Matokeo chanyA+ online




Sunday, December 31, 2023

NUKUU ZA MH RAIS DK SAMIA SULUHU HASANI, KUHUSU UCHUKUZI KATIKA HOTUBA YAKE YA MWISHO WA MWAKA 2023 KUKARIBISHA MWAKA 2024 KWA WATANZANIA.






NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+

NUKUU ZA MH RAIS DK SAMIA SULUHU HASANI KUHUSU SEKTA ZA UTALII NA MADINI, KATIKA HOTUBA YAKE YA MWISHO WA MWAKA 2023 KUKARIBISHA MWAKA 2024 KWA WATANZANIA.






 NUKUU ZA MH RAIS DK SAMIA SULUHU HASANI KUHUSU SEKTA YA KILIMO, KATIKA HOTUBA YAKE YA MWISHO WA MWAKA 2023 KUKARIBISHA MWAKA 2024 KWA WATANZANIA.







 NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+

 NUKUU ZA MH RAIS DK SAMIA SULUHU HASANI KUHUSU MAPITO YA KIUCHUMI NCHINI , KATIKA HOTUBA YAKE YA MWISHO WA MWAKA 2023 KUKARIBISHA MWAKA 2024 KWA WATANZANIA. 














NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+

Thursday, December 28, 2023

 Rais Samia Suluhu Hassan atunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi wa Utalii na Masoko katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Tunguu Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine akiwa kwenye maandamano ya Kitaaluma wakati walipokuwa wakiingia kwenye Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu kwa ajili ya kushiriki Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ambapo Chuo hicho kimemtunuku Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake wa kuifungua nchi kiuchumi kupitia Sekta ya Utalii tarehe 28 Desemba, 2023.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Aman Abeid Karume katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu walipohudhuria Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) tarehe 28 Desemba, 2023.










 RAIS MWINYI ARIDHIA UWANJA WA AMAAN KUITWA “NEW AMAAN SPORTS COMPLEX”








Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameridhia ushauri wa kuubadili jina uwanja wa Amaan na  kuitwa  “New Amaan Sports Complex” wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya Uwanja huo uliofanyika Desemba 27, 20203 kisiwani humo

Rais Mwinyi ameridhia ushauri huo uliotolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alipokua akitoa salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Kutokana  na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuufanya uwanja huu kuwa wa kisasa na wenye viwango vya Kimataifa, mimi naomba niubadilishe jina uitwe New Amaan Stadium" alisema Dkt. Ndumbaro.

Hafla ya Uzinduzi wa Uwanja huo ilipambwa na Burudani mbalimbali ikiwemo Muziki na mechi ya mpira wa miguu ya kirafiki baina ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania Bara "Kilimanjaro Stars"  na Timu ya Mpira wa Miguu ya  Zanzibar "Zanzibar Heros ambazo zilitoka sare ya bila kufungana.

Saturday, December 23, 2023

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI ZAWADI KWA WATOTO YATIMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekabidhi zawadi katika Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo Kimara Jijini Dar es salaam. Zawadi hizo ni pamoja na vyakula, vinywaji, sabuni, mafuta ya kupikia pamoja na mavazi. 

 

Akikabidhi zawadi hizo Msaidizi wa Sheria wa Makamu wa Rais Bw. Elisha Suku amesema Makamu wa Rais ametoa zawadi hizo kwa lengo la kusheherekea pamoja na watoto hao sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya. Aidha ameongeza kwamba Makamu wa Rais amewatakia heri na afya njema watoto pamoja na walezi wao.

 

Akizungumza mara baada ya kupokea zawadi hizo, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam Wilbroad Matsai amemshukuru Makamu wa Rais kwa zawadi hizo pamoja na viongozi wote wanaojitoa kwaajili kwaajili ya kusaidia wenye uhitaji.


Msaidizi wa Sheria wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Elisha Suku (mwenye koti jeusi) akikabidhi zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango katika Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo Kimara Jijini Dar es salaam. Watatu kutoka kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam Wilbroad Matsai. Tarehe 23 Desemba 2023.





Msaidizi wa Sheria wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Elisha Suku (mwenye koti jeusi) akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo Kimara Jijini Dar es salaam mara baada ya kukabidhi zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango. Wengine katika picha ni walezi wa kituo hicho pamoja na  Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam Wilbroad Matsai. Tarehe 23 Desemba 2023.


Wednesday, December 20, 2023


Miradi ya maji inayoendelea katika Wilaya ya Ludewa nchini Tanzania

Serikali inatekeleza jumla ya miradi saba ya maji. Gharama ya miradi yote ni Tsh. 13,866,290,252.86.

Maeneo Yanayofaidika na Miradi hii ni kata za Mavanga, Ludewa, Iwela, na Manda. Vyanzo vya maji ni Mavanga
Ukaguzi umefanyika kwenye ujenzi wa ofisi za vyombo vya usimamizi wa watumia maji ngazi ya jamii (CBWSO). Vituo vya ugawaji wa maji kwenye jamii vimekaguliwa.

