Matokeo chanyA+ online




Tuesday, January 16, 2018

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA APONGEZA KASI YA MATENGENEZO MAGARI YA POLISI,MAGEREZA,JWTZ


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepongeza hatua ambayo kampuni ya kutengeneza mabodi ya magari ya Dar Coach Ltd imefika y'all kutengeneza na kukarabati mabasi 11ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Jumla ya Sh milioni 830 mmiliki wa kampuni hiyo anatumia katika kukarabati magari yote 11

Akizungumza leo baada ya kukagua magari hayo katika kampuni hiyo iliyopo Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani,Makonda amesema hatua ya ukarabati magari hayo umefikia pazuri na ameahidiwa kukabidhiwa baadhi ya magari hayo mwishoni mwa mwezi huu.

 Baadhi ya magari ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanaendelea kutengenezwa ambayo yalipelekwa yakiwa yameharibika kabisa 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza leo wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati alipoenda kukagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama yanayotengenezwa na Kampuni ya  Dar Coach. 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo leo na Mkurugenzi wa kampuni ya Dar Coach Manmeet Lal kuhusu hatua waliyofikia katika kufanya matengenezo ya magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanatengenezwa mabodi yake yaliyokuwa yameharibika.Matengenezo hayo yanafanywa na Kampuni ya Dar Coach Ltd
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua moja ya gari la Jeshi la Magereza yanayofanyiwa matengenezo na Kampuni ya Dar Coach Ltd


No comments:

Post a Comment