Matokeo chanyA+ online




Tuesday, July 25, 2023

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KWA VIONGOZI WANAOSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU RASILIMALI WATU, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 25 JULAI, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu wakati wa hafla ya Chakula cha jioni, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.




Matukio mbalimbali wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na wageni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi, Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova, Rais wa Madagascar Mhe. Andry Nirina Rajoelina pamoja na Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Biowakati wakiangalia vikundi mbalimbali vikitumbuiza katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Wonie Bio wakati wa hafla ya chakula cha jioni Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.








Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi pamoja na Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova kabla ya hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.

Wakuu wa nchi mbalimbali pamoja na Viongozi wengine wakiwa kwenye hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya viongozi hao wanaoshiriki Mkutano wa Rasilimali watu Jijini Dar es Salaam Julai 25, 2023.


Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Madagascar Mhe. Andry Nirina Rajoelina kabla ya kuelekea kwenye hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu jijini Dar es Salaam .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe tarehe 25 Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Madagascar Mhe. Andry Nirina Rajoelina, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.


Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa pamoja na viongozi wengine kutoka nchi mbalimbali wakielekea kwenye hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi

 

MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. PHILIP MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA AFRIKA WA RASILIMALI WATU

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifuatilia Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam wakati alipowasili kufungua mkutano huo leo tarehe 25 Julai 2023.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mke wa Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela mama Graca Machel wakati alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. Tarehe 25 Julai 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba wakati alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC)  Jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. Tarehe 25 Julai 2023



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia viongozi wakiwemo mawaziri kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakati akifungua Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam. Tarehe 25 Julai 2023.








Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema taasisi za kifedha za kikanda na kimataifa zinapaswa kujishughulisha zaidi katika kubuni na kutoa  masuluhisho ya kifedha ili kuunga mkono azma ya nchi za Afrika  ya kuharakisha maendeleo ya rasilimali watu.

 

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akihutubia viongozi mbalimbali wa Afrika akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ufunguzi wa Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam. Amesema uwekezaji katika Rasilimali watu ni wa muda mrefu hivyo unahitaji ufadhili wa gharama nafuu kutoka taasisi hizo za fedha za kimataifa. 

 

Aidha, Makamu wa Rais ametoa wito kwa taasisi za mafunzo na elimu kuhakikisha zinasaidia bara la Afrika kuimarisha uwezo wa wazawa katika kusimamia na kutumia kikamilifu rasilimali zilizopo. Amesema Bara la Afrika linatumia rasilimali nyingi za kifedha katika kutafuta maarifa na rasilimali watu kutoka nje ya bara hilo kwa ajili ya kutumia maliasili zilizopo. Ameongeza kwamba kutokana na umuhimu wake taasisi za mafunzo barani Afrika zinapaswa kushirikiana na kutafuta suluhisho ya changamoto zinazolikabili bara hili.

 

Halikadhalika, Makamu wa Rais ametoa rai kwa mkutano huo kutafuta njia bora zaidi ya kuihamasisha sekta binafsi kushirikiana na serikali katika kuzalisha rasilimali watu iliyo bora kwa kuwa sekta binafsi ni wanufaika wakubwa wa maendeleo ya rasilimali watu.

 

Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa Bara la Afrika na Wadau wa maendeleo kuwekeza zaidi katika Elimu, Afya, Lishe, Maendeleo jumuishi pamoja na ulinzi wa jamii. Ametoa wito kwa wahudhuriaji wa mkutano huo kujadili na kupata sera za kibunifu zitakazosaidia katika kuboresha maendeleo ya rasilimali watu na kuwapa uwezo idadi kubwa ya vijana inayoongezeka barani Afrika.

 

Makamu wa Rais amesema Tanzania inaendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha inaboresha rasilimali watu kwa kuwekeza katika sekta za elimu, afya na kilimo ikiwemo kuongeza bajeti na kuhakikisha miundombinu rafiki katika sekta hizo. Amesema hatua zilizochukuliwa zimesaidia katika kupata matokeo chanya ikiwemo ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kuanza shule kutoka asilimia 85 mwaka 2015 hadi 97 mwaka 2021 huku kiwango cha wanaohitimu elimu ya msingi kufikia asilimia 100 mwaka 2022 kutoka asilimia 80 mwaka 2015. Ameongeza kwamba vyuo vya ufundi nchini Tanzania vimejengwa katika mikoa 30 kati ya 31 pamoja na kuongezeka kwa uwiano wa kijinsia wa 1:1 katika kupata elimu.

