Waziri
wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba
Kabudi akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
alipofika kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Waziri
wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba
Kabudi wa Pili kutoka Kushoto akielezea msimamo wa Wizara yake katika
kuzitangaza fursa za Uwekezaji zilizopo Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Ramadhan Muombwa.
Profesa
Palamagamba Kabudi(katikati) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo
yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa kwanza kulia akimpongeza
Profesa Palamagamba Kabudi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Balozi Seif kulia na Profesa Palamagamba Kabudi
wakibadilishana mawazo mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Vuga
Mjini Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa
Palamagamba Kabudi amesema Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
imefanikiwa kuwa na Taifa linaloendelea kudumu muda wote kutokana na
misingi imara iliyowekwa na Waasisi wa Taifa hilo.
Alisema yapo Makabila mengi katika Mikoa na Wilaya mbali mbali Nchini
Tanzania lakini muungano wa sauti moja inayozungumnzwa na Wananchi
wake Bara na Zanzibar imekuwa mfano kwa Mataifa mengine Duniani.
Profesa Palamagamba Kabudi alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar
alipofika kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.
Alisema yapo Mataifa mengi Duniani yaliyowahi kuunganisha Nchi zao
akaitolea Mfano iliyokuwa Yugoslavia na sasa imesambaratika Senegal na
Gambia kwa Afrika lakini zimeshindwa kuendeleza Miungano hiyo.
Waziri Palamagamba alisema wakati Serikali zote mbili Nchini Tanzania
zinaendelea kuheshimu kwa kuweka Kumbukumbu za Waasisi hao Marehemu
Mzee Abeid Amani Karume na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
Vizazi vya sasa vinapaswa kujifunza tabia ya Viongozi hao walioacha
msingi imara wa Umoja ndani ya Ardhi ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment