andrew Nyerere na wa kwanza kushoto ni Magige Nyerere. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
IMG_2432
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akimsikiliza Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
IMG_2440
 Afisa anayesimamia Dawati la Viongozi Wastaafu wa Kitaifa, Bi. Nyasinde Mukono, akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Mkuchika ya kuwatembelea Viongozi Wastaafu wa Kitaifa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Thursday, March 28, 2019

SAMATTA KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KIMATAIFA

Bodi ya Utalii Tanzania(TTB), Ipo katika hatua za mwisho za Mazungumzo na Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Klabu ya Genk iliyopo nchini Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta kuwa Balozi wa kutangaza Utalii wetu Kimataifa.

akziungumza na Waandishi wa habari Mapema leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Muendeshaji wa Bodi hiyo, Devotha Mdachi amesema kuwa katika hatua ya kutangaza utalii kimataifa wameona wamtumie Mbwana Samatta.

"wote tunajua umaharufu wa Mchezaji wetu katika ligi ya ubegiji na soka la barani ulaya kwa sasa hivyo katika Malengo yetu ya kutumia watu maharufu ambao ni Vijana wa kitanzania tumezungumza na Mbwana Samatta na ametuambia kuwa ifikapo mwezi May atakapokuja katika mapumziko yake kila kitu kitakamilika"anasema Mdachi.

ametaja kuwa mbali ya Mbwana Samatta wapo wasanii wengi na Vijana Maharufu ambao wanataraji kuwafikia hili wawe mabalozi wa utalii wetu nchini lakini kwa kuanzia wameanza na Samatta pamoja na Miss Tanzania .

Samatta atakuwa Kijana wa Pili wa Kitanzania Mwenye Mafanikio ambaye atapata nafasi ya kuwa balozi wa TTB ambapo ametanguliwa na Miss Tanzania 2018/2019 Queen Elizabeth Mukune ambaye amesaini Mkataba leo.

OSHA YAPONGEZWA KWA UTENDAJI

Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi umepongezwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi ili kusaidia nguvu kazi iliyopo kutumika kuchochea maendeleo.

Akizungumza wakati wa semina kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyofanyika Machi 27, 2019 katika Bungeni Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Mohamed Mchengelwa amesema kuwa  Wakala huo umeonesha mfano bora katika kutekeleza majukumu yake na pia kwa kuwajengea uwezo wabunge  kuhusu masuala ya usalama mahala pa kazi na umuhimu wake katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

 “Elimu tuliyopata ni muhimu kwetu na kwa wananchi hivyo pamoja na kazi nzuri mnayofanya ni vyema sasa elimu hii ikatolewa kwa wananchi wote na wabunge kwa ujumla ili kusaidia kupunguza athari zinazotokana na kukosekana kwa elimu kuhusiana na masuala ya Usalama Mahali Pa Kazi ikiwemo namna ya kutoa huduma ya kwanza,” alisisitiza Mchengelwa

Akifafanua amesema kuwa katika masuala ambayo Kamati hiyo imetoa ni pamoja na kuongeza kiwango cha utoaji wa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wabunge wanapata uelewa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya OSHA.

Aliongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa wakuwajengea uwezo wabunge kama wawakilishi wa wananchi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Lengo letu kama Serikali ni kuhakikisha kuwa tunalinda nguvu kazi iliyopo ili iweze kusadia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na maendeleo ya Taifa kwa ujumla,” alisisitiza Mavunde

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi. Khadija Mwenda amesema kuwa wameandaa semina hiyo kwa wabunge ili kuwajengea uwezo wa kujikinga na athari za ajali au panapotokea mgonjwa anayehitaji kupata msaada wa huduma ya kwanza katika mazingira yao ya kazi na mengine yanayowazunguka.

Aliongezea kuwa OSHA itaendelea kutoa elimu kwa umma ili kujua namna bora za kujilinda na kujiepusha na madhara yanayoweza kuwapata wawapo kazini pamoja na mazingira yote yanayowazunguka kwa kuzingatia misingi ya elimu ya utoaji wa huduma ya kwanza endapo kunatokea dharula au majanga kazini.

“Tumejipanga kuwafikia watanzania kwa wingi wao ili kutoa elimu kwa umma juu ya masuala ya Usalama mahala Pa Kazi kwa kuzingatia unyeti wa masuala hayo kwani ni muhimu wananchi wakaelewa namna bora za kujilinda kuepuka madhara wawapo kazini,”alisema Bi.Mwenda

OSHA imekuwa ikiwajengea uwezo makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo wabunge na wananchi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuilinda nguvu kazi iliyopo kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi Bi. Khadija Mwenda akieleza umuhimu wa kuzingatia kanuni za kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa au mtu aliyepata ajali wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 27, 2019 Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Mafunzo na Tafiti na Takwimu kutoka Wakala wa Afya na Usalama mahala pa Kazi (OSHA) Joshua Matiko akiwasilisha mada wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wabunge ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuongeza tija.
 Mkurugenzi wa Mafunzo na Tafiti na Takwimu kutoka Wakala wa Afya na Usalama mahala pa Kazi (OSHA) Joshua Matiko akiwasilisha mada wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wabunge ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuongeza tija.
 Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia semina ya kuwajengea uwezo kuhusu majukumu ya OSHA leo jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. David Mathayo akichangia jambo wakati wa mafunzo hayo.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

