Matokeo chanyA+ online




Monday, September 30, 2019

SERIKALI IMETENGA SH. 1.5 BILIONI KWA AJILI YA UPANUZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA CHALINZE


Madarasa Manne (4) yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Kibindu kwa Msaada wa TANAPA yamekamilika na yameanza kutumika katika Jimbo la Chalinze,Mkoani Pwani.                                                                                                          Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika jimbo hilo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani  ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo.


Akizungumza katika ziara hiyo Ridhiwani amesema kuwa ujenzi wa vituo cha afya katika Halmashauri ya Chalinze umefanyika kwa kiwango kikubwa kwa kujenga Zahanati kila kijiji na  vijiji vichache ambavyo Zahanati zao hazijakamilika.

Madarasa Manne (4) yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Kibindu kwa Msaada wa TANAPA yamekamilika na yameanza kutumika katika Jimbo la Chalinze,Mkoani Pwani

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete akizungumza na wananchi (hawapo kwenye picha) katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika jimbo hilo,Mkoani Pwani
Muonekano wa kituo cha afya Kibindu ambapo Serikali ilitoa fedha shilingi milioni 400 kufanikisha ujenzi huo katika Jimbo la Chalinze mkoani Pwani.
Naibu Katibu Mkuu Tamisemi-Afya Dr. Dorothy Gwajima na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete wakikagua ramani katika Hosptali ya Wilaya ya Chalinze alipofanya ziara Mkoani Pwani  
Kwa upande wa vituo vya Afya amesema  kazi inaendelea kwa  kila Kata ambapo amesema mpaka sasa bado kata tatu ambazo ujenzi wake uko mbioni kuanza na kuongeza kuwa Serikali imetenga 1.5 Billion kwa ajili ya Upanuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze.

Aidha amesema kwa upande wa elimu kumejengwa  vyumba vya madarasa 48,na kwa upande wa umeme umesambazwa katika eneo kubwa katika jimbo  la Chalinze.

Ridhiwani amesema kuwa Serikali imepanga kutumia shilingi 158.5 Milioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mji wa Chalinze ambazo zitajengwa kwa kiwango cha lami na ujenzi wa madaraja madogo.

Muonekano wa kituo cha afya Kibindu ambapo Serikali ilitoa fedha shilingi milioni 400 kufanikisha ujenzi huo katika Jimbo la Chalinze mkoani Pwani.
Serikali imetenga 1.5 Billion kwa ajili ya Upanuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze, ambapo Tsh.500M zitatumika kuanza ujenzi huo 2019/20, akizungumza hayo  Naibu Katibu Mkuu Tamisemi-Afya Dr. Dorothy Gwajima alipofanya ziara kujionea Maendeleo ya Hospitali hiyo.

Mbunge wa Jimbo wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akikagua kituo cha afya Kibindu ambapo Serikali ilitoa fedha shilingi milioni 400 kufanikisha ujenzi huo. 

Mbunge huyo ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuipatia Chalinze Shilingi Bilioni 16 kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji ambapo fedha hizo zinakwenda kumaliza tatizo la maji  Chalinze  na maeneo ya jirani ikiwemo  Ngerengere na Magindu kwa upande wa Kibaha Vijijini.
 
Mbunge huyo  pia amewapongeza wanawake kwa jinsi wananvyokuwa mstari wa mbele katika ufanisi wao wa kuchangamkia fursa ndondogo za halmashauri. 

Amesema hadi sasa vikundi zaidi ya 80 vya wanawake vimeweza kufikiwa katima kata mbalimbali na kupongeza namna wakinamama hao wanavyorudisha mikopo ili watu wengine weweze kukupo kufanya shughuli za maendeleo na kujipatia kipato.




No comments:

Post a Comment