Matokeo chanyA+ online




Thursday, February 28, 2019

PROF MBALAWA AHIMIZA JAMII KUSHIRIKI KULIENDELEZA BONDE LA MTO ZAMBEZI


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa  Makame Mbarawa, amefungua Mkutano wa Saba wa Mawaziri wa Maji wa nchi nane  zilinazohusiana na Bonde la Mto Zambezi (Zambezi Watercourse Commission – ZAMCOM) na kuitaka jamii ya mataifa hayo kuona umuhimu wa kamisheni ya chombo hicho kuendelea kuimarika na kusimamia raslimali za ZAMCOM kwa manufaa yaliyokusudiwa.
Waziri Mbarawa alikuwa anafungua kikao cha Baraza la Mawaziri wa Maji katika Ukumbi  wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, vikao vikiwa ni Mkutano wa Sita wa Baraza la Mawaziri Februari 26 – 27 na Mkutano wa saba wa Kamati ya Wataalaam ya ZAMCOM, nchi husika zikiwa ni Angola, Botswana, Msumbiji, Malawi, Namibia, Zambia, Zimbambwe na Mwenyeji Tanzania.
Mkataba wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi ulianza rasmi mwaka 2011 kwa lengo la kusimamia raslimali za maji za Bonde la Mto Zambezi, Tanzania ambayo ni mwanachama maji yake toka Ziwa Nyasa, kwa wastani wa asilimai 16 ya maji yaingiayo Ziwa Zambezi kwa mito,  humwagika Ziwa Zambezi na Bonde hilo linahitaji hifadhi na zipo fursa za kuwepo miradi ya manufaa kwa nchi hizo.
Baraza limepokea Mpango kazi (Strategic Plan) na  Mfumo  wa kubadilishana, kutumia na kuhifadhi takwimu za raslimali za Maji kwa njia ya TEHAMA, ambapo Tanzania imemaliza muda wake wa Uenyekiti na nafasi hiyo kupewa Zambia.

No comments:

Post a Comment