Matokeo chanyA+ online




Thursday, December 31, 2020

RAIS WA ZANZIBAR DK HUSSEIN ALI MWINYI AWATUNUKIA SHAHADA WAHITIMU WA SUZA

 

Wahitimu wa Shahada ya Kwanza ya Benki na Fedha wakitunukiwa Shahada yao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk,Hussein Ali Mwinyi wakati wa Mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 30-12-2020.
Wahitimu wa Shahada ya Usimamizi wa  Teknolojia ya Habari wakishangilia wakati wa kutunukiwa Shahada yao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA ) ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati wa hafla ya Mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.
Wahitimu wa Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Kemia wakitunukiwa Shahada ya Uzamili na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya Mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo.
Wahitimu wa Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Usimamizi wa Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi  wakitunukiwa Shahada yao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja. (Picha na Ikulu.)

No comments:

Post a Comment