 

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amesema Tanzania inapitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Sheria ya Elimu na Mitaala mapitio yanayolenga kuboresha mfumo wa elimu ili kukidhi ukuzaji wa vipaji, ujuzi wa vitendo, umahiri wa kujenga, fikra chanya na kuwafanya wahitimu kutambua teknolojia ya hali ya juu. Amesema jambo hilo linatarajiwa kuongeza tija kwa vijana, ushindani katika soko la ajira pamoja na kuwaandaa wahitimu kuwa wabunifu wa kazi kwa kujiajiri zaidi kuliko kuajiriwa.

 

Pia amesema katika jitihada za kuimarisha rasilimali watu juhudi zinaelekezwa katika utoaji wa mafunzo, mapinduzi ya kidijitali, kuongeza utoaji wa huduma za jamii pamoja na usambazaji wa nishati ya umeme ili kufikia vijiji vyote. Vilevile, kuimarisha miundombinu ya TEHAMA kwa kutambua ongezeko la wanaotumia intaneti kutoka asilimia 36.5 mwaka 2015 hadi asilimia 49 mwaka 2021.

Thursday, July 6, 2023

KUWAJALI WATOTO YATIMA NA WALE WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI NI JUKUMU LETU SOTE KAMA JAMII. NEEMA GOSPEL CHOIR

Katika dunia hii, tunahitaji kusimama pamoja na kuleta mabadiliko chanya. Tarehe 22 Julai 2023, The Super Dom, Masaki, tunakuja na tukio la kipekee la chakula cha hisani linaloitwa "INSPIRE, EMPOWER, TRANSFORM for a Better World" kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan,kulinda,kusaidia watoto yatima na wale wenye uhitaji maalumu, wapozaidi ya Arobaini waliotufikia kuomba msaada wa jamii na kwa pamoja tumeamua kushirikisha umma kujumuika nasi kusaidia kwa hali na mali. 
Watoto hawa Wanahitaji upendo wetu, huduma yetu, na fursa ya kuwa na mustakabali mzuri. Kwa kujiunga nasi kwenye tukio hili, tunawapa tumaini la kuwa na maisha yaliyojaa furaha na mafanikio.
Tutaimba pamoja, tutawawezesha kwa Pamoja na tunakuomba popote ukiguswa Changia mchango wako kwa kutumia njia za malipo zifuatazo: Vodacom MPesa: 5922779, CRDB: 0133549137200, NMB: 20702302010. Amesisitiza Samuel Nkola. Mwenyekiti wa Neema Gospel Choir

Neema Gospel Choir

Na Mwandishi wetu.

KUWAJALI WATOTO YATIMA NA WALE WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI NI JUKUMU LETU SOTE KAMA JAMII. 

Hapa kuna njia kadhaa ambazo jamii inaweza kuchukua ili kuwajali watoto hawa:

1.   Kutoa msaada wa msingi: Jamii inaweza kutoa msaada wa msingi kwa watoto hawa kwa kuhakikisha wanapata mahitaji muhimu kama chakula, mavazi, malazi, huduma za afya, na elimu. Serikali, mashirika ya kiraia, na watu binafsi wanaweza kuchangia kwa kutoa michango, kusaidia katika miradi ya maendeleo, au kuanzisha vituo vya kulea watoto. 

2.   Kupatia elimu na mafunzo: Kutoa fursa za elimu na mafunzo kwa watoto yatima na wale waishio katika mazingira hatarishi ni muhimu. Jamii inaweza kusaidia kwa kuanzisha shule za bure, kuwapatia fursa za ufadhili wa elimu, na kutoa mafunzo ya ujuzi unaowasaidia kupata ajira na kujitegemea.

"Kuwajali watoto yatima na wale waishio katika mazingira hatarishi ni jukumu letu sote kama jamii."

3.   Kuendeleza utamaduni wa kujali na kuheshimu: Jamii inaweza kujenga utamaduni wa kujali na kuheshimu watoto yatima na wale waishio katika mazingira hatarishi. Hii inaweza kufanyika kwa kuelimisha jamii juu ya changamoto wanazokabiliana nazo na kuhamasisha uelewa na ushiriki wa watu katika kuwasaidia na kuwapa nafasi sawa za kukua na kufanikiwa.

4.   Kujenga familia mbadala: Kuhamasisha na kuunga mkono familia mbadala kama vile ulezi wa watoto na kupitishwa kunaweza kuwasaidia watoto hao kupata upendo, usalama, na malezi bora. Serikali na mashirika yanaweza kutoa miongozo na msaada kwa familia mbadala ili kuhakikisha mazingira salama na yanayowajali watoto hao.

"Maandiko ya dini yanatuhimiza kutekeleza wema na kuwasaidia wanyonge, ikiwa ni pamoja na watoto yatima."

5.   Kutoa ushauri na huduma za kisaikolojia: Watoto yatima na wale waishio katika mazingira hatarishi mara nyingi wanakabiliwa na changamoto za kisaikolojia kutokana na uzoefu wao. Jamii inaweza kuhakikisha upatikanaji wa huduma za ushauri na msaada wa kisaikolojia kwa watoto hawa ili kuwasaidia kushughulikia mafadhaiko, kuimarisha ustawi wao wa kiakili, na kujenga uwezo wa kujitegemea.

6.   Kuhamasisha uwezeshaji wa kiuchumi: Kuwezesha watoto hawa kiuchumi ni muhimu ili waweze kujitegemea baadaye. Jamii inaweza kuwasaidia kwakuwapa fursa za kujifunza ujuzi na stadi za kiuchumi, kutoa mikopo ndogo ya kuanzisha biashara, au kuunda programu za kazi kwa watoto wadogo wanaoweza kufanya kazi. Hii itawasaidia kujenga ujasiri na uwezo wa kujitegemea katika maisha yao.

7.   Kukuza uelewa na kupunguza unyanyapaa: Jamii inaweza kufanya kazi kwa bidii katika kuondoa unyanyapaa na ubaguzi unaowakabili watoto yatima na wale waishio katika mazingira hatarishi. Elimu ya umma na kampeni zinaweza kusaidia kubadilisha mitazamo potofu na kuwafanya watu wawe na uelewa zaidi na huruma kuelekea watoto hawa.

"Kupitia jitihada za pamoja, tunaweza kujenga mazingira salama na yenye upendo kwa watoto hawa."

Maandiko ya dini na kanuni zinazojenga msingi wa kuwasaidia watoto hawa zimeainishwa katika vitabu vitakatifu

1.   Ukristo: Katika Biblia, Mathayo 25:40 linasema, "Amin, nawaambieni, kwa kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo kabisa, mlinitendea mimi." Hii inaonyesha umuhimu wa kuwajali na kuwasaidia watu walio katika mazingira magumu, ikiwa ni pamoja na watoto yatima na wale waishio katika mazingira hatarishi.

2.   Uislamu: Katika Qur'an, Surat Al-Israa, aya ya 31 inasisitiza wajibu wa kutekeleza wema kwa wazazi, ndugu, mayatima, na masikini. Pia, Hadithi nyingi zinasisitiza umuhimu wa kuwajali na kuwasaidia watoto na mayatima kwa kuwapatia upendo, malezi bora, na msaada wa kimaisha.

3.   Uyahudi: Katika Tanakh (Agano la Kale), kuna amri nyingi zinazolenga kujali mayatima na kuwasaidia watoto walio katika mazingira magumu. Kwa mfano, Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 10:18 linasema, "Huwalinda mayatima na wajane na huwapenda wageni na kuwapa chakula na nguo." Hii inaonyesha wajibu wa kusaidia na kuhudumia watoto yatima na wale walio katika mazingira hatarishi.

4.   Ubuddha: Ingawa hakuna maandiko maalum yanayozungumzia moja kwa moja suala la watoto yatima, mafundisho ya ubinadamu, huruma, na upendo wa ubuddha yanaweza kuongoza kuhusu umuhimu wa kuwajali na kuwasaidia watoto hao. Kufuata mafundisho ya Ahimsa (kutoharibu) na Metta (upendo wa ukarimu) kunaweza kusisitiza uhisani na kuwasaidia watoto katika hali ngumu.

Misingi ya upendo, wema, ukarimu, na kuwajibika kwa jumla inaweza kuwa msingi wa kushiriki katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi au yatima.

Watoto yatima na wale waishio katika mazingira hatarishi ni wajibu wetu kama jamii na inahitaji jitihada za pamoja. Serikali, mashirika ya kiraia, taasisi za kidini, familia, na jamii kwa ujumla, wanahitaji kushirikiana ili kutoa mazingira salama, yenye upendo, na yanayowajali watoto hawa, ili waweze kuishi maisha yenye hadhi na kupata fursa za kufikia uwezo wao kamili.