NAIBU SPIKA AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR)

 Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson akifungua kikao cha Tano cha Kamati ya Demokrasia na Utawala cha Baraza la Wabunge wa Mabunge ya Jumuiya ya nchi za Maziwa makuu (FP-ICGLR) kilichofanyika hii leo Jijini Arusha.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kikao cha Tano cha Kamati ya Demokrasia na Utawala bora cha Baraza la Wabunge wa Mabunge ya Jumuiya ya nchi za Maziwa makuu (FP-ICGLR) kilichofanyika hii leo Jijini Arusha. (Picha na Ofisi ya Bunge)

WAZIRI KABUDI ATOA POLE ZIMBABWE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba Joh Kabudi akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Zimbabwe uliopo jijini Dar es Salaam,Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba Joh Kabudi akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Zimbabwe uliopo jijini Dar es Salaam,Tanzania huku kaimu Balozi wa Zimbabwe hapa Nchini Bw. Martin Tvenyika akishuhudia.

Kaimu Balozi wa Tanzania hapa nchini Bw Martin Tvenyika akimuonesha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi katika ramani maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko yaliyotokana na Kimbunga Idai nchini humo.

Wednesday, March 27, 2019

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA 7 LA AFYA NA SAYANSI AFRIKA MASHARIKI

3
09
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
04
5
8
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasha mwenge kama ishara ya ufunguzi wa Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
6
Sehemu ya Wataalamu waliohudhuria ufunguzi wa  Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA PRINCESS SARAH ZEID

20
04
05
7
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Binti wa Mfalme wa Jordan Sarah Zeid (katikati) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa WFP Bw. Michael Dunford (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.
18
9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Binti wa Mfalme wa Jordan Sarah Zeid (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.
17
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa maelezo ya viungo vya chai vya Zanzibar wakati wa kumkabidhi zawadi  Binti wa Mfalme wa Jordan Sarah Zeid (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU AIPONGEZA OFISI YA RAIS - UTUMISHI KWA KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI YAKE KWA WAKATI KWENYE MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) amewapongeza viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa usimamizi mzuri uliopelekea kumalizika kwa ujenzi wa ofisi hiyo  kwa wakati iliyopo mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Pongezi hizo amezitoa mapema  leo, alipotembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa, ameridhishwa na kiwango cha ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyojengwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu na kwa gharama nafuu ya kiasi cha shilingi bilioni moja iliyotengwa na serikali.
 “Serikali imekuwa ikifuatilia hatua zote za ujenzi katika mji wa serikali ili kuhakikisha ujenzi unafanywa kwa viwango, na jengo la Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora limekuwa likienda vizuri sana katika hatua zote” amesema Mhe. Majaliwa.
Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa, anatambua kwamba Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora imeshafanya uzinduzi wa jengo lake, jambo ambalo ni jema na limeonyesha namna ambavyo ofisi hiyo imetekeleza vema maelekezo ya serikali.
Aidha, Mhe. Majaliwa ameweka bayana kuwa, uzinduzi rasmi wa Ofisi zote zilizojengwa kwenye mji wa serikali utafanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika tarehe rasmi atakayoipanga.
Mhe. Majaliwa ametoa wito kwa ofisi hiyo kuboresha mandhari ya nje ya  ofisi ili iweze kupewa kipaumbele na serikali kuwa ofisi itakayotumika kwa ajili ya  uzinduzi wa ofisi zote  zilizojengwa kwenye mji huo wa serikali. 
Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) kwa kutenga muda wake kuitembelea Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora katika mji wa serikali, na kumshukuru kwa namna alivyowahimiza mawaziri kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa ofisi zao kwenye mji wa serikali ili ukamilike kwa wakati.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, amemuahidi Mhe. Majaliwa kuwa, ofisi yake itatekeleza maelekezo aliyoyatoa na itaendelea kutekeleza maagizo anayoyatoa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Awali, Kaimu Meneja wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Bw. Herman Tanguye amesema kuwa, Wakala ya Majengo Tanzania imekamilisha ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa asilimia 99.5% kwa muda uliopangwa na kwamba hatua iliyobakia ni kukamilisha mandhari ya nje ya ofisi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa ameitembelea Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za serikali kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma, kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuzindua ofisi hizo rasmi hivi karibuni.
IMG_6194
 Muonekano wa jengo jipya  la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
IMG_6220
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) na ujumbe wake wakiwasili katika jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
IMG_6236
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akiwa ndani ya ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) iliyopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael.
IMG_6253
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akizungumza  na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
IMG_6270
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akifurahia jambo mara baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
IMG_6296
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb), mara baada ya Mhe. Majaliwa kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
IMG_6326
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael wakifurahia jambo na viongozi wengine mara baada ya kukamilika kwa ziara ya Mhe. Kassim M. Majaliwa ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.