Matokeo chanyA+ online




Tuesday, July 30, 2019

WAZIRI WA NISHATI AAGIZA MKANDARASI KUTOA AJIRA 50 KWA VIJANA WA KARATU

Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani amemwagiza Mkandarasi wa Kampuni ya Nipo Group Mhandisi Shija Magese kuhakikisha anatoa ajira kwa vijana 50 wa Kijiji cha khusumay Wilayani Karatu, ili wasaidie kazi za uwekaji umeme kwenye Vijiji 39 vya wilaya hiyo.

Alitoa agizo hilo jana alipotembelea Wilaya hiyo na kuzindua Rea awamu ya tatu, iliyofanyika kiwilaya katika Shule ya Sekondari ya Baray Khusumay na kuhudhuriwa na wananchi wa Wialaya hiyo.

Alisema ameagiza utoaji wa ajira hiyo kwa sababu mkandarasi huyo amepewa kumaliza kazi ya uwekeaji miundombinu ya umeme na kuwaunganishia wananchi nishati hiyo kwa muada wa miezi 24, lakini mpaka sasa bado nusu ya kazi hajamaliza.

“Sasa naagiza ajiri vijana 50 wa eneo hili ili muda wako tuliowekeana mkataba umalize ni Juni mwaka 2020, lakini nataka umalize kazi hii Desemba 30 mwaka huu, sasa hawa vijana watakusaidia na wakati huo watanufaika na ajira na Meneja wa Wilaya simamia hawa,”alisema

Dk.Kalemani aliahidi kurudi kijijini hapo kufuatilia kama kazi hiyo imeisha kwa wakati muafaka ili wananchi wapate umeme na kuzalisha viwanda vidogovidogo.

Aidha aliagiza Meneja wa Wilaya hiyo Tanesco, Edward Mwakapuja kufungua vituo kwenye vijiji husika ili wananchi wapate unafuu wa kuwafikia na kulipa Sh.27,000 ili waunganishiwe umeme huo wa Rea.

Pia aliwataka Wafanyakazi wa Tanesco kuhakikisha wanafanya kazi za kuhudumia wananchi na kuepuka kuvaa suti kama wanakwenda Kanisani.

“Nimepiga marufuku wafanyakazi Tanesco kuvaa suti labda kama mnaenda kanisani Jumapili, sababu hapa kazi tu, suti na kazi wapi na wapi acheni kabisa pigeni kazi,”alisema Aliwasisihi pia wanachi hao kutunza miundombinu ya umeme wakiwekewa ili waendelee kunufaika nao na kupata maendeleo.

Dk.Kalemani aliwaagiza wanafunzi wa Shule yya Sekondari ya Baray Khusumay kuhakikisha wanafanya vizuri masomo yao na kufaulu vizuri kwa sababu umeme wameshapata.“Someni usiku na msachan lakini pia umeme huu utawamulika msifanye maovu maana shule hii ya wavulana na wasichana mkisimama kwa yale mambo yenu umeme huu utawamulika, someni mfaulu na shule hii mpya,”alisema

Kuhusu suala la kukatika kwa umeme aliagiza Tanesco kuhakikisha wanamaliza tatizo hilo harka, sababu umeme upo wa kutosha hadi ziada.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo alishukuru serikali kwa kuwafikishia umeme kijiji hicho ambacho tangu Uhuru hakijawahi pata umeme, lakini aliomba Waziri kufuatilia changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara wilayani humo.

“Tunaamini tatizo hili litaisha baada ya uzinduzi wa Rea awamu ya tatu kufanyika, sababu kukiwa na umeme tunaamini usalama utakuwa juu na hata ufaulu kwenye shule utaongezeka,”aisema

Akijibu suala la kukatika kwa umeme, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Mhandisi Herin Mhina alisema sababu ya kukatika kwa umeme huo kulitokana na utengenezaji wa nguzo zaidi ya 600 ambazo zimewekwa mpya.

Kwa upande wake Mkandarasi wa kampuni ya Nipo Group Shija Magese, aliahidi kumaliza kazi hiyo Desemba mwaka huu na mpaka sasa kati ya Vijiji 39 anavyotakiwa kuweka umeme wa Rea, vijiji 23 ameshajenga miundombinu ya kuweka umeme na kati ya hivyo nane ameshawasha umeme. 
Wafanyakazi kutoka kampuni ya Booygues Energies &services wakiendelea na Mradi wa ujenzi wa njia za kusafirisha umeme Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK wa laini kubwa ya msongo wa kilovolti 400 inayoanzia Singida unapita Babati nakuja mkoa wa Arusha hadi Namanga ,ujenzi huo unaendelea katika kijiji cha Kisongo jijini Arusha (Picha na Woinde Shizza, Arusha 
WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani akiongea na wananchi .
WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani alipotembelea Wilaya ya Karatu na kuzindua Rea awamu ya tatu, iliyofanyika kiwilaya katika Shule ya Sekondari ya Baray Khusumay 
WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani akiongea na viongozi wa Tanesco pamoja na mkuu wa wilaya ya karatu wakati alipotembelea kituo cha Tanesco cha wilaya hiyo .

No comments:

Post a Comment