Matokeo chanyA+ online




Monday, November 30, 2020

KATIBU MKUU DKT BASHIRU ALLY AFUNGA SEMINA YA SIKU MBILI YA KAMATI ZA UTEKELEZAJI ZA JUMUIYA ZA CCM ,UVCCM,UWT NA WAZAZI LEO JIJINI DODOMA



Meza kuu ikiimba Nyimbo ya Chama mara baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally Kakurwa alipowasili katika Ukumbi wa Halmashauri kuu ya CCM Leo jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally Kakura akizungumza na Viongozi wa jumuiya za CCM Wakati wa kufunga Semina ya Siku mbili ya Viongozi wa Jumuiya zote za CCM iliyofanyika katika Ukumbu wa White House Jijini Dodoma


Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala akizungumza wakati wa Kuwasilisha taarifa mbalimbali za Jumuiya hiyo.


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Komred Kheri D James akizungumza  Semina ya Siku mbili ya Viongozi wa Jumuiya zote za CCM iliyofanyika katika Ukumbu wa White House Jijini Dodoma


Washiriki Wasemina hiyo wakifuatilia

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania akizungumza katika  Semina ya Siku mbili ya Viongozi wa Jumuiya zote za CCM iliyofanyika katika Ukumbu wa White House Jijini Dodoma


Katibu wa Idara ya Oganaizesheni wa Chama cha Mapinduzi Ndg Pereila Silima akitoa ufafanuzi wa jambo katika  Semina ya Siku mbili ya Viongozi wa Jumuiya zote za CCM iliyofanyika katika Ukumbu wa White House Jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally Kakurwa (kulia) akimkabidhi kitabu Cha ilani ya CCM YA 2020-2025 pamoja na hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Komred Kheri James kwa niaba ya Viongozi wote wa UVCCM kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa ahadi za CCM.

 Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally Kakurwa (kulia) akimkabidhi kitabu Cha ilani ya CCM YA 2020-2025 pamoja na hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa CCM  kwa niaba ya Viongozi wote wa UVCCM kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa ahadi za CCM.

Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally Kakurwa (kulia) akimkabidhi kitabu Cha ilani ya CCM YA 2020-2025 pamoja na hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa CCM Komred Kheri James kwa niaba ya Viongozi wote wa UVCCM kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa ahadi za CCM. (PICHA ZOTE NA UVCCM)


MTATURU AANZA KUTEKELEZA AHADI ZA WANANCHI


Wachungaji na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kiaskofu Msalaba Mrefu mjini Singida, wakiwa na pikipiki walizokabidhiwa hivi karibuni na Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu kwa ajili ya kazi za kanisa hilo,
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akimkabidhi pikipiki, Mkuu wa Jimbo la Kusini Usharika wa Issuna, Mchungaji, Obedi Msele.
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akimkabidhi pikipiki, Mchungaji Joyce Madadi wa Usharika wa Ikungi.

 Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akimkabidhi pikipiki, Mchungaji, Felix Kibiriti.


Na Dotto Mwaibale, Singida.


Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ameanza kutekeleza ahadi zake kwa wananchi kwa kasi ya 4G.

Mtaturu ametekeleza ahadi yake  kwa kutoa pikipiki tano kwa Usharika wa Kiaskofu Msalaba Mrefu mjini Singida ambazo alimkabidhi Mchungaji Felix Kibiriti kwa niaba ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dkt. Alex Mkumbo kwa ajili ya matumizi ya shughuli mbalimbali za kanisa hilo mkoani Singida.

Mbali ya kukabidhi pikipiki hizo zenye thamani ya sh.milioni 11, Mtaturu pia alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo pikipiki mbili zenye thamani ya sh.milioni 4.6 kwa ajili ya Kituo cha Polisi cha Wilaya hiyo ili ziweze kusaidia kwa kazi.

Akizungumza hivi karibuni katika hafla ya kukabidhi pikipiki hizo Mtaturu alisema utoaji wa pikipiki hizo ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa kusaidia kanisa hilo kupata usafiri wa uhakika kwa watumishi wake wanapo kwenda kuhubiri neno la Mungu.

