Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba akiongea na wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali ambao kwa
pamoja wanaunda kikosi kazi cha kusimamia utekelezaji wa katazo la
mifuko ya plastiki hapa nchini. Wajumbe hao ni kutoka Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Mapato Tanzania,
Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Shirika la Viwango
Tanzania, Mamlaka ya Chakula na Dawa, Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkemia
Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Kikao hicho kimefanyika hii leo katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango –
Dodoma.
Sehemu
ya wajumbe wanaounda kikosi kazi cha kusimamia utekelezaji wa katazo la
mifuko ya plastiki hapa nchini wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Hayupo
pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika hii leo katika Ukumbi wa
Chuo cha Mipango.
No comments:
Post a Comment