Kwa mwaka 2022, Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ilipokea Tsh. 2,108,673,191 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maji. Miradi ni pamoja na ujenzi na uboreshaji wa mfumo wa Maji Ludewa Mjini, madope, Madindo, Ibumi, Lifua, na Ihela.

Hii inaonyesha jitihada za Serikali katika Wilaya ya Ludewa kutekeleza miradi ya maji ili kuboresha upatikanaji wa huduma hiyo katika eneo hilo.

 Lengo la mradi  huu ni kuhakikisha kuwa Wana-Ludewa wanapata huduma ya Maji bora, safi, salama na yenye kutosheleza.

Na Haya Ndiyo Matokeo Chanya+

 Rais Samia Suluhu Hassan Awaapisha Viongozi Wateule Ikulu Jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu Maryam Ahmed Muhaji kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu George Nathaniel Mandepo kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana,  Kamishna wa Maadili Jaji Mhe. Sivangilwa Mwangesi, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Ndugu Mahendeka, Mkuu wa Mkoa Manyara Mhe. Queen Sendega na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala walioapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.




 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya, ametoa pole kwa mama ambaye amepoteza mume na mtoto wake kutokana na tukio la mauaji lililotokea Desemba 12, 2023, katika kijiji cha Hangomba, Kata ya Bara, wilayani Mbozi.


Kamanda Mallya amethibitisha kuwa Jeshi la Polisi linashughulikia suala hilo kwa kufanya uchunguzi ili kubaini waliohusika katika mauaji hayo na kuchukua hatua stahiki. Aidha, ametoa wito kwa jamii kutojichukulia sheria mkononi, bali badala yake kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ili hatua ziweze kuchukuliwa ipasavyo.


Mwenyekiti wa kijiji hicho, Martine Mbembela, ameishukuru Jeshi la Polisi kwa kuonesha ushirikiano na kufika kumpa pole mama huyo ambaye familia yake imekumbwa na mkasa huo. Hii inaweza kuashiria umoja na msaada unaotolewa na jamii kwa waathirika wa tukio hilo la kusikitisha.

Friday, December 15, 2023

Bonde la Stiegler's Gorge ni sehemu ya Bonde la Mto Rufiji nchini Tanzania. 

Eneo hili ni maarufu kutokana na mto wake, pamoja na mazingira yake ya asilia na kijiolojia. Hata hivyo, ujenzi wa Bwawa la Stiegler's Gorge, rasmi unaojulikana kama Mradi wa Umeme wa Rufiji (Rufiji Hydropower Project), ni wa kisasa.

Bonde la Stiegler's Gorge liko kati ya Mlima Uluguru na Mlima Selous, na ni sehemu ya mfumo wa Mto Rufiji. Eneo hili lina miamba mikubwa, mteremko mkali, na mandhari nzuri ya asili. Kijiolojia, mazingira haya yana miamba ya kale na mchanga uliogawanyika.

Bwawa la Stiegler's Gorge limejengwa karibu na Bonde la Rufiji, katika eneo ambalo linajulikana kama Stiegler's Gorge, karibu na Hifadhi ya Taifa ya Selous. Bwawa hilo lina lengo la kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji ya Mto Rufiji.



Sababu za Kimkakati za Ujenzi wa bwawa hili.

Upatikanaji wa Nishati: Mojawapo ya sababu kuu za ujenzi wa Bwawa la Stiegler's Gorge ni kuzalisha umeme wa kutosha kusaidia mahitaji ya nishati Tanzania. Umeme utakaozalishwa unatarajiwa kuboresha upatikanaji wa umeme nchini, kukuza viwanda, na kuongeza ufanisi wa shughuli za kijamii na kiuchumi.


Kupunguza Utegemezi wa Nishati ya Umeme: Kwa kujenga bwawa na kuzalisha umeme wa kutosha, Tanzania inalenga kupunguza utegemezi wake kwa vyanzo vingine vya nishati, kama vile mafuta na gesi.



Manufaa yake kwa Nchi na Jamii:

Upatikanaji wa Umeme, Wananchi watanufaika na upatikanaji wa umeme wa uhakika, ambao unaweza kuchochea maendeleo ya viwanda na biashara, pamoja na kuboresha maisha ya kila siku.

 

Fursa za Ajira, Ujenzi wa bwawa hilo na shughuli zinazohusiana na mradi zinaweza kutoa fursa za ajira kwa watu wa eneo na wengineo.

 

Mradi huu umeleta utata kutokana na wasiwasi wa athari za mazingira na kijamii, ikiwa ni pamoja na tishio kwa Hifadhi ya Taifa ya Selous. Baadhi ya watu wanahofia kwamba ujenzi wa bwawa unaweza kusababisha uharibifu wa mazingira asilia na kuhatarisha wanyamapori na mfumo wa ikolojia. Je Mtazamo wako ukoje juu ya mradi huu?



Na Haya Ndiyo Matokeo Chanya+