 "Nitaendelea kutimiza ahadi zangu na kushirikiana na wananchi kwa kasi ili kuunga mkono jitihada ya Rais Dkt. John Magufuli ya kutekeleza miradi ya maendeleo" alisema Mtaturu.

Aidha Mtaturu alisema kuwa pikipiki hizo zitatumika katika sharika za Mang'onyi, Issuna, Mungaa na Ikungi zilizopo Jimbo la Singida Mashariki.

 Mtaturu alitoa ahadi hiyo Novemba 8, 2020 wakati akizindua kitabu cha Misemo na Methali za Wanyaturu kilichoandikwa na Mchungaji Dkt.Syprian Yohana Hilinti (PhD) kilichozinduliwa katika Kanisa Kuu la Kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT) Singida mjini na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi huko mshereheshaji katika hafla ya  uzinduzi wa kitabu hicho akiwa ni Mbunge wa Iramba  Mwigulu Nchemba.

KAMATI YA USALAMA WILAYA YA IKUNGI SINGIDA YAKAGUA MIRADI YA ELIMU NA AFYA




Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wakijadiliana wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya Elimu na Afya wilayani humo. Kamati hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo.
Moja ya chumba cha darasa kilicho kaguliwa na kamati hiyo.
Baadhi ya madarasa yaliyokaguliwa.
Muonekano wa vyoo vya Shule ya Msingi vilivyo kaguliwa na kamati hiyo.
Muonekano wa baadhi ya madarasa yaliyokaguliwa na kamati hiyo.
Muonekano wa baadhi ya madarasa yaliyokaguliwa na kamati hiyo.
Ukaguzi ukiendelea. 
Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua ujenzi wa Chuo cha Veta. Kushoto mbele ni  Mwenyekiti wa kamati hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo.

Muonekano wa ndani wa baadhi ya madarasa ya shule za sekondari yaliyokaguliwa na kamati hiyo.


Muonekano wa ndani wa baadhi ya madarasa ya shule za sekondari yaliyokaguliwa na kamati hiyo.

Moja ya chumba cha darasa cha shule ya sekondari kilicho kaguliwa na kamati hiyo.

Jengo la Maabara lililokaguliwa na kamati hiyo.

Muonekano wa vyoo vilivyo kaguliwa na kamati hiyo.



Na  Mwandishi Wetu, Ikungi


KAMATI ya Usalama ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya Elimu na Afya ambapo mbali na kupongeza usimamizi wa fedha zilizoletwa na Serikali juu ya miradi hiyo, iliwataka baadhi ya wasimamizi wa miradi hiyo kukamilisha kwa wakati ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wa miradi ya Elimu, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,  Edward Mpogolo, alisema ni lazima madarasa na vyoo vikamilike kwa wakati ili yaanze kutumika mapema mwakani na kuondoa changamoto ya vyumba vya madarasa iliyokuwepo kwenye shule hizo .

Aidha pamoja na mapungufu machache yaliyobainishwa na kamati wakati wa ukaguzi, kamati iliridhishwa na miradi hiyo kwa kuwa thamani ya fedha za serikali katika miradi inaonekana ambapo pia ilimtaka Mhandisi wa Halmashauri kuhakikisha anasimamia  maboresho na mapungufu yaliyojitokeza na kutoa msaada wa kitaalamu kwa kila mradi uliokutwa na dosari. 

Kwa shule zenye idadi kubwa ya wanafunzi, Mpogolo alizielekeza Serikali za vijiji na Kamati za Maendeleo ya Kata kuanza mchakato wa kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule hizo na kuongeza kuwa serikali itaunga mkono katika ukamilishwaji wa majengo ya shule hizo huku akiagiza afisa Mipango Miji na Mhandisi wa wilaya kukagua na kupima maeneo yote yenye shule shikizi na kupeleka mapendekezo  katika vikao vya halmashauri juu ya ukamilishwaji wa shule hizo.

Katika mradi wa ujenzi wa  Hospitali ya Wilaya, Mpogolo, aliitaka kamati ya ujenzi iliyoteuliwa na Mkurugenzi Mtendaji kwa ajili ya usimamizi wa mradi ambao unaendeshwa kwa mfumo wa  “Force Account” kuhakikisha wanakuwepo  eneo la mradi kila siku kwa ajili kushauri kitaalamu na kusikiliza changamoto ambazo mafundi wanakumbana nazo wakati wa ujenzi. 

Alisisitiza mradi huo, ambao ulitengewa kiasi cha sh. Bilioni 1.5 unatakiwa ukamilike kwa wakati na kwa thamani halisi kama ambavyo iliagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, katika ziara yake ya kampeni, ambapo alitoa siku 60 ili kukamilika kwa mradi huo na kuahidi kufika kwa ajili ya uzinduzi.

Katika ziara hiyo ya siku tatu, kamati pamoja na wataalamu wa halmashauri walitembelea na kukagua miradi yote ya Afya na Elimu inayotekelezwa katika Wilaya ya Ikungi katika mwaka wa fedha 2019/2020  na  yote ikiwa na thamani ya zaidi ya  sh. Bilioni 4.5.

Wakati huo huo, mkuu wilaya hiyo amemuagiza Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani humo kuchunguza taratibu zote za ujenzi wa Madarasa Matatu na vyoo vya Shule ya Msingi Matongo baada ya kubainika ukiukwaji wa taratibu mbalimbali za ujenzi. 

Ukiukwaji huo ulibainika baada ya kamati ya usalama kufika katika shule hiyo kukagua ujenzi unaoendelea wa madarasa na vyoo hivyo na kubaini mapungufu mengi na hivyo, Mpogolo kuagiza kufanyika kwa uchunguzi na ikibainika hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa wahusika wote wa usimamizi wa mradi huo na katika kipindi hicho cha uchunguzi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo amtafute mwalimu atakaekaimu nafasi ya mwalimu mkuu.

Hata hivyo, Kamati ya Usalama ilimshukuru Rais Magufuli kwa kuleta fedha nyingi zaidi ya 4.5 bilioni za maendeleo kwa muda mfupi. Pia imempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Justice Kijazi, kwa kuendelea kusimamia vizuri fedha ya serikali katika miradi inayoletwa katika halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. 

Miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo ni ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari na msingi, mabweni, mabwalo, ununuzi wa madawati, ujenzi wa vyoo, maabara na ujenzi wa Chuo cha Ufundi cha Veta.


SEKTA YA MISITU IKISIMAMIWA VIZURI INAWEZA KULETA MAPINDUZI MAKUBWA YA MAENDELEO KWENYE VIJIJI


Muwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Nanjita Nzunda  akifungua Warsha na Mkutano Mkuu wa 20 wa Mwaka wa MJUMITA mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa MJUMITA, Revocatus Njau akitoa nasaha zake mbele ya wajumbe kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua mkutano huo.


Mkurugenzi wa MJUMITA, Rahma Njaidi  akieleza malengo ya Warsha na Mkutano huo Mkuu wa 20 wa Mwaka wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.


 Mkurugenzi Msaidizi wa TFCG, Emmanuel Lyimo, akitoa salamu za Shirika lake mbele ya wajumbe wa mkutano huo wa Mwaka wa MJUMITA.

Wajumbe wa Mkutano huo Mkuu wa 20 wa Mwaka wa MJUMITA kutoka Kanda zote sita wakifuatilia hotuba na nasaha za ufunguzi wa mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano huo Mkuu wa 20 wa Mwaka wa MJUMITA kutoka Kanda zote sita wakifuatilia hotuba na nasaha za ufunguzi wa mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano huo Mkuu wa 20 wa Mwaka wa MJUMITA kutoka Kanda zote sita wakifuatilia hotuba na nasaha za ufunguzi wa mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano huo Mkuu wa 20 wa Mwaka wa MJUMITA kutoka Kanda zote sita wakifuatilia hotuba na nasaha za ufunguzi wa mkutano huo.



 Na Calvin  Gwabara, Morogoro.


Imeelezwa kuwa Sekta ya Misitu ikisimamiwa vizuri na kwa uendelevu italeta mchango chanya katika sekta zinazotegemea mifumo ikolojia ya Misitu ya asili kama vile Kilimo, Maji,Wanyamapori, na nishati.

Hayo yalisemwa na  Nanjita Nzunda Muwakilishi wa KatibuTawala wa Mkoa wa Morogoro kwenye ufunguzi wa Warsha na mkutano Mkuu wa 20 wa mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misiti Tanzania MJUMITA uliofanyika Mkoani Morogoro.

Alisema  kuwa sera na sheria ziko wazi na zinawezesha vijiji kuanzisha na kurasimisha misitu yao na kuandaa mipango yao ya usimamizi, sheria ndogondogo na mipango ya uvunaji.

“Kwa kurasimisha Misitu yao ya hifadhi, vijiji vinakuwa na mamlaka ya kusimamia na kunufaika kwa asilimia Mia moja na Misitu huo lakini pia kunatoa fursa kwa Kijiji husika kuusimamia huo Msitu kwa manufaa ya Wananchi na kupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa Misitu” alisema  Nzunda.

Aliongeza kuwa Usimamizi shirikishi wa Misitu ya Jamii ni nyenzo kuu ya uhifadhi wa Misitu kwani wananchi wanakuwa na na mamlaka ya kuusimamia Msitu husika kulingana na Mipango yao ya Usimamizi na sheria ndogo walizojiwekea.

Nzunda alibainisha kuwa pamoja na faida hizo lakini kila Mwaka Tanzania inapoteza hekta zaidi ya 460,000 za Misitu kiasi ambacho ni kikubwa sana hivyo kila Mtanzania anapaswa kuchukua za makusudi kunusuru Misitu.

“ Nawapongeza sana MJUMITA na TFCG kwa kuwezesha vijiji kuanzisha misitu ya hifadhi ya vijiji Kilosa,Mvomero,Morogoro,Kilwa,Lindi, Liwale,Tunduru, Nachingwea, Handeni na Kipindi ambako zaidi ya vijiji 100 vimewezeshwa na nimefurahi kusikia kwamba mashirika haya mawili yamewezesha Misitu ya Hifadhi zaidi ya 50 kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali (Gazettment).

Aliongeza kuwa Misitu hiyo ina jumla ya Hekta 168,331.38, na kwamba hayo ni mageuzi makubwa katika sekta ya Misitu na nu Misitu ya mfano kufikia hatua hiyo.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi huyo kufungua warsha na mkutano huo Mkuu Mwenyekiti wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania MJUMITA, Revocatus Njau  alisema kuwa MJUMITA ni chombo cha Kitaifa ambacho kinaunganisha Jamii zinazoishi kandokando ya misitu ya asili na kuwa na sauti ya pamoja juu ya usimamizi wa Misitu na utawala Bora.

Mwenyekiti huyo alisema mtandao huo ulianzishwa Mwaka 2000 na ilisajiliwa Kama NGO Mwaka 2017 na mtapa sasa ina mitandao 100 katika Kanda sita za Tanzania na kwamba ina wanachama katika vijiji 452 kwenye mikoa 30 ya Tanzania bara.

“ Kupitia jitihada hizo kubwa za TFCG na MJUMITA zinewwzesha kuboresha maisha ya jamii kupitia shughuli mbalimbali kama vile ufugaji wa Nyuki,Kilimo,Kilimo hifadhi,miradi ya maji,ufugaji vipepeo, uzalishaji wa Mkaa Endelevu na uanzishwaji wa ViCOBA” alibainisha Njau.

Mwenyekiti huyo alifafanua kuwa MJUMITA ineweza kuwaleta Pamoja takribani Wanachama 15,000 katika usimamizi wa Misitu ya asili vijijini wakisimamia Misitu zaidi ya hekta 1,800,000 katika vijiji viwili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MJUMITA, Rahma Njaidi alisema kuwa Warsha na Mkutano huo Mkuu wa Mwaka hufanyika kila Mwaka na kuwakutanisha wajumbe kutoka nchi nzima ili kujadili changamoto na mafanikio yanayopatikana kila Mwaka na kuyatafutia ufumbuzi wa pamoja.

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa misitu bado inaangamia kutoakana na kazi mbalimbali za kibinadamu hivyo kuna kila sababu ya kurasimisha Misitu hiyo iliyo kwenye vijiji nchi nzima ili kupunguza uharibifu unaofanyika kiholela ili itunzwe na kutumika kwa njia endelevu kwa maslahi ya vijiji na Taifa kwa ujumla.

“ Tukiacha uharibifu huu uendelee tutaifanya nchi yetu kuwa jangwa na sisi hatuwezi kuruhusu Hilo litokee hivyo tuisaidie Serikali maana sisi ndio tupo huku chini tunajua kinachoendelea” alisisitiza, Njaidi.

Mkurugenzi Msaidizi wa TFCG, Emmanuel Lyimo alisema kuwa kwa mujibu wa utafiti wa NAFOMA uliofanyika Mwaka 2017 ulionyesha zaidi ya hekta 4069 inapotea kutokana na uharibifu wa aina mbalimbali za misitu.

“ Ni wajibu wetu wananchi kuhakikisha tunatunza misitu yetu nchi nzima kwa kupanga namna bora  ya kusimamia lakini pia mapato yanayopatikana kutokana na mazao ya misitu hiyo yatumike kwenye vijiji kwenye miradi ya maendeleo kama motisha ya usimamizi huo” alisema Lyimo.

Lyimo aliwataka wajumbe wa mkutano huo kutambua kuwa wakati umefika jamii na serikali iwekeze kwenye Misitu ili itangazwe kwenye gazeti la Serikali ili kuvipa vijiji nguvu za kuisimamia vizuri kisheria na kuongeza misitu ya hifadhi ya jamii inayosimamiwa kutoka hekta milioni mbili kwa sasa na kuifikia misitu hekta milioni 22 ambayo haijaifadhiwa kwa sasa.

Mashirika ya MJUMITA na TFCG wanatekeleza Mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu ya jamiii(USMJ) chini ya Mradi wa kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) na mradi wa kuhifadhi Misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya Misitu (CoFOREAT) kwa ufadhili wa Shirika la  Maendeleo la Uswis (SDC).


Sunday, November 29, 2020

MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA DODOMA YAFANA




Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ibenzi Ernest akimuongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe (aliyevaa kaunda suti) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk. Doroth Gwajima  (wa tatu kulia) kwenda kuzindua ukarabati wa chumba cha dharula na uangalizi wa wagonjwa mahututi  (ICU),  wakati wa maadfhimisho ya miaka 100 tangu Hospitali hiyo hiyo ianzishwe 1920. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe  (wa pili kushoto ) akikata utepe kuzindua rasmi ukarabati wa chumba cha dharula na uangalizi wa wagonjwa mahututi (ICU), katika Hospitali hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk. Doroth Gwajima. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe akikagua chumba cha uangalizi wa wagonjwa mahututi (ICU).


Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ibenzi Ernest akimuongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe kukagua wodi ya wanawake ambayo imekarabatiwa na kuwekwa vifaa vipya ikiwemo vitanda, magodoro na vinginevyo.



Jengo la Wazazi
Jengo la Bima ya Afya

Wanafunzi wa Chuo cha Afya Mirembe, mkoani Dodoma wakitumbuiza kwa wimbo maalumu wakati wa maadhimisho hayo.

Sehemu ya wafanyakazi na wageni waalikwa


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk. Doroth Gwajima  akitoa neno  wakati wa maadhimisho hayo.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akitoa ahadi ya kujenga choo na bafu eneo la wananchi wanaosubiria wagonjwa wao katika Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Meja mstaafu John Salingo akielezea kuwa mafanikio ya Hospitali hiyo ni Utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Baadhi ya watumishi na wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo.


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Best Magoma akitoa nasaha zake wakati wa maadhimisho hayo.

Aliyekuwa Muuguzi Mkuu wa Mkoa  Anatolia Mkindo akikabidhiwa cheti cha kutambua mchango wake katika hospitali hiyo kabla ya kustaafu.  Baadhi ya watumishi wa hospitali waliostaafu walitunukiwa vyeti.

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali hiyo, Dk. Ezekiel Mpuya akimkabidhi tuzo  maalumu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe.

Happy Mwaikugile ambaye ni mmoja wa wafanyakazi bora akilakiwa kwa furaha na wafanyakazi wenzie baada ya kutunukiwa tuzo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe (kulia) akimkabidhi tuzo maalumu Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ibenzi Ernest kwa uongozi wake thabiti.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Best Magoma akitoa nasaha zake wakati wa maadhimisho hayo.